Rais Magufuli alia na ufisadi Jeshi la Polisi na Rushwa ofisi ya DPP

..ndugu yangu ule ulikuwa ni WIZI.
Tena wizi wa mchana kweupee! Hasara taifa limepata ni kubwa kuliko tunavyofikiria.
..Sasa lazima haya MAJIZI tuyaseme tu hakuna kuoneana aibu.
Ni kweli kabisa, hatukubali kufungwa midomo...kuyaonea aibu haya majizi ni dhambi kubwa pia.
..huu ni wakati wa kutumbua majipu. Kila mtu atumbue jipu kwa nafasi yake.
Bahati mbaya mtumbuaji naye ni jipu. Kwa nafsi zetu tutaendelea kupiga kelele hadi watu wote wazinduke.
 
Tena wizi wa mchana kweupee! Hasara taifa limepata ni kubwa kuliko tunavyofikiria.

Ni kweli kabisa, hatukubali kufungwa midomo...kuyaonea aibu haya majizi ni dhambi kubwa pia.

Bahati mbaya mtumbuaji naye ni jipu. Kwa nafsi zetu tutaendelea kupiga kelele hadi watu wote wazinduke.

..hii nchi imeoza.

..kwamba mtumbuaji majipu naye ana jipu ni kielelezo cha wapi tumefika kama taifa.

..humu JF tunaye MsemajiUkweli lakini anashambulia wachangiaji wanaosema ukweli!!
 
Tatizo hatuna mahakama huru. Kama tungekuwa na mahakama huru, msemaji wa makakama angekuwa tayari kakemea matamshi ya hatari kama aliyotoa Magufuli ya kuingilia uhuru wa mahakama. Bahati mbaya hata majaji wenyewe wanateuliwa na Rais hivyo hawana uthubutu wa kumkosoa hata akiwaingilia. Bunge nalo badala ya kuisimamia serikali imegeuka na kuwa chombo cha kuitetea.

Mahakama ingekuwa huru na ya haki hapo sawa. Lakini mahakama huru halafu ya kifisadi, hapo hapana. Sasa ni kipindi cha mpito. Na mzani sawia ni kati ya Mahakama huru na fisadi AU Mahakama isiyo huru bila ufisadi. Chaguo ni lako. Lakini mimi naona ni bora JPM awakaripie, hata kuwaingilia ilihali lengo lake ni safi. Kumbuka Rais wa Tanzania ana nguvu kubwa sana, hata hao wanaodhani hawezi kutumbua mijipu mingine tumpe huo muda anaosema.
 
..hii nchi imeoza.
Nikikumbuka chaguo la mungu Kikwete alivyoingia madarakani kwa kasi ari na nguvu mpya pamoja na sifa kem kem za kutokuwa na mbia kwenye Urais. Leo hao hao waliokuwa mstari wa mbele kumsifia sasa hawataki hata kusikia jina lake. Bahati nzuri bado tupo tuliotazama mbele na kusema hapana hapa tumepata gharasha. Tulipiga kelele toka anaapishwa lakini tuliambiwa tumpe muda...matokeo yake tukapoteza miaka kumi.
..kwamba mtumbuaji majipu naye ana jipu ni kielelezo cha wapi tumefika kama taifa.
Kwamba kuna watu wako tayari kufumbia macho ufisadi wa wazi kabisa kama uuzwaji wa nyumba za serikali, ufisadi wa wazi kabisa uliogubika ununuzi wa kivuko chakavu, ufisadi wa mabilioni uliohusisha Tanroad...kwa sababu mhusika mkuu kawa mtumbuaji majipu! Kama ni kulogwa, kweli tumelogeka.
..humu JF tunaye MsemajiUkweli lakini anashambulia wachangiaji wanaosema ukweli!!
Kwa namna huyo anayejiita MsemajiUkweli anavyohangaika kutetea jipu moja kunatuondolea wasiwasi kwamba hatujakosea, kisu kinagonga kwenye mfupa.
 
Nimeishiwa ladha ya kumsikiliza kutokana na kukaa kimya kwake kwenye suala la Bunge.
 
Hizi hoja za kusema Rais Magufuli alikuwepo serikali kwa miaka 20 na kwa maana hiyo hawezi kupambana na maovu ni kama mnajaribu kuturudisha kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Huyo ambaye hakuwepo serikali ambaye unataka tumtambue kama angeweza kupambana na uovu mbona hakuchaguliwa na wananchi wengi?

Uchaguzi ulifanyika na wananchi wengi wakamchagua Magufuli kuwa Rais wao wa Tanzania, bahati nzuri au mbaya huyo mtu wako hakuchaguliwa na wananchi wengi.

Hoja za kusema hiki au kile kita define uongozi wa serikali ya Rais Magufuli ni kujifurahisha tu kifikra kwa sababu wewe kura yako ni moja tu katika sanduku la kura.

Nani amekuambia kuwa Rais anafanya kazi ili kuwa defined?

Kama uhalifu nwingine anaongelea nyuma ya pazia na kamera kama unavyodai, umejuaje suala la Lugumu ameliongelea nyuma ya pazia na kamera?

Kampeni za Uchaguzi zimeisha na Rais wa Tanzania ni John Magufuli!

Get used to it.
Sijui hayo mengine yametoka wapi. Hoja iliyoko mezani ambayo unajaribu kuikwepa ni hii, Rais Magufuli alishiriki katika uuzaji wa nyumba za serikali
1. Anapata wapi moral authority ya kukemea ya Polisi Osterbay, kabla hajatuomba radhi kwa kuuza nyumba zetu?
2. Anapouzngumzia mikataba ya jeshi la Polisi tena akizungumzia Lugumi kwa kuzunguka analalamika kwa nani?
3. Kwanini hawatumbui kama akina Kabwe?

Mwisho, Je si kweli alikuwa katika serikali miaka 20? Je si kweli kuwa alishiriki uuzwaji nyumba za serikali?
 
Sijui hayo mengine yametoka wapi. Hoja iliyoko mezani ambayo unajaribu kuikwepa ni hii, Rais Magufuli alishiriki katika uuzaji wa nyumba za serikali
1. Anapata wapi moral authority ya kukemea ya Polisi Osterbay, kabla hajatuomba radhi kwa kuuza nyumba zetu?
2. Anapouzngumzia mikataba ya jeshi la Polisi tena akizungumzia Lugumi kwa kuzunguka analalamika kwa nani?
3. Kwanini hawatumbui kama akina Kabwe?

Mwisho, Je si kweli alikuwa katika serikali miaka 20? Je si kweli kuwa alishiriki kugawa nyumba zetu?
Mkuu Nguruvi3, ajabu ni kwamba wapo wanaotutaka tunyamazie ufisadi huu ambao umeliingizia taifa hasara ya mamilioni na mabilioni. Mapele yanapotumbuliwa wanapiga vigelegele, wakimsifu mtumbuaji lakini tukiwakumbusha je majipu kama yeye? Kimyaaaa, wanaanza kulalama...mara oh, tumuache kwa kisingizio cha hapa kazi tu.

Hapana katu hatunyamazi...mimi nilimtahadharisha Magufuli toka awali kabisa, atuombe radhi Watanzania kwa ushiriki wake wa miaka ishirini ndani ya serikali ya kifisadi. Nilimwambia tupo wengine tuko tayari kumsamehe na kumuunga mkono mradi akiri kuwa naye ni jipu na kutuomba tusahau ya kale na kwa pamoja tugange yajayo.
 
..hii nchi imeoza.

..kwamba mtumbuaji majipu naye ana jipu ni kielelezo cha wapi tumefika kama taifa.

..humu JF tunaye MsemajiUkweli lakini anashambulia wachangiaji wanaosema ukweli!!
Mimi sishambulii wanaosema ukweli bali ninapingana na wanafiki wanaokuja wamevaa nguo za uzalendo wakiuza hoja za kinafiki.

Rais siyo maraika na Watanzania walimchagua Rais Magufuli wakifahamu siyo maraika.

Mapungufu ya Rais magufuli yalipimwa na wananchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na wakafanya uamuzi kwenye sanduku la kura.

Mapungufu ya Rais Magufuli hayawezi kumzuia kufanya kazi yake ya kutumbua majipu, and infact, hana sababu ya kuomba msamaha kwa sababu ya kikundi cha watu wanafiki wanapiga kelele.

Mnaoshangaza ni ninyi mnajaribu kuturudisha kwenye hoja za kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015 wakati taifa limeishapiga hatua.

Nimewaambia Uchaguzi Mkuu umepita na inabidi mzoee tu kuwa Rais wa Tanzania ni John Magufuli.
 
Mkuu Nguruvi3, ajabu ni kwamba wapo wanaotutaka tunyamazie ufisadi huu ambao umeliingizia taifa hasara ya mamilioni na mabilioni.

Mapele yanapotumbuliwa wanapiga vigelegele, wakimsifu mtumbuaji lakini tukiwakumbusha je majipu kama yeye?

Kimyaaaa, wanaanza kulalama...mara oh, tumuache kwa kisingizio cha hapa kazi tu.

Hapana katu hatunyamazi...mimi nilimtahadharisha Magufuli toka awali kabisa, atuombe radhi Watanzania kwa ushiriki wake wa miaka ishirini ndani ya serikali ya kifisadi. Nilimwambia tupo wengine tuko tayari kumsamehe na kumuunga mkono mradi akiri kuwa naye ni jipu na kutuomba tusahau ya kale na kwa pamoja tugange yajayo.
Mkuu nadhani umefuatilia hoja ya JokaKuu . Amekuwa mkweli katika kueleza suala la nyumba za serikali.
Wanaopinga hoja zake hawajibu hoja.
Ni kweli kuwa Rais alikuwa waziri nyumba za serikali zinauzwa

Pili, uuzwaji wa nyumba umeacha utata hadi leo na kila mmoja anatambua haukuwa wazi

Tatu, Jokakuu kama sisi wengine tunahoji, leo kwanini Rais ahoji mikataba na hata kushauri Polisi wachukue mikopo ikiwa jambo kama hilo halikufanyika siku za nyuma?

Ndio maana akatumia neno 'moral authoriy' tunayokubaliana nayo

Nne, Rais kasema kuna matumizi mabaya ya fedha za kununulia vifaa na sare na mikataba inayotiliwa mashaka.
Hapa tunahitaji nini kujua mikataba tata ni kama Lugumi?

Sasa watetezi wanakuja na hoja, Rais amechaguliwa tayari! ebo! kama amechaguliwa maana yake tufunge manyanga kuserebuka tu hata kama mirindimo hatuijui! No way, 'watumishi' watafanya hivyo, Raia watahoji na hilo si kosa

Umefika wakati Watanzania wajenge utamaduni wa kuhoji, kukosoa na kupongeza.

Tuachane na fikra za 'kushangilia tuu' tukizifinyanga na kuvia akili zetu.

Huu ututusa hatutaunyamazia, hoja inajibiwa na hoja na si bla bla.

Hii ni nchi yetu , tunatakiwa kusonga mbele pamoja.
Hatuwezi kusonga mbele tukiwa na wapiga zumari na wanakwaya na wapiga debe

Tuukatae huu utumwa wa malipo kwa gharama za vizazi vyetu.
 
Mimi sishambulii wanaosema ukweli bali ninapingana na wanafiki wanaokuja wamevaa nguo za uzalendo wakiuza hoja za kinafiki.

Rais siyo maraika na Watanzania walimchagua Rais Magufuli wakifahamu siyo maraika.

Mapungufu ya Rais magufuli yalipimwa na wananchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na wakafanya uamuzi kwenye sanduku la kura.

Mapungufu ya Rais Magufuli hayawezi kumzuia kufanya kazi yake ya kutumbua majipu, and infact, hana sababu ya kuomba msamaha kwa sababu ya kikundi cha watu wanafiki wanapiga kelele.

Mnaoshangaza ni ninyi mnajaribu kuturudisha kwenye hoja za kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015 wakati taifa limeishapiga hatua.

Nimewaambia Uchaguzi Mkuu umepita na inabidi mzoee tu kuwa Rais wa Tanzania ni John Magufuli.
Ahaa! Unapokubali kuna ukweli unaosemwa na wakweli huna sababu za kuwaita wakweli hao wanafiki.
Wakweli wanakuwa wazalendo kwasababu umekubali wanasema ukweli, ukakiri uwepo wa mapungufu.

Huna sababu za kuendelea kuwaita wanaosema ukweli na kukuonyesha mapungufu wanafiki, maana wanasema unachokubali ni kweli na uwepo wa mapungufu

Tofauti ya wazalendo na wasio wazalendo ipo katika ukweli. Wazalendo watasema ukweli na huo ndio uzalendo

Inatosha kusema, umekubali kuwa Magufuli alikuwa na mapungufu ya kushiriki kuuza nyumba za Serikali.

Rais wa Tanzania ni Magufuli. Hiyo haina maana ni Malaika na kwamba tupige zumari tu bila kujua mirindimo

Ukisema kikundi cha watu unakosea, hicho kikundi si Watanzania? Na wangapi kule vijijini wanopigana na mijoka mashambani, wanaosinzia na vibali wanajua kuwa nyumba walizolipia kodi uuzwaji wake ulimshirikisha Magufuli?

Hata sisi wa mjini hatukujua Lugumi hadi jitihada za kuificha zilipoanza na sasa inazungumziwa nyuma ya pazia. Eti tuwe wazalendo inabaidi tuseme ni mradi mzuri saana ulioleta mafanikio!! No way, not this time dude

Hii habari ya kuchagua majipu unaionaje mkuu?
 
amuilize summaye au mbowe wanajua maamuzi ya kuuza nyumba yalikuwa ya nani , hata ukawa hawawez kutumia hiyo hoja kama kick kwa sababu wanafaham ukweli
Hiki sio kigezo. Hao watu hawako serikalini. Tunataka Rais wetu a address hii issue. Na jinsi ninavyosikiasikia hii mikataba inaweza ikawa imekiukwa.
 
Mkuu, mnada wa nyumba za serikali haukukupata au uliwahiwa na wajanja wakachukua nyumba ambayo ulitegemea utaipata?

Nimekuuliza kwa sababu ikianzishwa hoja kuhusu nyumba za serikali huwa unaibuka haraka kuja kutoa mchango kuhusu uuzaji wa nyumba za serikali huku ukimlaumu Rais Magufuli wakati suala hili lilishatolewa maelezo na Frederick Sumaye.

Suala la uuzaji wa nyumba za serikali ni sawa na jini lililotoka nje ya chupa na hauwezi kulirudisha, kwa maana kuwa, hata ukipiga kelele hakuna atakayezirudisha tena serikalini. Hiyo ilishatoka! Chill out!

The issue of government houses is finished and closed.

Hii ni sawa na mtu amekufa huku ukimdai pesa na hakuna uwezekano wa kuzipata pesa zako halafu unaanza kulalamika kila mara kwa watu kuhusu deni lako kwa marehemu. A pure waste of time and energy!
Mimi sijauona huo mkataba, lakini nilivyosikia ni kwamba ha waruhusiwi kujenga majengo mengine wala kubadili matumizi ndani ya miaka 25, endapo serikali ikiamua kuzirudisha mikononi mwake hawatapata hasara. Kwani hiyo mikataba ni Siri?
 
Rushwa Ofisi Ya DPP:-
Naomba mnitajie majina ya wala rushwa/waomba chochote toka AG chamber tumfikishie JPM.

Tafadhali usimwinee mtu,siri itatunzwa,na tutashughulikia hilo.
Nasubiri
 
Back
Top Bottom