zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Mkuu Zomba hiyo ni kweli kabisa nina ndugu kakimbilia USA miaka 15 iliyopita karejea nyumba mwaka jana Dec na jeans akidhani ni kitu cha maana sana.Mbaya zaidi kakuta Ndugu,jamaa na marafiki wengi wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo.
Mwaka jana nilitembelea huko, nimeongea na baadhi ya Watanzania, niliowakuta kwenye hali nzuri ni wale ambao nawajuwa walienda kusoma na wakasoma kiukweli, lakini wale walioingia kutafuta maisha na wakawacha kusoma, nimewakuta hali ni mbaya sana, kuna mmoja au wawili nikawauliza kwanini hamrudi? mmoja akasema "aah kaka, nirudi hivi si aibu, baada ya miaka 15 sina hata nyumba nyumbani, bora nifie hukuhuku tu". Mwingine akanambia anataka kuvuka border aende akajaribu Canada maana hapo sasa kashindwa, huyu yupo US kwa miaka 8.
Kusema kweli wengi wanasikitisha. Kuna mmoja nilimkuta New York, huyu alikuwa wa kike na ana maisha mazuri kwa kwango cha wengine, nae hana kazi. Nikaambiwa kinachomsaidia ni kuwa aligunduliwa ana UKIMWI na ukiwa na hilo gonjwa huko Serikali inahakikisha hulisambazi kwa hiyo wanakuhudumia kwa kila kitu kuliko wale disables.