DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 301
Habari zenu wapendwa,kuna met wangu hapa oficn ana tatizo ambalo hata yeye mwenyewe haelewi ni tatizo gani,ni mtu ambaye relation zinamsumbua sana,amekuwa akitendwa mara kwa mara kwa ni mtu mwenye hasira na wivu sn,japo huwa akipenda anapenda kweli na wala huwa hatoki nje ya uhusiano anapokuwa mtu,relation yake ya mwisho ilikuwa na maumivu makali sana kwake kwan alimpata mtu aliyeza kumtuliza hasira na wivu wake na wakawa wameshatambulishana,wakiwa wanaendelea na relation met wangu akagundua jamaa ana mke wa ndoa na mtoto kupitia simu yake ila mke wake yuko mkoa mbeya ni mwalimu,alipomuuliza jamaa kutokana na ushahidi ikabidi akiri na kuomba msamaha ila ndio met wangu akakasirika na kuachana naye.
Sasa ni miezi minne tangu yuko single amekuwa ni mtu wa mawazo sn amepungua na ameshindwa hata kujipendezesha km awali,anasema upweke ndio tatizo anataman kuwa na mpnz na anahic hawezi kuwa peke yake, anataman apate mtu wa kumwonyesha mapnz yake na watu wanaomtokea wapo ila anashindwa kuwaamin na hata kuwa nao,nimejitahidi kumshauri nahata kumwonyesha sred za humu za kufanana na matatizo yake lkn tatizo haliishi na ameendelea kuwa hivyo,saa nyingine unakuta analia tu,nikimuuliza anasema anataman angekuwa na mpenz akamweleza anavyojisikia,kwakweli ni hali ambayo mie km binadamu mwenzia inanihuzunisha na nimeshindwa namna ya kumsaidia na kuamua nilete kwenu wadau tuone tumsahuri nn japo kumsaidia,nawakilisha.
Ashukuru kwanza Mungu amekuwa akimpigania kumuonyesha wapenzi ambao alikuwa nao sio waaminifu.Isije ikawa huko kulia ni kwasababu anampenda huyo mume wa mtu na alikuwa na mategemeo makubwa nae. Amsahau na awe na amani na amuombe Mungu atapata wa ukweli.