Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

Watu walio karibu nae wanasema kwamba kapata madhara macho yote mawili lakini moja ndio limeharibika sehemu ya juu na atalazimika kupandikizwa sehemu nyingine nje ya nchi baada ya kuwa amepona kabisa. Taarifa zinasema hospitali imejaa jamaa sake ndani na nje kiasi cha kufanya hali ibadilike kabisa.

Mgonjwa mwenyewe anaweza kuzungumza japo hadi saa Saba usiku huu alikua amefungwa mashine sehemu ya pua Huku madaktari wakimpa huduma maalumu na hatosafirishwa hadi apone majeraha na kwamba upandikizaji umeelezwa si jambo la haraka kwa sasa.

katika hali isiyo ya kawaida, polisi wanahaha kutafuta wahusika kwa nguvu kubwa tofauti na usiku tulipokua Muhimbili alipoumizwa Kibanda, na huenda hadi kesho akakamatwa mhusika.

Who is Kibanda in this country?!! (George Wassira, 2013)...
 
Duuh sasa siku hizi sijui tuwe tunatembea tumevaa helmet!! Maskini sura zetu.
Dawa yake ni Sodium Hydroxide labda - kwa mawazo yangu!! Naona mbinu hizi za tindi kali zinashika kasi sana nchini, kwa nini hawaweki udhibiti wa kutosha katika manununuzi - au zinahibiwa kwenye mahabara ya Sekondari.
 
Naona tangu amwagiwe tindikali Saed Kubenea na Tigambwage, basi imekuwa kama ndiyo fashioni hivi sasa. Kila mtu anamwagiwa tindikali. Ni adhabu ya kitoto sana na ya watu wasiokuwa na hata tone la fikra.

Wanaofanya hayo, raha yao ni nini? Je ni kuona wenzako wakiwa na ulemavu wa ngozi au ni kuona tu vile wanavyobadilika na kuwa na sura mbaya? Maana kwa imani yangu hata ummwagie tindikali, kama mtu ana roho mbaya, atabaki hivyo hivyo. Kama ni fisadi atabaki fisadi tu, hakuna utakachokuwa umesolve zaidi ya kumsababishia maumivu ya muda tu.

Tubadilike watanzania.

Lukolo unaongea KITOTO SANA. Think a little bit big
 
Nchi yetu pendwa ina amani, tunailinda na kuitukuza kwa njia mbalimbali.
Next to the police station!
 
ufataani hehehe afadhali mwalimu wa Kiswahili umerudi, huyu jamaa wa home shopping center atakuwa anajua siri ya maswaibu yake, ila tindikali ni noma jamani, don't wish it to anyone...
 
subiri wana lumumba team waje utasikia chadema wanahusika

wamwaga tindikali wanajulikana, tangu enzi za akina kubenea, mtoa mada anadai polisi watawashika wahusika!!!!!!!!!!!!!!!!! Mimi nakataa, polisi hawana uwezo wala utashi wa kuwatafuta! Subirini mtaona!
 
"Ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga heri nife kwanini nisife maisha haya dunia sio mbaya walimwengu ndio wabaya hawakawii flani ana hiv"-sugu
 
Polisi nao wamevamiwa na wezi kwenye kituo chao Mwanza na kuibiwa laptop 2 na vielelezo.

Gongo la mboto wametekwa hapohapo kituoni kwao, wakapewa kichapo na kuswekwa lupango.. hadi huruma sasa..
 
Tanzania kila mtu anaruhusiwa kuuza acid..H2CO4 zipo madukani
kila gaidi anaweza kujinunulia
Sdhani kama ipo sheria ya kulinda haya makitu
serikali iweke sheria kali kuhusu uuzaji na ununuzi
mtu awe na kibali maalumu ndio auziwe kama mashule nk..
la sivo tutakwisha wengi....................................
nimesahu kusema utasikia CHADEMA wanahusika au green guard wanahusika
tunakimbilia kutaja watu bila kuangalia madhara yanayoendelea.

mimi ni mwanafunzi nasoma kemia, H2CO4 ni acid gani hii? Msaada tafadhari
 
hivi tindikali ndo nini wakuu,mi nasikiaga tu chumvi miiingi maji kidogo ndo mixa yake,eti kweli eeeh?

Conc. Sulphuric Acid,Nitric Acid,Chromic Acid ni mojawapo ya strong acids. Hukunusa kabisa masomo ya sayansi maishani mkuu?
 
Kuna anaelindwa zaidi ya Rais wa USA? J. F. Kenedy kauliwa kwa risasi na ulinzi na walinzi wote aliokuwa nao, Ronald Reagan kasalimika kuuliwa lakini risasi ilimpata.

Usilete ushabik wa kinafik na kifataani wakati ukweli unaujuwa.

Wamemheshimu sana kwa kumwagia hiyo tindikali. Walipaswa WAMWOGESHE kabisa, Laana tululaiy yule!
 
mda wote unapoishi duniani lazima ujue kua binadamu ni watu wa kuishi nao vzuri usijifanye wewe ndio wewe hadi kumsahau mwenyezi mungu pole sana.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom