Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,731
- 218,313
TLS wanaendesha kongamano la kujadili Muswada wa Sheria ya uchaguzi wa Rais wabunge na madiwani , muswada huu umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni .
Miongoni mwa wazungumzaji wamo Freeman Mbowe na Tundu Lissu , hakika sijawahi kuona mjadala moto kama huu kwa kipindi kirefu mno.
Mbowe hajamung'unya maneno , amesema ccm haina dhamira ya kweli ya kuboresha sheria za uchaguzi , na kwamba lengo lao kubwa ni kudanganya dunia kwamba wanafanya mabadiliko , huku ni uongo mtupu , ameuita muswada huu kuwa COSMETICS na kwamba muswada huu ni matusi ya nguoni kwa watanzania wote na ni matusi kwa kila mpenda demokrasia duniani .
Akichangia kwenye kongamano hilo Tundu Lissu amedai kwamba , Muswada uliopelekwa Bungeni haujagusa matatizo ya uchaguzi , huku akisema tatizo kubwa la Uchaguzi wa Tanzania ni kuwepo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kama Wasimamizi wa Uchaguzi , hili ndio tatizo la kwanza kwenye chaguzi zote za Tanzania tangu 1995 , bila kuondoa huo uchafu ni kazi bure .
Juhudi za kuweka video zinaendelea , ni uhondo mtupu !