Bunge kuanza kupokea maoni kuhusu miswada sheria za uchaguzi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kamati za Kudumu za Bunge zimeitisha maoni ya wadau kuhusu miswada mitano iliyosomwa kwa mara katika mkutano wa 13 ukiwemo Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023.

Maoni hayo ya miswada hiyo iliyowasilishwa kwa mara ya kwanza Novemba 10 mwaka huu itawasilishwa kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Desemba 18, 2023 na kitengo ha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa cha Bunge, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria itasilikiliza maoni ya miswada minne.

Miswada hiyo ni wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais wa Madiwani wa Mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba tano wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2023.

“Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau utafanyika Januari 6, 8 na 10 mwaka 2024 katika ukumbi Frank Mfundo ghorofa tano, jengo kuu la utawala, ofisi ya Bunge jijini Dodoma,”imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema PIC inawaalika wadau kutoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma wa Mwaka 2023.

Imesema kamati hiyo itasikiliza maoni hayo Januari 10 katika ukumbi wa jengo dogo la utawala bungeni jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imesema maoni hayo yanaweza kuwasilisha kwa njia ya Posta kupitia ofisi ya Bunge au kupitia barua pepe cna@bunge.go.tz ma kamati@bunge.go.tz.

Hatua hiyo inakuja wakati mijadala ya uchambuzi wa miswada hiyo katika mikutano mbalimbali nje ya Bunge ikiendelea.

MWANANCHI
 
Tunalitaka Bunge lianze kupokea Maoni ya Nyongeza juu ya Katiba ya Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mapendekezo Juu ya Tarehe ya Kuipigia Kura Rasimu ya Katiba Pendekezwa ili iwe Katiba Kamili ya Nchi hii.

Hatutaki blah blah zao za kisiasa wanazofanya.

Katiba ni Mali ya Wananchi Wote Katika Nchi, Katiba Siyo Mali ya Serikali na wala Siyo Mali ya Wanasiasa.

Kamati za Kudumu za Bunge zimeitisha maoni ya wadau kuhusu miswada mitano iliyosomwa kwa mara katika mkutano wa 13 ukiwemo Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023...
 
Kamati za Kudumu za Bunge zimeitisha maoni ya wadau kuhusu miswada mitano iliyosomwa kwa mara katika mkutano wa 13 ukiwemo Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023.

Maoni hayo ya miswada hiyo iliyowasilishwa kwa mara ya kwanza Novemba 10 mwaka huu itawasilishwa kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Desemba 18, 2023 na kitengo ha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa cha Bunge, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria itasilikiliza maoni ya miswada minne.

Miswada hiyo ni wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais wa Madiwani wa Mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba tano wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2023.

“Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau utafanyika Januari 6, 8 na 10 mwaka 2024 katika ukumbi Frank Mfundo ghorofa tano, jengo kuu la utawala, ofisi ya Bunge jijini Dodoma,”imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema PIC inawaalika wadau kutoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma wa Mwaka 2023.

Imesema kamati hiyo itasikiliza maoni hayo Januari 10 katika ukumbi wa jengo dogo la utawala bungeni jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imesema maoni hayo yanaweza kuwasilisha kwa njia ya Posta kupitia ofisi ya Bunge au kupitia barua pepe cna@bunge.go.tz ma kamati@bunge.go.tz.

Hatua hiyo inakuja wakati mijadala ya uchambuzi wa miswada hiyo katika mikutano mbalimbali nje ya Bunge ikiendelea.

MWANANCHI
Bunge lipi? hili? Kuna bunge tanzania? Majizi ya kura na uchaguzi.....majizi hayana uhalali wa kuwa pale....Takataka tupu!
 
Nje ya mada kidogo,, hivi kwa hiyo mchakato wa katiba mpya ndo umetushinda kabisa!!???
 
Kamati za Kudumu za Bunge zimeitisha maoni ya wadau kuhusu miswada mitano iliyosomwa kwa mara katika mkutano wa 13 ukiwemo Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023.

Maoni hayo ya miswada hiyo iliyowasilishwa kwa mara ya kwanza Novemba 10 mwaka huu itawasilishwa kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Desemba 18, 2023 na kitengo ha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa cha Bunge, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria itasilikiliza maoni ya miswada minne.

Miswada hiyo ni wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais wa Madiwani wa Mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba tano wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2023.

“Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau utafanyika Januari 6, 8 na 10 mwaka 2024 katika ukumbi Frank Mfundo ghorofa tano, jengo kuu la utawala, ofisi ya Bunge jijini Dodoma,”imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema PIC inawaalika wadau kutoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma wa Mwaka 2023.

Imesema kamati hiyo itasikiliza maoni hayo Januari 10 katika ukumbi wa jengo dogo la utawala bungeni jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imesema maoni hayo yanaweza kuwasilisha kwa njia ya Posta kupitia ofisi ya Bunge au kupitia barua pepe cna@bunge.go.tz ma kamati@bunge.go.tz.

Hatua hiyo inakuja wakati mijadala ya uchambuzi wa miswada hiyo katika mikutano mbalimbali nje ya Bunge ikiendelea.

MWANANCHI
watoa taarrifa eti hawajaona hii halafu mwisho wa siku kulalamika kwa sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom