Posho na Mishahara ya wabunge...

May be sijaelewa posho zenyewe walizogomea ni zipi kwanza au ni shilingi ngapi?
 
May be sijaelewa posho zenyewe walizogomea ni zipi kwanza au ni shilingi ngapi?

Katika pendekezo la waziri wa fedha kivuli ambalo litatolewa kama BAJETI mbadala wametoa kauli kuwa Serikali ifute posho za vikao kwa vile ni sehemu ya kutekeleza majukumu yao, hivyo hakuna sababu ya kuwalipa SITTING ALLOWANCE. Makosa kidogo ya uchapaji imetokea WAGOMEA badla ya WAGOMEE. Nia ya andiko hili ni kuwaasa wabunge wa CDM watekeleze kwa vitendo mtazamo wao wa kuishauri na kuishinikiza serikali iachane na mtindo wa kutoa posho ya VIKAO.
 
Nilivyoelewa mimi, ni zile posho ambazo huko serikalini wakiwa na vikao huwa wanalipwa. It is just to walk from your office to the conference room unakamata mshiko. Na inategemea na title yako. Mkubwa hupata kikubwa zaidi na mdogo kidogo na hapo msosi na maji upo. Wapo sahihi sana. Kilichobaki pia wapigie kelele matumizi mabaya ya magari. Sioni kama ni sawa gari la serikali lipeleke watoto wa ofisa shule au sokoni. Gari la ofisi liwe for office use only. Hata tokea nyumbani to office watumie magari yao binafri. Ninapata hasira ngoja nipumzike.
 
It's ok, magamba yatakubali na hivi yako mengi?? Ngoja tutaona wasaliti ni kina nani ili 2015 tuwashigulikie vizuri
 
Hawa ni kweli wamekusudia au ni danganya toto? Kamati ya Zitto (POAC) tumeona imekataa hesabu nyingi za mashirika na kuwaambia wakutane nao tena Dodoma. Hii kwa wale watu walio Serikalini huwa ni janja ya kutengeneza vikao vingine ili posho iongozeka. Wanakwambia tukutane Dodoma, mkienda kikao kinafanyika posho inaingia na hesabu zinapita. Hii ndo itakayotokea.

CDM wana uhakika CCM hawatapitisha, ila nao wataendelea kupokea hizo posho na kuwadanganya wananchi kuwa sisi tulipendekeza ifutwe.
Kama kweli wako makini, CCM wakigomea wao wazikatae na watengeneze mfuko wa hizo pesa zikalete maendeleo. Utakuwa mfano na utawapa sifa ya kweli kuliko propaganda.

CDM wanatetea mfumo mzima, swala la kusema wao tu wasipokee halafu wengine waendelee ni ukengemfu. Kinachohitajika ni kubadili mfumo mzima wa ulipaji mishahara, mshahara uwe ni package ili kila mmoja aamue. hakuna posho za ajabu ajabu kama kumlipa dereva, matenegenezo ya gari, fedha za mafuta nk haya yote yawekwe kwenye mshahara. Halafu watu wafanye kazi, atakayekosa kikao apewe adhabu kali pamoja na kusimamishwa ubunge.

Mbunge asinunuliwe gari wala kukopeshwa fedha za serikali ili kununulia magari, waende kwenye mabenki kama wafanyakazi wengine. Na kama ni serikali kukopesha basi ikopeshe wafanyakazi wote.
 
Nimevutiwa sana na pendekezo la wabunge wa CHADEMA kuwa posho ya vikao ifutwe ili pesa zipelekwe katika kuboresha huduma za jamii.
Huo ni uzalendo wa hali juu kwa waheshimiwa wabunge katika kipindi hiki ambacho taifa letu linapitia katika mawimbi makubwa ya kuwepo kwa matatizo ya kiuchumi na kijamii.

Nachukua fursa hii kuwaomba waheshumiwa wakiongozwa na ZITO waepuke kupokea posho za vikao katika bunge la bajeti na pesa husika zifunguliwe mfuko maalum kwa kusaidia jitihada za wananchi kujiletea maendeleo. Kama tujuavyo wawapo DODOMA wabunge wetu wanapata posho za aina 2; za vikao na kuishi, hivyo living allowanze waendelee kupokea ili jioni waonekane PAKO NI PAKO na viwanja vingine. ILA SITTING ALLOWANCE WAIEPUKE.

Kuchezwa kwa ngoma, kuanzishwa na mpigaji!

CHAKO NI CHAKO mkuu na si PAKO NI PAKO
 
I am quite doubtful on this totodanganya lakini watu husema charity begins at home. Pengine tungesikia maposho ya vigogo kule CHADEMA yamepunguzwa basi ningejuwa kuwa hili ni la kweli. Penye maslahi ya wanasiasa hakuna watawala wala wapinzani.
Angalia Zitto anaanza kwa tone ya kudanganya anaposema kuwa ingawa jambo hili litapingwa lakini atalishauri bungeni. Kwanini awe na kauli ya shaka na mbona wanapoikomalia Serikali na Chama tawala (magamba) hutowa kauli za uhakika kama vile wao ndio wenye uwezo wa kufanya hayo wanayoyataka?
 
Nimevutiwa sana na pendekezo la wabunge wa CHADEMA kuwa posho ya vikao ifutwe ili pesa zipelekwe katika kuboresha huduma za jamii.
Huo ni uzalendo wa hali juu kwa waheshimiwa wabunge katika kipindi hiki ambacho taifa letu linapitia katika mawimbi makubwa ya kuwepo kwa matatizo ya kiuchumi na kijamii.

Nachukua fursa hii kuwaomba waheshumiwa wakiongozwa na ZITO waepuke kupokea posho za vikao katika bunge la bajeti na pesa husika zifunguliwe mfuko maalum kwa kusaidia jitihada za wananchi kujiletea maendeleo. Kama tujuavyo wawapo DODOMA wabunge wetu wanapata posho za aina 2; za vikao na kuishi, hivyo living allowanze waendelee kupokea ili jioni waonekane PAKO NI PAKO na viwanja vingine. ILA SITTING ALLOWANCE WAIEPUKE.

Kuchezwa kwa ngoma, kuanzishwa na mpigaji!
Basi badilisha kichwa cha habari cha hii posting tafadhali, naogopa utakuja kusutwa kwani hao hawaaminiki katika swali la mshiko, tulishawasikia wakihalalisha posho za mara mbili!
 
MWENYEKITI wa Chama cha UPDP, Faham Dovutwa, anajiandaa kupinga alichokiita ubadhirifu na ufisadi wa kitaasisi, unaofanywa na Bunge kwa kulipa posho za kujikimu kwa wabunge wanapokuwa katika vikao vyao mjini Dodoma.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Dovutwa alisema utaratibu wa kuwalipa posho za kujikimu wabunge wanapokuwa mjini Dodoma, ni makosa na ubadhirifu wa fedha za walipa kodi.Alisema wabunge hawastahili kulipwa fedha hizo kwa sababu wanalipwa mishara yao kwa kazi hiyo.

"Wabunge wanalipwa mishahara ya kila mwezi kama watumishi wa eneo lolote na miongoni mwa kazi zao ni wanazifanyia mjini Dodoma, sasa inashangaza wanapolipwa posho za siku huku wakiwa wanalipwa mishahara yao," alisema Dovutwa.

Dovutwa alisema kwa kawaida posho ya kujikimu inalipwa kwa mtumishi anapokwenda nje ya kituo chake cha kazi na kwamba kitendo cha kuwalipa posho wabunge wanapokuwa mjini Dodoma ni cha ubadhirifu.

Alisema Dodoma ndiyo kituo cha kazi za wabunge na kwa hiyo hakuna sababu ya kuwalipa posho ya kujikimu.

Alisema anakusudia kutafuta usahihi wa jambo hilo kabla ya kuamua kuchukua hatua za kisheria."Hoja yangu ni viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza taasisi na idara za umma, kuhusika katika hujuma za ubadhirifu na ufisadi huo, maana wakati mwingine inakuwa vigumu kuhoji kutokana na kuwa tuhuma zenyewe zinafanyika baada ya kubarikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni," alisisitiza. [/COLOR]
Kumbe hapo ndipo ilipotoka????
 
Hivi wewe MAFILILI ulishawahi kufanya kazi serikalini hata ya kukata nyasi! Mbona unatoa pendekezo ambalo ni la kitoto tena mtoto yule mjinga.

Mtu unapokea sitting allowance unapokuwa umehudhulia kikao husika na uka sign. Kama hujafanya hivyo hiyo sitting allowance hurudi kwa aliyeitisha kikao husika. Kwahiyo ni kwamba kama CDM watagomea sitting allowance itarudi kule ilikotoka. Haiwezekani eti CDM wakasema ile sitting allowance tuliyogomea iwekeni kwenye mfuko fulani ambao tumefungua kwaajili ya kusadia watu fulani. Hili ni wazo la kijinga mno hakuna taasisi inayo operate hivyo. Siku nyingine UTACHEKWA.

Hapa CDM wanachotaka ni kubadilisha mfumo mzima wa ki-taasisi wa kutoa hizo allowances. Kama magamba wanaona mantinki yake kwanini wasikubali kuliko kuleta hizo lame excuse!

Ni sawa ukasikia kwamba kijiji fulani cha jirani kuna njaa (read Watanzania), halafu bahati nzuri kijiji chenu kina neema ya chakula, tena mnakula hadi mnasaza (read watawala wa CCM), halafu wewe eti kwakuwa kijiji chako kina neema ya chakula, ukagoma kula simply because kijiji jirani kuna njaa (read wabunge CDM). Je utakuwa ume solve kitu gani kwa kugoma kwako kula? Sana sana hicho chakula ulichogomea kula kitaendelea kuwa abused na wanakijiji wenzako (wabunge CCM) wasiona madhila wanayopata kijiji jirani? Je hayo ndiyo unayoya suggest kwa wabunge wa CDM Ndg. MAFILILI

Kama ndivyo hivyo THEN YOU'RE AN OBSCURE PERSON!
 
Chadema waonyeshe mfano kwa hili na kama magamba ya kikataa wapate pointi ya kutoka nayo kwa wananchi baada ya bunge. Hii itawapa pointi nzuri sana wao wakomae nao tu!
 
Nimevutiwa sana na pendekezo la wabunge wa CHADEMA kuwa posho ya vikao ifutwe ili pesa zipelekwe katika kuboresha huduma za jamii.
Huo ni uzalendo wa hali juu kwa waheshimiwa wabunge katika kipindi hiki ambacho taifa letu linapitia katika mawimbi makubwa ya kuwepo kwa matatizo ya kiuchumi na kijamii.

Nachukua fursa hii kuwaomba waheshumiwa wakiongozwa na ZITO waepuke kupokea posho za vikao katika bunge la bajeti na pesa husika zifunguliwe mfuko maalum kwa kusaidia jitihada za wananchi kujiletea maendeleo. Kama tujuavyo wawapo DODOMA wabunge wetu wanapata posho za aina 2; za vikao na kuishi, hivyo living allowanze waendelee kupokea ili jioni waonekane PAKO NI PAKO na viwanja vingine. ILA SITTING ALLOWANCE WAIEPUKE.

Kuchezwa kwa ngoma, kuanzishwa na mpigaji!

Kama umepitia ile press release ya Zitto.
Kama nimemuelewa vizuri ni anaungumzia mfumo wote wa sitting allowance.
Amehusisha hili na matumizi sahihi ya rasilimali katika kutanua mapato zaidi ya umma.
So, hapo itaokolewa posho kwa wabunge wote sio CDM tu. Kama itakuwa ni CDM tu hayo
makato hayatakuwa na tija kwa mfumo wa sasa.
 
Haingii akilini kwa nini mbunge alipwe mshahara mkubwa kiasi hicho na bado apewe posho kwa vikao.
Hatuongelei sana mshahara wanaolipwa wabunge, ila tunachohoji ni pesa ya posho ya vikao, hicho kiwango wanacholipwa na wafanyakazi wengine wanapokaa semina pia walipwe kwa viwango hivyo hivyo, au la walipwe kwa ngazi wanazolipwa wengine. Kinyume chake hiyo ni kutengeneza matabaka ya matajili na maskini.
 
Unafiki umewajaa wabunge walio wengi kwani kwa nje wanapinga posho na marupurupu wanayopata wakati kiundani wanataka ziongezeke.
kama kuna wabunge wanaoona kuwa ujira wanaopta ni mkubwa sana basi nawaomba hizo hela wazipeleke kwenye watu wenye uhitaji kama kwenye vituo vya kulelea wazee na watoto yatima...
wanasema hela wapatayo ni nyingi ila hakuna anaeitoa ya kwake aonayo imezidi.
waache kutufanya wajinga.
 
Wakifuta posho za vikao Serikalini na mashirika ya umma litakuwa goli la nguvu kwa sekta binafsi kupata wafanyakazi wazoefu kwani hivi sasa Rasilimali watu kubwa inakimbilia huko Serikalini na Mashirika ya umma kwa ajili ya hizo posho
 
Back
Top Bottom