Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa lakanusha na kutoa ufafanuzi juu ya taarifa za kuuawa kwa mfanyakazi wa ASAS kwa kipigo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,274
9,717
Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limetoa taarifa inayokanusha taarifa ya kwamba mfanyakazi wa kampuni ya ASAS ndugu martin chacha aliuwawa kwa kipigo baada ya kutuhumiwa kuiba lita 200 za mafuta kwa muajiri wake ambaye ni ASAS.

Jeshi la polisi limesema kuwa taarifa hizo siyo za kweli, kwa kuwa ndugu martin chacha mpaka umauti unamkuta alikuwa anatumikia kifungo cha miezi mitatu jera mkoani Iringa ,ambapo alihukumiwa na mahakama ya mwanzo mkoani Iringa katika jinai namba 62/2024 kwa kukutwa na kosa la kuiba mafuta lita 383.

Ambapo baada ya kupatikana na hatia hiyo alipelekwa gerezani na aliendelea kutumikia kifungo chake cha miezi mitatu,na kwamba ndugu martin chacha alipatwa na mauti akiwa hospitali ya rufaa mkoa wa iringa, ambapo alipelekwa hapo kutokana na kujisikia maumivu makali upande wa moyo ambayo alilalamika kwa wafungwa wenzake wakiwa katika shughuli za kilimo eneo la mlolo gerezani.

Ndipo baadaye alikimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu, ambapo hata hivyo aliweza kufariki Dunia, ambapo jeshi la polisi lilipewa taarifa ya kifo hicho na mkuu wa gereza na kwamba linaendelea na uchunguzi wa tukio na kifo hicho. Ambapo taarifa za awali kutoka kwa daktari aliyempima zinadai na kuonyesha kuwa marehemu alikuwa na tatizo la moyo . Jeshi la polisi limewataka watu waache uzushi na kuzuia mambo yasiyo na ukweli ndani yake.

Lakini pia jeshi la polisi limemtaka mtu yeyote mwenye ukweli au taarifa zitakazo saidia kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo la kifo cha ndugu martin
Chacha basii aweze kufika polisi kutoa taarifa.

Ndugu zangu Watanzania mimi Mwashambwa nimeleta taarifa hii kama ilivyo bila kuongeza maneno yangu ya aina yoyote ile, lakini rai yangu nilikuwa namuomba Mdude Nyagali ambaye alitoa taarifa hii humu jukwaani, aweze kufika haraka polisi ili kutoa na kusaidia ushahidi wake utakaosaidia kupatikana kwa ukweli wa kifo cha ndugu Martin Chcha ,kama alivyodai kuwa ndugu yetu huyu alikufa kwa kipigo.

Ni vyema aende polisi kutoa ushahidi wake wa taarifa aliyodaia kuwa marehemu alikufa kwa kipigo cha muajiri wake akishirikiana na askari wa suma jkt. maana kwa mujibu wa Mdude Nyagali alidai kuwa marehemu baada ya kuwa ametoka kwa dhamana mahabusu alikwenda moja kwa moja katika ofisi za ASAS kwa ajili ya kuchukua passport yake na vifaa vingine vilivyokuwa katika gari alilokuwa akiendesha wakati wa utumishi wake katika kampuni hiyo.

Na sasa taarifa ya jeshi la polisi inasema kuwa martin Chacha alikuwa anatumikia kifungo cha miezi mitatu jera kwa kosa la kuiba mafuta lita 383.hivyo tupate ukweli ni upi na uongo ni upi.maana taarifa ya jeshi la polisi imenyooka kabisa .hivyo Mdude Nyagali aje hapa au ajitokeze hadharani apinge kama martin alikuwa hatumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani.

kama itathibitika kuwa ni kweli Martin alikuwa anatumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani basi Mdude Nyagali atakuwa ni muongo,mzushi na anayestahili kuchukuliwa hatua kali sana za kisheria kwa kuleta taharuki na uzushi unaoleta chuki na uhasama katika jamii na wenye kuchafua watu pasipo sababu.

Ndio maana nasema ni muhimu sana Mdude Nyagali ajitokeze haraka sana hadharani atoe ufafanuzi wa taarifa yake , kutokana na jeshi la polisi kuonyesha kuwa taarifa yake aliyoitoa na kuisambaza mitandaoni ni ya uongo na uzushi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Tunajua Asas ndio mnunuzi wa sare za Polisi Iringa
Jibu swali hili je una ushahidi wa aina yoyote ile kuipinga taarifa ya jeshi la polisi kuwa marehemu Martin chacha alikuwa anatumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani kwa kosa la kuiba mafuta lita 383?

Kama huna huo ushahidi na unakubaliana na taarifa ya jeshi la polisi.je ni vipi mtu anayetumikia kifungo jera na ambaye alikuwa hajamaliza kifungo chake apate nafasi ya kwenda kwa muajiri wake kuchukua passport Katika gari aliyo kuwa anaendesha awali?

Leteni ushahidi uliojitosheleza kupinga taarifa ya jeshi la polisi.uwekeni hapa ushahidi huo.
 
Vyawa katika ubora wenu...kwa hiyo na wewe unawaamini sana hao PT?
Hoja hupingwa kwa hoja na siyo hisia.jeshi la polisi limesema kuwa marehemu alikuwa anatumikia kifungo cha miezi mitatu jera.ambapo akiwa katika shughuli za kilimo alisikia maumivu upande wa moyo.sasa wewe kama una ushahidi unaoonyesha marehemu hakuwa anatumikia kifungo jera uweke hapa jukwaani .
 
Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limetoa taarifa inayokanusha taarifa ya kwamba mfanyakazi wa kampuni ya ASAS ndugu martin chacha aliuwawa kwa kipigo baada ya kutuhumiwa kuiba lita 200 za mafuta kwa muajiri wake ambaye ni ASAS.


Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Mtu yupo magereza ni mfungwa jeshi la polisi linafanya uchunguzi ila mdude ni mzushi!
 
Tunajua jeshi la polisi Iringa ni mnufaika mkubwa wa huyu ASAS. Anawapatia mafuta, wnawajengea nyumba hapa Iringa na kuwajengea vituo vya polisi. Kwahiyo hili kanusho tulilitegemea.
Inatakiwa sote tupate ukweli .jeshi la polisi limesema marehemu alikuwa anatumikia kifungo cha miezi mitatu jera.sasa wewe kama una ushahidi kuwa taarifa hiyo ni ya uongo basi weka hapa taarifa ya kupinga hiyo ya polisi.
 
Back
Top Bottom