Posho na Mishahara ya wabunge...

Wabunge wang`aka kuguswa posho zao
NA MWANDISHI WETU
3rd June 2011

1. Wamshambulia Zitto kuwa anasaka umaarufu
2. Wasema upinzani waziache, wao watachukua

Naye Mbunge wa Magomeni visiwani Zanzibar, Mohammad Chomboh (CCM), alisema suala hilo halitekeleziki kwa kuwa Sh. 80,000 anayolipwa mbunge kama posho ni ndogo ikilinganishwa na hali halisi ya maisha ilivyo sasa.
Alisema kulala nyumba ya wageni kwa siku wanapokuwa Dodoma ni Sh. 50,000 hapo bado hawajala hivyo kiasi hicho sio kikubwa kama inavyoelezwa na upinzani.

Kwa sasa mbunge analipwa Sh. 70,000 kwa siku kwa ajili ya kujikimu pamoja na Sh. 80,000 kama posho ya kikao kwa siku ambapo jumla analipwa Sh. 150,000 mbali na mshahara wake.

[/COLOR][/B]

Hawa Chama Cha Magamba huwa siwaelewi, anaposema kulingana na maisha ya sasa 150,000 haitoshi kwa siku, wakati watumishi wengi serikalini ndio mshahara wao sijui alimaanisha anatuma ujumbe gani kwao.

Hawa si wawakilishi wa wananchi bali wa CCM na mafisadi
 
Hivi tukiwa wa kweli 150,000/=Tshs kwa siku ni hela ndogo?mbona mwl wa shule ya msingu anaishi mwezi mzima kwa hela hiyo?analipa kodi, anasomesha na mahitaji mengine lakini mbunge anadai ni ndogo?inabidi ifike wakati watambue wamechaguliwa kutatua matatizo ya wananchi a sio kujipa utajiri.

ushauri wangu ni huu,

Hizi fedha wasipewe mkononi ila zikusanywe na kwenda jimboni kufanya maendeleo mengine na siku ambayo mbunge hatihudhuria zikatwe km kawaida na hapo wananchi watajua ni kiasi gani mbunge wao anawajibika na maendeleo yatakuja tu jimboni mfano siiting allowance ya 80,000 mara 14 ji sawa na 2,400,000/=Tshs hakika zinatosha sana kununua bati katika shule iliyoezuliwa kwa upepo au wananyasi kama paa lao, hebu chukulia posho hizi zipelekwe moja kwa moja jimboni na lazima kifanyike kitu cha kuonekana baada ya miaka 5 maendeleo yatakauwa yamefikia wapi?kama kweli wapo kwa maslahi ya wananchi lets them work on this
 
Posho za vikao ni dhuluma dhidi ya kodi za wananchi

Juzi Waziri Kivuli wa Fedha ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema, Zitto Kabwe, alisema kuwa kambi ya upinzani inapendekeza kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge na hata katika mikutano ya watumishi wa serikali ili kuokoa fedha zitakazoelekezwa kwenye mambo mengine muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Katika mkakati huo, ni dhahiri serikali itaokoa mabilion ya shilingi ambazo zitasaidia katika maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekosa fedha kwa sababu ya visingizio vya ufinyu wa bajeti, sekta ambazo zimekuwa zikiyumba kwa sababu ya ufinyu wa bajeti ni pamoja na elimu, afya, nishati na ujenzi wa miundombinu kama barabara na reli.
Kwa mwaka wa fedha ujao, yaani 2011/2012 serikali inatarajiwa kuwa na bajeti ya Sh. trilioni 12.8 ikiwa ni juu kwa Sh. trilioni 1.2 ikilinganishwa na bajeti inayomalizika ya mwaka 2010/2011 ambayo serikali ilikadiria kutumia Sh. trilioni 11.6.
Kama ilivyokuwa mwaka huu wa fedha unaomalizika, ambao kiasi cha Sh. trilioni 7.7 kilitumika kwa matumizi ya kawaida (ulaji tu) na Sh. trilioni 3.8 kwa shughuli ya maendeleo, mwaka ujao hali itakuwa mbaya zaidi kwani kiasi cha Sh. trilioni 8.8 kinatazamwa kama matumizi ya kawaida, wakati Sh. trilioni 4 tu ndizo kwa ajili ya maendeleo.
Kwa vyovyote itakavyoangaliwa bajeti ya namna hii ni ya kula, yaani theluthi mbili ni kwa shughuli za kulipana mishahara na posho nyinginezo wakati maendeleo yakiambulia theluthi moja tu. Huu umekuwa ni ugonjwa wa taifa hili kwa miaka mingi, nguvu nyingi sana zinaelekezwa kuhemea chakula, maendeleo yanapewa kipaumbele kwa uzito mdogo sana.
Katika mfumo wa namna hiyo si jambo la ajabu kusikia mbunge akishauri sasa posho za vikao zipigwe marufuku kwa sababu mbali ya kugharimu fedha nyingi za walipa kodi, pia zimejenga utamaduni wa kuishi kwa udanganyifu. Kazi hazifanyiki watu wakifukuzana na posho hizi, ufanisi unashuka katika sehemu za kazi kwa sababu kwa kawaida nguvu nyingi zinaelekezwa kusaka posho za vikao.
Kwa mtindo huo, kwanza serikali inashiriki kwa kusaidia watu kukwepa kulipa kodi kwa sababu mapato yote ya posho hayakatwi kodi, wanaokamuliwa ni watu ambao hawana nafasi ya kunufaika na vikao vya posho; lakini la pili ambalo ni kubwa na baya zaidi, posho hizi zinajenga mfumo wa malipo mara mbili kwa watumishi wa serikali na hata kwa wabunge.
Kama serikali inaweza kulipa posho za vikao vyote hivi, ni kwa nini inakuwa na kigugumizi cha kuboresha mishahara ya watumishi wake wote, ili iwe bora, na hivyo kuwa chachu ya uchapakazi na uwajibikaji uliotukuka na kwa njia hiyo kuwa na uwazi juu ya vipato halisi vya watumishi wa umma kuliko ilivyo sasa ambako asilimia kubwa ya mapato ya watumishi wake yamefichwa kwenye posho ambazo hata hivyo ni siri kati ya mtumishi na mtumishi; kati ya idara moja ya wizara na nyingine lakini pia kati ya wizara na wizara.
Kama ilivyo katika sekta binafsi, kila anayeajiriwa anajua wazi nini mapato yake, yameanishwa kwenye mkataba, hatarajiwi kuishi kwa ujanjaujanja, anapimwa utendaji wake kulingana na mkataba kwa kuwa hana kisingizio, kama ni mshahara ni mzuri kama ni mazingira ya kazi ni mazuri na mwisho wa yote kama ni kodi za serikali zinakatwa moja kwa moja kwenye mshahara wake ambao uko wazi.
Tunaamini na kwa kweli huo ndio ukweli, serikali ama kwa makusudi au kwa kutokujua imekuwa ikishiriki katika kulea utamaduni wa kukwepa kulipa kodi, mfano halisi ni ulipaji wa posho za vikao; haya ni mapato ambayo yanajulikana wazi kabisa. Kwa mfano wabunge wanajua kwamba kwa mwaka wana mikutano minne, Februari, Aprili, Juni na Novemba; mikutano yote hii ina vikao kadhaa kulingana na urefu wake, hivyo si jambo la kubahatisha, mbunge anafahamu vilivyo kila mwaka mapato yake kutokana na posho za vikao ni kiasi gani, si kitu cha kubahatisha hata kidogo.
Hali hii ya uhakika wa posho za vikao si kwa wabunge tu, watumishi wa ngazi fulani serikalini nao wanajua vilivyo kila mwezi hawawezi kukosa mapato ya kiwango fulani kutokana na vikao vingi vikiwa ni sehemu ya kazi zao za kawaida kabisa.
Katika hali hii tunashindwa kujua ni kwa nini wabunge wanalipwa posho za vikao ambavyo ndiyo msingi wa kazi ya ubunge, kadhalika hatuelewi inakuwaje watumishi wa umma nao wanalipwa posho wanapokuwa wanatekeleza wajibu wa ajira zao kwa kufanya kazi ambazo ndizo zinawapa mshahara mwisho wa mwezi. Kwa macho ya kiungwana na bila kutafuna maneno tunaamini kuwa malipo ya posho za vikao ni aina nyingine ya ulipaji ujira mara mbili kwa kazi moja.
Inawezekana ukawa ni ufisadi uliorasimishwa. Serikali ni lazima sasa ianze kujiondoa katika mitego hii mibaya kama kweli inataka kusonga mbele katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, si kuandaa bajeti ya kula mwaka baada ya mwaka.

CHANZO: NIPASHE
 
Posho za vikao ni dhuluma dhidi ya kodi za wananchi

KATUNI(458).jpg

Juzi Waziri Kivuli wa Fedha ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema, Zitto Kabwe, alisema kuwa kambi ya upinzani inapendekeza kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge na hata katika mikutano ya watumishi wa serikali ili kuokoa fedha zitakazoelekezwa kwenye mambo mengine muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Katika mkakati huo, ni dhahiri serikali itaokoa mabilion ya shilingi ambazo zitasaidia katika maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekosa fedha kwa sababu ya visingizio vya ufinyu wa bajeti, sekta ambazo zimekuwa zikiyumba kwa sababu ya ufinyu wa bajeti ni pamoja na elimu, afya, nishati na ujenzi wa miundombinu kama barabara na reli.
Kwa mwaka wa fedha ujao, yaani 2011/2012 serikali inatarajiwa kuwa na bajeti ya Sh. trilioni 12.8 ikiwa ni juu kwa Sh. trilioni 1.2 ikilinganishwa na bajeti inayomalizika ya mwaka 2010/2011 ambayo serikali ilikadiria kutumia Sh. trilioni 11.6.
Kama ilivyokuwa mwaka huu wa fedha unaomalizika, ambao kiasi cha Sh. trilioni 7.7 kilitumika kwa matumizi ya kawaida (ulaji tu) na Sh. trilioni 3.8 kwa shughuli ya maendeleo, mwaka ujao hali itakuwa mbaya zaidi kwani kiasi cha Sh. trilioni 8.8 kinatazamwa kama matumizi ya kawaida, wakati Sh. trilioni 4 tu ndizo kwa ajili ya maendeleo
.
Kwa vyovyote itakavyoangaliwa bajeti ya namna hii ni ya kula, yaani theluthi mbili ni kwa shughuli za kulipana mishahara na posho nyinginezo wakati maendeleo yakiambulia theluthi moja tu. Huu umekuwa ni ugonjwa wa taifa hili kwa miaka mingi, nguvu nyingi sana zinaelekezwa kuhemea chakula, maendeleo yanapewa kipaumbele kwa uzito mdogo sana.
Katika mfumo wa namna hiyo si jambo la ajabu kusikia mbunge akishauri sasa posho za vikao zipigwe marufuku kwa sababu mbali ya kugharimu fedha nyingi za walipa kodi, pia zimejenga utamaduni wa kuishi kwa udanganyifu. Kazi hazifanyiki watu wakifukuzana na posho hizi, ufanisi unashuka katika sehemu za kazi kwa sababu kwa kawaida nguvu nyingi zinaelekezwa kusaka posho za vikao.
Kwa mtindo huo, kwanza serikali inashiriki kwa kusaidia watu kukwepa kulipa kodi kwa sababu mapato yote ya posho hayakatwi kodi, wanaokamuliwa ni watu ambao hawana nafasi ya kunufaika na vikao vya posho; lakini la pili ambalo ni kubwa na baya zaidi, posho hizi zinajenga mfumo wa malipo mara mbili kwa watumishi wa serikali na hata kwa wabunge.
Kama serikali inaweza kulipa posho za vikao vyote hivi, ni kwa nini inakuwa na kigugumizi cha kuboresha mishahara ya watumishi wake wote, ili iwe bora, na hivyo kuwa chachu ya uchapakazi na uwajibikaji uliotukuka na kwa njia hiyo kuwa na uwazi juu ya vipato halisi vya watumishi wa umma kuliko ilivyo sasa ambako asilimia kubwa ya mapato ya watumishi wake yamefichwa kwenye posho ambazo hata hivyo ni siri kati ya mtumishi na mtumishi; kati ya idara moja ya wizara na nyingine lakini pia kati ya wizara na wizara.
Kama ilivyo katika sekta binafsi, kila anayeajiriwa anajua wazi nini mapato yake, yameanishwa kwenye mkataba, hatarajiwi kuishi kwa ujanjaujanja, anapimwa utendaji wake kulingana na mkataba kwa kuwa hana kisingizio, kama ni mshahara ni mzuri kama ni mazingira ya kazi ni mazuri na mwisho wa yote kama ni kodi za serikali zinakatwa moja kwa moja kwenye mshahara wake ambao uko wazi.
Tunaamini na kwa kweli huo ndio ukweli, serikali ama kwa makusudi au kwa kutokujua imekuwa ikishiriki katika kulea utamaduni wa kukwepa kulipa kodi, mfano halisi ni ulipaji wa posho za vikao; haya ni mapato ambayo yanajulikana wazi kabisa. Kwa mfano wabunge wanajua kwamba kwa mwaka wana mikutano minne, Februari, Aprili, Juni na Novemba; mikutano yote hii ina vikao kadhaa kulingana na urefu wake, hivyo si jambo la kubahatisha, mbunge anafahamu vilivyo kila mwaka mapato yake kutokana na posho za vikao ni kiasi gani, si kitu cha kubahatisha hata kidogo.
Hali hii ya uhakika wa posho za vikao si kwa wabunge tu, watumishi wa ngazi fulani serikalini nao wanajua vilivyo kila mwezi hawawezi kukosa mapato ya kiwango fulani kutokana na vikao vingi vikiwa ni sehemu ya kazi zao za kawaida kabisa.
Katika hali hii tunashindwa kujua ni kwa nini wabunge wanalipwa posho za vikao ambavyo ndiyo msingi wa kazi ya ubunge, kadhalika hatuelewi inakuwaje watumishi wa umma nao wanalipwa posho wanapokuwa wanatekeleza wajibu wa ajira zao kwa kufanya kazi ambazo ndizo zinawapa mshahara mwisho wa mwezi. Kwa macho ya kiungwana na bila kutafuna maneno tunaamini kuwa malipo ya posho za vikao ni aina nyingine ya ulipaji ujira mara mbili kwa kazi moja.
Inawezekana ukawa ni ufisadi uliorasimishwa. Serikali ni lazima sasa ianze kujiondoa katika mitego hii mibaya kama kweli inataka kusonga mbele katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, si kuandaa bajeti ya kula mwaka baada ya mwaka.

CHANZO: NIPASHE

hapo kwenye red hapo , sitaki hata kurudia kupasoma
 
Mimi nilikuwa najaribu kuifuta hii thread lakini kumbe sina maamlaka, maana inaniharibia wkend yangu, sipendi kunywa serengeti huku moyo unakwazwa na wafianchi
 
Ama Kweli inauma sana, wabakula zaidi ya mapato. Sasa hayoo maendeleo si ndoto
 
Wananchi sisi ndiyo tunaowapa ulaji huo wanaoutetea hata kuwafanya wawe vipofu kwa akuto kutona kama wapo kwa ajili yetu.

Kuna Mbunge mmoja ambaye alikuwa waziri kwa upofu wake wa fedha hizi hizi althubutu kusema wananchi watakula majani lakini ndege ya raisi itanunuliwa...huu upofu tu wa kutokujua yupo pale kwa matakwa ya wananchi.

Huyo huyo alishakuwa kwenye kundi fulani la wabunge kutetea maslahi ya wananchi kabla hajazibwa mdomo kwa kupewa uwaziri.
Leo hii tunashuhudia viongozi hawa wanaotujali siku za kampeni na uchaguzi wakituona sisi mambumbu wajinga mazumbukuku, hatuji kitu, tunafaa kununuliwa bajaji na pikipiki kama magari ya kubeba wagongwa, wakati kuna ndege zilinunuliwa kwa bei juu na kwa njia zisizo halali, tunashuhudia mishahara hewa, tunashuhudia bajeti yenye fedha za dhalura isiyo ya muhimu kubwa kuliko gari mia mbili za wagonjwa na wabunge wataipitisha hiyo pia.

Tumeshuhudia miswaada ya nyongeza za mishahara na posho za wabunge zikipitishwa kwa siku moja tu, hali mishahara ya walimu, wazee wa east africa wazee wa watu wakilala hata barabarani na kupigwa na na jua hata mabomu, huku wafanyakazi wa reli wakilia na mwajiri wao lakini hakuna mbunge hata mmoja anayethubutu kuyasemea hayo.

Sasa uchaguzi wa 2010 umepita ujao wa 2015 ndo umeanza hatutawasahau kabisa hawa wanaojiita wapo kwa ajili ya wananchi huku hawawatetei, tunanza kuwamurika mpaka 2015 lazima wote waangushwe hata wakihonga hawatachaguliwa.

Wananchi sisi ndo tumeshika hatima ya hawa wabunge wazembe wanaojiona wao ni wao na familia zao huku wanasahau kura zetu zimewapa kula kwao.

Wabunge mkumbuke hatutaki ushabiki mikwa kule bungeni, hapa sasa ni hawa wabunge wa CCM hatutaki ushabiki usiokuwa na maslahi ya wapiga kura wenu, tunataka heshima ya bunge letu, tunataka maendeleo ya kule kinusi, malolo, mlunga, kule mbinga/mbambabey, kule Image, kule matae, kule kamsamba, kule namanyere, kule tunduru, kule mlimba, kule ikungi, kule Mwiga, kule Mbaga, kule ushirombo, ndiko kura zenu mlikozipata.

Je hamuoni kuwa natakiwa kukataa siasa zinazowafanya wananchi wajinga? zinazowafanya wananchi wale mifuta na ninyi mle minofu?

Tunaahidi kuwachuja kuanzia sasa mpaka 2015 mtakapo kuwa mmechujika vya kutosha.

Aluta Continua!
 
Nilimsikia Fisadi Chiligati akiropoka ohh kama hwachukui waache. So far hakuna jibu lolote la kitaalamu toka CCM juu ya athari za kukatishwa posho hizo. Hapo zinanidhihirishia kuwa ni RUSHWA. Wananchi tuzipinge sasa wazi wazi posho hizo watu wanajilipa mara 2 kwa kutimiza wajubu wao waawaida kabisa. Huo no wizi.
 
wewe wasema kuna wajinga wengi sana inchi hii

mimi nadiriki kusema wabongo wengi ni majinga, wasaliti, wanafiki na wengi wao hawajui nini kinaendelea mimi sipendi mstakabali huu uliopo mpaka sasa ila sometimes naona bora yaendelee kunyonywa mpaka yawe kama nyonyo za mbwa mzee..

Mimi binafsi sina shida ila kila wakati najaribu kuwaelimisha watu kuhusu haki na wajibu wao wa msingi ilaa ni kama una mpigia mbuzi gitaa ila watu wengi wa kanda ya ziwa yaana Mwanza, Shinyanga, Mara, Bukoba, Kilimanjaro Arusha Mbeya Ruvuma na Iringa naona wapo makini na ndo watu walioendelea na wataendelea siku zote maana wako tayari kwa mabadiliko yaani kama Dar ni mavi matupu
 
U r right kwa kweli sisi wabongo ni wanafiki, wabaya tena dumilakuwili. I remembered working somewhere in one of the institution and i was fighting for our rights and employees incentives ---- things which were straight forward lakini hawa hawa wabongo wenzangu instead yakunisuport they turned against me. Yani ndio tulivyo wanafiki. That is why we cannot advance.

Unawezaje kuona mwizi na bado unambeba ??? Lets be realistic kwa kweli hizo posho is stealing. Hizo posho can put our infrastructures good in our country lakini nchi inatafunua na wachache na sisi tunapaki kukaa. Wenzako akisema wana fitini. Imefika wakati inabiidi watanzania tukuie kiakili.
 
U r right kwa kweli sisi wabongo ni wanafiki, wabaya tena dumilakuwili. I remembered working somewhere in one of the institution and i was fighting for our rights and employees incentives ---- things which were straight forward lakini hawa hawa wabongo wenzangu instead yakunisuport they turned against me. Yani ndio tulivyo wanafiki. That is why we cannot advance.

Unawezaje kuona mwizi na bado unambeba ??? Lets be realistic kwa kweli hizo posho is stealing. Hizo posho can put our infrastructures good in our country lakini nchi inatafunua na wachache na sisi tunapaki kukaa. Wenzako akisema wana fitini. Imefika wakati inabiidi watanzania tukuie kiakili.
 
Ama Kweli inauma sana, wabakula zaidi ya mapato. Sasa hayoo maendeleo si ndoto
ni sawa na mkulima kala mbeegu halafu anamwagilia akingojea kwenda kuvuna siku ya mavuno . wewe unategemea nini kipindi cha mavuno? atavuna kweli?
 
Nilimsikia Fisadi Chiligati akiropoka ohh kama hwachukui waache. So far hakuna jibu lolote la kitaalamu toka CCM juu ya athari za kukatishwa posho hizo. Hapo zinanidhihirishia kuwa ni RUSHWA. Wananchi tuzipinge sasa wazi wazi posho hizo watu wanajilipa mara 2 kwa kutimiza wajubu wao waawaida kabisa. Huo no wizi.

hawa ni wachumia matumbao na sisi wananchi tulivyo wajinga bado tunazdid kuwapa nchi tu huku tukipewa pipi na kanga
 
Kwenye hili hatuhitaji wataalamu wauchumi kutuelekeza kwa vile ni jambo ambalo liko wazi kabisa, kiasi kikumbwa cha fedha kinaelekezwa kwenye matumbo ya watu badala ya mambo ya msingi ya maendeleo ya nchi yetu. Kama tutapata kiongozi mzuri ni yule atakayetutoa kutoka hapa kwenye ukweli huu wa bajeti yetu. Hili ni jibu la kwa nini tanzania ni maskini.
 
Kama muheshimiwa zito alivyo taja baadhi ya taasisi za uma zinavyo ponda kodi ya wananchi kwa mgongo wa posho nadhani na hawa wanafunzi wa vyuo vikuu wapewe posho basi wakiingia kwenye lecture zao. Ni watu muhimu sana kwa taifa hili...jamani tuwafikirie, au mnasemaje wana jamii?
 
Back
Top Bottom