Rais Obama awakataza uhamiaji kurudisha 'young illegal immigrants'!...Wabeba maboksi wenzangu mpo?

Hao Watanzania wanaozamia huko ni Watumwa mambo leo. Nimewakuta wengi sana US na UK, wengi wao wana maisha ya taabu kuliko hapa nyumbani. Kinachowashinda kurudi mara nyingi huwa ni uoga wakuwa "failures" wameshindwa kimaisha Tanzania wakaona huko ndio watafanikiwa, kufika huko nako wameshindwa, kwani walifikiri maisha bora yanaletwa bila kufanya kazi.

Nnakuhakikishia anaefanikiwa Tanzania hata akienda huko pia atafanikiwa lakini anaeshindwa Tanzania hata aende wapi hatoweza. Tanzania kuna fursa nyingi sana kwa anaejituma.

Well spoken bro!!!
 
Hebu tuambie hizo fursa nyingi unazoziongelea; kwasababu kinachoendelea bongo ni ukosefu mkubwa wa ajira; miundo mbinu mibovu; mikopo mpaka utoe rushwa au ujuane na mtu; wengi tunajua maisha bora yanaletwa na kufanya kazi na ndio sababu tupo huku; kazi bongo hakuna wapo graduate wa chuo kikuu mwaka wa tatu huu tangu wamalize chuo kazi hakuna sasa utalaumu watu wakienda viwanja kutafuta maisha? Na lazima ufahamu mpaka watu wamekuja viwanja hivi jua fika hawana uoga wa maisha ni ujasiri mtupu haku hakuna kula kwa mjomba kulala kwa shangazi; mimi nadhani kama mnataka kuiletea maendeleo Tanzania mngeanza kwenda maeneo ya Kipunguni; Kariakoo, Manzese muwashauri warudi kijijini wakalime; pita asubuhi maeneo ya Magomeni uone watu walivyokata tamaa ya maisha wanatembea kwa mguu kuja Kariokoo kutafuta riziki ambayo hata uhakika nayo hawana; unajinasifu eti ulikuja kutembea porojo tu ndani ya JF aliyefika viwanja hivi anajua ukweli hakuna hata mmoja anayemshauri mtu arudi bongo; hizi hadithi za sungura sizitaki mbichi mtakufa nayo.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Kuwa mbali tu na kwenu kwa miaka 20 huna hata banda la kuku kwenu, wakati unapewa kula ya handout hiyo ni shida kubwa sana kama huelewi.

....wewe mtu kishakaa 20 yrs states, probability tayari ana familia yake,kazi etc na hapo ndio nyumbani, sasa hizo story za banda la kuku huko ili limsaidie nini tena? na watanzania wengi hawana hizo handout kama unavyosema
 
Mwaka jana nilitembelea huko, nimeongea na baadhi ya Watanzania, niliowakuta kwenye hali nzuri ni wale ambao nawajuwa walienda kusoma na wakasoma kiukweli, lakini wale walioingia kutafuta maisha na wakawacha kusoma, nimewakuta hali ni mbaya sana, kuna mmoja au wawili nikawauliza kwanini hamrudi? mmoja akasema "aah kaka, nirudi hivi si aibu, baada ya miaka 15 sina hata nyumba nyumbani, bora nifie hukuhuku tu". Mwingine akanambia anataka kuvuka border aende akajaribu Canada maana hapo sasa kashindwa, huyu yupo US kwa miaka 8.

Kusema kweli wengi wanasikitisha. Kuna mmoja nilimkuta New York, huyu alikuwa wa kike na ana maisha mazuri kwa kwango cha wengine, nae hana kazi. Nikaambiwa kinachomsaidia ni kuwa aligunduliwa ana UKIMWI na ukiwa na hilo gonjwa huko Serikali inahakikisha hulisambazi kwa hiyo wanakuhudumia kwa kila kitu kuliko wale disables.
Inaelekea maisha yako yamekunyookea kipindi cha kikwete ndio maana akisemwa povu linakutoka mwisho unakaribia mkuu zombi 2015 siyo mbali
 
mtanzania anakaa US or UK miaka 10 hana nyumba wala kiwanja..sana sana mnashindana kununua magari na kuvaa kukaa ulaya sio dili hayo mambo ya zamani. Mi nimeshakaa kote huko na nimerudi kujiendeleza na naweza kukwambia niko way better here than i ever was over there...
Nyie acheni kudanganya watu hapa......bongo hakuna jipya maisha ni magumu mabovu huduma mbovu kila kitu kibovu...hakuna proper system ya kuishi au kufanya kitu....kwa kifupi Tanzania watu wanaishi wakiwa hawajui kesho watafikaje...

tusidanganyane hapa wakuu...kama una maisha unaona poa majuu komaa huko huko haya mambo ya kujenga ya nini wakuu???? hujenge nini wakati unaishi majuu???? eti mnasema uwe na kitega uchumi??

Eeh kitega uchumi unacho majuu kwanza hapa bongo msilogwe kuwatumia ndigu zenu eti wawajengee au wawawekezee...mtalia aiseee......kuna msela alikuwa majuu alikuwa anamtumia dingi yake mapene amjengee nyumba...dingi kila wakati anaomba mkwanja aantumiwa akiulizwa nyumba imefuika wapi anamtyumia picha...

Kumbe hakuna nyumba wala nini.....pesa yote mdingi kala....picha alikuwa anatuma za watu.....mwingine mdogo wake alitumiwa pesa anunue daladala afanyie biashara matokeo yake akala na akapata UKIMWI.

maisha yapo majuu wakuu.....mlio majuu msirudi kaeni huko huko....kwanza dar nasikia maji hakuna wiki ya 6 now?? muulizeni @ New York karudi sasa anajuta.....
 
Bongo kwanza tengezeni uwanja mzuri wa golf nzuri ndiyo watu wafikirie kurudi.

Gymkhana haina hadhi kabisa. Jengeni mwengine wenye hadhi ya kimataifa. Halafu jengeni barabara kubwa. Haya mambo ya kutoka Mbezi mpaka mjini kuchukua saa nzima hayawezekani. Time is money.

Huwezi mtu kupoteza muda umesimama kwenye foleni. Halafu jengeni hospitali zenye hadhi nzuri. Siyo leo ukitaka kung'oa jino mpaka uende South Africa. Mpo hapo nyie wazalendo?
 
Kurudi nyumbani mikono mitupu sio nzuri utakuwa mgeni wa nani ahhhhhh ... Mkuu inauma hiyo... Roulette Umebadilisha jina lako la Rusian Roulette?

Mkuu MziziMkavu, unayosema ni kweli, lakini pia nadhani unakumbuka usemi unaosema kua "ikisha bidi imebidi". na ukweli ni kwamba hakuna mtu anaejua hatma yake. Wakati nilivokuwa kijana mdogo, niliona vijana wengi, wakizamia. Nyumbani ilikua kwenye kona. Unaweza amka asubuhi mara unasikia masela wanne wameondoka. Baada ya mwezi mara unamuona mmoja au wawili wamekaa kona, ukiuliza unaambiwa, ahh kurudishiwa msumbiji. Lakini hakuna dharau dhidi yao au kokolo yoyote. Ama kwa hakika, walionekana kama changamoto, hasa walipokua wakihadithia their misfortunes zilisababishwa kurudishwa. Masela wengine walikua wanajifunza wasirudie mistakes.
Na kwa upande mwingine, wale wanaofanikiwa kuzamia (dangerous journey) na kupata vibarua huko mtoni, kuna wakati walikua wanarudi nyumbani. Kuna waliokua wanarudi na mavazi mazuri na pesa kidogo. kuna wanaorudi na gari, nguo na pesa kidogo. na kuna walio rudi wakiwa na Mascania na kununua nyumba nzuri. Na kuna wale waliokua wakitumwa kusoma nje. hao walirudi bila vitu vingi vya fahari. Hawa wote walipokelewa na baadae kuchanganyika katika jamii.

Katika makundi yote nilio taja hapo juu, kundi lililo fanikiwa in a long run hapa nyumbani, ni la wale waliorudi bila magari wala vitu vingine vya kunyesha mafanikio yao. Kuna wakati binadamu tunatafuta kitu mbali kumbe kiko hapo karibu yetu. Kaka MziziMkavu, nadhani umekwisha wahi tafuta funguo kumbe zilikuepo jirani tu. Nafikiri na maisha ni hivo hivo, tusiogope kurudi nyumbani kwa kuogopa kukunyanyaswa. Huenda tunachotafuta tumekiacha kona.

Ningependa, atakae jaaliwa afanya hii quick study. (nimewahi kufanya hii na kaka yangu, tukatabasamu). Toka barabarani, halafu kadiria hesabu za nyumba zote mtaani. Kisha uliza, ngapi kati ya nyumba hizi wenye nazo wako ulaya au marekani au sauza? Ukipata jibu, utakuta nyumba nyingi ni za watu ambao wako hapo hapo,. Huku nje nadhani labda kuko over rated katika baadhi ya mambo.
Kitu kingine ningependa kurudia kuhusu wale waliorudiaga na Vitu vya thamani, baada ya muda wengi wao hupoteza mali walizorudinazo, mainly kutokana na bad management. Hawa tuwahurumie. Wamejidhili na kujitahidi kutunza fedha ili zikawasaidie nyumbani, lakini wengine huamini watu wajinga au wezi, wengine huingia biashara mbaya. Almuradi kuna njia nyingi za kupoteza fedha, hata huwezi laumu. Ukijaaliwa, soma kitabu kinachoitwa THE ALCHEMIST, by Pablo Coehlo. Kinahusu safari ya Bwana mdogo m'moja Mchunga Kondoo wa Andalusia jina lake Santiago ambaye Mara kwa mara alikua anaota kugundua hazina ya dhahabu huko Egypt (Misri)
 
Asingeitwa msanii kama alifanya mambo ambayo Watanzania wanastahili kujivunia. Asingechachamaliwa na Wabunge kufukuza Mawaziri wake kama Wabunge wa Magamba wangemuona ni Kiongozi anayetenda kazi zake.
Mkuu sidhani kama ni busara kubishana na kipofu kuhusu aina za rangi, inawezekana jamaa yupo kwenye neema tangu muheshimiwa alipoingia madarakani na ameridhika kuona watanzania walio wengi wanaishi katka mazingira magumu wakati hawakustahiri kuishi katika hali hiyo!
 
Nyie acheni kudanganya watu hapa......bongo hakuna jipya maisha ni magumu mabovu huduma mbovu kila kitu kibovu...hakuna proper system ya kuishi au kufanya kitu....kwa kifupi Tanzania watu wanaishi wakiwa hawajui kesho watafikaje...

tusidanganyane hapa wakuu...kama una maisha unaona poa majuu komaa huko huko haya mambo ya kujenga ya nini wakuu???? hujenge nini wakati unaishi majuu???? eti mnasema uwe na kitega uchumi??

Eeh kitega uchumi unacho majuu kwanza hapa bongo msilogwe kuwatumia ndigu zenu eti wawajengee au wawawekezee...mtalia aiseee......kuna msela alikuwa majuu alikuwa anamtumia dingi yake mapene amjengee nyumba...dingi kila wakati anaomba mkwanja aantumiwa akiulizwa nyumba imefuika wapi anamtyumia picha...

Kumbe hakuna nyumba wala nini.....pesa yote mdingi kala....picha alikuwa anatuma za watu.....mwingine mdogo wake alitumiwa pesa anunue daladala afanyie biashara matokeo yake akala na akapata UKIMWI.

maisha yapo majuu wakuu.....mlio majuu msirudi kaeni huko huko....kwanza dar nasikia maji hakuna wiki ya 6 now?? muulizeni @ New York karudi sasa anajuta.....

we usiwachuze wenzako...au unaogopa watu wakirudi kutoka marekani watachukua kazi zenu? haya bana wabeba maboksi naona wameungana wote haya nyie kaeni huko muendelee kuchamba mavi ya wazungu...
 
Bado haitasaidia wengi as watu huwa wanakuwa juu ya 16 years wakiingia USA wenyewe kusoma wa kutoka bongo yetu pia baada ya fomu six. Hao wa chini ya 16 wengi wameendaga na wazazi. Wa hispana ndo shangwe juu zaidi I guess.

Na bado wanatoa elfu 50+ kila mwaka ktk lottery.
Mnang'ang'ania nini huko kwenye nchi za watu? Kutazama maghorofa kila asubuhi? Baadhi ya kazi mnazofanya (wenye bahati ya kuwa nazo) ni za kujidhalilisha. Chukuweni mawazo (ideas) mrudi nyumbani muyatumie. Baadhi yenu mmekaa huko siku nyingi bila kurudi nyumbani picha mlizonzo vichwani ni za miaka 20 iliyopita. Kuna matatizo, ndiyo, lakini mbona wengi tunaishi tena maisha ya kuridhisha? Huko tulikuja, tukaona, tukadharau, tukarudi nyumbani. EAST, WEST, HOME IS BEST.
 
unaniuliza swali kwani unajua mie napoishi na unasema nimeng'ang'ania nini?

unakuja kujisifia humu labda hamna kitu, achia walio kimya.

nenda katangaze uliyoyafanya kama umeyafanya kusaidia nchi yako ndio uje ulete na mifano, unaomba watu warudi wanakuhusu nini?

kwani kule Baghdad uliombwa uondoke?
 
Usikasilike sana, jibu rahisi ni kwamba bado hujafikia uamuzi wa kurudi home, ikifikia utatinga tu! Na hata ukiamua kutokomea huko shwari tu utakuwa unatengeneza kina Obama wengine, mwah! Pambaneni tu huko, maisha ni popote!
 
ungesoma na kuelewa ungeelewa mie nimechangia thread na haimaanishi naishi huko, labda ninatembelea ila hapanihusu.
kwani mtu uki post kwenye thread ndio inakuhusu? mbona news zimejaa kila mahala siku hizi unaweza kusoma hata kujifanya unahusika kama ukitaka. google map inasaidia kuelezea maeneno utadhani umeshafika.....

kwa wewe kusema maisha ni popote hapo umenena.
 
Mnang'ang'ania nini huko kwenye nchi za watu? Kutazama maghorofa kila asubuhi? Baadhi ya kazi mnazofanya (wenye bahati ya kuwa nazo) ni za kujidhalilisha. Chukuweni mawazo (ideas) mrudi nyumbani muyatumie. Baadhi yenu mmekaa huko siku nyingi bila kurudi nyumbani picha mlizonzo vichwani ni za miaka 20 iliyopita. Kuna matatizo, ndiyo, lakini mbona wengi tunaishi tena maisha ya kuridhisha? Huko tulikuja, tukaona, tukadharau, tukarudi nyumbani. EAST, WEST, HOME IS BEST.

Pumba at work!! That was your fu2king choice so don`t use life to dictate ours; I am glad if you make it well, we are doing very fine over here, I think some of you who talk shit don`t have life; get your shit straight, you over there we are over here so what is the deal?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
mtanzania anakaa US or UK miaka 10 hana nyumba wala kiwanja..sana sana mnashindana kununua magari na kuvaa kukaa ulaya sio dili hayo mambo ya zamani. Mi nimeshakaa kote huko na nimerudi kujiendeleza na naweza kukwambia niko way better here than i ever was over there. Kuna baadhi ya watz sikatai huko nje wanakazi nzuri lakini unatumia maisha yako yote kuwachamba wazungu mavi au kubeba mapallet mtafanya hivyo mpaka lini.

Mkuu, tafadhali mkuu.

Majuu kuna kazi nyingi tu nzuri na za maana zenye kuingiza kipato halali.

Kazi hizo ulozitaja kuna baadhi ya watanzania ndio wamejengea nyumba huko TZ na kuchukua mortgage huko majuu na pia kuanzisha shughuli nyingi za kuingiza kipato kwa ndugu zao.

Unajichanganya sana kwani hizi kazi kwa huko TZ ni ndoto kuzipata na kazi kama hiyo unayosema ya kubeba pallets huwezi kuifanya mpaka uwe na leseni ya kuendesha forklift tena kwa ngazi kama conter ballance truck na reach truck.

Kazi ya "care assistant" au "support worker" ambazo wewe unasema ni za kuchamba wazungu ni kazi nzuri sana tena ndio zenye kipato cha maana kwa wale wenye uzoefu ambacho hata kama waziri (asiejishughulisha na wizi wa mali ya umma) au meneja wa kampuni hawezi kufikia mshahara wake.

Mkuu hio ndio inaitwa ughaibuni na upate nafasi uende utembelee watanzania sehemu mbalimbali na uachane na stories za watanzania ambao hawako "documented" na wamejitafutia matatizo wenyewe.
 
Hamna jipya wengi wenu mlishakwenda ubalozini mkadunda mmebakia kulalama tu hao wanaomaliza vyuo hamjui watakwenda wapi kazi hamna, isitoshe hakuna cha ajabu wanachofanya watanzania wa USA, kizuri zaidi wanalindwa na sheria za kazi; niambie Kariakoo hakuna wabeba box? Hivi mbeba box wa kariakoo analindwa na sheria kazi?

Mbona wengi wanatumikishwa na wahindi mithili ya watumwa hilo mbona hamlisemi? Basi mngeanza na hao wabeba box wa Karikoo warudi makwao; sisi hatujashindwa maisha. Kwa taarifa yako watanzania wanaoshi nje wanafanya vizuri kimaisha na wanajenga taifa kihalali angalia takwimu za Western Union na Moneygram tunatuma kiasi gani kwa mwaka?

Wengi ni hasira za maisha tu na inaonekana shule hamkwenda hata kujenga hoja hamjui; nina mifano hai ya vijana chapa kazi wa kitanzania wanasomesha ndugu zao vyuo vikuu hapo bongo kwa hizo pesa za mabox; kama hoja ni uhalifu upo kila sehemu tena hapo bongo ndio umezidi. Mbona hamuawambii wamanyema waliojazana Dar warudi Kigoma? Maisha popote tu

Chama
Gongo la Mboto DSM

Your right mkuu, mimi ni mmoja wa hao waliosomeshwa chuo kikuu na my brother..and he has done a lot of developments at home thou yeye hana mpango wa kuishi Tz tena. God bless him and you all who support your families.
 
Mkuu, tafadhali mkuu.

Majuu kuna kazi nyingi tu nzuri na za maana zenye kuingiza kipato halali.

Kazi hizo ulozitaja kuna baadhi ya watanzania ndio wamejengea nyumba huko TZ na kuchukua mortgage huko majuu na pia kuanzisha shughuli nyingi za kuingiza kipato kwa ndugu zao.

Unajichanganya sana kwani hizi kazi kwa huko TZ ni ndoto kuzipata na kazi kama hiyo unayosema ya kubeba pallets huwezi kuifanya mpaka uwe na leseni ya kuendesha forklift tena kwa ngazi kama conter ballance truck na reach truck.

Kazi ya "care assistant" au "support worker" ambazo wewe unasema ni za kuchamba wazungu ni kazi nzuri sana tena ndio zenye kipato cha maana kwa wale wenye uzoefu ambacho hata kama waziri (asiejishughulisha na wizi wa mali ya umma) au meneja wa kampuni hawezi kufikia mshahara wake.

Mkuu hio ndio inaitwa ughaibuni na upate nafasi uende utembelee watanzania sehemu mbalimbali na uachane na stories za watanzania ambao hawako "documented" na wamejitafutia matatizo wenyewe.

sawa kama wewe unaona kua care worker is a career job utaiweka kwenye cv yako hamna neno. Mi nimeshaishi ulaya na naweza sema wengi wanaofanya kazi za namna hiyo maisha yao sio mazuri wanaishi tu kama kawaida(bread n butter), but kila mtu kapangiwa pa kutafutia maisha sio, niliishi ulaya for more than 10yrs sikuona cha maana opportunities zipo lakini wanapewa wazungu zaidi nikaona upuuzi nikaamua kurudi bongo and right now am doing way better than when i was abroad. Mimi nina friends in the US wao ni kazi, house party, kupiga deals, kukamatwa na kuwekwa jela. Hayo maisha ya namna hiyo siwezi kuyafanya alafu such ppo unakuta huku nyumbani wana familia zenye uwezo wangeweza kuja huku wakaendeleza biashara za wazazi wao lakini toto halitaki kurudi na shule hajamaliza. but am sure kuna tanzanians huko wasomi na wana kazi nzuri sema ni asilimia chache sana.
 
Hapo umeongea vya maana kidogo. Mtu lazima ujue pale unaposhindwa halafu utafute njia zingine. Ni kama pale unapofanya mtihani. Kama kuna swali gumu limekushinda huwezi tuu kung'ang'ania kulijibu mpaka muda unakwisha. Liruke tuu hilo swali halafu jibu mengine. Kuna watu wengi majuu wameshindwa lakini bado wanang'ang'ania. Nasema tumia formula hii kujua kama maisha ya majuu yamekushinda. Kama upo US unafanya kazi huendi shule halafu mshahara wako wa ni chini ya dola USD 85,000 kwa mwaka, wewe umeshindwa. Tafuta plan B au rudi bongo. Using'ang'anie tuu Marekani. Maisha ni mafupi sana. Ukilala ukiamka utajikuta ujana umekupita wewe bado unayakimbiza maisha ya Marekani. Msikae tuu kuishi ma ghetto, watoto wenu wanaenda shule za wajinga wajinga maana US shule za watoto zinaenda na unakoishi. Ukiishi mashenzini na shule za watoto wako zitakuwa ni zile zile za wachovu. Tena sasa hivi uchumi wa Marekani uko dhoofu, ni muda mzuri sana wa wewe kufunga virago. Tena hakuna atakayekulaumu au kukucheka. Maana wengi wanataabika siyo wewe tuu.
 
Back
Top Bottom