Kwa hiyo swala zima la Katiba Mpya ni la KISIASA! - Ndio mguu tuloanza nao na ajabu watu wameshindwa pia kutazama hapa.
Unfortunately ndio hali tuliyonayo sasa. Na ndio maana nilisema makosa yalifanyika bungeni. Waziri mkuu na Spika walikuwa na every opportunity ya kuunganisha watanzania na kuifanya hii katiba iwe ya kitaifa - beyond party politics, but they both decided to look away!
Na kama hii katiba itaandikwa kwa kufuata kila kilichopo kwenye hii sheria Tanganyika ndio watakuwa loosers. CUF wanaungana na CCM kwenye hili sio kwa sababu wameambiwa wafanye hivyo na CCM ila kwa sababu inaonekana (after all these years) kukamilisha uhuru wa Zanzibar toka kwa -wakoloni' - Tanganyika. Huu ni mkakati wa Zanzibar wa kuondokana na kadhia hii ya 'kunyonywa' na Tanganyika. Wabunge wengi wa CUF wanatoka Zanzibar, na tutambue CUF Zanzibar sawa na CUF Tanganyika. Wakina Mh Barwan na Magdalena Sakaya sijui kama wanaelewa couldn't care less about Tanganyika?
Unless kufanyike marekebisho makubwa na muundo wa muungano upewe kipaumbele kwenye uundwaji wa hii katiba mpya, CCM watajikuta wapo upande mwingine wa historia! Majuto mjukuu!