Ramani Ya Helligoland Treaty: Ziwa Nyasa Lote Liko Malawi

Ni ukweli mchungu sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Ziwa lote ni la Wamalawi. Watanzania hatutaki vita wala ugomvi na majirani zetu, kama tuna hoja tuwahi mahakamani sheria ichukue mkondo wake.
Nimeipenda hii, that is to say Ziwa Nyasa lote lipo Malawi, Bandari ya Mombasa ipo Tanganyika, Milima Kilimanjaro upo Kenya na Hakuna nchi za Rwanda wala Burundi, that is History. Nadhani inabidi Kagame ajiandae kuachia nchi ama tutalazimika kuingia vitani tu tena si na nchi ya Malawi kama inavyodhaniwa bali East Africa against wavamizi wa mipaka baada ya kuangushwa utawala wa mjerumani.
 
Ni ukweli mchungu sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Ziwa lote ni la Wamalawi.

Watanzania hatutaki vita wala ugomvi na majirani zetu, kama tuna hoja tuwahi mahakamani sheria ichukue mkondo wake.
Mbona husemi kuhusu Rwanda na Burundi? Kwa mujibu wa mkataba huo wa Wazungu hata nchi hizo ni sehemu ya Tanganyika na inabidi sasa twende Mahakama ya Kimataifa kudai hizo nchi za Rwanda na Burundi zirejeshwe kwetu, tuone kama litakubalika au kufumbiwa macho na hao Wazungu.

Ikumbukwe pia, hao Wazungu hawakuwashirikisha Wazawa wakati wanalitoa Ziwa Nyasa lote kwa Malawi, kwa hiyo siuoni mantiki ya kuheshimu huo Mkataba kanma upo maana hakukuwa na Bunge letu wenyewe wala Serikali yetu wenyewe, huo mkataba haukuingiwa na Serikali ya Tanganyika bali baina ya Ujerumani na Uingereza.

Tusipoangalia na kukaaa kama Waafrika kwenye haya masula ya mipaka, tutauana. Wala sioni mantiki ya huo mpaka kupita nnje ya Tanzania, Je, eneo huru litakuwa wapi?
 
Umechora mwenyewe halafu ndo unatuletea hapa
ivi ramani ndio inakuaga ivi ??? ... mbona haina kichwa wala miguuu....nani kachora hii ...he/she must be STD 3
Cha msingi ni kuthibitisha hiyo ramani illichorwa mwaka gani. Haijalishi nani alichora.

Kama zitapatikana ramani tatu zilizochorwa na watu tofauti kwa mwaka huo huo, je hauwezi kuwa ni ushahidi na hasa kama zinalingana?

Tunachobishania nini hasa? Huo mchoro usiokua na authority yoyote wala signatures?
Mkuu, artifacts don't mean anything to you, I guess
 
Nilishawahi sema hapo nyuma kwamba hilo ziwa Mjerumani hakuwa na interest nalo. Mjerumani alikuwa na meli moja tu humo kwenye ziwa Nyasa wakati Mreno alikuwa na mbili halafu Mwingereza kumi na tisa! Na hiyo meli moja ya Mjerumani ilikuwa ni gunboat. Halafu pia Uingereza ilikuwa na kampuni inaitwa Great Lakes Corporation ambayo ilijikita kwenye usafirishaji humo ziwani

Na hata kama itatokea Heligoland ikawa na utata kuna makubaliano mengine yalifanyika baada ya tume inayoitwa Joint Boundary Commission kuhakiki mpaka unaozigawa Zambia, Malawi na Tanzania mwaka 1898 ziwa lote ilipewa Malawi. Ujerumani iliridhia makubaliano hayo mwaka 1901
 
..ramani inaonyesha Rwanda na Burundi ni eneo la Tanganyika.

..pia ramani inaelekeza kwamba Msumbiji nayo haina haki na maji/eneo la ziwa Nyasa.

..mwisho, ramani haionyeshi jinsi Tanganyika, Kenya, na Uganda, zinavyo-share ziwa Victoria.

..je, ina maana na sisi tuanze kudai Rwanda na Burundi ziwe ni mikoa ya Tanganyika??
na kadri ziwa litakavyokuwa likihama na kula ardhi ya tz ndivyo mpaka utavyokuwa au kinyume chake kwamba kadri ziwa litakavyonyauka ndivyo nasi tutakavyotanuka kimpaka? kazi ipo!
 
Tumekabidhiwa nchi mwaka 1961 na Waingereza. Mipaka ilikuwa katikati ya Ziwa Nyasa. Kurudi nyuma mpaka 1890 ni kupotezeana muda kwani kabla ya 1884 hatukuwa na mipaka ya kinchi Afrika bali mipaka ya koo za makabila mbalimbali au unataka turudi huko?

Mpaka unapita katikati ya ziwa Nyasa hakuna zaidi ya hapo!
 
attachment.php


Msije mkasema mimi ninakinyongo na msimamo wa serikali. Nimeona ramani hii inayoonyesha mipaka ya ziwa nyasa. Sasa nashindwa kujua ugumu unatokea wapi wakati kumbe mambo yako wazi kabisa.

Imetoka blog ya Mjengwa
"Marker pen" gani hiyo isiyopauka toka 1885? Serikali gani inayoweka record ya kitu muhimu kama hicho kwa kuchora sketch mbovu kama hiyo bhana...Hata kwenye stationery yangu naweza kuchora sketch kama hiyo..
 
Wewe una uhakika gani na ramani hii? So wote tuanze kurejea nyuma kila mmoja asitambue mipaka katika kipindi fulani unafikiri itakuwaje? Hawa wa malawi hawna jipya, ni uroho wa kumiliki tu unawasumbua
 
"Marker pen" gani hiyo isiyopauka toka 1885? Serikali gani inayoweka record ya kitu muhimu kama hicho kwa kuchora sketch mbovu kama hiyo bhana...Hata kwenye stationery yangu naweza kuchora sketch kama hiyo..

umemena mkuu
 
Juzi mwanangu kachora ramani yake, ziwa lote letu.
Mimi mwanangu kachora leo tena na Kompyuta achana na hiyo takataka ya Manila sheet, yaani Kenya na Uganda zote zipo Tanzania.
Hivi ninavyoandika nina mpango wa kwenda kununua shamba Nairobi, nikitoka hapo nikanunue shamba la ndizi Uganda nianze kulisha Bunge la East Africa.
 
Nimeipenda hii, that is to say Ziwa Nyasa lote lipo Malawi, Bandari ya Mombasa ipo Tanganyika, Milima Kilimanjaro upo Kenya na Hakuna nchi za Rwanda wala Burundi, that is History. Nadhani inabidi Kagame ajiandae kuachia nchi ama tutalazimika kuingia vitani tu tena si na nchi ya Malawi kama inavyodhaniwa bali East Africa against wavamizi wa mipaka baada ya kuangushwa utawala wa mjerumani.
Kagame ajiandae kuwa mkuu wa mkoa wa Rwanda.
 
Hakuna kitu kama hicho hapo ni pasu kwa pasu kwani wao ndo walileta hilo ziwa lingekuwa ndai ya nchi yao sawa lakini mpakani kudadeki hatuachi kitu 50/50
 
Kwa swala hili la ziwa Nyasa, Ufumbuzi wake ni rahisi na utapatikana kwa amani.
Tanzania ni nchi huru na yenye maamuzi, na kwa upande wa Malawi pia ni sawa
na Tanzania. Kilichokuwepo ni kurudisha maisha ya matumizi ya ziwa nyasa, yali-
yokuwepo kabla ya weupe kuja kutuvuruga. Sasa hapa tupo katika kuyapinga
maamuzi ya mjerumani, Mwingereza na Mreno. Wao walikaa Ulaya na kuchora
ramani, na kujigawia ardhi wanavyotaka wao, bila kumshirikisha hata mwafrika
mmoja katika majadiliano na maamuzi. Kwani Afrika tulikuwa na utawala wetu wa
Machifu, na basi kama angeshirikishwa hata chifu mmoja kutoka kyela. basi hali
ya mpaka wa ziwa nyasa ingekuwa na mpaka wa katikati ya maji tokea wakati huo.
Sasa Tanzania na Malawi tuseme kuwa ramani hiyo iliyowekwa ni batili, na kama
mataifa huru tuandae ramani mpya ya mpaka wa Ziwa Nyasa. Na kufuta ramani
ya ziwa nyasa ya zamani. Hayo yote yapo katika uwezekano mezani,bila ugomvi.
 
Back
Top Bottom