Rais Kikwete asaini Muswada wa Katiba

Nilikwisha kusema tangu awali hatupati Katiba mpya Bali ni sheria ya kuhuisha Katiba ya CCM! Take ushauri wangu najua Mods wataiondoa hii ila njia ni moja tu tuanzishe maandamano ya kwenda Ikulu na kuichukua kwa mtindo wa Libya na Egypt au Yemen njia ya kupitia Bunge la makada wa CCM akina Makinda na Juha Kashlilah na zumbukuku wa CUF ambao wametosheka na serikali ya mseto Unguja ambayo imewapatia taifa la Zanzibar mimi simo kwani mabadiliko ya dhati hakuna labda karne ijayo.
 
Ikisha kuwa sheria ndio imetoka mkuu wangu, muda wenyewe uko wapi na huko Bungeni nambie hata kipengele kimoja cha sheria wabunge wa CCM hawakubaliani nacho maana kura ndio zitaweza badilisha lolote.

I smell something here.......hiyo iliyopitishwa ni sheria ya kuunda tume kwa ajili ya kushughulikia katiba mpya na sio sheria/katiba mpya!

Wengi wetu huwa hatuelewi tunaishia kuconclude mambo bila ya uelewa kwa ufupi kuna kundi walitaka na wao wawepo kwenye hilo jopo/tume ili watafune na posho ila nadhani JK atawateuwa watu wa kada mbalimbali ili kusitokee manung'uniko. Narudia kusema tena kwa kinywa kipana mnachotakiwa ni kumwamini JK sidhani kama atapoteza fursa hii adhimu kuingia kwenye historia ya Tanzania ya miaka 200 ijayo! JK hana cha kupoteza kwenye hiyo katiba mpya nina imani kuwa atafanya vizuri kuliko wengi wetu tunavyodhani.
 
Wakuu zangu hii ndio imetoka, tukubali matokeo hakuna cha kurekebisha lolote mpira ndio umeanza na filimbi imeshapigwa. Muda wa Mapumziko ni baada ya dakika 45..Ukicheza rafu kadi ya njano ukiendelea nyekundu..
Kifupi, CDM imeadhirika wala sii kidogo ila tu kama wananchi na taasisi zao watachukua hatua tofauti..
 
What? I was about to collapse!! How dare him? Inauma inaumiza inasikitisha. Nifanye nini na Tz. yangu?! Mungu wangu Mungu wangu mbona unatuacha?
 
I smell something here.......hiyo iliyopitishwa ni sheria ya kuunda tume kwa ajili ya kushughulikia katiba mpya na sio sheria/katiba mpya!

Wengi wetu huwa hatuelewi tunaishia kuconclude mambo bila ya uelewa kwa ufupi kuna kundi walitaka na wao wawepo kwenye hilo jopo/tume ili watafune na posho ila nadhani JK atawateuwa watu wa kada mbalimbali ili kusitokee manung'uniko. Narudia kusema tena kwa kinywa kipana mnachotakiwa ni kumwamini JK sidhani kama atapoteza fursa hii adhimu kuingia kwenye historia ya Tanzania ya miaka 200 ijayo! JK hana cha kupoteza kwenye hiyo katiba mpya nina imani kuwa atafanya vizuri kuliko wengi wetu tunavyodhani.
Mkuu ukisoma muswada wake, nadhani JK amekwenda hadi kuundwa kwa katiba kama sikosei..
 
Maoni ya cdm ni muhimu lakini yangechukuliwa kwa uzito stahili iwapo wangeshiriki mchakato mzima Bungeni hadi mwisho wake lakini staili ya kususa kisha unatoka kivingine naona haijasaidia.
 
Ikisha kuwa sheria ndio imetoka mkuu wangu, muda wenyewe uko wapi na huko Bungeni nambie hata kipengele kimoja cha sheria wabunge wa CCM hawakubaliani nacho maana kura ndio zitaweza badilisha lolote.
Kama Kikwete na serikali yake wakishindwa kufanya hayo marekebisho, ni suicide kwao kwa sababu hivi sasa nchi yote inajua kuwa alishakubali kufanya hivyo. Akiamua kuwa kigeugeu atajimaliza mwenyewe. Huu ni mtego kwake na amejiingiza
 
Ikisha kuwa sheria ndio imetoka mkuu wangu, muda wenyewe uko wapi na huko Bungeni nambie hata kipengele kimoja cha sheria wabunge wa CCM hawakubaliani nacho maana kura ndio zitaweza badilisha lolote.
JK akitimiza makubaliano na cdm, (hata unaposoma taarifa hii ya ikulu) maoni yanaendelea kupokelewa. Kitakachofanyika ni serikali kupeleka bungeni marekebisho ya sheria; na kwa kuwa wabunge wa ccm huunga mkono yanayoletwa serikali, then tutakuwas tumefaulu.
Mambo mawili yanatakiwa: Kwanza JK awe na nia ya dhati kutekeleza yale aliyokubaliana na cdm na awe tayari kutekeleza haya yaliyomo kwenye taarifa ya ikulu (ambayo kimsingi ni yaleyale) Pili sisi wananchi ambao ndio wadau kwa makundi yetu mablimbali tuhakikishe tunapeleka mawazo yetu. Kuna mtu ameandika humu kuwa hayo tutakayopeleka tubakize ushahidi ili yasipoingizwa tuwe na msingi wa kulalamika.
Ebu tupeleke hayo maoni yetu - let us act now!
 
Kwa kifupi kitendo cha CDM kususia bunge na kukimbilia Ikulu kimedhihirisha kuwa hawaelewi dhana ya mihimili mitatu na wala hawaamini nguvu ya Bunge.
 
Pamoja na mapungufu yote, makubaliano kati ya Chadema na Serikali yalikua ni kwamba Rais asaini kwanza muswada ili maoni ya chadema na wadau wengine yawasilishwe bunge lijalo kama schedule of amendments. Hapa JK ametimiza ahadi yake kwa Chadema. Tatizo ambalo tunaweza kujadili ni kama je, maoni yaliyowasilishwa na Chadema yana uzito? Na kama yana uzito kwa maslahi ya umma, je, yatazingatiwa yote? Hapo sasa!!
Tumesema siku zote hatua ya kwanza ndio muhimu sana ktk kuelekea unakokwenda. maadam tumeanza na mguu wa kushoto ktk mbio ni vigumu sana kubadilisha hatua mbeleni laa sivyo utajikwaa na kuanguka.

Mapendekezo ya CDM yanaweza kuwa ulivyosema lakini sivyo wananchi tulivyowatuma. Tulisema wazi RAIS ASISAINI MUSWADA, sasa kama CDM wameenda na kukubaliana rais aweke saini muswada huu na kuwa sheria, hayo ni mapendekezo yao ambayo pengine wameyabadilisha wakiwa Ikulu lakini nijuavyo toka mwanzo walitaka rais asi saini muswada.

Hii kitu imeshapita na kuwa sheria hizo amendments haziwezi kuwa na mabadiliko makubwa kama walivyoomba CDM.. Haiwezekani toka ombi la kwanza hadi la mwisho hakuna kitakachobadilika maana hakuna makubaliano yalofikiwa kuhusu utaratibu wa kukusanya mawazo ya watu na kuyapeleka bungeni juu ya amendments hizo.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Kitakachonishangaza mimi siyo JK kusaini muswada kuwa sheria, bali ni kutokuona "plan B" ya CDM na wanaharakati. Nasema hivyo kwa sababu hili tulilitarajia kwani Ccm wamekuwa na ajenda ya siri ya kuhodhi mchakato mzima wa kuandika katiba ndo maana hawakutaka kushirikiana na yeyote kwenye uandaaji wa huo mswaada hadi kupitishwa kwake bungeni.
Tarajio langu ni kwamba Cdm watakuwa na plan B ambayo tayari kuanza kufanyiwa kazi.
 
kitendo cha Rais kuwapokea kimedhihirisha kuwa Rais ni mkomavu na yuko tayari kusimamia vizuri mchakato wa katiba mpya na kumsikiliza kila mwananchi.
 
tusifanye hii kama mechi ya mpira, ukweli utabaki pale pale kwamba marekebisho yoyote yale yatafanyika bungeni na kule CDM hawana wingi wa kutosha hivi wanategemea nguvu ya JK. lazima tutafakari kwa upande huo
hivi mfikirie kelele zilizokuwa zinapigwa ni kwamba yeye JK asishiriki kwenye mchakato huo (+CCM ofcourse) unategemea hilo litakuwepo? hizo ni ndoto za mchana. This is their time otherwise tutabaki na manung'uniko tu
 
Back
Top Bottom