B.O.T fedha za sarafu ziko kwenye ma kamali ya wachina

madindigwa

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
2,453
2,849
Wakati wananchi tukihangaika uhaba wa fedha za sarafu hasa sisi wafanya biashra wadogo wadogo na wajasiriamali BOT wanakuja na sera eti wananchi wameweka sarafu kwenye vibubu

Kwa utafiti gani mlio fanya wakati sarafu zote wanazo wachina wameziweka kwenye mamashine yao ya kamali kila kwenye kona ya nchi
Kila kitongoji vijiji yameenea haya ma mashine ukila 1000 ya sarafu huondoki na sarafu unapewa noti haya hiyo sarafu inapatikanaje mtaaani
Yani mtu na usomi wake anahojiwa azam tv anasema watu waache kuweka pesa kwenye vibubu kwa utafiti gani mlio ufanya.

Katoeni mshine za kamari zinazo waharibu vijana wa taifa hili na hizo ndizo zinatengeneza majambazi wajao wa nchi hii kamali ni janga la taifa kama serekali hamta litazama hili kwa jicho la tatu kisa tu inachangia pato la taifa tutarajie majibu chanya baada ya muda mfupi sana
B.O.T sarafu yenu anayo mchina
 
Maswali muhimu.

1. Fedha hizi zinatengenezwa kwa madini gani?

2. Madini hayo kwa sasa yanauzwa kwa bei gani? Bei yake inategemewa kupanda vipi?

3. Je, inawezekana kuna watu wameona fedha za Tanzania yale madini yake yanaenda kuwa na thamani kuliko ile thamani ya nominal na hivyo kuanza kuzikusanya hizi fedha za sarafu na kuwapa watu fedha za noti ili wazichukue zile sarafu na kuuza kama madini?

Najiuliza maswali haya kuangalia sababu kwa nini fedha za sarafu zishikiliwe hivyo.
 
Nakubaliana kamari ikiwa ulevi wa vijana hatutakua na taifa la wazalishaji ila wacheza kamari tu.
 
Maswali muhimu.

1. Fedha hizi zinatengenezwa kwa madini gani?

2. Madini hayo kwa sasa yanauzwa kwa bei gani? Bei yake inategemewa kupanda vipi?

3. Je, inawezekana kuna watu wameona fedha za Tanzania yale madini yake yanaenda kuwa na thamani kuliko ile thamani ya nominal na hivyo kuanza kuzikusanya hizi fedha za sarafu na kuwapa watu fedha za noti iki wazichukue zile sarafu na kuuza kama madini?

Najiuliza maswali haya kuangalia sababu kwa nini fedha za sarafu zishikikiwe hivyo.

Vitu vya msingi sana mkuu
 
Wahuni Wamejaa Sana Serikalini Hao Wachina Ndiyo Tatizo Kubwa
Mashine Za Kamari Zimejaa Mpaka Vijijini Ndani Ndani Yaani Meatu Huko Mwanhuzi, Mpeta Huko Kigoma, Zamahelo Huko Dodoma

Sarafu Zote Zinashikiliwa Na Wachina
Cha Kufanya Zuieni Mashine Za Kamari Zote Zinazotumia Sarafu Za 50,100,200,500
Kuna Ule Mwaka Wajina Walikamatwa Morogoro Wakiwa Wa Sarafu Zenye Thamani Kubwa Mno Mpaka Zinakatikisa Mzunguuko Wa BOT Upande Wa Sarafu

WALIPOFUATILIA Wakakuta Wanatunza Ndani Kwenye Machupa Makubwa Ya Maji Safi
Millions Of Coins
 
Mashine zimesambaa Tanzania nzima harafu kila mashine ina chele chele za kutosha niliwahi kwenda sehemu niliona wakiweza mzigo wa hizo chele chele utadhani sio fedha ni nyingi mno harafu jamaa wana mchongo wa kuzipata mpya kabisa kutoka Bank ambazo hata kwenye mzunguko haziingii wanachukua wao ishu ya Kibubu ni ya Uongo kabisa...
 
Maswali muhimu.

1. Fedha hizi zinatengenezwa kwa madini gani?

2. Madini hayo kwa sasa yanauzwa kwa bei gani? Bei yake inategemewa kupanda vipi?

3. Je, inawezekana kuna watu wameona fedha za Tanzania yale madini yake yanaenda kuwa na thamani kuliko ile thamani ya nominal na hivyo kuanza kuzikusanya hizi fedha za sarafu na kuwapa watu fedha za noti ili wazichukue zile sarafu na kuuza kama madini?

Najiuliza maswali haya kuangalia sababu kwa nini fedha za sarafu zishikiliwe hivyo.
Hizo fedha zipo kwenye madubu ya Wachina na kwenye vyumba vyao. Huwezi amini unaweza kukuta Wachina na wanakaa na mpaka milioni kumi cha vichele ndani. Wachina hawapeleki hela benki bali wanakaa nazo ndani, na wengine wanalindwa na polisi wenye bunduki kabisa, hivyo hawaoni haja ya kupeleka hela za vichere benki ili wapewe za noti.
 
Back
Top Bottom