Sababu Za Kupinga Utengenezaji Wa Coin Ya Tsh 500 Nchi Tanzania Sasa

Nakumbuka wakati wanaleta fedha mpya walisema kwamba hazitoharibika haraka nashangaa haijapita hata mda ya noti ya jero na buku zinaenda halijojo.
 
Wadau tuangalie hizi sababu za kupinga sh 500 ya note kutobadilishwa to coins, kutoka kwa wataalamu wa uchumi nimeona tuichambue kidogo.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
BOT kufuta noti ya Sh.500/= na kuifanya sarafu. Huu ni wendawazimu mkubwa katika sekta ya uchumi "the most unpleasant economic decision" kwa sababu zifuatazo;

MOSI; fedha yoyote inapobadilishwa kuwa sarafu kutoka shillingi ni kuishusha thamani. Hii ni kwa sababu kiuchumi inabadilika matumizi na kuanza kutumika zaidi ktk sekta ya uchumi mdogo km wa wauza njugu mtaani, mama lishe, na maeneo mengine yasiyozalisha sana kiuchumi (less productive sector).

Maeneo yenye uzalishaji mkubwa (lead productive sector) yatashindwa kuitumia fedha hii kwa kuwa tu ni ya sarafu. Kw mfano kuanzia sasa haitakua rahisi kukuta sarafu hizi za 500/= maeneo kama Airport, Migodini au Supermarket.

Hiki ni kiashiria cha kushuka kwa thamani kwa fedha hiyo. (Indicator for currency devaluation).

Hivi hatujiulizi kwanini Marekani hadi dollar moja ni ya noti sisi 500/= tunaweka sarafu?? Dollar moja ina single digit lakini ipo kwenye noti, sisi tunalazimisha kuweka 500 kwny sarafu wakati ina tripple digit. Tunaforce Galloping inflation.

PILI; unapotengeneza sarafu ya pesa kubwa ina maana sarafu zinapotea na kujiondoa ktk mzunguko wa fedha. So tutegemee siku si nyingi sarafu za sh.100/= na sh 200/= hazitakuwepo tena mtaani.

Ikifikia hatua hii ujue nchi imeanza kuyumba kiuchumi na mfumko wa bei umevuka kiwango cha kawaida (extention from Moderate inflation to Galloping inflation).

Wenzetu Kenya hadi sarafu ya sh.10 inatumika. Ukienda Nairobi, Mombasa au maeneo mengine ya Kenya utata watoto wakinunua madafu, ice cream au matunda kwa sh.10.

Hapa kwetu sarafu ya sh.10 ilikufa na Nyerere. Ya sh.5 ikaenda na Sokoine. Ya sh.20 na 50 zimemfuata Kawawa. Sasa benki kuu wanalazimisha sarafu ya sh.100 na ya sh.200 zikamfuate Karume mahali pema peponi. Noti ya sh.1,000/= nayo inakaribia kwenda ahera maana BOT wameleta sarafu ya sh.1,500/=.

TATU; BOT kuwa wametoa hoja mufilisi kuwa wamefuta noti ya Sh.500/= na kuireplace kwa sarafu baada ya kugundua noti hiyo inachakaa haraka sn na inadumu kwa muda mfupi mno kwenye mzunguko.

Hoja hii ni mufilisi kwa sababu solution ya noti kuchakaa mapema si kureplace sarafu bali ni kuimarisha noti hiyo kwa kuitengeneza kwa material imara zaidi.

Hivi noti ya 10,000/= nayo ikichakaa mapema BOT wataleta sarafu instead?? Huu ni wendawazimu.

Mojawapo ya sifa za fedha imara ni uwezo wa kukaa kwny mzunguko muda mrefu (durability). Sasa fedha inapopoteza durability dawa sio kubadili muundo wake (changing of currency format is not a solution for impermanency)

Lakini hata hivyo BOT wameonesha hawakufanya utafiti wa kina kabla ya kuleta sarafu ya 500/=. Wanasema zinachakaa haraka ukilinganisha na noti nyingine. Hii ni hoja dhaifu sana kutolewa na mtu anayejiita Profesa wa uchumi Benno Ndullu.

Yani Profesa Ndulu anataka noti ya 500/= na ya 10,000/= zidumu kwenye mzunguko kwa muda sawa?? Yani 10,000/= ikidumu miaka miwili, 500/= nayo idumu miaka miwili. Bila shaka hapo ndo ataona noti ya 500/= haichakai haraka.

Hii ni "akili ndogo kujaribu kutawala akili kubwa". Noti ya 500 haiwezi kulinganishwa na noti nyingine kwenye mzunguko kwa sababu ina frequent circulation. Yani ktk uchumi noti yenye thamani ndogo huwa inazunguka zaidi kuliko ya thamani kubwa.

Hivyo noti ya 500/= inaweza kupita kwenye mikono ya watu 2000 ndani ya mwezi mmoja wakati ile ya 10,000/= imepita kwenye mikono 20 tu kwa mwezi.

Hii ni kwa sababu mzunguko wa noti hizi hutegemea matumizi. Ya 500/= itazunguka kwny daladala, wauza magazeti, vijiwe vya kahawa etc, wakati ile ya 10,000/= itazunguka Supermarket, Airport, hoteli kubwakubwa etc.

Hivyo ni dhahiri kuwa noti ya 500/= itaanza kuchakaa mapema kuliko noti. 10,000/= au ya 5,000/= au noti nyinhine kubwa. Sasa cha ajabu Profesa Beno Ndulu hajui hili na badala yake ameona solution ni kuleta sarafu. Aibu gani hii kwa mtu anayejiita Profesa wa uchumi kushindwa kujua vitu common km hivi ambavyo hata muuza machungwa wa Keko anavijua??

Mama lishe wa Tandale "kwa tumbo" anajua kuwa noti ya 500/= inachakaa haraka kuliko ya 10,000/= kwa sababu ina mzunguko mkubwa. Yeye anaweza kushika noti za 500/= hata mia kwa siku kwenye mauzo yake lakini asione hata noti moja ya 10,000/=.

Cha ajabu Profesa Ndulu hajui hili. Yeye amekerwa na noti ya 500/= kuchakaa haraka na ameona dawa ni kueeplace sarafu.

Naumia kuiona Tanzania ikiangamizwa na watu tuliowaamini, tuliowaheshimu, tukawapa madaraka, kwa kuamini ni wasomi watatusaidia. So sad, uchumi wa Tanzania ulale mahali pema peponi..!!

NNE. ........

Hoja namba tatu, tuko pamoja mkuu
 
Nakumbuka wakati wanaleta fedha mpya walisema kwamba hazitoharibika haraka nashangaa haijapita hata mda ya noti ya jero na buku zinaenda halijojo.

Watu walipiga pesa kwa project ile..ilikuwa hivi waligawa sana pesa kwenye uchaguzi zikabaki kwenye mzunguko (mifukoni mwa watu bila matumizi) ikasababisha serikar kukosa reserves na inflation ikawa juu.

Wakaona jibu ni kubadili pesa ili wananchi warudishe pesa za zamani mpaka leo hawana majibu ya maswali yao

Sasa Tanzania ndio nchi ya kwanza kutumia pesa yake kwa aina mbili.
 
Hoja namba tatu, tuko pamoja mkuu

Poa mkuu.

Tusaidie wachumi wetu wenye experience without current economic knowledge na kuendekeza ukada kwenye mambo ya mhimu ya nchi na uchumi kiujumla.
 
Sikubaliani na wewe na wakat mwingine nakubaliana na wewe kiasi.

Nilishasoma pepa ya Klein (2013) Time for Change. lakin kwa hili la kwetu wachumi wetu wamekurupuka sana.

Hivi sisi tunatumia mfumo gani wa uchumi? (ukijibu nitaendelea mkuu).

It does not matter whether you do or not!
Hatuwezi sote kuwa na mtazamo mmoja, hata kama tungekuwa "mapacha". Na utofauti huu ndiyo msingi wa maendeleo yote (ya kifikra na mengineyo).
Thumb-up ZERO IQ, mkuu nipo nawe!
 
Tutapiga kelele zote lakini msingi wa hoja hapa ni mfumuko wa bei (inflation). Hili ndiyo tatizo la msingi katika haya tunayoyaona ya kubadili "notes" kuwa "coins".

Mimi ningeomba nitoe maoni yangu kuwa kubadili "notes" kuwa "coins" kwa "small denomination notes" ni jambo zuri na msingi kwa ukuaji wa Taifa. Na msingi wa kauli hii inafuata sababu ileile iliyotolewa na BoT, kuwa "small denomination notes" huwa zinachakaa haraka. Kwa sababu hii, umuhimu wa "coins" unajitokeza sana kwa kuwa zinapunguza gharama. Kwa hili sitaeleza sana, kama tuna muda tunaweza ipitia pepa ya Klein (2013) inaitwa "Time for Change: Modernizing to the dollar coin saves taxpayers billions", ambayo hata kwa kugoogle inapatikana.

Shida tunayoipata akina sisi (Tanzania) hatuumizi akili kutibu katika mizizi ya tatizo, tunaangalia suluhu ya harakaharaka. Kinachotutokea sisi, mfumuko wa bei unaziua zile "small denominations" kama senti, shilingi moja, tano, kumi, ishirini, hamsini nk. kwa kuzitoa katika matumizi. Kwa mtindo huu "higher denominations" kama shilingi mia, mia mbili, tano nk zinaanza kuonekana zikichakaa haraka. Hapa ndipo BoT wanapopaona kuwa kuna tatizo. Kwao ufumbuzi ni kubadili "notes' kuwa "coins", na sio kuweka mikakati ya kushusha kwa kasi mfumuko wa bei.

Kwa wenzetu walioendelea kama USA, Canada, England na nchi nyingine za Ulaya, hili la kubadili "notes" kwenda "coins" walikwishafanya. Kwa kumbukumbu za harakaharaka, USA wamefanya hivi mara tatu (1970s, 1990s na 2005) kwa kutumia President Coin Act. Lakini hawa wenzetu hawabadili "notes" kwenda "coins" kwa msukumo wa mfumuko wa bei, ila ni katika harakati za kuokoa gharama za kuzitumikia "small denomination notes" ambazo huwa zinachakaa mapema. Hii ndiyo tofauti ya wao na sisi (wale wenzetu wanatumia neno sie).

Hivyo basi, kwa sasa hiki walichofanya BoT ni sahihi ili kuokoa gharama ya kuitumikia 500 ambayo sasa inachakaa mapema kwa kuwa ndiyo "small denomination note". Lakini, kama wale wachumi wetu wanafanya kazi, sasa ndiyo muda wao kuhakikisha mfumuko wa bei unashuka ili matumizi ya hela ndogo kuliko 500 yawepo.
Wasiwasi wangu ni kuwa, wataalamu wetu wameshindwa kuushusha mfumuko wa bei kiuhalisia. Wiki iliyopita nilisikia wakidai mwezi huu umeshuka. Lakini ni nani mwenye udhubutu wa kutaja maeneo yanayoakisi kushuka huko?!!! "Figures" tunazotajiwa za kushuka kwa mfumuko wa bei binafsi naona ni kiini macho (Tanzania ni zaidi ya
tuijuavyo).
QUOTE

Mkuu unajua kwa nchi zinazoendelea, ku-control mfumuko wa bei ni ngumu sana. Maana bei ya mambo mengi hatupangi sisi. Hatuna hio leverage ya kupanga bei za kuuza na kununua bidhaa katika soko la dunia. Vitu kama mafuta chakula nk ndio vinasababisha mufumuko na hayo mafuta ya (crude oil). Kuhusu suala la kutumia sarafu badala ya noti iko very challenging ukizingatia mazingira tuliyonayo hasa katika microeconomics part. For the long term watasave hela nyingi sana kwa kubadilisha fedha chakavu. Lakini pia wata-create another problem ya value depreciation.
Mimi nathani kwa knowledge ndogo niliyonayo bot wangetoa kwa urefu maelezo na wachumi watoe maoni yao.
Kama ulivyosema waafrica tumezoea kutafuta njia rahisi kusolve matatizo yetu badala ya kutambua kiini cha matatizo.


]




The king.
 
Mkuu frema120! Bado una imani na maprof.Wa Tanzania? Ni bora hata Maji Marefu kuliko hawa akina Benno na mwenzake Nkhoma wa TCRA! Hivi hakuna materials ambayo yanaweza kutumiwa kutengeneza noti imara?

Umemsahau na yule Katibu mkuu wa wizara ya elimu,Prof Mchome
 
Umemsahau na yule Katibu mkuu wa wizara ya elimu,Prof Mchome

Ha ha ha haaa! Yaani hii inji tunaweza kuwekwa kwenye Guinness Book na tukafit ile mbaya! Yaani maprof. wetu hovyo kabisa, sijui hii elimu imewasaidiaje mkuu nashindwa kuelewa kabisa. Sasa hivi nasikia wanatoa matokeo ya form 4 kwa GPA?
 
Nakumbuka wakati wanaleta fedha mpya walisema kwamba hazitoharibika haraka nashangaa haijapita hata mda ya noti ya jero na buku zinaenda halijojo.

Mabadiliko hayo waliyafanya 2010,wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu,tulipiga kelele sana juu ya ubora na uimara wa hizi noti,na BOT walitengeneza hadi vipindi maalum kuwaondolea wananchi hofu,leo hii kiko wapi!Mie bado naamini kuwa huu ni mradi wa chama tawala kujitafutia fedha za chaguzi zijazo...TUAMKE WATANZANIA.
 
....Kunani Tanzania Hapo..?,Wametengeneza Noti Ya 1,500/= Na Coin Ya 500/=. Mwigulu njemba Hayupo hapo BOT Na NDULLU?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umeongea kitu cha maana sana.mm nilifikir wanaleta not mpya zenye kudumu wao wanaleta saraf.bora waongeze sarafu za sh kum and ishirin na sh tano
 
in reality our country are being destroying with our educated Tanzanian...honestly they are doing bad.
 
RPRJRT (Right PEOPLE, Right Job, Right Time)

Ama kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
Tanzania ni nchi ya kwanza kuwa na ela za aina tatu zenye thamani moja katika mzunguko unaokaribiana mia tano iliyotolewa na mia tano tuliyonayo sasa hata miaka mitano haikupita nayo mpya inatolewa hata miaka mitano haikupita. Hapo wanatengeneza mianya ya ufisadi waendelee kutafuna nchi na sio vinginevyo. Sababu zao hazina mashiko kabisa, wanang'ang'ania kutengeneza pesa ambayo ni makaratasi baada ya kutengeneza uchumi unaoporomoka kila kukicha kwa siasa zao
 
Tanzania ni nchi ya kwanza kuwa na ela za aina tatu zenye thamani moja katika mzunguko unaokaribiana mia tano iliyotolewa na mia tano tuliyonayo sasa hata miaka mitano haikupita nayo mpya inatolewa hata miaka mitano haikupita. Hapo wanatengeneza mianya ya ufisadi waendelee kutafuna nchi na sio vinginevyo. Sababu zao hazina mashiko kabisa, wanang'ang'ania kutengeneza pesa ambayo ni makaratasi baada ya kutengeneza uchumi unaoporomoka kila kukicha kwa siasa zao

Yani inaumiza sanaaaa juu ya maamuzi ya wachumi wetu.
 
Mimi sio mtaalam wa mambo ya Kiuchumi lkn kwa uelewa wangu naamini Nchi kuendelea kutengeneza fedha kubwa huko kunaonyesha Uchumi kuharibika.

Kwa mfano Nchi ya Kenya fedha zake ziko juu sana ukilinganisha na Tanzania. eg Kshs 100 ni sawa na tshs 1870. Utaona ni kwa jinsi gani tulivyozidiwa.

Upande wa Kenya noti kubwa kabisa ni ya shs 1000 wakati ya Tanzania ni shs 10,000. kwa upande wa Sarafu shs 40 ndio Sarafu kubwa kabisa Kenya wakati Tanzania ni shs 500.

Mimi ninachojiuliza, hawa Watu wanaojiita Wachumi hapa Tanzania huwa kazi yao kubwa ni nini wakati Uchumi unaendelea kudorora?.

Naomba kama kuna mtaalam au wataalam wa Uchumi watuambie nini maana ya kuendelea kutengeneza sarafu kubwa badala ya kupunguza ukubwa wa Fedha?. Nategemea sana mchango wenu.
 

Attachments

  • 2014-10-13 15.24.33.jpg
    2014-10-13 15.24.33.jpg
    204.6 KB · Views: 211
  • UC_Photo_001.jpg
    UC_Photo_001.jpg
    41.6 KB · Views: 172
  • UC_Photo_002.jpg
    UC_Photo_002.jpg
    49.5 KB · Views: 166
  • UC_Photo_003.jpg
    UC_Photo_003.jpg
    54.3 KB · Views: 146
  • UC_Photo_004.jpg
    UC_Photo_004.jpg
    33.3 KB · Views: 165
Back
Top Bottom