Mbunge Tarimo Akabidhi Pikipiki Nne kwa Jeshi la Polisi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
Katika kuhakikisha Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linapata vitendea kazi vitakavyo tumika katika kutimiza majukumu yao,Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus tarimo amewezesha Jeshi hilo kwa kukabidhi Pikipiki nne ili kuongeza urahisi wa kusimamia ulinzi na usalama .

Akikabidhi Pikipiki hizo Januari 6 .2023 kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa,Mbunge Priscus Tarimo amesema kuwa uwezeshaji huo nikatika kusaidia doria na kupambana na madawa ya kulevya.

"Huu ni muendelezo wa kusaidia Jeshi la Polisi katika kupambana na kuweka doria ili kuzuia uhalifu pamoja na usalama barabarani,Jeshi la Polisi linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi ila Serikali bado inafanya jitihada za kuliwezesha Jeshi la Polisi ili litoe huduma nzuri na kwa wakati kwa wananchi wake" alieleza Tarimo.

Ameeleza kuwa vitendea kazi hivyo vitasaidia Jeshi hilo kupambana na watu wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya ikiwemo Mirungi katika mipaka ya Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na kufanya doria mbalimbali zenye kumlinda Mwananchi na mali zake.

"Bado tutazidi kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kutatua changamoto zinazo wakabili na waweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi tunataka kuona wananchi wakifikiwa haraka na kutatuliwa changamoto zao" Tarimo.

Akipokea Pikipiki hizo na kutoa shukrani kwa Mbunge huyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema kuwa pikipiki hizo zitatumia katika kuweka usalama barabarani na nyingine doria za kawaida.

"Tunashukuru kwa msaada huu wa kuliwezesha Jeshi la Polisi Pikipiki hizi ambazo nitazigawa mbili kwa kituo cha Polisi Majengo na nyingine mbili kwa kitengo cha usalama Barabarani " RPC Maigwa

Huo ni mwendelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo kusaidia vitendea kazi Jeshi la Polisi ambapo mwaka 2023 alilipatia Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Pikipiki mbili na sasa Pikipiki nne ili kuimarisha usalama.

GDOc7pFXoAAeRkR.jpg
GDOc8OGWkAAyhGp.jpg
WhatsApp Image 2024-01-08 at 02.26.35.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-08 at 02.26.35(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-08 at 02.26.36.jpeg
 
Back
Top Bottom