Sir robby
JF-Expert Member
- Jun 22, 2022
- 2,400
- 4,074
Wadau hamjambo? Nadhani kupokea posho au mishahara ukiwa huna sifa za kazi yako ni wizi.
Ndio maana watumishi wa vyeti fake yaliwakumba na kufukuzwa kazi na ripoti ya CAG ilionesha kiasi gani cha fedha za umma zilipotea na kuokolewa baada ya kuwafukuza.
Nimeshangazwa na Ripoti ya CAG kutokuonyesha upotevu wa fedha za umma unaotokana na kuendelea kuwalipa mishahara na posho Wabunge 19 waliofukuzwa uanachama wao na chama chao na kupoteza sifa za kuwa Wabunge lakini mpaka leo wanalipwa posho na mishahara.
Binafsi sioni tofauti na hao wengine wanaolalamikiwa leo kuwa ni wezi wa mali za umma na kwamba watupishe.
Tufike mahali tuwe wakweli, Wabunge 19 ni wezi wa fedha za umma kama wezi wengine kwani wanalipwa pisho na mishahara wakati wao sio Wabunge halali, ni wabunge feki tunaotaka Katiba ya nchi iheshimiwe waondolewe Bungeni na washtakiwe kwa uhujumu uchumi.