MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,223
- 22,299
Ninashangazwa sana na kauli za makada waandamizi wa hiki chama cha Mbowe.. ni kauli zinazoashiria ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia inayotajwa kuwepo. Zaidi ya mara moja makada wa CHADEMA hasa Lema na Sugu wamekuwa wakijinadi kuwa watagombea ubunge kwenye majimbo ya Arusha na Mbeya kana kwamba wao ndo wenye hatimiliki za ubunge kwenye hayo majimbo. Inafikirisha mno aina ya demokrasia iliyopo CHADEMA.. je, hakuna wanachama wengine wa CHADEMA wanaotamani kupata nafasi ya kuwakilisha wananchi wa hayo majimbo bungeni?
Lema, Sugu, Msigwa, Heche, Pumbulu, Mbowe, Mnyika na baadhi ya makada wengine waliowahi kuwa wabunge tayari ni kama wameshajipitisha kugombea ubunge bila kujali katiba ya chama chao inavyotaka. Hata kwenye urais tayari Lissu kashapitishwa nje ya utaratibu wa katiba yao. Kama hawawezi kuwa na heshima kwa katiba yao hawataweza kuisheshimu katiba ya nchi. Ninamshukuru Mungu kwa kuweza kuwafunulia watanzania jinsi hiki chama kilivyojaa mbwa mwitu walijivika ukondoo kwa nje. Watanzania hawawezi kuruhusu watu wasioiheshimu katiba yao wenyewe kuingia ikulu.
Huku CCM hadi muda huu hakuna mbunge mwenye uthubutu wa kujinadi kuwa lazima atagombea tena kwenye jimbo lake 2025 kwa sababu wanajua kazi ya wajumbe kwenye mchakato. Michakato ya majimboni huwa inawatoa jasho sio kitoto. Sisi tunafurahia kwasababu demokrasia ndo inavyotaka. CCM ilishaamua kufuata katiba yake inavyotaka na sio kujiamulia kama ilivyo CHADEMA. Imeshathibitishwa kuwa CCM ndo inaweza kuongoza nchi hii. Hata wapinzani wanajua bila CCM imara hata wao watayumba. CCM ndo imebeba matumaini ya watanzania wote wakiwemo wafuasi wa chama cha Mbowe.