Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,722
218,285
Hii ndio gia mpya waliyoamua kuja nayo baada ya Chaguzi zao kumalizika

Zaidi soma hapa

--
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 8 Machi 2024 jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema viongozi wa chama hicho watakutana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenzake wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussen Mwinyi kwa ajili ya kuwaeleza nia kujitoa kwenye serikali hiyo.

Ado amesema makubaliano yaliyofanywa kati ya Hayati Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Zanzibar, Dk. Mwinyi hayajatekelezwa.

Amesema moja ya makubaliano kati Maalim Seif na Dk. Mwinyi ni kurekebisho mifumo ya kiuchaguzi katika nchi ya Zanzibar ili kupatikane uchaguzi wa huru na haki na kuepusha machafuko yanayotokea katika kila uchaguzi visiwani humo.

Amesema Serikali ya SUK ni zao la umwagikaji damu za wananchi wa Zanzibar katika vipindi vyote vya uchaguzi.

“Tuliingia kwenye serikali ya umoja wa Kitaifa kwa sababu mbili ya kwanza hilo ni takwa la kisheria pili kwa sababu ya makubaliano ya Maalim Seif na Dk. Mwinyi,” amesema.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Zanzibar, inaundwa na CCM pamoja na ACT Wazalendo kupitia Mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Chanzo: Mwanahalisi
 
Katibu mkuu wa ACT Wazalendo Addo Shaibu amesema Uongozi wa Juu wa Chama chake utanataramia kuonana na Rais wa JMT Dr Samia na Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi kuwaeleza kuwa wanajiondoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar

Source: Mwanahalisi Digital
 
yaani wamekaa miaka minne leo ndio wanataka kujitoa.

Alafu hii SUK si upande wao wako viongozi watatu tu.
 
Tumeshawashtukia..
Uchaguzi umekaribia Serkali imeshindwa kuwatatulia shida wananchi na kwa nahati.mbaya Sana Serkali hiyo hiyo na wao walikuwa sehemu ya serikali watawaambia nini wananchi?

Watakuwa na sera gani za kuuza kwa wananchi?
Wakisema maisha magumu ..Swali ni kuwa wao wamefanya nini ikiwa walikuwa sehemu ya serkali..

Wakisema sijui nini huko.. jibu linatakiwa kuwa na wao wajitetee kuhusu Ugumu wa maisha wa Wananchi kwa sababu na wao.walikuwa ama ni sehemu ya serikali
 
Back
Top Bottom