night_shadow
Member
- Aug 4, 2022
- 11
- 34
Nina mpenzi wangu ambaye natarajia kabisa kufunga naye ndoa, lakini kuna mambo ambayo naona yanakwenda kinyume na matarajio yangu. Kibinafsi, sipendi kufanya sherehe za harusi zenye gharama kubwa ambazo mara nyingine huwa ni israfu. Hata hivyo, mpenzi wangu ni mtu ambaye anathamini na kupenda mambo ya kifahari na ya kifani. Hali hii imedhihirika wazi wakati nilipokuwa katika hatua za maandalizi ya uchumba wetu(sherehe za engagement).
Gharama za sherehe ya engagement, kama ilivyokadiriwa, inaonesha itapita milioni tatu, na hii ni kiwango kikubwa sana kwangu. Gharama ya mavazi anayotaka kuvaa kwenye sherehe kisio lake ni takriban laki nne, na pete ya engagement inahitaji angalau laki nne ndio minimal cost.
Wakati nikijaribu kumshauri tupunguze matumizi yasiyo ya lazima kwenye sherehe, mpenzi wangu amekuwa na majibu yasiyofurahisha. Mara nyingine, amejisikia kuumizwa na kusema kuwa ninaonyesha kutomjali. Kwa hakika, sina tatizo na uwezo wa kifedha wa kugharamia mahitaji haya yote, lakini nashawishika kuwa ninaweza kutumia fedha hizi vizuri zaidi, hasa kwa kuzingatia kuwa hatujakomaa sana kiuchumi na tunahitaji kujiandaa kwa maisha yetu ya baadaye.
Naja kwenu kwa ushauri; naamini kuna wengi miongoni mwenu ambao wamewahi kukabiliana na changamoto kama hizi katika mahusiano yenu au maandalizi ya ndoa. Je, mnashauri vipi katika kushughulikia hali hii? Je, ni sahihi kwangu kupunguza gharama hizi kimyakimya bila mpenzi wangu kujua au bila kumuumiza mpenzi wangu kihisia? Au mpenzi wangu yupo sahihi kusimamia maoni na matarajio yake? Najiuliza iwapo uamuzi wangu wa kumwacha ni wa busara, au kuna njia bora ya kutatua tofauti zetu hizi.