Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Nakubaliana kabisa na hoja yako.yaan hili la Zanzibar limewakalia vibaya sana ccm kweli wizi unamwisho ujanja ujanja wa ccm naona kama umegota.sasa leo rais magufuli kaamua kufunguka waziwazi kuwa Zanzibar ni nchi inakila kitu chake! wakati pinda alivyoulizwaga bungeni alisema ni moja ya kipande cha tanzania yaa mkoa.leo rais amethibitisha! kaenda mbali eti cuf warudie kuthibitisha ushindi wao!hiv kumbe ukishinda huwa unatakiwa kurudia uchaguz tena bila kampen! na hizo pesa za marudio nan atatoa?na aliye haribu uchaguzi yuko magereza au? tume wako wamoja au wamegawanyika? eee mungu simama upande wa haki yetu sisi wazanzibar
Hao CCM walikurupuka 'kumuamrisha' Jecha aufute uchaguzi ule na kutangaza uchaguzi wa marudio bila kuangalia impact yake.
Hao CCM waliamini ya kuwa haiwezekani CUF wakasusia uchaguzi wa marejeo.
Kitendo cha CUF kuendelea na msimamo wao wa kususia uchaguzi huo, kunafanya mkwamo huu wa kisiasa kutoweza kumalizika hata kama watalazimisha kufanya uchaguzi huo wa marejeo hiyo tarehe 20/03/2016.
Kwa kuwa kwenye makubaliano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa [SUK] ambayo yameingizwa kwenye Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, limewekwa sharti la vyama viwili vinavyounda SUK, ni lazima iwe kwa chama kilichoshinda na chama kilichopata ushindi wa pili, kwa sharti la kupata angalau asilimia 10 ya kura zote zilizopigwa na angalau kiwe kimepata viti 5 kwenye Baraza la wawakilishi.
Kwa mujibu ya matokeo yaliyokuwa yamebandikwa vituoni kwenye majimbo yote 54 ya Unguja na Pemba kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015, hivyo vyama vingine vyote vya upinzani zaidi ya 10 vilivosimamisha wagombea Urais na wajumbe wa Baraza la uwakilishi, wagombea wote wa Urais kwa ujumla wao waliambulia kura chini ya asilimia moja!
Kwa upande wa Baraza la Uwakilishi hakuna chama chochote kati ya hivyo zaidi ya 10 vinavyojiita vyama vya upinzani kilichoambulia angalau kiti kimoja kwenye Baraza la Uwakilishi!
Kwa kuwa hali ya kisiasa ya Zanzibar inajulikana ni ya vyama viwili vikuu vya CCM na CUF pekee, ambavyo ndivyo vinavyoweza kupata zaidi ya asilimia 10 ya kura za Urais na ndivyo pekee vinavyoweza kupata wajumbe kwenye Baraza la Uwakilishi.
Hiyo tafsiri yake ni kuwa hata kama hao CCM watalazimisha huo uchaguzi wao,hata hivyo baada ya kumalizika uchaguzi huo na matokeo yatakapotoka, mkwamo wa kisiasa utakuwa umesalia vile vile na tena ndiyo utakuwa umeongezeka maradufu.