Rais Magufuli alia na ufisadi Jeshi la Polisi na Rushwa ofisi ya DPP

Sawa mkulu nakubaliana na wewe,.......... ila kuna vitu vinatia mashaka hata kama sio mwanasheria kama hii kesi ya Mr, Muhando. ...........,vidhibitisho ubaoni halafu unaambiwa uchunguzi haukukamilika hii ni kweli au na wewe ni walewale!?
Sheria ichukue mkondo wake na sio matakwa ya mtu.
 
Kwa Ostabay namkumbuka mkuu wa kituo mmoja alifahamika kama Mr, Kalinga. enzi hizo ........ huyu alikuwa kama Mungu mtu pale sitokaa nimsahau maishani
 
Nimeiskia hii habari muda huu kupitia Channel 10 ila najiuliza ni kwanini Magu anashindwa kabisa kugusua sakata la Lugumi!

Alafu hivi Taasisi ya serikali inaruhusiwa kutumia hati ya ardhi inayomiliki kuchukua mkopo benki?Au mimi sijaelewa hapa?
Amekugusaa eeh anakuja
 
Mkuu, mnada wa nyumba za serikali haukukupata au uliwahiwa na wajanja wakachukua nyumba ambayo ulitegemea utaipata?

Nimekuuliza kwa sababu ikianzishwa hoja kuhusu nyumba za serikali huwa unaibuka haraka kuja kutoa mchango kuhusu uuzaji wa nyumba za serikali huku ukimlaumu Rais Magufuli wakati suala hili lilishatolewa maelezo na Frederick Sumaye.

Suala la uuzaji wa nyumba za serikali ni sawa na jini lililotoka nje ya chupa na hauwezi kulirudisha, kwa maana kuwa, hata ukipiga kelele hakuna atakayezirudisha tena serikalini. Hiyo ilishatoka! Chill out!

Hii ni sawa na mtu amekufa huku ukimdai pesa na hakuna uwezekano wa kuzipata pesa zako halafu unaanza kulalamika kila mara kwa watu kuhusu deni lako kwa marehemu. A pure waste of time and energy!

..nimesikiliza maelezo ya sumaye, hayajitoshelezi.

..kama wameweza kurudisha mashamba na viwanda walivyobinafsisha basi wanaweza kurudisha na nyumba walizoiba.

..JIZI KUU LA NYUMBA ZA SERIKALI bado lipo hai. Kwa hiyo wapenda haki na ukweli tutaendelea kusema tena na tena.

..hatuwezi kuchoka kusema ukweli.
 
Ukisoma hiyo press release utagundua kuwa kagusia hiyo Lugumi, aliposema "..mikataba ya mashaka inayotiwa saini kati ya jeshi la polisi na wawekezaji.."
Wengineee washazoeaa copy n paste awatakikuumiza akili n shidaa
 
..nimesikiliza maelezo ya sumaye, hayajitoshelezi.

..kama wameweza kurudisha mashamba na viwanda walivyobinafsisha basi wanaweza kurudisha na nyumba walizoiba.

..JIZI KUU LA NYUMBA ZA SERIKALI bado lipo hai. Kwa hiyo wapenda haki na ukweli tutaendelea kusema tena na tena.

..hatuwezi kuchoka kusema ukweli.
Mtu mwenye hekima na busara anafahamu kama umesikiliza maelezo na hayajitoshelezi basi unarudi tena kule yaliyotolewa hayo maelezo ili ukafafanuliwe vizuri ili yajitosheleze. Rudi kwa Sumaye.

Kukaa hapa na kupiga kelele bila kurudi kwa yule aliyekupa maelezo ambayo hayajitoshelezi ninadhani kwa watu wenye fikra pana watakuona ni mtu wa ajabu sana.

Kupiga kelele huku ukisema fulani ni mwizi bila vielelezo au bila kuchukua hatua kisheria ni kama kujifurahisha au kufurahisha genge la watu wenye fikra finyu.

Ukweli kwa suala unalopigia kelele hautafutwi kwa kupiga kelele, bali unatafutwa kisheria.

Anza kwanza kwa Frederick Sumaye ambaye yuko karibu na wewe kiitikadi na Mshauri Mkuu wa Chama.

By the way, hujajibu swali langu, Nimekuuliza, Mnada wa nyumba za serikali haukukupata au uliwahiwa na wajanja wakachukua nyumba ambayo ulitegemea utaipata?
 
Mmetuchosha na kujifanya kujua visheria vyenu hivi vya tumaini,saut,ruco.mwacheni RAIS afanye kazi jamani,nyie kila siku kukosoa tu yaani hamna jema lolote mnalotoka nalo kuhusu kauli ya MH.MAGUFULI?

Mkuu, Baadhi ya wana sheria ndio wahusika wakuu wa kudraft mikataba ya kihuni na makashifa chungu mzima - some of ' em are so arrogant mpaka wanafikia hatua ya kuamini kwamba they own this country!!!

Leo Dk.Magufuli kasema yale yote ambayo watanzania wenye akili timamu walikuwa wanayajua kwa muda mrefu lakini walikuwa hawajui wayasemee wapi.

Nikiona baadhi ya members wanamjia juu JPJM siwaelewi kabisa, kila kitu alicho sema ni sahihi - mara ngapi wananchi tumeshuhudia Serikali ikishindwa kesi ambazo hata mtoto wa darasa la saba anajua kwamba kilicho fanyika pale ni usanii mtupu - yaani Jaji, Jury, mawakili wa Serikali na wawakili wa watuhumiwa wote wanakuwa compromised kuishinda Serikali mahakamani!!

Vices tajwa hapo juu zinatumika sana kuvuruga kesi za RAIA ambao hawana fedha za kutosha kuwalipa mawakili wa utetezi, hata kama kesi yako ni straight 4ward inakuwa turned upside down inside out! Kama tuna nia thabiti ya kuendeleza Taifa letu basi upande wa Judicially Dk.Magufuli atapashwa kulifanyia a makeover ya hali ya juu - the soonest the better.
 
Mtu mwenye hekima na busara anafahamu kama umesikiliza maelezo na hayajitoshelezi basi unarudi tena kule yaliyotolewa hayo maelezo ili ukafafanuliwe vizuri ili yajitosheleze. Rudi kwa Sumaye.

Kukaa hapa na kupiga kelele bila kurudi kwa yule aliyekupa maelezo ambayo hayajitoshelezi ninadhani kwa watu wenye fikra pana watakuona ni mtu wa ajabu sana.

Kupiga kelele huku ukisema fulani ni mwizi bila vielelezo au bila kuchukua hatua kisheria ni kama kujifurahisha au kufurahisha genge la watu wenye fikra finyu.

Ukweli kwa suala unalopigia kelele hautafutwi kwa kupiga kelele, bali unatafutwa kisheria.

Anza kwanza kwa Frederick Sumaye ambaye yuko karibu na wewe kiitikadi na Mshauri Mkuu wa Chama.

By the way, hujajibu swali langu, Nimekuuliza, Mnada wa nyumba za serikali haukukupata au uliwahiwa na wajanja wakachukua nyumba ambayo ulitegemea utaipata?

..natofautiana na sumaye ktk suala hili.

..Mzee Ibrahim Kaduma, mwana ccm mkongwe, alisema uuzwaji wa nyumba za serikali ni doa ktk rekodi ya
Dr.Magufuli.

..kwa hiyo nakubaliana na Mzee Kaduma ktk suala hili, na zaidi alipomtaka Raisi atubu na kuzirudisha serikalini nyumba zile.

..vilevile nakubaliana na CAG Prof.Assad, ambaye aliuita uuzwaji wa nyumba zile kuwa ni "political entrepreneurship."

..Raisi anasema polisi wamekosea kuuza eneo la police mess o'bay. Je, yeye alikuwa sahihi kuuza nyumba za serikali zilizokuwa ktk prime areas kwa bei ya kutupa??
 
Mh.rais yuko sahihi kabsa ni kipofu tu atakayepinga, hao mawakili na majaji si malaika waweza kupokea rushwa ili kuijumu serikali,
 
naona akina REX ATTONEY wamejipanga ili kurescue ELLITE group lao . hivi ni wapi hapa tanzania umesikia tajiri/ mwenye pesa amehukumiwa , mleta mada huoni nchi yetu inabubujikwa na uonevu kwa mgongo wa haya makanjanja wa kujifanya wanaijua sheria , juzi hadi kwenye escrow majaji walipambana kwenye escrow kuhakikisha IPTL haijadiliwi , yote hayo ni kwa ajili ya fedha
 
..natofautiana na sumaye ktk suala hili.

..Mzee Ibrahim Kaduma, mwana ccm mkongwe, alisema uuzwaji wa nyumba za serikali ni doa ktk rekodi ya
Dr.Magufuli.

..kwa hiyo nakubaliana na Mzee Kaduma ktk suala hili, na zaidi alipomtaka Raisi atubu na kuzirudisha serikalini nyumba zile.

..vilevile nakubaliana na CAG Prof.Assad, ambaye aliuita uuzwaji wa nyumba zile kuwa ni "political entrepreneurship."

..Raisi anasema polisi wamekosea kuuza eneo la police mess o'bay. Je, yeye alikuwa sahihi kuuza nyumba za serikali zilizokuwa ktk prime areas kwa bei ya kutupa??
JokaKuu
You are mission is impossible!

Huyo Mzee Ibrahim Kaduma kuna uwezekano na yeye dili la kupata nyumba lilimpita kushoto au alizidiwa ujanja ambapo nyumba aliyokuwa akitegemea kuipata ikachukuliwa na wajanga.

Hoja yako haina tofauti na oparesheni vijiji vya ujamaa ambapo tulijikuta tunapoteza maeneo yetu mazuri lakini mpaka leo hatujapata fidia au kurudishiwa na serikali. Hatuwezi kuendelea kupiga kelele kuhusu fidia au turudishiwe maeneo yetu kwa sababu haiwezi kutokea.

Hata wewe unapoteza muda wako kupiga kelele kuhusu uuzaji wa nyumba za serikali kwa sababu haziwezi kurudishwa serikali. Hiyo ilitoka and finished.

Fikiria kwa sasa kilichoko mbele yako kimaisha kuliko kuishi kwenye dhana ya historia ambayo huwezi kuibadilisha.

Nyumba za serikali zilizouzwa haziwezi kurudishwa serikalini lakini kumbuka pia, waliouziwa ni Watanzania ambao kwa njia moja au nyingine walitoa mchango serikalini kama wafanyakazi na walipa kodi. Finito
 
dar kichwa ngumu kweli sijui ni makusudi au ni uwezo mdogo ...nani aliuza nyumba za serikali mbona watu wamefafanua sana hiyo hoja , sasa maamuzi ya seikali utapingana nayo ,
magufuli wala hakuwa mkuu wa shughuli za serikali
 
naona akina REX ATTONEY wamejipanga ili kurescue ELLITE group lao . hivi ni wapi hapa tanzania umesikia tajiri/ mwenye pesa amehukumiwa , mleta mada huoni nchi yetu inabubujikwa na uonevu kwa mgongo wa haya makanjanja wa kujifanya wanaijua sheria , juzi hadi kwenye escrow majaji walipambana kwenye escrow kuhakikisha IPTL haijadiliwi , yote hayo ni kwa ajili ya fedha
Sheria ichukue mkondo wake, na katika hilo sio lazima Serikali ishinde. Tuiache sheria iwe determinant na tukubali outcome ya kisheria mahakamani.
 
"Unapoona hali hiyo ya kila Siku Serikali inashindwa, halafu Siku hiyo hiyo unaenda kuiomba Serikali ikuwezeshe, kwa vyovyote Serikali inapata kigugumizi" Rais Magufuli, April 29, 2016.

Chanzo: ITV Habari.

Hapa kuna maswali ya kujiuliza,

1. Je, ni lazima Serikali ishinde kesi mahakamani?

2. Je, mawakili wa serikali sharti washinde kesi, ndipo wawezeshwe?

3. Je, kauli hii ya Rais haitasababisha unyamazishaji na ukandamizaji wa Haki mahakamani, kwa kesi zinazoihusu Serikali?

USHAURI: Baadhi ya Maneno yangekuwa yanapimwa kabla Kiongozi wa nchi hajayasema. Hapo ndipo unapoona umuhimu wa written speech.
Kila kesi inavigezo vyake vya kuipa ushindi. Sasa kama mpelelezi na mwendesha shitaka anashindwa kuita mashahidi wa msingi mahakamani au kushindwa kuchora ramani ya tukio kwa wakati wasilaumiwe?
Anachokisema Rais ni kwa wale wanaoifanya jinai ni biashara. Kuna mwendesha mashitaka aliwahi ondoa kesi mahakamani kisa mpelelezi hakuandika kwenye kumbukumbu yake ya upelelezi jambo ambalo si takwq la kisheria bali ni utamaduni mzuri tu wa kufanya kazi. Haya yanapotokea haya usilaumu.
Ingependeza ukaweka na mazingira ambayo Rais kasema kesi huharibiwa. Si kila kesi ikishindwa mahakamani ni kwa zile ambazo polisi pp wamefanya uzembe wa wazi kushjndwa kuithibitisha.
 
JokaKuu
You are mission is impossible!

Huyo Mzee Ibrahim Kaduma kuna uwezekano na yeye dili la kupata nyumba lilimpita kushoto au alizidiwa ujanja ambapo nyumba aliyokuwa akitegemea kuipata ikachukuliwa na wajanga.

Hoja yako haina tofauti na oparesheni vijiji vya ujamaa ambapo tulijikuta tunapoteza maeneo yetu mazuri lakini mpaka leo hatujapata fidia au kurudishiwa na serikali. Hatuwezi kuendelea kupiga kelele kuhusu fidia au turudishiwe maeneo yetu kwa sababu haiwezi kutokea.

Hata wewe unapoteza muda wako kupiga kelele kuhusu uuzaji wa nyumba za serikali kwa sababu haziwezi kurudishwa serikali. Hiyo ilitoka and finished.

Fikiria kwa sasa kilichoko mbele yako kimaisha kuliko kuishi kwenye dhana ya historia ambayo huwezi kuibadilisha.

Nyumba za serikali zilizouzwa haziwezi kurudishwa serikalini lakini kumbuka pia, waliouziwa ni Watanzania ambao kwa njia moja au nyingine walitoa mchango serikalini kama wafanyakazi na walipa kodi. Finito

..kwa hiyo unakubali kwamba ziliuzwa KIFISADI lakini unashauri "tumezee."??

..kwanini una assume haziwezi kurudishwa serikalini?

..je unamaanisha watawala wana KIBURI kilichopitiliza kinachowazuia kutubu na kurekebisha makosa yao?

..Naomba unijibu swali hili: je ungekuwa na banda/gofu ktk prime area ungeuza kwa bei ya hasara/kijinga/kifisadi kama zilivyouzwa nyumba za serikali?
 
naona akina REX ATTONEY wamejipanga ili kurescue ELLITE group lao . hivi ni wapi hapa tanzania umesikia tajiri/ mwenye pesa amehukumiwa , mleta mada huoni nchi yetu inabubujikwa na uonevu kwa mgongo wa haya makanjanja wa kujifanya wanaijua sheria , juzi hadi kwenye escrow majaji walipambana kwenye escrow kuhakikisha IPTL haijadiliwi , yote hayo ni kwa ajili ya fedha
Yawezekana kabisa Rais alikuwa na point muhimu ya kusema, lakini kwa namna ilivyokuwa presented, inaleta shida sana kuielewa mantiki ya kiklichotamkwa.
 
Sheria ichukue mkondo wake, na katika hilo sio lazima Serikali ishinde. Tuiache sheria iwe determinant na tukubali outcome ya kisheria mahakamani.

wew unakomaa na sheria nimekuuliza umeshwahi kusikia mwenye fedha au tajiri yeyote amefungwa ukiachilia mbali akina pesa mbili waliownda kufanya kazi palestina ? sheria zinaegemea kwa masikini tuu . huo mkondo wa sheria unaosema ni upi wa kuwaonea maskin na wenye fedha zao za kuhonga kutopatikana na hatia hata kama kila kitu kipo clear ?
 
dar kichwa ngumu kweli sijui ni makusudi au ni uwezo mdogo ...nani aliuza nyumba za serikali mbona watu wamefafanua sana hiyo hoja , sasa maamuzi ya seikali utapingana nayo ,
magufuli wala hakuwa mkuu wa shughuli za serikali

..Mzee Ibrahim Kaduma mwenye mtizamo kama wangu naye ana makusudi?

..je, cag Prof.Assad aliyesema nyumba ziliuzwa kifisadi naye ana uwezo mdogo?
 
wew unakomaa na sheria nimekuuliza umeshwahi kusikia mwenye fedha au tajiri yeyote amefungwa ukiachilia mbali akina pesa mbili waliownda kufanya kazi palestina ? sheria zinaegemea kwa masikini tuu ?
Bila sheria hata maskini hawezi kupata Haki. Utawala wa sheria hauwezi kulinganishwa na matamko tata yenye mlengwa wa kiimla.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom