BoT yasema Noti za Tsh. 10,000 zimeongezeka mtaani hadi Tsh. Trilioni 6.3

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Ripoti ya Dondoo za Takwimu za Robo mwaka inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeonyesha ongezeko kubwa la thamani na mzunguko wa noti ya Sh10,000.
Ufuatao ni mwenendo wa thamani ya mzunguko wa noti za Sh10,000 mtaani.

Desemba 2018 ➡ Sh3.6 trilioni
Desemba 2019 ➡ Sh4 trilioni
Desemba 2020 ➡Sh4.2 trilioni
Desemba 2021 ➡ Sh4.8 trilioni
Desemba 2022 ➡Sh5.5 trilioni
Desemba 2023 ➡Sh6.3 trilioni

Mbali na kuongezeka kwa mzunguko wa Sh10,000 pia noti ya Sh2,000 imeongezeka kutoka Sh177.2 milioni Desemba 2018 hadi Sh230.8 milioni Desemba 2023 sawa na ongezeko la asilimia 15.

Noti ya Sh5,000 thamani ya mzunguko wake ilipungua kutoka Sh732.2 Desemba 2018 hadi Sh713.7 mwaka 2023 sawa na kupungua kwa asilimia 2.5.

Kuelewa maana ya ongezeko hilo na kauli ya Benki Kuu, soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi; Noti za Sh10,000 zaongezeka mitaani, wachumi, BoT watofautiana

Chanzo: Ripoti ya Dondoo za Takwimu za Robo ya mwisho ya mwaka 2023, BoT
 
Kitendo cha noti ya elfu kumi kuongezeka mtaani ni wazi pesa yetu inashuka thamani,
Kwasasa matumizi yangu ambayo nilikuwa nayaona ni ya anasa tu najikuta natumia elfu 30 kwa siku,hapo bado yale matumizi ya lazima.

Salary slip haiongezeki,
Marupurupu ni kama hakuna,
Na matumizi yapo juu zaidi.
 
Tuliowahi kutumia hela za Nyerere kwa mfano cent 50, shilingi 1, shilingi 5, shilingi 10, shilingi 20, na hizi shilingi 50 na 100 zinazoelekea kuzimu; tunaona mauza uza tu kwenye huku kuporomoka kwa thamani ya pesa yetu.

Sijui ni nani atakuja kurejesha thamani ya fedha ya nchi hii! Maana tusipokuwa makini tutaendelea kuongeza tu 0 kwenye fedha zilizopo sasa! Badala ya kuzipunguza hizo 0.
 
uchumi sio hinna.

mtu anaongeza mshahara elfu 60 halafu anaongeza gharama za maisha kwa kupandisha bei bidhaa muhimu,nauli.
kinachotokea ni elfu 10 kuwa na kazi ya jero.
 
Duh kinachonisikitisha ni kuwa kati hizo noti za 10,000 za thamani ya tr 6 mimi binafsi ninazo 10 tu!
 
Back
Top Bottom