S V Surovikin
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 13,625
- 32,751
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Iko hivi, kipindi kulivyoibuka vita ya maneno kati yetu na Malawi niliangalia mpaka wetu na Malawi kupitia picha za satellite nikaona mpaka huo umepita katikati ya ziwa Nyasa.
Siku chache mbeleni nikaangalia tena nikaona mpaka upo pale pale lakini sehemu hiyo/mpaka huo ukiwa umebadilishwa rangi kuwa nyekundu.
Kuchorwa mpaka huo kwa rangi nyekundu ni kuashiria kuna mzozo ambao umoja wa mataifa haujaelewa ni nani hasa mwenye haki na eneo hilo kati ya Tanzania na Malawi.
Tangu 2015 sikuwahi kuchungulia tena eneo hilo, ila leo nimeangalia mpaka huo kupitia camera za satellite nikashtuka baada ya kuona mpaka huo umehamishwa alafu wakabadili na jina la ziwa hilo na kuliita ziwa Malawi 😠
Yaani kwa kifupi lile ziwa hatuna mamlaka nalo tena! Tumeporwa kilomita nyingi sana za mraba huku serikali yetu ikiwa haijui kinachoendelea juu ya ziwa hilo lenye utajiri wa gesi, mafuta na spish za samaki zaidi ya 1500.
Mpaka huo umehamishwa kutoka katikati ya ziwa hadi kwenye fukwe za nchi yetu huku wakibadili kabisa jina la ziwa letu na kuliita ziwa Malawi kama inavyoonekana kwenye picha.
Linganisha na mpaka ambao tuliachiwa na wakoloni katika picha hii.
Ikumbukwe kwamba miaka michache kipindi cha serikali ya Jakaya kikwete tulikuwa na mzozo Malawi kuhusiana na hili ziwa hadi kukatokea vitisho vya kuingia vitani kila nchi ikidai italinda mpaka wake. Malawi wakidai ziwa lote ni lao huku Tanzania tukidai mpaka wa wakoloni ambao ulipita ndani ya ziwa huku sisi tukiwa na eneo lenye upana zaidi ya Malawi.
Hii maana yake nini? Sisi ni wapole sana au hatupo tayari kulinda mipaka yetu?
Kwanini wazungu wameridhia kumega nchi yetu na kuikabidhi Malawi?
Naomba serikali yetu tukufu itoe maelezo kuhusu hili jambo maana sio dogo.
Tukiendelea kunyamaza kuna siku watasema mkoa wa Mbeya ni wao