Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Wakuu,

Tetesi zilizonifikia ambazo SI NZURI (kwa tunaopenda kuona wenzetu hata tukiwa na tofauti nao) zinaashiria kama kuna kitu kisicho cha kawaida kimemkuta bwana huyu hii leo.

Vyanzo vyangu vya kuaminika vinanihabarisha kuwa bwana huyu yamemkuta ya kumkuta. Kuna mwenye kuwa na 'ukweli' au 'tetesi' zaidi?

==============
UPDATES:
==============

Taarifa za awali zinadai kamwagiwa Tindikali maeneo ya Msasani City Mall muda wa saa 2.

Ni jirani na Ubalozi wa Marekani na jirani kabisa na Police Oysterbay.

Jamaa aliyefanya kitendo hicho alitoka mbio, mlinzi akamkimbiza lakini bahati mbaya akateleza na kuanguka na jamaa akawahi pikipiki na kutoweka eneo la tukio.

Said amelazwa Trauma (AMI) Hosp - Masaki.

Kapata madhara macho yote mawili ila moja ndilo limeumia zaidi sehemu ya juu.

Mwenyewe anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua na madaktari wanamhudumia.

Polisi wanahaha kutafuta wahusika kwa nguvu kubwa na huenda akakamatwa mhusika mapema sana.


==============

Some useful topics on JF:

===============
Mmiliki wa Home Shopping Centre amwagiwa tindikali usoni|Dar es Salaam.


Mtu asiyejulikana juzi usiku alimvamia mmiliki wa maduka ya Home Shopping Centre, Said Mohammed Saad (pichani) na kumwagia maji usoni yanayodhaniwa kuwa ni tindikali.

Tukio hilo lililotokea juzi saa 1 usiku karibu na kituo cha Polisi cha Oysterbay, lilithibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ally Mlege kwa kusema kuwa bado polisi wanaendelea na uchunguzi wao ili kuwabaini waliohusika.

"Ni kweli tukio hili limetokea ila polisi wanaendelea na uchunguzi. Tukikamilisha uchunguzi tunatarajia kutoa taarifa kamili za tukio zima," alisema na kuongeza;

"Hatuna haja ya kuficha ukweli wa tukio hili, uchunguzi wetu ukikamilika na watuhumiwa wakikamatwa kila mtu atajua."

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa mtu huyo, alimkuta Saad akiwa anazungumza na mmoja wa wafanyakazi wake katika duka lake jipya lililopo karibu na Kituo cha Polisi cha Oysterbay.

"Wakati akizungumza na mfanyakazi wake, huyo mtu alikuwa kama anapita na alichomoa kitu fulani na kummwagia Saad usoni na kisha kukimbia," zilieleza taarifa hizo na kuongeza;

"Baada ya tukio hilo alipelekwa katika Hospitali ya AMI, sasa hatujui kama bado yupo hapo au ameondoka, ila sisi tulizungumza naye na alitueleza mwonekano wa mtu aliyemwagia tindikali."

Taarifa hizo zilifafanua kwamba polisi wanazitumia taarifa hizo walizopewa na Saad, ili kuweza kumkamata mhusika.

Taarifa hizo zilifafanua kuwa polisi wanapanga tena siku ya kumhoji kwa mara ya pili Saad, kwamba watataka kufahamu kama mfanyabiashara huyo alikuwa akipewa vitisho au ujumbe wowote, kabla ya kukutwa na tukio hilo.

Hata hivyo, habari nyingine zilizolifikia Mwananchi Jumapili zilieleza kuwa mtu huyo baada ya kummwagia Saad tindikali, alipanda pikipiki na kutokomea eneo hilo.


"Walikuwa wawili, mmoja alikwenda kufanya unyama na mwingine alibakia katika pikipiki, baada tu ya kumwagia tindikali mtu yule alikimbia mpaka pale alipokuwa imesimama pikipiki, alipanda na kuondoka kwa kasi," zilieleza habari hizo.

Taarifa zilizopatikana jana asubuhi zilieleza kuwa ndugu na marafiki wa mfanyabiashara huyo, walikuwa katika mipango ya kumpeleka nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Chanzo: Mwananchi
==============
Katika picha, ni eneo lilipotokea tukio la kumwagiwa Tindikali

attachment.php
 

Attachments

  • eneo-la-tukio.jpg
    eneo-la-tukio.jpg
    29 KB · Views: 54,082
Ni kweli, amemwagiwa tindikali usiku huu na watu wasiojulikana. Ni Said Mohammed Mahmoud, mdogo wake Gharib.
 
Aisee! Ile 'mall' ya jirani na ubalozi wa Marekani imefunguliwa? Au ni yake?
 
Mmmh! Hii nchi kila kunapokucha kunazidi kuwa siyo sehemu salama ya kuishi, Mola amsaidie
 
Ukicheka sana ipo siku utalia sana

Ukilia sana ipo siku utakuja cheka sana

Ukiwa mgovi sana kuna siku utakuwa mpole sana

Ukiwa malaya sana kuna siku utakipa kilichopo kwenye huo umalaya(ukimwi)

Ukiwa mchimbaji wa madini na ukavumilia ipo siku utatoka na chochote kama sio kuishia humo humo na shimo lako kuwa kaburi lako

Ukiwa muongeaji sana ipo siku utakuwa mc wa harusi ama mlopokaji

Ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga

Maisha hayawi maisha bila kuishi

Ikiwamwagia sana wenzako ipo siku na wewe utamwagiwa, iwe maji, soda, bia, mafuta ya taa, petroli,acid etc...

Pole sana bro, kama ni kweli wakuwaishe tu india kabla hujadhurika sana, wanadamu kuna mda wanakosa damu wanabakia wana tu
 
Kazi kweli kweli..! Kila mtu has to be responsible for his own safety..! hakuna wa kutulinda nchi hii..!
 
Bila shaka kuna fahari mwenzio wana ugomvi wao maana si rahisi mbuzi kugombana na tembo, tumwombee asidhurike ili atoe hints kwa vyombo vya usalama.Jeshi letu la polisi lina kazi ya ziada mwaka huu!
 
Back
Top Bottom