Sababu Za Kupinga Utengenezaji Wa Coin Ya Tsh 500 Nchi Tanzania Sasa

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,337
Wadau tuangalie hizi sababu za kupinga sh 500 ya note kutobadilishwa to coins, kutoka kwa wataalamu wa uchumi nimeona tuichambue kidogo.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
BOT kufuta noti ya Sh.500/= na kuifanya sarafu. Huu ni wendawazimu mkubwa katika sekta ya uchumi "the most unpleasant economic decision" kwa sababu zifuatazo;

MOSI; fedha yoyote inapobadilishwa kuwa sarafu kutoka shillingi ni kuishusha thamani. Hii ni kwa sababu kiuchumi inabadilika matumizi na kuanza kutumika zaidi ktk sekta ya uchumi mdogo km wa wauza njugu mtaani, mama lishe, na maeneo mengine yasiyozalisha sana kiuchumi (less productive sector).

Maeneo yenye uzalishaji mkubwa (lead productive sector) yatashindwa kuitumia fedha hii kwa kuwa tu ni ya sarafu. Kw mfano kuanzia sasa haitakua rahisi kukuta sarafu hizi za 500/= maeneo kama Airport, Migodini au Supermarket.

Hiki ni kiashiria cha kushuka kwa thamani kwa fedha hiyo. (Indicator for currency devaluation).

Hivi hatujiulizi kwanini Marekani hadi dollar moja ni ya noti sisi 500/= tunaweka sarafu?? Dollar moja ina single digit lakini ipo kwenye noti, sisi tunalazimisha kuweka 500 kwny sarafu wakati ina tripple digit. Tunaforce Galloping inflation.

PILI; unapotengeneza sarafu ya pesa kubwa ina maana sarafu zinapotea na kujiondoa ktk mzunguko wa fedha. So tutegemee siku si nyingi sarafu za sh.100/= na sh 200/= hazitakuwepo tena mtaani.

Ikifikia hatua hii ujue nchi imeanza kuyumba kiuchumi na mfumko wa bei umevuka kiwango cha kawaida (extention from Moderate inflation to Galloping inflation).

Wenzetu Kenya hadi sarafu ya sh.10 inatumika. Ukienda Nairobi, Mombasa au maeneo mengine ya Kenya utata watoto wakinunua madafu, ice cream au matunda kwa sh.10.

Hapa kwetu sarafu ya sh.10 ilikufa na Nyerere. Ya sh.5 ikaenda na Sokoine. Ya sh.20 na 50 zimemfuata Kawawa. Sasa benki kuu wanalazimisha sarafu ya sh.100 na ya sh.200 zikamfuate Karume mahali pema peponi. Noti ya sh.1,000/= nayo inakaribia kwenda ahera maana BOT wameleta sarafu ya sh.1,500/=.

TATU; BOT kuwa wametoa hoja mufilisi kuwa wamefuta noti ya Sh.500/= na kuireplace kwa sarafu baada ya kugundua noti hiyo inachakaa haraka sn na inadumu kwa muda mfupi mno kwenye mzunguko.

Hoja hii ni mufilisi kwa sababu solution ya noti kuchakaa mapema si kureplace sarafu bali ni kuimarisha noti hiyo kwa kuitengeneza kwa material imara zaidi.

Hivi noti ya 10,000/= nayo ikichakaa mapema BOT wataleta sarafu instead?? Huu ni wendawazimu.

Mojawapo ya sifa za fedha imara ni uwezo wa kukaa kwny mzunguko muda mrefu (durability). Sasa fedha inapopoteza durability dawa sio kubadili muundo wake (changing of currency format is not a solution for impermanency)

Lakini hata hivyo BOT wameonesha hawakufanya utafiti wa kina kabla ya kuleta sarafu ya 500/=. Wanasema zinachakaa haraka ukilinganisha na noti nyingine. Hii ni hoja dhaifu sana kutolewa na mtu anayejiita Profesa wa uchumi Benno Ndullu.

Yani Profesa Ndulu anataka noti ya 500/= na ya 10,000/= zidumu kwenye mzunguko kwa muda sawa?? Yani 10,000/= ikidumu miaka miwili, 500/= nayo idumu miaka miwili. Bila shaka hapo ndo ataona noti ya 500/= haichakai haraka.

Hii ni "akili ndogo kujaribu kutawala akili kubwa". Noti ya 500 haiwezi kulinganishwa na noti nyingine kwenye mzunguko kwa sababu ina frequent circulation. Yani ktk uchumi noti yenye thamani ndogo huwa inazunguka zaidi kuliko ya thamani kubwa.

Hivyo noti ya 500/= inaweza kupita kwenye mikono ya watu 2000 ndani ya mwezi mmoja wakati ile ya 10,000/= imepita kwenye mikono 20 tu kwa mwezi.

Hii ni kwa sababu mzunguko wa noti hizi hutegemea matumizi. Ya 500/= itazunguka kwny daladala, wauza magazeti, vijiwe vya kahawa etc, wakati ile ya 10,000/= itazunguka Supermarket, Airport, hoteli kubwakubwa etc.

Hivyo ni dhahiri kuwa noti ya 500/= itaanza kuchakaa mapema kuliko noti. 10,000/= au ya 5,000/= au noti nyinhine kubwa. Sasa cha ajabu Profesa Beno Ndulu hajui hili na badala yake ameona solution ni kuleta sarafu. Aibu gani hii kwa mtu anayejiita Profesa wa uchumi kushindwa kujua vitu common km hivi ambavyo hata muuza machungwa wa Keko anavijua??

Mama lishe wa Tandale "kwa tumbo" anajua kuwa noti ya 500/= inachakaa haraka kuliko ya 10,000/= kwa sababu ina mzunguko mkubwa. Yeye anaweza kushika noti za 500/= hata mia kwa siku kwenye mauzo yake lakini asione hata noti moja ya 10,000/=.

Cha ajabu Profesa Ndulu hajui hili. Yeye amekerwa na noti ya 500/= kuchakaa haraka na ameona dawa ni kueeplace sarafu.

Naumia kuiona Tanzania ikiangamizwa na watu tuliowaamini, tuliowaheshimu, tukawapa madaraka, kwa kuamini ni wasomi watatusaidia. So sad, uchumi wa Tanzania ulale mahali pema peponi..!!

NNE. ........
 
nashukulu mtoa mada kwa uchambuzi wako yakinifu, ila kwa hili Tanzania tumekurupuka kwa kuwa sio pekee devaluation ya sarafu ya shiringi mia na mia mbili hata noti ya elfu moja itashuka thamani
 
Mkuu frema120! Bado una imani na maprof.Wa Tanzania? Ni bora hata Maji Marefu kuliko hawa akina Benno na mwenzake Nkhoma wa TCRA! Hivi hakuna materials ambayo yanaweza kutumiwa kutengeneza noti imara?
 
nashukulu mtoa mada kwa uchambuzi wako yakinifu, ila kwa hili Tanzania tumekurupuka kwa kuwa sio pekee devaluation ya sarafu ya shiringi mia na mia mbili hata noti ya elfu moja itashuka thamani

Inauma sanaaa, tunaalibu sana uchumi wetu now $ ina panda yet chin kweli ni sh 1680.
 
Mkuu frema120! Bado una imani na maprof.Wa Tanzania? Ni bora hata Maji Marefu kuliko hawa akina Benno na mwenzake Nkhoma wa TCRA! Hivi hakuna materials ambayo yanaweza kutumiwa kutengeneza noti imara?
Nishida sana kwa Prof Nkoma simlaumu sana coz sector yake ina vitu vingi nje na professional yake.

Sasa kwa Prof Ndullu ni ujinga sana kwa kufikila ki analogy wakat dunia sasa ni Digital... na shida BOT kuna makada wa chama wenye experience wasio na knowledge ya ki Digital ndio washauri wake.

Kikubwa ni kuwa na mfumo mpya wa kuongeza nchi hii basi.
 
Kuna viongozi wa hii nchi wangekua baba zangu walahi ningempiga hata kibao 1 siku 1 aisee! Dah!
Yani hii mijitu unaweza dhani sio waTanzania!
 
Tutapiga kelele zote lakini msingi wa hoja hapa ni mfumuko wa bei (inflation). Hili ndiyo tatizo la msingi katika haya tunayoyaona ya kubadili "notes" kuwa "coins".

Mimi ningeomba nitoe maoni yangu kuwa kubadili "notes" kuwa "coins" kwa "small denomination notes" ni jambo zuri na msingi kwa ukuaji wa Taifa. Na msingi wa kauli hii inafuata sababu ileile iliyotolewa na BoT, kuwa "small denomination notes" huwa zinachakaa haraka. Kwa sababu hii, umuhimu wa "coins" unajitokeza sana kwa kuwa zinapunguza gharama. Kwa hili sitaeleza sana, kama tuna muda tunaweza ipitia pepa ya Klein (2013) inaitwa "Time for Change: Modernizing to the dollar coin saves taxpayers billions", ambayo hata kwa kugoogle inapatikana.

Shida tunayoipata akina sisi (Tanzania) hatuumizi akili kutibu katika mizizi ya tatizo, tunaangalia suluhu ya harakaharaka. Kinachotutokea sisi, mfumuko wa bei unaziua zile "small denominations" kama senti, shilingi moja, tano, kumi, ishirini, hamsini nk. kwa kuzitoa katika matumizi. Kwa mtindo huu "higher denominations" kama shilingi mia, mia mbili, tano nk zinaanza kuonekana zikichakaa haraka. Hapa ndipo BoT wanapopaona kuwa kuna tatizo. Kwao ufumbuzi ni kubadili "notes' kuwa "coins", na sio kuweka mikakati ya kushusha kwa kasi mfumuko wa bei.

Kwa wenzetu walioendelea kama USA, Canada, England na nchi nyingine za Ulaya, hili la kubadili "notes" kwenda "coins" walikwishafanya. Kwa kumbukumbu za harakaharaka, USA wamefanya hivi mara tatu (1970s, 1990s na 2005) kwa kutumia President Coin Act. Lakini hawa wenzetu hawabadili "notes" kwenda "coins" kwa msukumo wa mfumuko wa bei, ila ni katika harakati za kuokoa gharama za kuzitumikia "small denomination notes" ambazo huwa zinachakaa mapema. Hii ndiyo tofauti ya wao na sisi (wale wenzetu wanatumia neno sie).

Hivyo basi, kwa sasa hiki walichofanya BoT ni sahihi ili kuokoa gharama ya kuitumikia 500 ambayo sasa inachakaa mapema kwa kuwa ndiyo "small denomination note". Lakini, kama wale wachumi wetu wanafanya kazi, sasa ndiyo muda wao kuhakikisha mfumuko wa bei unashuka ili matumizi ya hela ndogo kuliko 500 yawepo.
Wasiwasi wangu ni kuwa, wataalamu wetu wameshindwa kuushusha mfumuko wa bei kiuhalisia. Wiki iliyopita nilisikia wakidai mwezi huu umeshuka. Lakini ni nani mwenye udhubutu wa kutaja maeneo yanayoakisi kushuka huko?!!! "Figures" tunazotajiwa za kushuka kwa mfumuko wa bei binafsi naona ni kiini macho (Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo)...
 
Biafsi naona tatizo ni mfumuko wa bei,ambao umekuwepo hapa nchini kwa kipindi kirefu,naamini takwimu zinazotolewa na vyombo husika kama B.0.Tna NBS Huwa si realistic ni kama viini macho kuepusha madhara ya kisiasa.kutokana na kutokuwa na wafatiliaji wa taarifa hz na vyombo vilivyo huru vya kuratibu haya mambo si rahisi kufahamu ukweli uliopo,huu ubadilishaji wa hii noti kwenda coin ni uthibitisho tosha.
In fact b.o.t wpo sahihi kufanya hv,ili kupunguza gharama za kuprnt note ya mia 5 ambayo ndo ipo kwa wng ktk mzunguko ila isiwe ndo long run solution.
The only soln 4 this problem is to produce more and reduce importation.while encourage the flow of foreigh inflow+ capital inflow.
 
Tutapiga kelele zote lakini msingi wa hoja hapa ni mfumuko wa bei (inflation). Hili ndiyo tatizo la msingi katika haya tunayoyaona ya kubadili "notes" kuwa "coins".

Mimi ningeomba nitoe maoni yangu kuwa kubadili "notes" kuwa "coins" kwa "small denomination notes" ni jambo zuri na msingi kwa ukuaji wa Taifa. Na msingi wa kauli hii inafuata sababu ileile iliyotolewa na BoT, kuwa "small denomination notes" huwa zinachakaa haraka. Kwa sababu hii, umuhimu wa "coins" unajitokeza sana kwa kuwa zinapunguza gharama. Kwa hili sitaeleza sana, kama tuna muda tunaweza ipitia pepa ya Klein (2013) inaitwa "Time for Change: Modernizing to the dollar coin saves taxpayers billions", ambayo hata kwa kugoogle inapatikana.

Shida tunayoipata akina sisi (Tanzania) hatuumizi akili kutibu katika mizizi ya tatizo, tunaangalia suluhu ya harakaharaka. Kinachotutokea sisi, mfumuko wa bei unaziua zile "small denominations" kama senti, shilingi moja, tano, kumi, ishirini, hamsini nk. kwa kuzitoa katika matumizi. Kwa mtindo huu "higher denominations" kama shilingi mia, mia mbili, tano nk zinaanza kuonekana zikichakaa haraka. Hapa ndipo BoT wanapopaona kuwa kuna tatizo. Kwao ufumbuzi ni kubadili "notes' kuwa "coins", na sio kuweka mikakati ya kushusha kwa kasi mfumuko wa bei.

Kwa wenzetu walioendelea kama USA, Canada, England na nchi nyingine za Ulaya, hili la kubadili "notes" kwenda "coins" walikwishafanya. Kwa kumbukumbu za harakaharaka, USA wamefanya hivi mara tatu (1970s, 1990s na 2005) kwa kutumia President Coin Act. Lakini hawa wenzetu hawabadili "notes" kwenda "coins" kwa msukumo wa mfumuko wa bei, ila ni katika harakati za kuokoa gharama za kuzitumikia "small denomination notes" ambazo huwa zinachakaa mapema. Hii ndiyo tofauti ya wao na sisi (wale wenzetu wanatumia neno sie).

Hivyo basi, kwa sasa hiki walichofanya BoT ni sahihi ili kuokoa gharama ya kuitumikia 500 ambayo sasa inachakaa mapema kwa kuwa ndiyo "small denomination note". Lakini, kama wale wachumi wetu wanafanya kazi, sasa ndiyo muda wao kuhakikisha mfumuko wa bei unashuka ili matumizi ya hela ndogo kuliko 500 yawepo.
Wasiwasi wangu ni kuwa, wataalamu wetu wameshindwa kuushusha mfumuko wa bei kiuhalisia. Wiki iliyopita nilisikia wakidai mwezi huu umeshuka. Lakini ni nani mwenye udhubutu wa kutaja maeneo yanayoakisi kushuka huko?!!! "Figures" tunazotajiwa za kushuka kwa mfumuko wa bei binafsi naona ni kiini macho (Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo)...

Sikubaliani na wewe na wakat mwingine nakubaliana na wewe kiasi.

Nilishasoma pepa ya Klein (2013) Time for Change. lakin kwa hili la kwetu wachumi wetu wamekurupuka sana.

Hivi sisi tunatumia mfumo gani wa uchumi? (ukijibu nitaendelea mkuu).
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom