Rais Obama awakataza uhamiaji kurudisha 'young illegal immigrants'!...Wabeba maboksi wenzangu mpo?

Kwani tatizo liko wapi kama ni hela yangu? Si nalipa hoteli na hela yangu? Narudi tena December nafikia Sea Cliff. Nitafute nikupige bia moja mbili.

Inaonesha wewe ni wa Dodoma. Maana ungekuwa wa Kaskazini usingeyasema hayo.
 
Sasa unataka wajenge bongo wakati wao wanakaa Marekani si ni kupoteza hela huko? Kwani wameshaamua kurudi nyumbani? Wakiamua kurudi wanaweza kujenga au hata kununua nyumba iliyosha jengwa.

Duu...Nifikiri nawasiliana na mtu mwenye uelewa, kufikia Kempisky whatever fancy hotel wakati huna kitu kijiji/mjini cha kukuhifadhi wakikutimua uko unako ishi kusiko kihalali....ni deal safi sana.
 
Mkuu Buswelu

Watu wengi hapa naona wanapeana zile "story" za vijiweni......tena "gogovivu style"...........wengine walifika mamtoni kwa kuchomolewa nyumbani already wakiwa established.......sio wote walioko mamtoni basi akili yao imelala.......hata huko home bado kuna wenye vipato vizuri na maisha yao si stable.......kwa hiyo maendeleo ya mtu ni pamoja na akili ya kujua jinsi gani atakamilisha mambo/malengo muhimu maishani mwake.........iwe popote pale ulimwenguni.........

Kuna vijana wengi sana wanapenda kuja mamtoni....lakini ndio hivyo tena......story wanazopewa kuhusu huku.......ni kunyume na matarajio yao wakifika...........wacha watu tupige "Boksi".......kwani unapopiga boksi na kupata sense of satisfaction ya jasho lako na kuweza kutimiza mahitaji yako muhimu....what else do you want.........

Nilipokuwa Tanzania.......niliwahi kupigwa transfer kwenda to a very remote area i.e. vijijini ndani ndani kweli kweli huko........basi washkaji zangu ikawa story kwao........"daah mwenzetu wewe ndio basi tena umeshaumia/kwisha kazi"......cha ajabu nilipokuwa kule niliweza kufanya mambo MENGI sana ya maendeleo juu yangu na familia yangu.......i could not believe myself kufanya maendeleo yale kutokea kijijini kule (mind you sikupiga mishe mishe wala nini)........wenzangu walikuita kule "uswekeni"...........sasa wengine tupo mamtoni sasa bado mnaleta za kuleta.........

......acheni hizoo nyie........
 
Last edited by a moderator:
Duu...Nifikiri nawasiliana na mtu mwenye uelewa, kufikia Kempisky whatever fancy hotel wakati huna kitu kijiji/mjini cha kukuhifadhi wakikutimua uko unako ishi kusiko kihalali....ni deal safi sana.

Mkuu Buswelu

Pengine na wewe umekosa uelewa..........hakuna atakaye-dispute umuhimu wa maendeleo yake nyumbani yaani bongo.......however.........ukae pia uelewe.....watu tunatofautiana kuanzia akili hadi vipato..........akili za biashara/uwekezaji/matumizi vile vile......wewe unapoona uinue tofali....mwenzio anafikiri afanyie nini hiyo hela ya tofali ili impe other opportunities za kimaisha na kwenye investments zenye return.........hizi tabia za show offs.......zinatuua sana wabongo.......last time nilikuwa bongo.......nilishangaa kuona watu wakisifiana/kupongezana baada ya kununua magari ya kifahari (tena second hand) huku wakiomba pesa ya mafuta na hata wakti mwingine matengenezo/service.......

.......waacheni vijana wapewe hati/makaratsi za/ya makazi hapa US ili milango ya opportunities iwafungukie.......it will be good for them and their families huku ughaibuni na hata nyumbani pia..........
 
Last edited by a moderator:
Huu mpambano wa wapiga box na wala vumbi huwa unakuja na kuondoka. Hivi kama mtu ameamua yeye box ndo mkombozi wake wewe mwenzangu mimi tatizo lako nini?. kama wewe unakula bata bongo basi yote kheri, mwache huyu naye ale jasho lake la box huko alipo!.
 
Duu...Nifikiri nawasiliana na mtu mwenye uelewa, kufikia Kempisky whatever fancy hotel wakati huna kitu kijiji/mjini cha kukuhifadhi wakikutimua uko unako ishi kusiko kihalali....ni deal safi sana.

Siyo kila mtu anaweza kutimuliwa. Kuna watu wameshakuwa raia wa hizo nchi. Wanatembelea maganda mekundu na ya blu. Upo hapo?
 
Mkuu Ngongo.
Ukienda UK mpaka wanatia huruma kuna mji mmoja unaitwa Milton Keynes, utadhani upo Kariakoo...kuna kuna vijana wa Dar, Mwanza, Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Zanzibar..

Ritz
Wacha porojo hizo hivi unataka kusema balozi za UK na USA zikiweka milango wazi ya kutoa viza hamtakwenda? Ya UK siyajui lakini kama unataka kuona wabongo wanaishi kwa nafasi USA siku yeyote kama unapata nafasi ya kutembea USA sema watu wakuonyeshe wanavyoishi, maisha mahali popote tu kujenga nyumba bongo si hoja ni uamuzi wapo wabongo wengi tu wamejenga bongo kwa nafasi zao na isitoshe ni suala la kujenga ni uamuzi binafsi;

Isitoshe wengi wameshaamua retirement zao zitakuwa US sasa bongo wamjengea nani wakati tayari nyumba wanazo? Hizi njaa zenu zisiwanyime fikra; kukosa makaratasi hakumzuii mtu kumiliki nyumba pia labda kuna jambo hamlielewi wamarekani hawarudishi kama huna tatizo na sheria zao ipo mifano mingi ya wabongo waliokamatwa kwa makosa madogo tu barabarani ICE iliwaachia kaeni na porojo zenu kibongo hakuna mbongo homeless na alieshindwa na maisha kataka mwenyewe; USA maisha tambarare.

Vijana wengi wa kibongo ni wachapa kazi msitumie mifano ya wachache walioharibu
Ritz siku yeyote ukiwa USA nitumie simu yako kwenye PM nikuonyeshe watu wanavyoishi sio wewe yeyote yule mwenye wasiwasi na maisha ya USA.

All travelling expenses within US will be on my tab and I promise you will suprised to see how large wel live; It does not matter what we do to make our living only matter is how much we get paid; We have a very good number of Tanzanian professionals in US, our community expand everyday.

I was in Dar last April you don`t need to tell me a shit about life there; the system might be working fine for you but not for everybody; majority takes life on day by day basis; they don`t have a clue how tomorrow is gonna be, so if you call that life then fu2k the shit I will die in US because I know how I am gonna make it tomorrow

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
mimi sielewi kwanini mtanzania yuko UK or US alafu unasikia wanajihusisha na uhalifu mara wengine wameshafungwa...wanachezea tu maisha..warudi tanzania kuendeleza nchi yao na wajiendeleze wenyewe pia..mtabeba maboksi mpaka lini
 
ila hiii ipo kwaajili ya watu flani tu..ingewahusu wale ambao ni school dropouts ingesaidia watu wengi sana...ambao majority ya illegal immigrants waliacha shule na kuingia mitaani kutafuta maisha..
 
mimi sielewi kwanini mtanzania yuko UK or US alafu unasikia wanajihusisha na uhalifu mara wengine wameshafungwa...wanachezea tu maisha..warudi tanzania kuendeleza nchi yao na wajiendeleze wenyewe pia..mtabeba maboksi mpaka lini

Hamna jipya wengi wenu mlishakwenda ubalozini mkadunda mmebakia kulalama tu hao wanaomaliza vyuo hamjui watakwenda wapi kazi hamna, isitoshe hakuna cha ajabu wanachofanya watanzania wa USA, kizuri zaidi wanalindwa na sheria za kazi; niambie Kariakoo hakuna wabeba box? Hivi mbeba box wa kariakoo analindwa na sheria kazi?

Mbona wengi wanatumikishwa na wahindi mithili ya watumwa hilo mbona hamlisemi? Basi mngeanza na hao wabeba box wa Karikoo warudi makwao; sisi hatujashindwa maisha. Kwa taarifa yako watanzania wanaoshi nje wanafanya vizuri kimaisha na wanajenga taifa kihalali angalia takwimu za Western Union na Moneygram tunatuma kiasi gani kwa mwaka?

Wengi ni hasira za maisha tu na inaonekana shule hamkwenda hata kujenga hoja hamjui; nina mifano hai ya vijana chapa kazi wa kitanzania wanasomesha ndugu zao vyuo vikuu hapo bongo kwa hizo pesa za mabox; kama hoja ni uhalifu upo kila sehemu tena hapo bongo ndio umezidi. Mbona hamuawambii wamanyema waliojazana Dar warudi Kigoma? Maisha popote tu

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
mtanzania anakaa US or UK miaka 10 hana nyumba wala kiwanja..sana sana mnashindana kununua magari na kuvaa kukaa ulaya sio dili hayo mambo ya zamani. Mi nimeshakaa kote huko na nimerudi kujiendeleza na naweza kukwambia niko way better here than i ever was over there. Kuna baadhi ya watz sikatai huko nje wanakazi nzuri lakini unatumia maisha yako yote kuwachamba wazungu mavi au kubeba mapallet mtafanya hivyo mpaka lini.
 
mtanzania anakaa US or UK miaka 10 hana nyumba wala kiwanja..sana sana mnashindana kununua magari na kuvaa kukaa ulaya sio dili hayo mambo ya zamani. Mi nimeshakaa kote huko na nimerudi kujiendeleza na naweza kukwambia niko way better here than i ever was over there. Kuna baadhi ya watz sikatai huko nje wanakazi nzuri lakini unatumia maisha yako yote kuwachamba wazungu mavi au kubeba mapallet mtafanya hivyo mpaka lini.

Umeishiwa la kusema mambo ya kusikia kwenye vilinge vya kahawa; hapo Tanzania Breweries hakuna pallet? Muhimbili hakuna manesi? Hapo umetaja taaluma za kawaida sana; Usisahau wapo wabongo wengi tu waliopo huku wanafanya vizuri kuliko wewe; yupo jamaa yangu alidanganywa na ndugu zake arudi kila kitu kitakuwa safi nilimkuta hapo Dar anajuta la kufanya hana na kurudi US hawezi; Usitake kudanganya watu.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Hamna jipya wengi wenu mlishakwenda ubalozini mkadunda mmebakia kulalama tu hao wanaomaliza vyuo hamjui watakwenda wapi kazi hamna, isitoshe hakuna cha ajabu wanachofanya watanzania wa USA, kizuri zaidi wanalindwa na sheria za kazi; niambie Kariakoo hakuna wabeba box? Hivi mbeba box wa kariakoo analindwa na sheria kazi? Mbona wengi wanatumikishwa na wahindi mithili ya watumwa hilo mbona hamlisemi? Basi mngeanza na hao wabeba box wa Karikoo warudi makwao; sisi hatujashindwa maisha. Kwa taarifa yako watanzania wanaoshi nje wanafanya vizuri kimaisha na wanajenga taifa kihalali angalia takwimu za Western Union na Moneygram tunatuma kiasi gani kwa mwaka? Wengi ni hasira za maisha tu na inaonekana shule hamkwenda hata kujenga hoja hamjui; nina mifano hai ya vijana chapa kazi wa kitanzania wanasomesha ndugu zao vyuo vikuu hapo bongo kwa hizo pesa za mabox; kama hoja ni uhalifu upo kila sehemu tena hapo bongo ndio umezidi. Mbona hamuawambii wamanyema waliojazana Dar warudi Kigoma? Maisha popote tu

Chama
Gongo la Mboto DSM

Mkuu mbona unawaka hivyo!??
 
Back
Top Bottom