Rais Magufuli: Suluhu ya Zanzibar ni Uchaguzi wa marudio

Mbalozi si tu aliwakimbia lakini waliohusika na kuwakaribisha
walishindwa kabisa hata ustaarabu mdogo tu
picha zinaonesha mabalozi walitakiwa kusimama mbele ya vikaratasi
inaoneshwa vikaratasi viliwekwa majina yao wakaambiwa wasimame hapo
sura zao ziko very frustrated...

Awamu hii ina mbwembwe nyingi huku makosa ni mengi kupita kiasi
Na endapo dhifa ilitakiwa kufanywa na waziri, njia bora ilikuwa kuandaa Hotelini (naogopa watakurupuka gharama)

Leo wanaitwa 'nyumbani' mwenye nyumba kasepa! hata katika logic za mitaani haiingi akilini
Unamwalika rafiki yako 'host' anakuwa mdogo wako! teh teh

Mabalozi ni wawakilishi wa wakuu wa mataifa mengine. Inawezakaje kuwakimbia?

Nadhani hofu ni lile tangazo la kuwazuia wasifanye kazi zao au hili la ZNZ au kuna jingine. Haiwezekani lipo jambo!

Hivi the Boss unakumbu kumbu zozote ikiwa ilishawahi kutokea huko nyuma mabalozi kuitwa Ikulu na Rais akakacha?
 
The Boss hii jambo ni zito, watetezi wa #Hapakazi wakiwemo ''46 wanaofikiriwa'', nawaona wanyoonge! Sura zimeswajika, wamekumbwa na mfadhaiko, simanzi tele huku wakiwa wametunduwaa

Wanajiuliza waanzie wapi kutetea hili.
 
Lipo jambo linafichwa, tutajua tu

Tuliambiwa kusafiri kwa gari kwenda Dodoma ni kubana matumizi.
Leo tunashuhudia mawaziri na serikali yote ikhamia Singida 'bila matumizi' Tunaambiwa wanakwenda kwa pesa za chama!

Tutajua tu, lipo jambo na wengine tuliliona ingawa mashabiki, wanazi na wapenzi hawaelewi hawasikii!

#Hapakusepa tu

Una hakika nani rais ndiye aliwaalika mabalozi na sio Foreign Minister? Na ni wapi imeandikwa kuwa event ya mabalozi lazima rais awepo?

Kwenye matumizi, Yes, serikali inabana matumizi, lakini haizui vikundi vya hiari kufanya sherehe zake.
 
Magufuli &co pelekeni vifaru na majeshi huko zanzibar ili mufanye uchaguzi ila nakuhakikishia wazanzibar hawatorudi nyuma kurejesha mamlaka yao,na hata kama mtawauwa wote basi haki yao haipotei itarudi tu kwa wazanzibar.
 
Una hakika nani rais ndiye aliwaalika mabalozi na sio Foreign Minister? Na ni wapi imeandikwa kuwa event ya mabalozi lazima rais awepo?

Kwenye matumizi, Yes, serikali inabana matumizi, lakini haizui vikundi vya hiari kufanya sherehe zake.
Wapi imeandikwa event ya mabalozi ifanyike Ikulu hata kama ni waziri ameandaa!

Serikali inabana matumizi wakati serikali nzima imesafiri kwa gharama za umma kwenda shughuli za vikundi binafsi! ebo!

Ulinzi, magari, madereva, wasaidizi n.k. unadhani vinatolewa na CCM
 
Wanasiasa wanatuona majuha sana...

Wakati tunaambiwa hayo, majuzi msafara wa mawaziri na viongozi ulikuwa Singida ukitumia rasilimali za Taifa kwa birthday ya CCM.

Uongozi wote wa kitaifa ulikuwepo pale, gharama zote za itifaki, ulinzi n.k. ni za Watanzania.
Kubana matumizi kuko wapi? Hivi mipasho ya Singida na ujio wa mabalozi kipi muhimu?
Baada ya Singida, kubana matumizi ilihamia Dodoma.
DSC_0359.jpg

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu Maalum ya CCM, leo, Ikulu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.

DSC_0331.jpg
 
Mkuu, ni kweli dhuluma ina mwisho na mwisho wa dhuluma ni kuundwa tume huru ya uchaguzi hata huku bara tunapigania kupata tume huru ya uchaguzi. Bila tume huru dhuluma kwa CCM haitakoma. Sasa kama Seif hataki kuingia kwenye uchaguzi chini ya tume huru je, anataka nini?
Tume huru ipi unayoisema hapa Kirikou? Tume ya Jecha? Weka wazi, Tume huru ipi hiyo?
Kama CCM imeshinda Tanganyika(Tanzania bara) kwa nini pia uchaguzi huku haurudiwi ili watanzania wajiridhishe kama kweli CCM walishinda? Kama CCM walishinda,watashinda tena, wapiga kura waliopigia CCM ni wale wale, wanaogopa nini kuitisha uchaguzi wa marudio?
Tume ya Lubuva ni huru? Kwa nini ilitupilia mbali maombi ya Chadema ilipolalamikia kasoro za uchaguzi?
 
Yaani CUF wakithibitisha uchaguz hautarudiwa?
Anadai wathibitishe kwa kukubali kushiriki uchaguzi na kushinda.
Hata hivyo najua kuna kitu wanakiogopa. Kama ameshasema kuwa vyama vingine pamoja na CCM wanautaka uchaguzi wa marudio, kuna haja gani ya kuitajataja CUF kila mara? By the way, hivyo vyama vingine vilivyoshiriki mazungumzo ndio vipi?
 
Una hakika nani rais ndiye aliwaalika mabalozi na sio Foreign Minister? Na ni wapi imeandikwa kuwa event ya mabalozi lazima rais awepo?

Kwenye matumizi, Yes, serikali inabana matumizi, lakini haizui vikundi vya hiari kufanya sherehe zake.
Moja Waziri awaalike Mabalozi lakini asome hutuba ya Rais? Inawezekana wanahabari wameandika kimakosa kuwa Mahiga alimwakilisha Rais?

Pili, Wizara ya Mahiga haina ukumbi wake wa mikutano? Kwa nini Mkusanyiko huo haukufanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Mahiga au Ukumbi wa hoteli ya bei poa?

Tatu kwa nini Mahiga amewasimamisha Mabalozi kama watoto wa shule wanaotakiwa kuimba kwaya?
 
Rais Magufuli ameyaeleza hayo katika hotuba yake kwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa Balozi Augustine Mahiga leo ikulu jijini Dar es salaam.

....
Hapa Kikwete anajiwakilisha.
 
Tume huru ipi unayoisema hapa Kirikou? Tume ya Jecha? Weka wazi, Tume huru ipi hiyo?
Kama CCM imeshinda Tanganyika(Tanzania bara) kwa nini pia uchaguzi huku haurudiwi ili watanzania wajiridhishe kama kweli CCM walishinda? Kama CCM walishinda,watashinda tena, wapiga kura waliopigia CCM ni wale wale, wanaogopa nini kuitisha uchaguzi wa marudio?
Tume ya Lubuva ni huru? Kwa nini ilitupilia mbali maombi ya Chadema ilipolalamikia kasoro za uchaguzi?

Mkuu kabla hatujakwenda mbali kujadili Tume ya Jaji Lubuva, mkuu napenda kujua uchaguzi bara unataka urudiwe kumfurahisha nani?
 
Wateuane tu kwani hamna haja ya kupiga kura tena inchi hii iwe tanganyika au zanzibar naona kiini macho tu
 
yaan hili la Zanzibar limewakalia vibaya sana ccm kweli wizi unamwisho ujanja ujanja wa ccm naona kama umegota.sasa leo rais magufuli kaamua kufunguka waziwazi kuwa Zanzibar ni nchi inakila kitu chake! wakati pinda alivyoulizwaga bungeni alisema ni moja ya kipande cha tanzania yaa mkoa.leo rais amethibitisha! kaenda mbali eti cuf warudie kuthibitisha ushindi wao!hiv kumbe ukishinda huwa unatakiwa kurudia uchaguz tena bila kampen! na hizo pesa za marudio nan atatoa?na aliye haribu uchaguzi yuko magereza au? tume wako wamoja au wamegawanyika? eee mungu simama upande wa haki yetu sisi wazanzibar
 
.Amesema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.


Hapo ndipo ninapothibitisha ya kwamba Raisi wangu ni kilaza. hii statement kaandika yeye na wala haihitaji kuwa na elimu ya Rocket science kumjibu huu utumbo hapa.


Jibu lake: Zanzibar ni visiwa 2. Kama matatizo yalitokea ya uchaguzi yalitokea Pemba jee yale ya Unguja ambayo yamemalizika kulikuwa na haja gani kuufuta uchaguzi wote.

Amesema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo, na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.

Mheshimiwa Just curious jee mutakuwa tayari kuanzisha tume huru ya uchaguzi kwa uchaguzi wa marudio ama mutakuwa tayari UN wasimamie Uchaguzi huu!

Si watanzania wote ni vilaza!

Kama mapungufu yalionekana Pemba, kwa nini kufuta uchaguzi wote? Nani aliyelalamika kuhusu mapungufu hayo ya Pemba?
 
Sio Bure wanahitaji maombi!
this
wazungu sio wa wajinga wa kuletewa hotuba ya chekechea hii,yeye angesema zanzibar haiwezi kutawaliwa na CUF hapo wazungu wangemwelewa.sasa kama pemba ndio matatizo yalitokea kwanini uchaguzi wa unguja umefutwa?,hivi ni kweli majimbo yote ya pemba uchaguzi uliharibika,halafu kwanini tume ya uchaguzi haikuisikiliza mapingamizi ya CUF badala yake CCM wakasikiliza pingamizi la CUF na CCM ikaamua uchaguzi urudiwe na ZEC ikaungamkono na kutangaza uchaguzi mwigine.hata kichaa hawezi kukubali kurudia uchaguziiiii wa namna hii?
magu's speech is purely propaganda
 
This is a joke kwa mabalozi ambao walituma waangalizi sehemu zote na kuridhika.
Kwanza kawakimbia mabalozi .
Sijawahi kusikia mtu kualika wageni halafu ukajifungia chumbani
Yaani hapo ndo simuelewi JPJM! Kwa nini anapenda kuwakilishwa kila mahali; hata humu humu nchini? Mimi nafikiri ikulu inabidi wafike mahali watuambie tu ukweli wa tatizo au mkakati wa huyu mheshimiwa sana!
 
The Boss hii jambo ni zito, watetezi wa #Hapakazi wakiwemo ''46 wanaofikiriwa'', nawaona wanyoonge! Sura zimeswajika, wamekumbwa na mfadhaiko, simanzi tele huku wakiwa wametunduwaa

Wanajiuliza waanzie wapi kutetea hili.
Huu uharamia wanaoufanya hao mahafidhina wa CCM wachache sana ambao idadi yao inawezekana haizidi hata watu 100, naamini kabisa mamilioni ya wanaccm wenzao watakuwa hawapendezwi nayo hata chembe.

Hiyo ndiyo siri kubwa inayofanya hata wale ambao tunawaita die hard JF Lumumba team, wamelazimika waingie mitini kukwepa kabisa kujadili hoja hii, kwa kuwa hata wao nafsi zao zinasonononeka sana namna wanavyoona haki ya wazanzibari inavyotaka kuporwa kwa nguvu kwa kutumia vifaru vya kijeshi.
 
Anadai wathibitishe kwa kukubali kushiriki uchaguzi na kushinda.
Hata hivyo najua kuna kitu wanakiogopa. Kama ameshasema kuwa vyama vingine pamoja na CCM wanautaka uchaguzi wa marudio, kuna haja gani ya kuitajataja CUF kila mara? By the way, hivyo vyama vingine vilivyoshiriki mazungumzo ndio vipi?
Hivyo 'Vyama Vngine' kwa mujibu wa babu duni aliponukuliwa na Mwananchi hata kura 80 havikufikisha,na kwa mujibu wa KATIBA YAO ILI KUUNDA SUK ni kwamba chama kinachofuata kuna asilimia fulani kinapaswa kufikisha
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom