Rais Magufuli alia na ufisadi Jeshi la Polisi na Rushwa ofisi ya DPP

..Mzee Ibrahim Kaduma mwenye mtizamo kama wangu naye ana makusudi?

..je, cag Prof.Assad aliyesema nyumba ziliuzwa kifisadi naye ana uwezo mdogo?

nakushangaa kweli mkuu unavyobwabwaja hoja zako siku hizi
kwa hiyo magu ndiye aliyeuza nyumba
 
Si mlisema mnataka raisi dikteta

Imekuwaje tena
Kiongozi bora ni yule anayefuata Sheria kanuni na taratibu za nchi katika matamko na matendo yake. Kwa kifupi matamko ya Rais wetu huwa yanaacha utata zaidi badala ya suluhisho.
 
"Unapoona hali hiyo ya kila Siku Serikali inashindwa, halafu Siku hiyo hiyo unaenda kuiomba Serikali ikuwezeshe, kwa vyovyote Serikali inapata kigugumizi" Rais Magufuli, April 29, 2016.

Chanzo: ITV Habari.

Hapa kuna maswali ya kujiuliza,

1. Je, ni lazima Serikali ishinde kesi mahakamani?

2. Je, mawakili wa serikali sharti washinde kesi, ndipo wawezeshwe?

3. Je, kauli hii ya Rais haitasababisha unyamazishaji na ukandamizaji wa Haki mahakamani, kwa kesi zinazoihusu Serikali?

USHAURI: Baadhi ya Maneno yangekuwa yanapimwa kabla Kiongozi wa nchi hajayasema. Hapo ndipo unapoona umuhimu wa written speech.

Ninapata wasiwasi na uelewa wa Magufuli kuhusu utendaji wa mihimili hii mitatu yaani Serikali, Mahakama na Bunge. Angekuwa na uelewa anaopaswa kuwa nao rais asingetoa kauli tata kama hizi. Kwa kauli hii ni kama vile serikali kwa kuzihudumia mahakama inapaswa kulipwa fadhila kwa kushinda kesi zake-hii ni hatari kwa utawala wa kisheria unaoheshimu haki za binadamu. Serikali inakusanya kodi kuzihudumia mahakama na organs nyingine za nchi ni haki yake si favour suala la kushinda au kushindwa kesi halina uhusiano wowote na huduma inazopaswa kuzitoa seriakli kwa mihimili mingine ikiwemo mahakamani.

Hii si mara ya kwanza kutoa kauli tata kama hii ipo haja ya wasaidizi wake kumsaidia kwenye hili eneo anajidhalilisha na anatudhalilisha sisi anaotuongoza. Nadhani mtakumbuka aliwahi kutoa ofa kwa mahakama kwamba wakimaliza kesi za kodi za billion kadhaa zilikokuwa pending atawapa % ya kadhaa ya kile kitakachokusanywa toka kwenye hizo kesi. Hii ni kauli mbaya sana toka kinywani kwa rais kwani ni kama vile anawaeleza mahakimu wahukumu kesi in favour of serikali kwani wakifanya hivyo mgao wao unaongezeka. Na ni kama vile anasema serikali imekwishashinda kesi kabla ya hukumu.

Juzi alipokuwa anaongea na viongozi wa ccm ikulu aliwaambia mambo ambayo serikali imepanga kuyafanya mwaka ujao wa fedha. The way alivyokuwa anaongea ni kama vile budget imekwishapitishwa na bunge kitu ambacho bado. Bunge lina nafasi yake ni mhimili independent si rubber stamp. Mheshimwa ni vizuri ukajiorient vizuri namna hii mihimili mitatu inavyopaswa kufanya kazi.
 
..kwa hiyo unakubali kwamba ziliuzwa KIFISADI lakini unashauri "tumezee."??
JokaKuu
Hakuna asiyefahamu kama kuna maeneo mengine nyumba za serikali ziliuzwa below house market price kwa wakati huo lakini ikumbukwe kuwa waliouziwa hizo nyumba ni Watanzania ambao walitumikia taifa.

Sisi wakati wa operesheni vijiji 1974 tuliondolewa kwenye nyumba zetu kwa nguvu halafu zikachomwa moto na tulitupwa barabarani. Hatujapa fidia yoyote mpaka leo. Bora hawa Watanzania waliouziwa nyumba kwa below market price.

..kwanini una assume haziwezi kurudishwa serikalini?
Tanzania ya sasa inaendeshwa kisheria na nyumba ziliuzwa kisheria.

Serikali haiwezi kuwa mvunjaji wa sheria badala ya kuwa mlinda sheria.

Haziwezi kurudi serikalini kwa sababu ni mkataba wa serikali kisheria kwa wananchi wake. Nyumba hazikuuzwa kwa foreigners.

..je unamaanisha watawala wana KIBURI kilichopitiliza kinachowazuia kutubu na kurekebisha makosa yao?
Kurekebisha makosa na kurudisha nyumba ni vitu viwili tofauti.

Ninaamini watawala na wanasiasa wamejifunza kutokana na suala hili lakini usitegemee kupata samahani kutoka kwa watawala au wanasiasa.

Samahani ni neno gumu sana kutamkwa na watawala au wanasiasa.

Just imagine, Mpaka sasa hatujapata samahani kutoka kwa watawala au wanasiasa kutokana na kadhia ya operesheni vijiji 1974.

..Naomba unijibu swali hili: je ungekuwa na banda/gofu ktk prime area ungeuza kwa bei ya hasara/kijinga/kifisadi kama zilivyouzwa nyumba za serikali?
Kukaa na kufikiria ni kupoteza muda kwa sababu biashara ilifanyika na haiwezi kubadilishwa.

Kuna watanzania walinufaika na matunda ya kazi zao serikalini kwa kuuziwa hizo nyumba. Ninaamini wanakushangaa sana unapopiga kelele eti serikali izichukue!

Mazee, sorry kama wajanja walikuwahi kwenye dili la kununua hizo nyumba za serikali!
 
nakushangaa kweli mkuu unavyobwabwaja hoja zako siku hizi
kwa hiyo magu ndiye aliyeuza nyumba

..waziri mwenye dhamana na nyumba za serikali ni waziri wa ujenzi.

..kama Magu alikuwa waziri wa ujenzi basi yeye ndiye aliyeuza na ndiyo wa kwanza kuwajibika kwa jambo lolote lilokwenda kombo.

..sasa kama wewe unamfahamu waziri tofauti aliyeuza nyumba zile nakuomba umtaje.

NB:

..uamuzi unaweza kufanywa na baraza la mawaziri, lakini mtekelezaji huwa ni waziri wa wizara inayohusika.

..kama waziri hakubaliani na uamuzi wa baraza la mawaziri anatakiwa kujiuzulu.

..pia waziri mhusika ndiye mjenga hoja wa masuala na ekta anayoisimamia ktk vikao vya baraza la mawaziri.
Cc MsemajiUkweli
 
Magufuli yupo sahihi, kila kazi ina tageti yake haiwezekani wakili wa serikali kesi zote unazosimamia unashindwa sasa faida yako nini kam sio kula mshahara bure.
Yaani kusema ukweli inakera sana. Maana kushindwa kwao mwisho wa siku wanaoumia ni sie wananchi pale aliyekuwa anashitakiwa akija kudai fidia
 
JokaKuu
Hakuna asiyefahamu kama kuna maeneo mengine nyumba za serikali ziliuzwa below house market price kwa wakati huo lakini ikumbukwe kuwa waliouziwa hizo nyumba ni Watanzania ambao walitumia taifa.

Sisi tuliondolewa kwenye nyumba zetu na kwenda kuwekwa barabarani wakati wa operesheni vijiji. Hatujapa fidia yoyote mpaka leo. Bora hawa Watanzania waliouziwa nyumba kwa below market price.

Tanzania ya sasa inaendeshwa kisheria na nyumba ziliuzwa kisheria.

Serikali haiwezi kuwa mvunjaji wa sheria badala ya kuwa mlinda sheria.

Haziwezi kurudi serikalini kwa sababu ni mkataba wa serikali kisheria kwa wananchi wake. Nyumba hazikuuzwa kwa foreigners.

Kurekebisha makosa na kurudisha nyumba ni vitu viwili tofauti.

Ninaamini watawala na wanasiasa wamejifunza kutokana na suala hili lakini usitegemee kupata samahani kutoka kwa watawala au wanasiasa.

Samahani ni neno gumu sana kutamkwa na watawala au wanasiasa.

Just imagine, Mpaka sasa hatujapata samahani kutoka kwa watawala au wanasiasa kutokana na kadhia ya operesheni vijiji 1974.

Kukaa na kufikiria ni kupoteza muda kwa sababu biashara ilifanyika na haiwezi kubadilishwa.

Kuna watanzania walinufaika na matunda ya kazi zao serikalini kwa kuuziwa hizo nyumba. Ninaamini wanakushangaa sana unapopiga kelele eti serikali izichukue!

Mazee, sorry kama wajanja walikuwahi kwenye dili la kununua hizo nyumba za serikali!

..Duh!!

..wapo waTz wamefaidika kwa ufisadi wa iptl, escrow, hati fungani, etc etc

.. Je, tunapaswa kufumbia macho ufisadi huo kwasababu kuna wachache wachoyo miongoni mwetu wamefaidika?
 
..Duh!!

..wapo waTz wamefaidika kwa ufisadi wa iptl, escrow, hati fungani, etc etc

.. Je, tunapaswa kufumbia macho ufisadi huo kwasababu kuna wachache wachoyo miongoni mwetu
wamefaidika?
Unakosea unapoanza kulinganisha uuzaji wa nyumba za serikali kwa watanzania wengi na wizi wa mali ya watanzania uliofanywa na watu wachache ambao wengine ni wageni.
 
Tunauhitaji sana huu udikiteta ili mambo yakae sawa. Maana huko unaposema sheria zinafuatwa (mahakamani) ni rushwa tu. Ngoja awanyooshe kwanza akili ikae sawa ndo hizo sheria zitafanya kazi.

By the way....JPM alikuwa anaongea na watu gani? Ukipata jibu then utajua alimaanisha kitu gani!!!!!
 
WIKI moja baada ya Serikali kutangaza kuanzishwa kwa Divisheni ya Mahakama ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu, Rais John Magufuli amewaibukia mawakili wa Serikali, akiwatuhumu kwa kushirikiana na mawakili wa wahalifu ili Serikali ishindwe kesi. Aidha amewaonya polisi kwa kuingia mikataba inayotia mashaka baina yao na wawekezaji.

Mahakama ya ufisadi inatarajiwa kutumika kushughulikia watuhumiwa wa rushwa na ufisadi, wakiwemo waliokwisha tumbuliwa, lakini kesi zake zinatarajiwa kuanza kunguruma Julai mwaka huu.

Akizungumza mkoani Dodoma jana wakati akifungua kikao kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa Serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi, Rais Magufuli alisema mawakili hao wakiona kesi inayohusu fedha imeingia, wanasema ‘dili’ limeingia.

“Kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache, nasema wachache... Panapokuwa na kesi inayohusu fedha, wana misemo yao wanasema dili limepatikana.

“Saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani wanashirikiana na mawakili wa Serikali na mawakili wanaomtetea mhalifu na wanaposhirikiana siku zote Serikali inashindwa,” alisema.

Alionya kuwa hali hiyo inapoonekana kila siku Serikali inashindwa katika kesi, kunakuwa na kigugumizi cha kuwezesha mawakili hao pale wanapopeleka maombi. “Niwaombe mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslahi ya nchi mbele,” alisema na kuongeza kuwa amekuwa akisikitishwa na vitendo vya Serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.

Ulaji wapelelezi Awali kabla ya kutoa hotuba yake, Rais Magufuli aliwapa nafasi makamanda na mawakili wafawidhi hao kutoa maoni yao juu ya changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu wa kufanya upelelezi na kuendesha mashitaka.

Katika maoni yao, watendaji hao wanaohusika zaidi katika kupeleleza na kushitaki watuhumiwa mahakamani, walidai ufinyu wa bajeti ndio sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa kesi hizo.

Akizungumzia changamoto hiyo, Rais Magufuli aliahidi kuwatafutia fedha watendaji hao kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hizo, lakini akawataka fedha zitakazotafutwa zitumike vizuri.

Mikataba ya hovyo Akisisitiza umuhimu wa fedha hizo kutumika vizuri, Rais Magufuli alisema kuna taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi, limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.

Alitoa mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununua vifaa na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.

“Oysterbay pale ni eneo ambalo ni zuri sana, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba mnayoijua nyinyi, mkapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa.

“Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka kitegauchumi na polisi wenu wakakaa pale?

“Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu. Nataka muelewe na muelewe ukweli mwelekeo ninaoutaka mimi,” alisema Rais Magufuli.

Alisisitiza kwa Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa ambazo zimekuwa zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maofisa wa Polisi kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa ujambazi.

Hata hivyo, Rais Magufuli alilipongeza jeshi hilo na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na ametaka apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha vyombo hivyo.
 
Tatizo hatuna mahakama huru. Kama tungekuwa na mahakama huru, msemaji wa makakama angekuwa tayari kakemea matamshi ya hatari kama aliyotoa Magufuli ya kuingilia uhuru wa mahakama. Bahati mbaya hata majaji wenyewe wanateuliwa na Rais hivyo hawana uthubutu wa kumkosoa hata akiwaingilia. Bunge nalo badala ya kuisimamia serikali imegeuka na kuwa chombo cha kuitetea.
Unakosea unapoanza kulinganisha uuzaji wa nyumba za serikali kwa watanzania wengi na wizi wa mali ya watanzania uliofanywa na watu wachache ambao wengine ni wageni.
Duh, kwa hiyo kuna ufisadi unaokubalika? Je hii ndiyo sera mpya ya CCM ya Magufuli? Nadhani tunakoelekea si kuzuri kabisaa. Ufisadi wa nyumba za serikali umefumbiwa macho, ufisadi wa kivuko cha Bagamoyo umefumbiwa macho, ESCROW umefumbiwa macho...kwa mtindo huu tusione ajabu Lugumi kufumbiwa macho
 
Nahisi wewe ni kati ta wale mnaowachukia walimu kupanda daladala bure!, ila pole kwa kukosa ufahamu wa kile kinachoandikwa.

Sasa kama tayari yumo humu kwa nini unataka mchangiaji am_tag? Nyie watu sijui kitu gani kimewaleta JF, si heri mngebakia huko huko kwenye mipasho? Kama kitu hukijui si heri uulize tu uambiwe?

Kwani ni Mbowe ndiye alisimamia utekelezaji huo kiasi cha kuwagawia hadi ndugu zake na washikaji wake baadhi ya nyumba za serikali? Utetezi mwingine hata hauna mantiki yoyote.
 
Unakosea unapoanza kulinganisha uuzaji wa nyumba za serikali kwa watanzania wengi na wizi wa mali ya watanzania uliofanywa na watu wachache ambao wengine ni wageni.
JokaKuu nilikuwa nafuatilia majadiliano yenu, nashukuru umesimama katika hoja hadi sasa wanatengeneza mazingira ya dhambi ndogo na dhambi kubwa!

Eti nyumba za serikali ziliuzwa kwa Watanzania!

Nyumba za serikali waliuziana na Magufuli alikuwa kiungo muhimu katika hilo. Period!

Magufuli alikuwepo serikalini miaka 20, nyumba za serikali prime area akaziuza leo anapata wapi moral authority ya kukemea polisi ikiwa alishiriki kuuza nyumba tena kwa bei ya kutupa!

Alishiriki kuuza nyumba za umma tena wakiuziana wao kwa wao na kuna taarifa ziliuzwa hadi kwa ushemeji na alikuwa kiongozi wa zoezi hilo!

Hoja hapa ni kuwa anapata wapi nguvu ya kukemea uhalifu wa Obei ikiwa aliuza nyumba za obei hapo hapo! Aliuza nyumba mawaziri wakakaa Hotelini !!!!

aombe radhi kwa kuuza nyumba, halafu twende mbele

Pili, unamsikia la LUGUMI analiongelea kwa mafumbo. Tulisema hili ni gumu sana kwa maana linawagusa , hawezi kukabiliana nao. Anatumbua akina Kabwe kwa mwendo wa hadharani, uhalifu mwingine anaongelee kwenye mikutano nyuma ya pazia na kamera

Lugumi ita define legacy yake na uwezo wake wa kupambana na maouvu
LUGUMI ita define anaongea nini na anatenda nini.
 
..nimesikiliza maelezo ya sumaye, hayajitoshelezi.

..kama wameweza kurudisha mashamba na viwanda walivyobinafsisha basi wanaweza kurudisha na nyumba walizoiba.

..JIZI KUU LA NYUMBA ZA SERIKALI bado lipo hai. Kwa hiyo wapenda haki na ukweli tutaendelea kusema tena na tena.

..hatuwezi kuchoka kusema ukweli.
Ni ukweli mtupu, Magufuli rudisha nyumba zetu. LUGUMI isemwe hadharani isinong'wenwe nyuma ya pazia.
 
JokaKuu nilikuwa nafuatilia majadiliano yenu, nashukuru umesimama katika hoja hadi sasa wanatengeneza mazingira ya dhambi ndogo na dhambi kubwa!

Eti nyumba za serikali ziliuzwa kwa Watanzania!

Nyumba za serikali waliuziana na Magufuli alikuwa kiungo muhimu katika hilo. Period!

Magufuli alikuwepo serikalini miaka 20, nyumba za serikali prime area akaziuza leo anapata wapi moral authority ya kukemea polisi ikiwa alishiriki kuuza nyumba tena kwa bei ya kutupa!

Alishiriki kuuza nyumba za umma tena wakiuziana wao kwa wao na kuna taarifa ziliuzwa hadi kwa ushemeji na alikuwa kiongozi wa zoezi hilo!

Hoja hapa ni kuwa anapata wapi nguvu ya kukemea uhalifu wa Obei ikiwa aliuza nyumba za obei hapo hapo! Aliuza nyumba mawaziri wakakaa Hotelini !!!!

aombe radhi kwa kuuza nyumba, halafu twende mbele

Pili, unamsikia la LUGUMI analiongelea kwa mafumbo. Tulisema hili ni gumu sana kwa maana linawagusa , hawezi kukabiliana nao. Anatumbua akina Kabwe kwa mwendo wa hadharani, uhalifu mwingine anaongelee kwenye mikutano nyuma ya pazia na kamera

Lugumi ita define legacy yake na uwezo wake wa kupambana na maouvu
LUGUMI ita define anaongea nini na anatenda nini.
Hizi hoja za kusema Rais Magufuli alikuwepo serikali kwa miaka 20 na kwa maana hiyo hawezi kupambana na maovu ni kama mnajaribu kuturudisha kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Huyo ambaye hakuwepo serikali ambaye unataka tumtambue kama angeweza kupambana na uovu mbona hakuchaguliwa na wananchi wengi?

Uchaguzi ulifanyika na wananchi wengi wakamchagua Magufuli kuwa Rais wao wa Tanzania, bahati nzuri au mbaya huyo mtu wako hakuchaguliwa na wananchi wengi.

Hoja za kusema hiki au kile kita define uongozi wa serikali ya Rais Magufuli ni kujifurahisha tu kifikra kwa sababu wewe kura yako ni moja tu katika sanduku la kura.

Nani amekuambia kuwa Rais anafanya kazi ili kuwa defined?

Kama uhalifu nwingine anaongelea nyuma ya pazia na kamera kama unavyodai, umejuaje suala la Lugumu ameliongelea nyuma ya pazia na kamera?

Kampeni za Uchaguzi zimeisha na Rais wa Tanzania ni John Magufuli!

Get used to it.
 
..ndugu yangu ule ulikuwa ni WIZI.

..Sasa lazima haya MAJIZI tuyaseme tu hakuna kuoneana aibu.

..huu ni wakati wa kutumbua majipu. Kila mtu atumbue jipu kwa nafasi yake.
 
Back
Top Bottom