Rais Magufuli: Suluhu ya Zanzibar ni Uchaguzi wa marudio

Rais Magufuli ameyaeleza hayo katika hotuba yake kwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa Balozi Augustine Mahiga leo ikulu jijini Dar es salaam.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli amewaeleza mabalozi hao kuwa licha ya Tanzania kuwa nchi moja, Zanzibar ina mfumo wake wa siasa, ina serikali yake, Katiba yake na pia tume yake ya uchaguzi inayojitegemea.

Amesema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Amesema mazungumzo ya kutatua mgogoro huo yalifanyika bila mafanikio ambapo chama kikuu cha upinzani (CUF) kimeendelea kupinga uchaguzi wa marudio huku vyama vingine kikiwemo chama tawala vikionesha uhitaji wa uchaguzi huo wa marudio.

Amesema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo, na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.

Amewaeleza mabalozi hao kuwa serikali pamoja na watanzania walio wengi wangependa kuona CUF inathibitisha madai yake ya kushinda uchaguzi huo kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa marudio.

“Tunakiasa chama cha CUF kama ambavyo watanzania wengi wangependa kuona, kuthibitisha madai ya ushindi wao katika sanduku la kura, hakuna jinsi nyingine ya kutatua suala hili zaidi ya kukubali kufanya uchaguzi wa marudio” imesema sehemu ya hotuba hiyo.

Magufuli amewahakikishia mabalozi hao kuwa nchi ni salama na hali ya amani na utulivu ni ya kuridhisha katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa marudio.
Hapa JPM amechemsha! Ni dhahiri kwamba kurudia uchaguzi ambao kufutwa kwake kulikuwa na utata mkubwa kutaleta mpasuko mkubwa sana Zanzibar. Itakuwa miaka 5 michungu sana kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Busara ingetumika kutatua kiini cha mzozo huo ambacho kimejikita katika historia ya visiwa hivyo. Kurudia uchaguzi si jambo la busara hata kidogo.
 
Namkumbuka marehemu Mtikila alipohutubia Wazanzibari Kibandamaiti mjini Zanzibar 2015 na kuwabatiza vingozi wa CCM Zanzibar kuwa wanasumbuliwa na ugonjwa wa UNYANI -wao wakishaongozwa na mapikipiki basi hawajali tena maslahi na mustakabali wa wananchi wanaowaongoza !

Hawajali kuwa wanatuweka kwenye wakati mgumu sana kwa kuwa wagumu kukubali matokeo na sasa wanatuimbia wimbo wa Bwana ( his master's voice) kwenye saturi pengo wa kurudiwa uchaguzi.

Lakini hawatuelezi kuwa uchaguzi uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani CUF ndio utakuwa suluhisho au kuzaliwa matatizo mengine mpya ya Kikatiba. Tuangalie yafuatayo:

1. Matokeo bila shaka CCM itashinda kwa kishindo uchaguzi huo uliosusiwa.

2. Iwapo chama kitakachotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa rais kitapata chini ya asilimia kumi (10) ya kura zote za uchaguzi wa rais, au.

3.Endapo rais atakuwa hana mpinzani, basi nafasi ya makamu wa kwanza wa rais itapewa chama chochote cha upinzani kitakachotokea cha pili kwa wingi wa viti vya majimbo katika Baraza la Wawakilishi.

4 Vyama vya siasa vilivyotangazwa kuwa vitashiriki katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu, mbali na CCM, havijawahi kupata hata asilimia moja (1%) ya kura zilizopigwa Zanzibar katika chaguzi zote zilizopita na havijawahi kushinda hata jimbo!

5. Hiyo ndiyo kusema kuwa chama kitakachoshiriki kuunda SUK kwa mujibu wa Katiba ni lazima kipate angalau asilimia 10 (10%) ya kura za urais au kishinde viti vingi katika Baraza la Wawakilishi.

Matakwa haya hayatofikiwa na hivyo kuukaribisha mkwamo mwengine. Kwa vile ndugu zetu wanaugua ugonjwa wa UNYANI, Ugonjwa wa kusindikizwa na mapikipiki na vin'gora hawasikii la muadhini wala mnadi sala.

Je hapa pana uchaguzi au kuharibu pesa tu kwa kununua mgogoro mwengine, au ni UNYANI
 
Magufuli anamaani uteuzi dio uchaguzi...yaani selection not election
Tayari wamesha mteua sheni ...
Na kasema ndoto wapinzani kutawala..sasa anadanganya watu wazima mabalozi
Kwani unadhani kwa nini kakimbia hiyo hafla ya hao mabalozi wa nje na badala yake akamtuma Dr Mahiga amwakilishe?

Ni dhahiri kitu 'kilichomkimbiza' kwenye mjumuiko huo ni kile kitu kinachoitwa guilty concsiousness.

Kwa kuwa hulka ya JPM naturally siyo 'msanii' tofauti sana na hulka ya mtangulizi wake JK ambaye ni msanii wa kutupa!

Kwa hali hiyo aliamini kuwa kama angehudhuria hafla hiyo angeteseka sana nafsi yake, kwa kuwa anajua wazi kuwa ni Chama chake cha Majipu ndiyo 'waliomuamrisha' Jecha aufute uchaguzi ule, ambapo hivi sasa kutokana na uamuzi wao huo wa 'kizembe' umesababisha Tanzania idharaulike sana kwenye Jumuiya ya Kimataifa, ambao walituma waangalizi wao kwenye uchaguzi huo ambao walitoa taarifa zao kuwa uchaguzi ule ulikuwa wa uhuru na haki.

Vile vile mkwamo huo wa kisiasa umeisababishia nchi yetu mgogoro mkubwa sana wa kikatiba ambao haujawahi kushuhudiwa tokea nchi yetu iingie kwenye chaguzi za vyama vingi mwaka 1995.
 
Zanzibar kwa sasa inatawaliwa kikoloni na Tanganyika ni koloni la Tanganyika bado hawajapata Uhuru wao, vyombo vya dola vyote vinatoka Tanganyika hawana msitu wa kuingia kupambana bali njia pekee ni kuingia misikitini kuomba Dua zisizo na kikomo mpaka mungu asikie maombi yao.

Hata humo misikitini watatuambia tusiende. Tuswalie majumbani mwetu maana kukutana miskitini ndio itakuwa mwanya wa kuanza fujo kwa pamoja. Wazanzibari tuko wachache na kama tunataka kusikilizwa basi hata wa bara mnabidi mtuunge mkono kwa wenye kuyaona maovu yanatendeka. Kwani si ndio muungano bwana? For better or for worse...
 
Kwani unadhani kwa nini kakimbia hiyo hafla ya hao mabalozi wa nje na badala yake akamtuma Dr Mahiga amwakilishe?

Ni dhahiri kitu 'kilichomkimbiza' kwenye mjumuiko huo ni kile kitu kinachoitwa guilty concsiousness.

Kwa kuwa hulka ya JPM naturally siyo 'msanii' tofauti sana na hulka ya mtangulizi wake JK ambaye ni msanii wa kutupa!

Kwa hali hiyo aliamini kuwa kama angehudhuria hafla hiyo angeteseka sana nafsi yake, kwa kuwa anajua wazi kuwa ni Chama chake cha Majipu ndiyo 'waliomuamrisha' Jecha aufute uchaguzi ule, ambapo hivi sasa kutokana na uamuzi wao huo wa 'kizembe' umesababisha Tanzania idharaulike sana kwenye Jumuiya ya Kimataifa, ambao walituma waangalizi wao kwenye uchaguzi huo ambao walitoa taarifa zao kuwa uchaguzi ule ulikuwa wa uhuru na haki.

Vile vile mkwamo huo wa kisiasa umeisababishia nchi yetu mgogoro mkubwa sana wa kikatiba ambao haujawahi kushuhudiwa tokea nchi yetu iingie kwenye chaguzi za vyama vingi mwaka 1995.

Ugonjwa ukianza kudhuru kucha utaenea kidole kizima, mpaka mkono wote uathiriki ulete maradhi mwili wote na mwishowe kuangamiza. Mkono wa kulia ukihisi huu ugonywa wa kidole cha mkono wa kushoto haunihusu mie, basi its matta of time mpaka effect za yale maradhi yataadhiri mpaka uwezo wa mkono wa kulia. Hivyo ndugu zetu wa bara.... Tuamke. Kitakachoanzwa Zanzibar kimalizwe bara. La sivyo mtakuwa kama mnahudhuria michezo unaoonyeswa sinema tu!
 
Hiyo hotuba ya Presidaa iliyosomwa na huyo mwanadiplomasia Dr Mahiga, ni miongoni ya hotuba za kipuuzi kupindukia ambazo zimewahi kutolewa na Presidaa wa nchi yetu tokea nchi yetu ijitawale mwaka 1961.

Ngoja tuhoji maswali machache kuhusu hotuba hiyo:

1. Presidaa amesema solution pekee ya mkwamo wa kisiasa wa Zanzibar ni kurejea uchaguzi huo ila akaeleza ni vyema yakaandaliwa mazingira ya kuufanya uchaguzi huo kuwa wa uhuru na haki.

Swali: Uchaguzi huo utawezaje kuwa huru na haki kama utaendelea kusimamiwa na huyo huyo Jecha, ambaye Umma wote wa watanzania unajua kuwa ufutaji wake wa uchaguzi na matokeo yake yote ulikuwa ni uamuzi batili kwa kuwa ulivunja Katiba ya Zanzibar na sheria ya uchaguzi ya Zsnzibar?

2. Katika hotuba hiyo ya Presidaa amedai kuwa kasoro za uchaguzi zilitokea Pemba pekee.

Swali; Sasa kama mapungufu hayo ya uchaguzi yalitokea Pemba pekee, iweje huyo Jecha ayafute matokeo yote pamoja na ya Unguja, ambapo kwa mujibu wa hotuba hiyo hakukuwa na kasoro zozote?

3. Hivi nini maana ya nchi yetu kuwaleta waangalizi wa uchaguzi kutoka nje ya nchi na kuruhusu waangalizi wa ndani ya nchi kufuatilia uchaguzi huo?

Swali hilo linakuwa muhimu kuwauliza watawala wetu wa CCM, kwa kuwa waangalizi wote wa nje ya nchi na wale wa ndani ya nchi walitoa taarifa zao kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki. Sasa inakuwaje mtu mmoja anayeitwa Jecha awe na fikra zake za kufikirika na fikra zake zitofautiane kabisa na wengine kuwa uchaguzi ule ulikuwa na kasoro chungu nzima?

4. Iweje Jecha avunje kanuni mojawapo muhimu sana ya natural justice inayosema kuwa MAN CAN NOT BE A JUDGE ON HIS OWN CASE?

Kwa kuwa katika 'kesi' hii ya uchaguzi huu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana tumeshuhudia Jecha akiwa mlalamikaji na wakati huo huo akiwa Polisi aliyefanya uchunguzi na baadaye akawa mwendesha mashitaka na hatimaye akawa Jaji na kuhukumu kuwa uchaguzi ule ulikuwa na kasoro chungu nzima kwa hiyo unastahili kurejewa wote!!!!!!

5. Hivi hao wasimamizi wa uchaguzi huko Zenji walikuwa 'machizi' hadi wafikie hatua ya kuwapa vyeti vya ushindi wawakalishi wote wa majimbo 54 kwenye Baraza, kama kweli uchaguzi ule ulikuwa umeharibika kupita kiasi?

6. Hivi huyo Jecha ambaye Umma wa watanzania unafahamu kuwa yupo mafichoni alikopelekwa na watawala wa CCM na akipewa ulinzi mkali kutoka vyombo vya usalama vya nchi. Hivi atausimamia uchaguzi huo akiwa huko mafichoni kwa kutumia remote control?!

Ni vyema huyo balozi Dr Mahiga aliyesoma hotuba ya Presidaa au Kurugenzi ya habari ya Ikulu ikatujibia maswali hayo machache.

Mkuu, ninakubaliana na wewe asilimia MIA.

Magufuli, pengine, asingependa kusema UONGO na kujiunga na Mafisi, hivyo anamtuma Mahiga ambaye sijawahi ona Diplomat BOGUS kama huyu. Ni kwa vipi anaweza kukwepa kujibu hoja ya kuwa Jecha amevunja Sheria, kwa kujiamulia kufuta uchaguzi? Anarukia kwenye kurudia uchaguzi??

Hii ni kuweka Mzigo mbele ya Punda, ili auvute! Ngoma mbichi hapo.
 
Ni zarau na kuwdhalilisha wazanzibar tu .because wanaitwa maamiri jeshi wakuu .wazanzibari kama kweli wathibisge mara ngapi kama walishinda ? Zipo document zilizopatikana kuroka katika masanduku ya kura je apelekewe huyu raisi .wanadharau sana wazanzibar na waangalizi wote waliothibitisha uhuru na haki . Endeleeni tu na uchaguzi wenu mnataka cuf washiriki hawashiriki ng'o .jama haki za watu zinalika fakamieni tu
 
Mwizi akikosa cha kuiba huwa anafanya mazowezi hata kwenye dirisha lake
DSC_0709.JPG
 
Mkuu, ninakubaliana na wewe asilimia MIA.

Magufuli, pengine, asingependa kusema UONGO na kujiunga na Mafisi, hivyo anamtuma Mahiga ambaye sijawahi ona Diplomat BOGUS kama huyu. Ni kwa vipi anaweza kukwepa kujibu hoja ya kuwa Jecha amevunja Sheria, kwa kujiamulia kufuta uchaguzi? Anarukia kwenye kurudia uchaguzi??

Hii ni kuweka Mzigo mbele ya Punda, ili auvute! Ngoma mbichi hapo.
Magu ameitwa kupewa msimamo wa Chama.
DSC_0359.jpg

DSC_0331.jpg

Magu alishaonesha kuwa amekubali kushiriki katika ubakaji wa demokrasia. Nini alisema siku anahutubia Bunge?
Link Jecha alitumwa na nani kufuta matokeo ya Uchaguzi Zanzibar
 
Mambo ya Zanzibar watajuana wenyewe

Asie Muunga Mkono Rais Magufuli Akapimwe Akili
 
Kila mtu ana uhuru wa kuongea,lakini naamini kwa vile JPM ni binadamu,roho yake inamsuta.Rohoni mwake anaamini kwamba anachosema sio kweli,kwa kuwa anajua mshindi halali ni Maalim seif.Nani asiyejua kwamba tume ya Jecha sio huru.Katika mazingira hayo what do you expect,si uchaguzi usio huru na haki.Magufuli kwa uamuzi wake huu is directly contributing towards chaos in Zanzibar and history will judge him.
Rais Magufuli ameyaeleza hayo katika hotuba yake kwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa Balozi Augustine Mahiga leo ikulu jijini Dar es salaam.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli amewaeleza mabalozi hao kuwa licha ya Tanzania kuwa nchi moja, Zanzibar ina mfumo wake wa siasa, ina serikali yake, Katiba yake na pia tume yake ya uchaguzi inayojitegemea.

Amesema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Amesema mazungumzo ya kutatua mgogoro huo yalifanyika bila mafanikio ambapo chama kikuu cha upinzani (CUF) kimeendelea kupinga uchaguzi wa marudio huku vyama vingine kikiwemo chama tawala vikionesha uhitaji wa uchaguzi huo wa marudio.

Amesema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo, na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.

Amewaeleza mabalozi hao kuwa serikali pamoja na watanzania walio wengi wangependa kuona CUF inathibitisha madai yake ya kushinda uchaguzi huo kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa marudio.

“Tunakiasa chama cha CUF kama ambavyo watanzania wengi wangependa kuona, kuthibitisha madai ya ushindi wao katika sanduku la kura, hakuna jinsi nyingine ya kutatua suala hili zaidi ya kukubali kufanya uchaguzi wa marudio” imesema sehemu ya hotuba hiyo.

Magufuli amewahakikishia mabalozi hao kuwa nchi ni salama na hali ya amani na utulivu ni ya kuridhisha katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa marudio.
 
Masikini rais wangu anaenda The Hague kabla ya kufurahia urais wa magumashi!
 
Wanasiasa wanatuona majuha sana. Kama Rais anaona suluhu ni marudio ya uchaguzi, na tayari chama tawala na vingine vitashiriki, wasi wasi wa nini kuhusu CUF? Si aendelee tu na uchaguzi wa marudio bila CUF?

Pili, wako wapi akina Msekwa waliosema Rais hana mamlaka na Zanzibar?
Leo anaongea kwa mamlaka gani ambayo akina Msekwa hawayakuyaona?

Tatu, Rais anasema hali ya nchi ni salama na uchaguzi utafanyika kwa Amani.
Huyu tuliambiwa hana mamlaka na mambo ya Zanzibar, haya yanatoka wapi tena?

Kubwa Zaidi ni hili la Rais kualika watu nyumbani kwake na kisha 'kutohudhuria'.
Hili linazidi kutoa picha ambayo wao hawajui ni mbaya sana.

Hao mabalozi leo wanajiuliza , tangu uhuru linI haya yametokea na kwanini yanatokea sasa?

Tutaambiwa Rais hakuhudhuria kwasababu anabana matumizi.

Kwanini basi waziri aSiandae hafla pale Hyatt hotel! Tutaambiwa ni kubana matumizi.

Wakati tunaambiwa hayo, majuzi msafara wa mawaziri na viongozi ulikuwa Singida ukitumia rasilimali za Taifa kwa birthday ya CCM.

Uongozi wote wa kitaifa ulikuwepo pale, gharama zote za itifaki, ulinzi n.k. ni za Watanzania.
Kubana matumizi kuko wapi? Hivi mipasho ya Singida na ujio wa mabalozi kipi muhimu?

Tulisema ni suala la muda Watanzania wataona felia ! Tulidanganya?
'Kukimbia' mabalozi nako ni #Hapakazi!

Tendo la' kukimbia' mabalozi, si kufelia kidiplomasia bali kufeli kwa nchi

Lakini lazima tujiulize Zaidi, mkuu wetu kutotaka kukutana na wenzake lipo jambo! Kuna jambo!

Nyani Ngabu The Boss JokaKuu

Kuna kitu kinafichwa....
hali hii sio kawaida...lakini wana pretend all is well

Nimejiuliza inawezekana Magufuli kaamua kumpa Mahiga all the power kwenye diplomacy?
yeye ameshakata tamaa kama atakuja weza ku handle diplomacy inavyostahili?
 
Masikini rais wangu anaenda The Hague kabla ya kufurahia urais wa magumashi!
 
Kuna kitu kinafichwa....
hali hii sio kawaida...lakini wana pretend all is well

Nimejiuliza inawezekana Magufuli kaamua kumpa Mahiga all the power kwenye diplomacy?
yeye ameshakata tamaa kama atakuja weza ku handle diplomacy inavyostahili?
Lipo jambo linafichwa, tutajua tu

Tuliambiwa kusafiri kwa gari kwenda Dodoma ni kubana matumizi.
Leo tunashuhudia mawaziri na serikali yote ikhamia Singida 'bila matumizi' Tunaambiwa wanakwenda kwa pesa za chama!

Tutajua tu, lipo jambo na wengine tuliliona ingawa mashabiki, wanazi na wapenzi hawaelewi hawasikii!

#Hapakusepa tu
 
Mbalozi si tu aliwakimbia lakini waliohusika na kuwakaribisha
walishindwa kabisa hata ustaarabu mdogo tu
picha zinaonesha mabalozi walitakiwa kusimama mbele ya vikaratasi
inaoneshwa vikaratasi viliwekwa majina yao wakaambiwa wasimame hapo
sura zao ziko very frustrated...

Awamu hii ina mbwembwe nyingi huku makosa ni mengi kupita kiasi
 
Back
Top Bottom