BoT, je kuna uwezekano wa kuongeza quality za noti zetu ili kupunguza gharama za kuchapisha mara kwa mara?

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,309
4,017
Leo nimepokea huu ujumbe kutoka benki kuu.

"Ewe Mwananchi Benki kuu ya Tanzania inakukumbusha kutunza vyema Noti na Sarafu zetu ili taifa lisipate gharama kuchapisha fedha kila mara kufidia uharibifu"

IPi ni nafuu zaidi? waongeze ubora ili kuchelewa kuchakaa kwa noti zetu au quality iendelee hivi hivi na kuwapa watu elimu za kumaintain noti zisichakae sana?
 
hilo ni Jambo Muhimu sana, hata hivyo noti za Tanzania ni imara zaidi, ile muhimu hapo inasisitizwa ni heshima, usafi na unadhifu unapoishika na kuihifadhi noti ili kutunza ubora na thamani yake 🐒

sio umekamata grisi unashika noti unaitia mfukoni imejikunja kunja, umelowana mafuta au maji unashika noti unaitia mfukoni imekunjamana n.k
 
Ulaji utatoka wapi wakiongeza ubora wa noti? Noti hizi zina ubora duni ili kutengeneza madili ya mara kwa mara ya kuchapisha noti mpya. Wanapochapisha Noti mpya hapo hapo ndipo wanapata nafasi ya kuchapisha noti kwa idadi ya ziada na Kisha hizo noti za ziada zinachepushwa na kuzichukua wao binafsi na kuziweka mifukoni mwao. Hukusikia ile skendo ya kutoroshwa bandarini kwa makontena manne yaliyobeba noti mpya zilizochapishwa huko Ulaya na Kisha kusafirishwa hadi bandari ya Monrovia kule nchini Liberia?
 
hilo ni Jambo Muhimu sana,
hata hivyo noti za Tanzania ni imara zaidi, ile muhimu hapo inasisitizwa ni heshima, usafi na unadhifu unapoishika na kuihifadhi noti ili kutunza ubora na thamani yake 🐒

sio umekamata grisi unashika noti unaitia mfukoni imejikunja kunja, umelowana mafuta au maji unashika noti unaitia mfukoni imekunjamana n.k
Kweli kabisa
 
Ulaji utatoka wapi wakiongeza ubora wa noti ??? Noti hizi zina ubora duni ili kutengeneza madili ya mara kwa mara ya kuchapisha noti mpya. Wanapochapisha Noti mpya hapo hapo ndipo wanapata nafasi ya kuchapisha noti kwa idadi ya ziada na Kisha hizo noti za ziada zinachepushwa na kuzichukua wao binafsi na kuziweka mifukoni mwao. Hukusikia ile skendo ya kutoroshwa bandarini kwa makontena manne yaliyobeba noti mpya zilizochapishwa huko Ulaya na Kisha kusafirishwa hadi bandari ya Monrovia kule nchini Liberia??
Aiseee
 
Elimu itolewe namna ya kutunza hizi fedha,,,, nyengine unazikuta zimeandikwa kabisa na peni

Hapo Bado watu wa mkaa hawaja zishika
 
Wanaoongoza kuchakaza noti ni wamama wa mboga wanafunga kwenye mafundo ya kanga


Ila makonda wapewe heshima yao kwa kuzinyoosha na kuweka kwenye kuzipanga vizuri
 
Back
Top Bottom