Nyalandu asitukanwe, kazi aliyoifanya CHADEMA inatosha

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,849
Ni mwanasiasa gani hapa nchini anaweza acha ubunge ndani ya chama tawala akaenda chama cha upinzani ndani ya utawala wa kidicteta?

Ni mbunge gani wa CCM angeweza kwenda Kumjulia hali Tundu lissu Nairobi na hata Ubeligiji ndani ya utawala wa Dikteta?

Ni mbunge gani wa CCM angeacha chakula na kuishi bila mshahara wa ubunge kwa miaka 4 tena ndani ya utawala wa kikatili kama wa Magufuli?

Naombeni tutunze akiba ya maneno binafsi sina tatizo na Nyarandu kilichomtoa ccm ni juu ya uminyaji wa haki za binadamu ulifanywa na Magufuli.

Sasa kama ameona aliyekuja sio katiri na hana visasi juu ya wengine kwanini asimuunge mkono?

Tujifunze kuishi kwa kupokea hisia za watu Ila kama watu ambao wanatakiwa kuheshimiwa na chadema basi ni hawa watu wawili ni Dr Slaa na Nyalandu.

Wameacha athari ndani ya chadema tuache kumsimanga Nyalandu tumtakie maisha mema

Siasa sio uadui.
 
BAVICHA hawawezi kuacha kumtukana Nyalandu!

Kama Mdee anatukanwa leo kwa kuitwa mzee Nyarandu ni nani?

Kama Dr Slaa leo anatukanwa pamoja na kuumia na kutokwa damu kwa ajili ya chadema Nyarandu ni nani?

Kamwe Bavicha hawawwzi kuacha tabia yao ya kutukana watu wanaotofautiana nao.

Hata Lisu leo akitoka chadema atatukanwa sana!
 
Na pia tuelewe , ndani ya miaka Mia ijayo wote tuliopo hai leo tutakuwa maiti , hata hvyo Tanzania itakuwepo ikichanja mbunga , sometime inabd utazame hatima yako , kuliko kuwaangalia wananchi wenye akili za darasa la saba

Hili nalo neno.
 
Katukanwa wapi?
hebu kwanza alitekwa wapi nasikia amesema alikuwa mateka au alikuwa mkimbizi
 
Sioni kama una haja yoyote ya kuja na huu upotoshaji, kwamba Nyalandu anatukanwa, kama anatukanwa basi ni sehemu ndogo sana kuliko ukweli anaopewa. Kimsingi Nyalandu kwa alichochuma alikuwa hategemei ubunge kuendesha maisha yake.

Nyalandu hakuuondoka ccm kwenda cdm kwa kufuata sera, bali alihitilafiana na Magufuli baada ya kumnyima uwaziri, ambao Nyalandu aliamini ni haki yake ya kudumu. Alikwenda kumsalimia Tundu Lisu sio lazima iwe kwa utu, bali pia ilikuwa ni kama sehemu ya kutingisha kiberiti dhidi ya Magufuli baada ya kunyimwa alichotegemea. Kumchanganya Slaa na Nyalandu ni kutaka kumtakatisha Nyalandu kwa Utetezi dhaifu. Kwahiyo huko ccm akipishana na huyo mama atahamia chama kingine tena? Maneno aliyoongea Nyalandu wakati anahamia cdm ndio yanamponza sasa. Hilo neno kutukanwa unalitumia tu kama bendera fuata upepo, lakini matusi ni machache kuliko ukweli anaopewa, na kimsingi matusi ya hapa na pale hayawezi kukosekana, maana hii ni mitandao ya kijamii na tabia zote zimo humu.
 
Bavicha hawawezi kuacha kumtukana Nyarandu!

Kama Mdee anatukanwa leo kwa kuitwa mzee Nyarandu ni nani?

Kama Dr Slaa leo anatukanwa pamoja na kuumia na kutokwa damu kwa ajili ya chadema Nyarandu ni nani?

Kamwe Bavicha hawawwzi kuacha tabia yao ya kutukana watu wanaotofautiana nao.

Hata Lisu leo akitoka chadema atatukanwa sana!

Naona unarukia kila uzi ili uweze kubeba ajenda zako za kumtetea yule dhalimu. Kwa bahati mbaya kila uzi unaorukia bado haubebi ajenda zako. Watu tuko next level na tuna uwezo wa kupima hoja ni ipi, na upotoshaji ni upi.
 
Wanasiasa wetu wengi ni wachumia tumbo.......wanafanya siasa za kimalaya malaya......

Popote penye uelekeo fedha au cheo wapo.....na popote wanapokinzana na maslahi yao hawapo.......

Ni aina ya wanasiasa ambao hawafai kuwepo kwenye jamii ya watu wanaopigania kujikwamua kutoka kwenye ukandamizaji......
 
Bavicha hawawezi kuacha kumtukana Nyarandu!

Kama Mdee anatukanwa leo kwa kuitwa mzee Nyarandu ni nani?

Kama Dr Slaa leo anatukanwa pamoja na kuumia na kutokwa damu kwa ajili ya chadema Nyarandu ni nani?

Kamwe Bavicha hawawwzi kuacha tabia yao ya kutukana watu wanaotofautiana nao.

Hata Lisu leo akitoka chadema atatukanwa sana!
Nani kamtukana? Hivi mitandao ndio press release ya chama? Kwanini maneno ya washabiki ndio huchukuliwa kwamba ni maoni ya Kamati kuu?

Badilikeni
 
Bavicha hawawezi kuacha kumtukana Nyarandu!

Kama Mdee anatukanwa leo kwa kuitwa mzee Nyarandu ni nani?

Kama Dr Slaa leo anatukanwa pamoja na kuumia na kutokwa damu kwa ajili ya chadema Nyarandu ni nani?

Kamwe Bavicha hawawwzi kuacha tabia yao ya kutukana watu wanaotofautiana nao.

Hata Lisu leo akitoka chadema atatukanwa sana!
Wacha umbea,na kamtukana? Nyie nguruwe wa Lumumba ndiyo mlimtukana alipokuja Chadema,mkasema ni mhujumu uchumi kwa kuuza Twiga wetu. Jifunzeni kufanya siasa za kistaarabu. Wacheni siasa za chuki na visasi alizo asisi yule dhalim mwendazake.
 
Heshima na matusi vitatokana na Nyalandu mwenyewe akitulia aliko kwenda CCM hakuna wa kumtukana lakini akijifanya kuwafurahisha CCM kwa kuisemea CHADEMA mambo ambayo hayapo atakuwa amejitukanisha mwenyewe kabla hajatukanwa na mtu yeyote.
 
Bavicha hawawezi kuacha kumtukana Nyarandu!

Kama Mdee anatukanwa leo kwa kuitwa mzee Nyarandu ni nani?

Kama Dr Slaa leo anatukanwa pamoja na kuumia na kutokwa damu kwa ajili ya chadema Nyarandu ni nani?

Kamwe Bavicha hawawwzi kuacha tabia yao ya kutukana watu wanaotofautiana nao.

Hata Lisu leo akitoka chadema atatukanwa sana!
Kwan mzee ni tusi??
Pumbavu mkubwa wewe
 
Na pia tuelewe , ndani ya miaka Mia ijayo wote tuliopo hai leo tutakuwa maiti , hata hvyo Tanzania itakuwepo ikichanja mbunga , sometime inabd utazame hatima yako , kuliko kuwaangalia wananchi wenye akili za darasa la saba
Mi mwenyewe nipo kwa maslahi yangu

Kila mtu apambane na hali yake

Yaan niache kula bata nipige kelele kwenu?? Maendeleo yana letwa na wewe mwenyewe

Wewe endelea kusubiri nikuletee maendeleo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom