Posho na Mishahara ya wabunge...

kwa kuanza hizo posho zao cdm ziingie kwenye mfuko maalum kila mwaka wazipangie matumizi kwenye maeneo yaliyopotezewa na bajeti ya serikali huo utakuwa mwanzo mwema
 
Usanii mtupu mbona milioni 90 Chadema waliramba!
Chadema wanapigania kubadilisha mfumo wa hayo malipo sio kususia mtu mmoja mmoja, mbona wewe mgumu kuelewa Mkuu? Unasusia na mfumo unaendelea utakuwa umefanya nini? Nimewasikia hata akina Chiligati na Nape wakizungumza kama wewe na hii inaonyesha kuwa hata viongozi wenu hawaelewi CHADEMA wanazungumzia nini. SHAME
 
Chadema waache siasa za kutufanya sisi watanzania hatuna akili.
Kama wanaona posho wapatayo ni kubwa basi waichukue na kila mmbunge aipeleke ya kwake kwenye maeneo yenye upungufu wa fedha kama hospitali za majimbo yao,makazi ya wazee na yatima etc.
hii siasa ya kusema hawataki posho na bado wanachukua kila siku na hatuoni waitumie kama wanavyohubiri nadhani inatosha.
kwa kuwa wao ni wema sana wachukue posho na chama kipangie bajeti hela hiyo kuleta maendeleo ya watanzania.
wafanye hivyo kama hawajauana.
 
Chadema waonyeshe mfano kwa hili na kama magamba ya kikataa wapate pointi ya kutoka nayo kwa wananchi baada ya bunge. Hii itawapa pointi nzuri sana wao wakomae nao tu!

:mod:Lakini wabunge kwa ujumla wamejisahau sana, tena ni wasaliti wa umma bila kujali chama gani. Kuna haja sasa ya kuwa na National scale ya salary au guidelines ambazo zitamchukua mtu kama profesor, na kusema**** mfano mshahara wa mbunge utakuwa asilimia 50 ya ule wa profesor, ili kusiwe na abuse of parliamentary powers, kwa kuwa hawa wabunge wanajipangia maslahi wenyewe, hii ni conflict of interest, Milioni 12, duhh, kwa kipi ukilinganisha na profesor millioni 3.:tonguez:, halafu sitting allowance kwenye jumba la bunge ambalo ndio office yao na wana mshahara? Hii haifai. Ila najua tu wabunge wa ccm kwa usaliti wao watapinga hili. Seating allowance ifutwe kwa wote walioajiriwa. Ila kama mtu ameitwa bungeni na hajaajiriwa, siku hiyo anahitaji mkate apewe.:grouphug:
 
Wabunge wang`aka kuguswa posho zao
NA MWANDISHI WETU
3rd June 2011

1. Wamshambulia Zitto kuwa anasaka umaarufu
2. Wasema upinzani waziache, wao watachukua

Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe
Ukitaka kuona sura halisi za wabunge wa Tanzania gusa posho zao, huo ndio msimamo wao wa miaka na miaka na jana ulijidhihirisha kufuatia ushauri wa Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, wa kutaka kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge katika bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012.
Jana baadhi ya wabunge hasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walipinga kwa nguvu zao zote mapendekezo ya Zitto ya kutaka posho za vikao wanazolipwa ziondolewe.

Wa kwanza kupinga mapendekezo hayo bila hata kutafuna maneno alikuwa ni Mbunge wa Manyoni Mashariki (CCM), John Chiligati, ambaye alisema kama wabunge wa kambi ya upinzani hawataki kuzipokea fedha hizo waziache.
Chiligati alitoa msimamo huo jana jijini Dar es Salaam, alipotakiwa kutoa maoni yake kama anaona kuna haja posho za wabunge kuondolewa kama ilivyopendekezwa na Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Zitto Kabwe.
Akizungumza na NIPASHE katika viwanja vya ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam, Chiligati ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), alisema hoja hiyo sio ya wabunge wote bali ya upinzani na hivyo kama wao wanaona hawazihitaji posho hizo wasizichukue.
“Hii kambi ya upinzani kama haitaki hailazimishwi kupokea posho hizo za vikao wanaweza kuziacha sio lazima wazipokee,” alisema.

Naye Mbunge wa Magomeni visiwani Zanzibar, Mohammad Chomboh (CCM), alisema suala hilo halitekeleziki kwa kuwa Sh. 80,000 anayolipwa mbunge kama posho ni ndogo ikilinganishwa na hali halisi ya maisha ilivyo sasa.
Alisema kulala nyumba ya wageni kwa siku wanapokuwa Dodoma ni Sh. 50,000 hapo bado hawajala hivyo kiasi hicho sio kikubwa kama inavyoelezwa na upinzani.

Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza (CCM), alisema hoja ya kutaka posho ifutwe ni mawazo ya mtu kwani waliopanga malipo ya posho hiyo nao pia wana sababu zao.
Hata hivyo, alimtaka mbunge yeyote mwenye hoja kama hiyo, aipeleke bungeni ikajadiliwe huko, badala ya kuizungumzia nje ya Bunge.

Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Hamisi Kigwangalla, alisema haungi mkono hoja ya Zitto, kwa vile imejaa unafiki na kujitafutia umaarufu.
“Kama kweli tuna dhamira ya msingi ya kutumikia Watanzania kuna vitu vingi vilipaswa viondolewe na si posho peke yake. Kwa mfano, mashangingi yangefutwa kwa sababu yana gharama kubwa kuendesha.
Lakini yanahitajika kwa wabunge kutumia kuwafikia wananchi vijijini,” alisema Dk. Kigwangalla.
Alisema posho za vikao, ambazo Zitto anataka zifutwe, ni ndogo kulinganisha na majukumu yanayomkabili mbunge.

Dk. Kigwangalla alisema hata shida binafsi za wananchi, wanategemea zitatuliwe na mbunge, hivyo ni vigumu mbunge kufanya kazi bila kulipwa posho.
“Vinginevyo wanataka mbunge arudi mitaani kuganga njaa. Kwa hiyo, hiyo ni kauli ya unafiki, ya wanasiasa wanaotafuta umaarufu, mimi siwezi kuiunga mkono,” alisema Dk. Kigwangalla.
Kwa sasa mbunge analipwa Sh. 70,000 kwa siku kwa ajili ya kujikimu pamoja na Sh. 80,000 kama posho ya kikao kwa siku ambapo jumla analipwa Sh. 150,000 mbali na mshahara wake.

Kwa upande wake, mbunge wa viti maalum (CCM), Dk. Maua Daftari alipoulizwa kuhusu hoja hiyo hakuwa na jibu la kutoa.
Badala yake mbunge huyo alibaki anaguna na kukata simu bila ya kuiunga mkono ama kuikataa hoja hiyo.

Akitoa maoni yake, Ali Khamis Seif mbunge wa jimbo la Mkoani (CUF), alisema hoja ya kutaka posho ziondolewe ni nzuri lakini kwa sasa bado sio wakati wake.
Alisema mbunge ana kazi nyingi za kuwasaidia wananchi hivyo ikiwa ataondolewa posho watashindwa kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Hata hivyo alisema ikiwa fedha hizo zitaondolewa kwa mbunge ziingizwe kwenye mfuko wa jimbo ili zisaidie kusukuma mbele maendeleo ya wananchi.
Alitoa mfano kuwa kuna wabunge wengine wanatumia fedha hizo kuwasaidia wapiga kura wao kupata elimu pamoja na kupata matibabu kazi ambayo ingepaswa kufanywa na serikali.

Akizungumzia hoja hiyo, mbunge wa viti maalum (CCM), Diana Chilolo, alisema Zitto ana mtazamo finyu juu ya hoja hiyo ya kutaka posho ya vikao iondolewe. Alisema fedha anayoipata mbunge sio ya kwake pekee bali inawasaidia wananchi wengine wakiwemo yatima, walemavu, wajane katika kupata mahitaji yao.
Kila anapokuwa mbunge wananchi wake wanamuona kama nguzo na kimbilio lao, hivyo posho hizo zinasaidia kutatua matatizo madogo madogo kama hayo.
Mbunge wa jimbo la Meatu (Chadema), Meshack Opulukwa, akitoa maoni yake alisema bado anatafakari hoja hiyo.
Aliongeza kuwa hoja hiyo aliisikia jana, lakini kama Waziri Kivuli wa Kilimo, Chakula na Ushirika bado anaitafakari ili kuona kama ataiunga mkono hoja hiyo itakapopelekwa bungeni.

Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali, aliunga mkono hoja ya Zitto ya kutaka wabunge wasiwe wanalipwa posho za vikao.

Mkosamali alisema si posho tu, bali anataka pia mishahara wanayolipwa wabunge pia ipungue na kuwa chini ya ile wanayolipwa hivi sasa kwani hatua hiyo itasaidia kudhibiti mafisadi kuwania ubunge.
“Hatuhitaji watu wagombee kwa ajili ya kupata posho, maana kuna watu huwa wanagombea kwa lengo la kutafuta maslahi binafsi na si kuwawakilisha Watanzania, hivyo posho ikiondolewa na mishahara ikapunguzwa waroho wa madaraka watapungua” alisema Mkosamali.
Aliongeza: “Kwa hiyo, naunga mkono hoja ya kufutwa posho. Lakini mishahara ya wabunge pia ipungue, maana haiwezekani posho zipungue wakati mishahara iko palepale,” alisema. Mkosamali alisema kufutwa kwa posho kwa wabunge ni hatua muhimu kwani kuna maeneo mengi ya kijamii, kama vile hospitali, fedha hizo zinaweza kupelekwa kusaidia.
Alisema pia kupunguzwa kwa mishahara ya wabunge, ni muhimu kwani kutasaidia kuwafanya wanaotaka kuwania ubunge, kufanya hivyo kwa lengo la kuwawakilisha wananchi kwa dhati.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, naye pia aliunga mkono kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge, lakini alishauri posho hizo zibaki kwa vikao vya watumishi wasio na mishahara, kama vile wenyeviti wa vijiji.
“Mtumishi yeyote alipwe posho ya vikao, ambavyo sio sehemu ya majukumu yake,” alisema Kafulila.
Hata hivyo, alisema malipo ya posho za vikao, yasiishie tu kufutwa kwa wabunge, bali yafutwe serikalini na kwenye mahakama pia.
“Hatupaswi kulipwa kwa kukaa. Pesa nyingi inavuja. Mfumo wa sitting allowance (posho za vikao) must end (ikomeshwe),” alisema Kafulila.
Alisema pia posho nyingine zote zinapaswa kutozwa kodi na suala hilo liwe ni utaratibu na sera kwa mihimili yote ya dola; Bunge, Serikali na Mahakama.
Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu, aliunga mkono si kufutwa tu kwa posho za vikao kwa wabunge, bali hata mishahara nayo pia ifutwe akisema kazi ya ubunge haitakiwi malipo.
“Mimi maoni yangu ni kwamba, kwa kazi ya ubunge, wabunge hawapaswi kabisa kulipwa hata mshahara, ikifanyika hivyo itawafanya watu kujikita zaidi katika kuwatumikia wananchi,” alisema Mangungu.


Kwa upande wake, mbunge wa Mpanda mjini (Chadema), Said Arf aliunga mkono hoja hiyo ya Zitto na kusema kuwa umefika wakati wabunge kuwajali wananchi wenzao kwa kukubali kuachia posho zao ili ziweze kuwasaidia.
Aliwataka viongozi kupunguza anasa ili fedha hizo zisaidie watu wenye mahitaji ya lazima ikiwemo kuwapatia maendeleo.
Alisema mfumo unaotumiwa na Bunge wa kusema “ndiyoooo au hapanaaa” katika kupitisha hoja mbalimbali haufai kwa kuwa huo ni mfumo wa kijima.
Aliongeza kuwa hoja hiyo ya kutaka posho hizo ziondolewe inaweza kukwamishwa kwa kutumia mfumo huo wa upigaji kura kwa kusema ndiyo au hapana.


Juzi Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema haoni sababu mbunge kuendelea kulipwa posho nono kwa ajili ya kuhudhuria vikao kwa kuwa hiyo ni sehemu ya kazi yao ya kila siku.
Alisema anataka sheria ya Bunge inayotoa mwanya kwa wabunge kulipwa posho hizo ibadilishwe haraka ili kiasi hicho cha fedha kitumike kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania wengine wenye matatizo.

Zitto alisema ingawa suala hilo ni gumu, lakini ataliwasilisha katika mkutano wa Bunge la bajeti wakati atakapowasilisha bajeti yake kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi.
Alisema ana imani wabunge wenzake watakubali pendekezo hilo na kumuunga mkono kubadilisha sheria hiyo ili posho hizo zisiwe zinatolewa.

Katika Bunge lililopita aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibroad Slaa (Chadema), aliwahi kutoa wazo kama hilo pamoja na kupendekeza mshahara wa wabunge upunguzwe kwa kuwa ni mkubwa, lakini wabunge wenzake walipinga hoja hiyo kwa nguvu zote.

Dk. Slaa alishindwa kupitisha hoja yake katika Bunge lililopita baada ya wenzake kukataa kumuunga mkono huku baadhi yao wakitoa kauli za kumkejeli na kumuona kama mtu aliyekuwa akitafuta umaarufu wa kisiasa. Kiutaratibu wabunge wote hulipwa posho ya vikao ya Sh. 80,000 kwa siku, na posho ya kujikimu kwa kuwa nje makazi ya Sh. 70,000 hivyo kwa siku moja tu wabunge hulipwa wastani wa Sh. 150,000 siku za kazi, wakati mwishoni mwa wiki hulipwa Sh. 70,000, kwa maana hiyo kati ya wabunge wote waliopo ambao ni 350 kama posho hizo zitaondolewa serikali itaokoa kiasi cha Sh. milioni 52.5 kwa siku.
Mkutano wa Bunge la Bajeti unatarajiwa kuanza Juni 7, mwaka huu hadi Agosti 15, mwaka huu, kwa maana hiyo kutakuwa na siku za kazi 48 ambazo zitaigharimu serikali Sh. bilioni 2.52 kama posho ya vikao kwa wabunge.
Kiasi hicho kikiongozewa Sh. milioni 490 za posho ya kujikimu ya mwishoni mwa wiki ambazo ni kwa siku 20, serikali itakuwa inaokoa jumla Sh. bilioni 3.01 ambazo ni posho za wabunge bila mshahara.
Kiasi hicho kinaweza kuelekezwa kutunisha bajeti ya elimu, barabara au afya, ambako kuna upungufu mkubwa wa fedha.
Mshahara wa mbunge kwa sasa ni Sh. milioni 2.5, kiasi hicho kikichanganywa na posho ya mafuta, kuendesha ofisi mapato yake ya ubunge yanafika kiasi cha Sh. milioni 7.19.
Serikali inatarajia kutumia Sh. trilioni 12.8 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, kati ya hizo Sh. trilioni 8.8 ni kwa matumizi ya kawaida, yaani posho na mishahara na ulaji mwingine, wakati fungu la maendeleo ni Sh. trilioni nne tu.
Utaratibu wa kupitisha bajeti ya ulaji umekuwa ni utamaduni wa taifa hili, kwani hata mwaka huu wa fedha unaomalizika serikali ilipitisha bajeti ya Sh. trilioni 11.6, kati yake Sh. trilioni 7.7 zilikuwa kwa fungu la kawaida na Sh. trilioni 3.8 kwa ajili ya maendeleo.
Soma maoni yetu ukurasa wa sita
 
Makala yako na title vina gongana.
Nilivyoelewa unapendekeza wabunge wa CDM waache kuchukua posho za vikao, si kwamba tayari wamegoma au kutoa tamko la kufanya hivyo
 
Hili suala la posho za wabunge linalemaza sana baadhi ya wabunge kwa sababu hawagombei kwa maslahi ya wananchi wanagombea kwa maslahi yao wenyewe. Serikali ya CCM ilipotufikisha ni mahali pabaya kwa sababu imefikia mahali watu kuacha fani zao na kukimbilia bungeni kwa ajili ya kutafuta maslahi.
Ndugu WANAJF tuangalie majibu ya CHIGATI ambaye anategemewa na taifa la watanzania, ambao ni masikini na msemaji wa chama. Haiingii akilini kuwa na majibu kama hayo. Inamaana hilo ni tamko la chama au?
Chiligati na wenzie wanaokataa kupunguzwa kwa posho hizo wakumbuke waliowachagua na wao wanataka kuona maendeleo ya taifa lao sio maendelea ya familia zenu.
 
Wabunge wa ccm wapo ili waile hii nchi na sio kuijenga wanaobisha mabo kama haya yanapotokea watakubali tu!Unless wanamatatizo ya akili!
 
Serikali inatarajia kutumia Sh. trilioni 12.8 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, kati ya hizo Sh. trilioni 8.8 ni kwa matumizi ya kawaida, yaani posho na mishahara na ulaji mwingine, wakati fungu la maendeleo ni Sh. trilioni nne tu.
Utaratibu wa kupitisha bajeti ya ulaji umekuwa ni utamaduni wa taifa hili, kwani hata mwaka huu wa fedha unaomalizika serikali ilipitisha bajeti ya Sh. trilioni 11.6, kati yake Sh. trilioni 7.7 zilikuwa kwa fungu la kawaida na Sh. trilioni 3.8 kwa ajili ya maendeleo.
Soma maoni yetu ukurasa wa sita
 
Serikali inatarajia kutumia Sh. trilioni 12.8 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, kati ya hizo Sh. trilioni 8.8 ni kwa matumizi ya kawaida, yaani posho na mishahara na ulaji mwingine, wakati fungu la maendeleo ni Sh. trilioni nne tu.
Utaratibu wa kupitisha bajeti ya ulaji umekuwa ni utamaduni wa taifa hili, kwani hata mwaka huu wa fedha unaomalizika serikali ilipitisha bajeti ya Sh. trilioni 11.6, kati yake Sh. trilioni 7.7 zilikuwa kwa fungu la kawaida na Sh. trilioni 3.8 kwa ajili ya maendeleo.
Soma maoni yetu ukurasa wa sita

hivi tunairudishaga ccm madarakani kwa sasbabu sisi ni wajinga au kwa sababu hatujui au ka sababu hatuna elimu ya kutosha
 
Najiuliza ni kwanin hao wabunge walipwe posho ya vikao wakati ndo kazi yao? Kama ndio hivyo wafanyakaz wote wakienda kazini walipwe posho!
 
hivi tunairudishaga ccm madarakani kwa sasbabu sisi ni wajinga au kwa sababu hatujui au ka sababu hatuna elimu ya kutosha

Zitto,

Ombi langu la kwanza futilia mbali ubunge wa viti maalum ni mzigo kwa taifa. Pili marupurupu ya posho yafutwe kwani milioni 8 wanazolipwa wabunge zinawatosha kutumikia wananchi sio mtaji wa utajiri bali ni wito. Hili taifa linaangamia halizalishi kitu wakati linatumia pesa kama serikali ya brunei .

Kama wakiwa wakaidi waache kwani matatizo ya Greece hayako mbali kuyakumba Tanzania.
 
Nimevutiwa sana na pendekezo la wabunge wa CHADEMA kuwa posho ya vikao ifutwe ili pesa zipelekwe katika kuboresha huduma za jamii.
Huo ni uzalendo wa hali juu kwa waheshimiwa wabunge katika kipindi hiki ambacho taifa letu linapitia katika mawimbi makubwa ya kuwepo kwa matatizo ya kiuchumi na kijamii.

Nachukua fursa hii kuwaomba waheshumiwa wakiongozwa na ZITO waepuke kupokea posho za vikao katika bunge la bajeti na pesa husika zifunguliwe mfuko maalum kwa kusaidia jitihada za wananchi kujiletea maendeleo. Kama tujuavyo wawapo DODOMA wabunge wetu wanapata posho za aina 2; za vikao na kuishi, hivyo living allowanze waendelee kupokea ili jioni waonekane PAKO NI PAKO na viwanja vingine. ILA SITTING ALLOWANCE WAIEPUKE.

Kuchezwa kwa ngoma, kuanzishwa na mpigaji!

Kama serikali itakuwa sikivu basi itakuwa imeondoa mkanganyiko uliotokea katika kipindi hiki baada ya uchaguzi kama:
1. Kusafisha ofisi mara wanaposhindwa uchaguzi, kama walivyofa akina.........
2. Kutokudai madawati na kusema wamenunua kwa pesa zao nk.

CHADEMA WATAWANYOOSHA TU. :A S-rose:
 
Swali zuri sisi ni wajinga uelewa uko chini,ukiachilia mbali wizi wa kura wa ccm wakisaidiwa na usalama wa taifa.
 
Kuna mijitu migumu sana kuelewa, hapa kinachosemwa ni badiliko la mfumo wa sitting allowance, hii ikianza na wabunge wakapata uchungu itashika mpaka kwenye ngazi za chini kabisa na hapa maendeleo na uzalendo wa kweli utaonekana maana watu watajituma kwa ajili ya taifa ila sio maslahi binafsi.
 
Sidhani kama kuna mtu asiependa hela. Si mbunge wa upinzani au wa chama tawala. Atakaesema hapendi hela basi amepungukiwa.
Lakini hili sio swala hapa.
Swala ni priorities za viongozi, haki za wananchi na viongozi, wajibu na transparency, responsibility, focus etc
Attributes za wabunge zinaonekana wazi sasa.
Wanaosema eti wanaotaka kuitoa basi waache zao, inaonyesha dharau kwetu, au ujinga wa ajabu!!!
Hivi walisema kweli au ni waandishi wa habari wanachochea tu?
Mie nasita kuamini.
Manake kwa uelewa wangu, kinachotakiwa hapa ni kubadili MFUMO mfumo ambao utaondoa wabunge kuwa walezi wa masikini katika majimbo yao, na kufanya wabunge wawe viongozi na chachu ya maendeleo, tupunguze foleni wa kuombwa misaada kila wanapokuja majimboni, bali tuongeze watu wanaofanya kazi kuendeleza majimbo mbunge akiwa mbele.

Huwa nashangaa sana, tukienda kwenye vikao, eti wafanyakazi wa serikali wanalipwa kwa kuja kwenye mikutano inayowahusu, ambayo ni part ya kazi yao???
halafu sie tunaondoka tu
Hapa kuna tatizo KUBWA SANA si bungeni tu, ni mfumo mzima wa serikali. Sishangai kwanini mishahara inaonekana kama haiwezi kuongezwa, kwani hela yote inaishia kwenye posho za wachache wenye kuitwa kwenye warsha, semina, mikutano, trainings etc.

JE HUU NI MUDA AMBAO TUNAWEZA KUIPIGANIA HII HOJA YA UPINZANI?
 
Kama CDM wana uchungu na Nchi hii suala lisipopitishwa bungeni, basi posho zao wao waziashie mfuko maalum wa shughuli za maendeleo nchini. Hapo ndipo nitaamini wanachodai wanamaanisha hivyo..
 
Back
Top Bottom