Rais Magufuli: Suluhu ya Zanzibar ni Uchaguzi wa marudio

Huo ni mtazamo wake ,wala sio mtazamo wa wazanzibari wote milion nne
Wazanzibar nyinyi ni koloni la Tanganyika hamna cha kusema wala kuamua maamuzi yote yatatoka Tanganyika, Nyerere alijua ipo siku Zanzibar utazinduka ndiyo maana alikuwa akiililia sana Serikalini moja kuondokana na Ukoloni huu. Sasa pesa nyingi itatumika kuilinda Zanzibar matokeo yake huduma nyingi zitasimama, Hii si njia sahihi ya matumizi ya pesa zitokanazo na Kodi.
 
Duu !!1kumbe jamaa si kuzungumza tu kumbe hata kusoma hio lugha hajui! hadi asemewe na Mahiga!
hapa kazi tu ya kukimbia tu
Mhe anatoa majibu kama vile sio rais wa ya muungano. Maana yake ni kuwa siku wakianza kudhuriana hataingilia inakuja kweli hiyo. Anachojua ni vipele kuviita majipu
 
Mhe anatoa majibu kama vile sio rais wa ya muungano. Maana yake ni kuwa siku wakianza kudhuriana hataingilia inakuja kweli hiyo. Anachojua ni vipele kuviita majipu
Zanzibar sasa ni koloni la Tanganyika ina maana akiamua kuwaacha wauane wenyewe kwa wenyewe anaweza kwa sababu yupo kule akiwa na majeshi yake ambayo ni rahisi kuyarejesha Tanganyika haraka pindi akiona kimenuka, muungano huu wa sasa si ule muungano wa Nyerere ambapo Rais wa muungano alikuwa na nguvu pande zote pasipo kutumia majeshi.
 
Duu !!1kumbe jamaa si kuzungumza tu kumbe hata kusoma hio lugha hajui! hadi asemewe na Mahiga!
hapa kazi tu ya kukimbia tu
wewe akili yako haiko sawa. hajui kusoma kivipi? Accent za lugha ni kawaida, ndio maana hata waingereza wanatofautiana accent kulingana na mtu anakotoka/alikokulia. Kiingereza cha mtu wa Australia ni tofauti na wa USA na wa UK, ingawa lugha ni hiyo hiyo. Na hata hao wazungu huwa kuna maneno wanatamka isivyotakiwa ila kwa sababu mmezoea ukoloni mambo leo basi mnadhani ngozi nyeupe ni sahihi kila jambo. shame
 
Kwa hiyo Huyu Magufuli ameona ni tatizo dogo, akamtuma mwakilishi wake akasome hotuba. Haya ndo ninayoona.
1. Magufuli ni mwoga. Angetakiwa awepo pale kukabilinmaswali.
2. Rais huyu hana vipaumbele au ana dharau. Suala la Zbar angepaswa kulianza haraka zaidi
3. Hajui siasa na si mwanasiasa
4. Kauli ya "Hapa kazi tu" ni vitisho tu na haina ukweli halisi ndani yake. Nguvu za hii kauli zinaelekezwa kwa wanyonge wakati wale big fish hawaguswi. Mfano bomoabomoa, Muhimbili, Zanzibar, wabunge wa upinzani, madiwani wa upinzani... Kama hali hii ya vitisho itaendelea, Tanzania itaumia. Sio Zanzibar pekee
 
Hiyo hotuba ya Presidaa iliyosomwa na huyo mwanadiplomasia Dr Mahiga, ni miongoni ya hotuba za kipuuzi kupindukia ambazo zimewahi kutolewa na Presidaa wa nchi yetu tokea nchi yetu ijitawale mwaka 1961.

Ngoja tuhoji maswali machache kuhusu hotuba hiyo:

1. Presidaa amesema solution pekee ya mkwamo wa kisiasa wa Zanzibar ni kurejea uchaguzi huo ila akaeleza ni vyema yakaandaliwa mazingira ya kuufanya uchaguzi huo kuwa wa uhuru na haki.

Swali: Uchaguzi huo utawezaje kuwa huru na haki kama utaendelea kusimamiwa na huyo huyo Jecha, ambaye Umma wote wa watanzania unajua kuwa ufutaji wake wa uchaguzi na matokeo yake yote ulikuwa ni uamuzi batili kwa kuwa ulivunja Katiba ya Zanzibar na sheria ya uchaguzi ya Zsnzibar?

2. Katika hotuba hiyo ya Presidaa amedai kuwa kasoro za uchaguzi zilitokea Pemba pekee.

Swali; Sasa kama mapungufu hayo ya uchaguzi yalitokea Pemba pekee, iweje huyo Jecha ayafute matokeo yote pamoja na ya Unguja, ambapo kwa mujibu wa hotuba hiyo hakukuwa na kasoro zozote?

3. Hivi nini maana ya nchi yetu kuwaleta waangalizi wa uchaguzi kutoka nje ya nchi na kuruhusu waangalizi wa ndani ya nchi kufuatilia uchaguzi huo?

Swali hilo linakuwa muhimu kuwauliza watawala wetu wa CCM, kwa kuwa waangalizi wote wa nje ya nchi na wale wa ndani ya nchi walitoa taarifa zao kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki. Sasa inakuwaje mtu mmoja anayeitwa Jecha awe na fikra zake za kufikirika na fikra zake zitofautiane kabisa na wengine kuwa uchaguzi ule ulikuwa na kasoro chungu nzima?

4. Iweje Jecha avunje kanuni mojawapo muhimu sana ya natural justice inayosema kuwa MAN CAN NOT BE A JUDGE ON HIS OWN CASE?

Kwa kuwa katika 'kesi' hii ya uchaguzi huu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana tumeshuhudia Jecha akiwa mlalamikaji na wakati huo huo akiwa Polisi aliyefanya uchunguzi na baadaye akawa mwendesha mashitaka na hatimaye akawa Jaji na kuhukumu kuwa uchaguzi ule ulikuwa na kasoro chungu nzima kwa hiyo unastahili kurejewa wote!!!!!!

5. Hivi hao wasimamizi wa uchaguzi huko Zenji walikuwa 'machizi' hadi wafikie hatua ya kuwapa vyeti vya ushindi wawakalishi wote wa majimbo 54 kwenye Baraza, kama kweli uchaguzi ule ulikuwa umeharibika kupita kiasi?

6. Hivi huyo Jecha ambaye Umma wa watanzania unafahamu kuwa yupo mafichoni alikopelekwa na watawala wa CCM na akipewa ulinzi mkali kutoka vyombo vya usalama vya nchi. Hivi atausimamia uchaguzi huo akiwa huko mafichoni kwa kutumia remote control?!

Ni vyema huyo balozi Dr Mahiga aliyesoma hotuba ya Presidaa au Kurugenzi ya habari ya Ikulu ikatujibia maswali hayo machache.
 
Ni heri muovu mmoja akijiunga na watakatifu wengi, maana watambadilisha kuwa mtakatifu, kuliko msafi mmoja akijiunga na waovu wengi maana watamuambukiza uovu wao na atakuwa muovu zaidi na atashangaza wengi. Hayo tayari yamedhihirika. #CCM_ni_ileile.
 
" Zanzibar ina katiba yake, ina tume yake ya Uchaguzi, ina wimbo wake wa Taifa, ina jeshi lake , ina rais wake, ina bunge lake, ina mwenyekiti wake wa tume ambaye ni Mh.Jecha"
 
Hak
hakuna haja ya kupoteza pesa kurudia uchaguzi Zanzibar kwani matokeo ni Shein atakuwa mshindi wapende wasipende, hizo pesa wanazopoteza kwa uchaguzi wa maigizo ni bora zingetumika kwenye shughuri za maendeleo kuliko kufanya janbo la kudanganya Dunia.

Acha kujifanya unajua wewe sio Mzanzibar. Wazanzibar wenyewe wanasema kuwa hawaitaki CCM. Sasa basi kama ikiundwa tume huru ya uchaguzi wewe una uhakika gani kuwa Shein atashinda?
 
Mwingine kaandika Pumba eti ikiundwa tume huru halafu Jecha nd'o mwenyekiti inakuwaje?

Hivi mtu unapoambiwa tume huru, unaelewa nini au unapoambiwa neno "huru" unaelewa nini?

Maoni yangu viongozi wa CUF wakubali kurudia uchaguzi kwa kuundwa tume huru ili wathibitishe ushindi wao katika sanduku la kura. Hii ndio njia pekee kwa CUF kudhibitisha ushindi wao na kuwaumbua CCM. Sioni sababu kwa CUF kuogopa kurudia uchaguzi kama wanajua walishinda uchaguzi bila uwepo wa tume huru, sasa chini ya tume huru kinachowafanya waogope ni kitu gani?
 
Lkn hii ni kali jamani hata viti!
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1454993636.354469.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1454993636.354469.jpg
    39.7 KB · Views: 24
  • ImageUploadedByJamiiForums1454993671.793469.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1454993671.793469.jpg
    39.7 KB · Views: 23
  • ImageUploadedByJamiiForums1454993689.960467.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1454993689.960467.jpg
    37.6 KB · Views: 27
This is a joke kwa mabalozi ambao walituma waangalizi sehemu zote na kuridhika.
Kwanza kawakimbia mabalozi .
Sijawahi kusikia mtu kualika wageni halafu ukajifungia chumbani

Kwa hiyo unafagilia mabalozi kuliko presidaa wako?
 
Rais Magufuli ameyaeleza hayo katika hotuba yake kwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa Balozi Augustine Mahiga leo ikulu jijini Dar es salaam.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli amewaeleza mabalozi hao kuwa licha ya Tanzania kuwa nchi moja, Zanzibar ina mfumo wake wa siasa, ina serikali yake, Katiba yake na pia tume yake ya uchaguzi inayojitegemea.

Amesema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Amesema mazungumzo ya kutatua mgogoro huo yalifanyika bila mafanikio ambapo chama kikuu cha upinzani (CUF) kimeendelea kupinga uchaguzi wa marudio huku vyama vingine kikiwemo chama tawala vikionesha uhitaji wa uchaguzi huo wa marudio.

Amesema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo, na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.

Amewaeleza mabalozi hao kuwa serikali pamoja na watanzania walio wengi wangependa kuona CUF inathibitisha madai yake ya kushinda uchaguzi huo kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa marudio.

“Tunakiasa chama cha CUF kama ambavyo watanzania wengi wangependa kuona, kuthibitisha madai ya ushindi wao katika sanduku la kura, hakuna jinsi nyingine ya kutatua suala hili zaidi ya kukubali kufanya uchaguzi wa marudio” imesema sehemu ya hotuba hiyo.

Magufuli amewahakikishia mabalozi hao kuwa nchi ni salama na hali ya amani na utulivu ni ya kuridhisha katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa marudio.
Ukweli uko wazi kuwa mahafidhina wa Zanzibar hawataki kabisa Sir awe Rais,hivyo watamzuia kwa kila jinsi,kumlaumu Magufuli au Kikwete ni kazi bure.Hawa jamaa wanajuana na wana vitisho vya ajabu
 
Ukweli uko wazi kuwa mahafidhina wa Zanzibar hawataki kabisa Sir awe Rais,hivyo watamzuia kwa kila jinsi,kumlaumu Magufuli au Kikwete ni kazi bure.Hawa jamaa wanajuana na wana vitisho vya ajabu

Mkuu, tuambie ukweli kwa faida ya wengi hao Mahafidhina ni kina nani na wanatoka wapi ndani au nje ya CCM?
 
Mkutano na mabalozi ameukimbia pia? Tatizo ngeri magu inasumbua...lkn angezungumza kiswahili tu.
 
Mkuu, tuambie ukweli kwa faida ya wengi hao Mahafidhina ni kina nani na wanatoka wapi ndani au nje ya CCM?
Kwa faida ya wote mahafidhina ni genge la wanasiasa ambao kamwe hawakubali mwanasiasa yoyote atawale zanzibar isipokuwa yule aliyeshiriki kuleta mapinduzi ya kumwondoa sultani,hivyo hawaungi mkono kabisa mtanzania yoyote au mzanzibari yoyote mwenye asili ya kiarabu kutawala zenj,hivyo kwso wanakuona cuf kuwa ni vibaraka wa waarabu ambao wanataka kurudi kuitawala zenj kwa mlango wa nyuma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom