Naomba ushauri anipenda au kanichoka?

Bwajilo

JF-Expert Member
Dec 5, 2021
345
880
Kwa kweli kaka Mimi naanza kwa kukiri katika mkasa huu Mimi ndiye chanzo cha matatizo na nimekuja kupata akili baada ya huyu mtu wangu kuwa haniamini, amekata tamaa na Mimi baada ya mlolongo wa matukio yangu kwake.

Nitajitahidi kujieleza kwa ufupi kiasi kwako ili upate pa kuanzia kutolea maamuzi na uvae uhalisia wake kama mwanaume halafu ndio unipe ushauri kwamba Kuna uwezekano wowote wa huyu kubaki na Mimi kaka?

KAKA D, kama uijuavyo familia yetu pale nyumbani nalelewa na mama, mzee wangu alishafariki tangu nikiwa mdogo, kwa kweli uzao wa mama yangu haujawahi kuwa bora kwa maana hakuna dada na kaka zangu walioonyesha njia ya kuwa wamepata malezi bora, dada yangu pekee hakumaliza kidato cha nne, bahati mbaya form two alizalishwa na sasa yuko nyumbani anauza genge lisilo na mbele wala nyuma.

Kaka zangu Yule G kama unavyomuona akiamka asubuhi ni bangi tu hataki kazi wala maongezi na mtu hataki, kula kwa mama na umri ule mpaka namwonea huruma anavyokonda kwa kuvuta bangi.

Yule kaka yangu mkubwa P ndio kama ujuavyo kazi yake ya bodaboda na tangu amepata ajali na alivyovunjika miguu sasa hivi hataki hata kusikia kuhusu bodaboda, kazi yake ni kuuza vikaranga stand Moshi ndio apate kula yake na ameshampa mwanamke mimba na nasikia wanaishi wote.

Hebu muangalie mama yangu, kazi yake ndio ile ya ulinzi mshahara nakumbuka aliniambia laki mbili, tunapanga vyumba viwili, tule, nisome na tuvae. Kwa maana hiyo mama amekuwa si mtuliaji wa nyumbani usiku ataingia kazini Kuna muda hata siku tatu nyumbani hayupo. Kwa kweli ni mapito makubwa tunayopitia.

Tukija upande wangu Mimi mwenyewe, kama unavyojua nilirudi tu nyumbani kiubishi baada ya kuona shule hawakubali mwanafunzi yeyote abaki, sasa kesho natakiwa 7/01 nilejee shule. Lakini Kuna kitu naona hakipo sawa ndani ya nafsi yangu. Nahisi nakwenda kumpoteza mtu ambae nauona moyo wake ulikuwa na nia ya kunifikisha mbali, ila utoto na ujana unakatisha ndoto nizionazo.

Iko hivi kaka kwa mazingira ya malezi na hali ya kiuchumi ya familia yangu na namna watu wanavyotudharau, ukuaji wangu kama binti umekumbwa na changamoto kubwa kubwa, na siongei kama tu binti wa uzuri wa wastani, bali kama unionavyo mdogo wako ni mrembo, rangi ya kichaga inawasumbua sana wanaume, tangu napata usichana nimepitia mkululo wa mapito ya wanaume na majaribu yao.

Nikiwa shuleni olevel walimu waliniwinda kama swala wa kitoweo, hatimae nikiwa kidato cha tatu mwalimu mmoja wa kujitolea pale shuleni alifanikiwa kunilaghai nikajikuta tumeanza mapenzi. Wanafunzi wenzangu nao wasio na idadi hawakuacha kunisumbua. Mtaani yaani nilibakwa na rafiki Yule wa kakaangu G, yeye tulikuwa tumemzoea kama rafiki wa kaka lakini alikuja kufanya kosa kubwa sana, nikamwambia mama nilishangaa tu limeisha kimya kimya na wazazi wa Yule kijana.

Kwa sababu ya matatizo ya kifamilia shuleni kote walijua kuanzia wanafunzi hadi walimu kwamba natoka familia duni, yaani sikuweza kulipa mchango wowote wa shule, kuanzia remedial mpaka mitihani ya wiki. Kuna baadhi ya walimu nashukuru waliikubali hali yangu na walinipa hali ya kupambana, kwa kweli waliniombea mpaka kwa wenzao nikatolewa kwenye huduma za malipo yote shuleni. Lakini pia Kuna waliotaka kutumia uduni wangu na unyonge wa mama yangu kunitendea unyanyasaji wa kijinsia.

Nikiwa kidato cha tatu mwishoni Kuna mkaka mmoja wa miaka kama 30 hivi ni mfanyabiashara alitokea kunipenda sana. Uzuri wa huyu kaka alikuwa muwazi sana, hakuhitaji tujihusishe na mapenzi alitaka nisome Kwanza nimalize mambo mengine yatajulikana baadae. Kwa kweli kwa kipindi hiki sikuwa najua hata uhalisia wa kumpenda mtu, na ukizingatia ukatili niliofanyiwa huko nyuma na wanaume, tena wengine ndio hao ambao jamii inawachukulia kama kioo, nilitokea kuwachukia mnoo viumbe ninyi. Ila kwa vile niliona amenipa plan ya now and future by that time nikaona hakuna madhara kumkubalia.

Basi bhana maisha yangu yalianza kupata nuru kuanzia hapo. Kutoka kushinda na njaa shuleni mpaka kuachiwa 5000 Kila siku, wiki 35,000/_ naapewa za kula shuleni najua kaka utanishangaa lakini nikikuambia kwa mwanafunzi huu ni mpunga mrefu na ukizingatia sipandi gari kwenda shule. Basi ukiacha gharama za shule lakini hata mahitaji yangu yote kama binti aliyabeba yeye na nilishukuru alimpunguzia mama majukumu lakini hata shuleni nilianza kupata utulivu wa kiakili na ufaulu wangu uliongezeka maradufu.

Kwa kweli huyu kaka hajawahi kuchoka na mpaka namaliza kidato cha nne hakuwahi kuniambia tufanye mapenzi ukiacha spoil zote hizo alizofanya. Kama nilivyosema kwa umri wangu sikuwa najua utii na maana ya mtu kukupenda, so Kuna wakati nilikuwa tu naona kama mtu aliyejitolea kunisaidia tu na sio mpenzi.

Nilipo maliza kidato cha nne, nikawa niko nyumbani, hapa nikaanza kuona uchungu wa kubaki home, ile 35,000 kwa wiki imekata, na ratiba ya home kula msosi mmoja daily yaan saa 9 Leo utakula tena kesho muda kama huo. Nikamwita Yule mkaka tukakaa nikamweleza ajaribu kunitafutia sehemu ya kujishikiza kwa kipindi nasubiri matokeo. Yaani uwezi amini nilivyomwambia tu akaniambia dukani kwake, duka la jumla alikuwa anataka kuongeza mdada wa kuangalia mahesabu anaona nitafaa na nitaweza. Hivyo akanitaka jumatatu ya next week nikaanze. Akaniambia atanilipa laki 2 na kula ni pale asubuhi, mchana. Kwangu niliona hela ni kubwa mno, yaani umri wangu naenda kupokea mshahara sawa na mama yangu, na kula juu nikaona Mungu ni mwema.

Nilipoanza tu kazi akaninunulia simu ambayo hata mama angu au familia yangu hakuna aliyewahi kuimiliki, na wote wakabaki kunishangaa. Simu hii ninayokuambia kaka ndio chanzo cha ushauri huu ninaokuomba sasa. Nilipokuwa pale dukani upande wa cash tulikuwa wadada wawili, kiukweli ile sehemu ilikuwa na changamoto kwa wadada, kulikuwa wanafika wateja wengi wa kiume, na wengi watataka namba waweke order wakiwa mbali. Changamoto kubwa ikawa ni kutongozwa Kila saa, yaani Kila mteja atataka akutongoze. Hapa kaka kama unavyonijua Mimi ni mpole na msio nzuri sana kwenye mabishano ukichanganya na nilivyolelewa kumkatalia au kumbishia mtu nilikuwa naona kama ujeuri. Nilichokuwa nafanya mtu akinitongoza Basi nitamwambia sawa, japo sina dhamira ya kufanya.

Yule boss na mpenzi wangu alikuwa busy kidogo unakuta my be week ataniita baada ya kazi tunakutana sehemu atataka kujua maendeleo yangu, ananikumbusha dhamira yake na atanisisitiza niendelee kujitunza na kuepuka vishawishi. Yaani kitu ambacho hakuwahi ni kushika simu yangu, hii ikanifanya nijisahau kuondoa maseji mbaya za watu. Sasa nilivyozoea kwenye lile eneo Kuna fremu nyingi sana. Nikajikuta sijui nimepatwa na nini nikatembea na wakaka wawili, mmoja fundi simu na mwingine muuza chipsi japo hawakujuana. Kusema ukweli nilijisahau sana, Muuza chipsi alifahamu kwamba fundi simu ndio bwana angu na kwa vile alikuja anajua hakuwa na shida.

Kaka kama ujuavyo mapenzi hayajifichi, yule kaka akasikia msichana wako anatoka na fundi simu, nakumbuka hiyo ni mwisho wa mwezi wa 6 kwenda wa 7 2023. Siku moja muda tumefunga ofisi narudi home tumefuatana na Yule fundi simu kwa mahaba ghafla boss katokea huyu tumepishana barabarani. Alichofanya Yule boss na mpenzi wangu alinipita kama hana mpango na mimi kama mita 15 Kisha, akageuka akaniita J njoo nikashtuka by that time Yule fundi simu hajui kama yule ni boss wangu ni mchumba wangu, kabaki pale ananisubiri.

Kufika akanitaka twende sehemu tukaongee. Na mbaya zaidi siku hiyo aliyonifuma mchana wake aliniomba nikitoka kazini tukutane ila nilimdanganya nitatoka na mama atanipitia akitoka hospitalini, kumbe nilikuwa Jana yake tumepanga hii siku tukutane na fundi simu. Nikawa nimetengeneza msala kuanzia hapo. Tulipofika Kwanza aliniomba simu na nikampa. Akaendelea na maongezi kwamba Nina mahusiano gani na kijana yule, nikajitahidi kumpanga na hakuwa na tabu akanielewa. Ila aliomba abaki na simu kwa siku ile, hapo ndio balaa langu lilipoibuka.

Kumbuka huu ni mwezi 6 mwishoni, matokeo ya kidato cha nne yalishatoka nilifaulu vizuri tu kwa divion 1 na tulishapangiwa shule natakiwa nikasome PCB moja ya shule za advance Mkoa wa Pwani. Hapo umebaki mwezi mmoja kama na nusu kwenda kuripoti shuleni, mwaka Jana tulitakiwa kuanza form five mwezi wa 8 katikati. Na mpaka muda huu huyu kaka ndiye aliyevaa majukumu yangu yote ya shule na nashukuru na Mimi mishahara yangu yote nilimpa mama anitunzie nikijua muda wa maandalizi ukifika nisipate shida.

Turudi kwenye simu sasa, boss aliondoka na simu, na kwa vile yule fundi simu alibaki muda mrefu kunisubiri akaanza na kutuma mameseji mengi mengi kaanza na za kubebika baadae zikafuata za mamlaka ya kukoroma as if mtu anam command mke wake. Si yeye tu kwa vile wavulana wengi walizoea kuchart na kunitongoza, boss wangu yule alikuta vitu vingi mno. Nakumbuka nilipomaliza shule nilitembea na mvulana mmoja ambae tulisoma darasa moja, ila nilitoka nae mara moja tu. Sasa nae akaanza kutuma tuma meseji na Yule boss akajifanya ni Mimi yule mvulana akamwaga Siri zote mpaka lodge tuliokutania very Sad..

Kilichofuata kesho yake nimekuja kazini yule boss akanichenjia ghafla kwamba natakiwa niache kazi na mshahara wa mwezi ujao kwa maana wa 7 atanilipa japo sitoingia kazini, hapo alijaribu kunipoza kwamba natakiwa nipate muda wa kupumzika kabala kurudi shule. Basi sikuwa na namna ikabidi nidrop kazi nikawa niko nyumbani. Sasa changamoto nikiwa nyumbani mambo hayaendi yaani nakuta hovyo tu na home kwa kipindi nipo kazini nilishaanza kuwa tegemeo fulani yaan nilikuwa nikitoka job sikosi 5,000/= ya kuwaachia nyumbani waongezee issue za msosi. Kwa kweli hata home waliboeka na hali hii.

Baada kama ya wiki moja yule boss akataka tukutane kwa maongezi. Ni kweli tulikutana na akionyesha mwanaume mmoja badala ya mwingine. Kumbuka hapa nimekupa orodha ya wakaka watatu ambao nimekutambulisha na wote wamejimwaga kwenye simu yaani sina nukta ya kupinga, na Kuna mmoja yule teacher niliekuambia alinipata nikiwa form 3, yeye hatukuachanaga sema tu nilimkatia mawasiliano baada ya kumpata huyu boss wangu, ila Kuna siku moja wakati nafanyakazi nakumbuka ni mwisho wa mwezi wa 4/2023 tulikutana na tulifanya mapenzi mbaya zaidi ni nyumbani kwake coz alikuwa kijana tu mdogo amepanga chumba chake. Huyu boss yule teacher hakufanikiwa kuwa na uhakika kwa kipindi kile kutokana walivyochart hakujifungua sana. Aliponiuliza kuhusu huyu nilimkatalia kabisa na akaamini kweli si mtu wangu.

Kwa siku ile nilijua kabisa mapenzi yake kwangu lazima yaishe. Kinyume na matarajio yangu nilivyoonyesha kujuta na kulia sana, sikuamini aliponiambia amenisamehe na bado ananipenda. Ila sasa akaniambia kwa sababu nimeshaanza kufanya mapenzi kinyume na mategemeo yake, hawezi tena kunisubiri hivyo nitapaswa tuanze kufanya mapenzi, kitu ambacho sikuona kama ni tatizo. Tuka organize siku nzuri tukatoka for the first time, kufika namkuta mtu kabeba mavipimo vya HIV, niliogopa but hakukuwa na namna tukapima, vizuri ni kwamba wote tulikuwa negative. Toka siku ile ikawa ni mpenzi wangu rasmi na kwa kweli yeye alinijenga zaidi muda mwingi alikuwa anapenda kuona namna atakavyobadilisha maisha yangu na mama yangu tofauti na hao wengine niliowahi kutoka nao.

Nakumbuka hakutaka tena kuniachia simu. Kwa sababu hakutaka nikae na simu kwa Siri nilimcheck yule jamaa yangu fundi simu akanitafutia kiswaswadu na line, nikawa hewani bila mtu wangu kujua. Na wakati nipo homu mama mdogo aliniita niende Mbezi kumshikia kiduka chake. Kipindi nipo Mbezi nikawa natumia ile line ya fundi simu kuwasiliana na huyu mpenzi wangu lakini nikiitambulisha simu ya Paulina binti wa kazi wa mamdogo. Bila kujua aliamini na hakugombeza ila kiuhalisia Mimi bado nilikuwa na mahusiano ya Siri na fundi simu.

Ulipofika muda wa kuondoka shule kwa kweli huyu boss na mchumba wangu alinifanyia Kila kitu, yaani sikureport shule kinyonge, wengi walijua labda natoka familia bora sana kumbe sikuwa na mbele wala nyuma kajamba nani tu. Nakumbuka maandalizi na mahitaji ya shule na vifaa vyangu binafsi alitumia kama 800k ( laki nane) na mkononi akanishikisha 200k pocket money. Hapo kumbuka kwa mama nimesrve mishahara yangu 8 December to July.

Kurudi kwa bi mkubwa, kutaka kujua cash zangu uwezi amini mama ananiambia ziko 400k tu zingine kishafanya yake. Kwa kweli sikuuumia nilijisikia tu ufahari bi mkubwa kala jasho la mwanawe, na ukizingatia maisha magumu anayopitia nikaona ni baraka kwangu na nikamtoa hofu asijihisi vibaya kwani mahitaji nilishakamilisha, nilimdanganya kwamba kiasi kingine cha fedha nilisevu mwenyewe nikihofu kusevu sehemu moja ingeweza kuleta tatizo kama hili, labda ningetumia zote au na wewe mama ungeweza kuzimaliza. Hapa nikukumbushe kwa kipindi chote mama hakumjua yule mchumba wangu, japo alipajua nilipofanyia kazi ila hatukutaka kumtambulisha nilijua mama angemaindi tu kuniona najali mapenzi kuliko shule, na Yule mpenzi wangu alihofu Maza atakasirika kwamba anamuharibu mwanawe.

Siku ya kuondoka shule ikafika mchumba wangu alitaka anipeleke shule na at the same time Maza nae alitaka kunipeleka shule. So nikamstopisha mchumba wangu, niende na Maza na akanielewa nikasepa. Shule nikapokelewa fresh nikapewa admission namba yangu mzee maisha ya jela yameanza mdada mrembo kuanza kupambana na Fluid Mechanics. Maza akageuza zake huyo shaah. Kichekesho wakati ananiaga ananiambia aniachie pocket money sh. Elfu kumi tu kisa chakula kipo shule, yaan hiyo nijitahidi idumu mpaka likizo na ikifika likizo nisirudi kama shule wanaruhusu watu kubaki na Mimi nibaki ili nimpe nafasi ya yeye kutafuta pesa. Nikafikiri sana japo sijui maisha ya pale shule, lakini nikasema hapa mama wa kichaga anachanganya na upare. Nikamjibu sawa mama Mimi nitajitahidi kupambana kwa kadri ya uwezo, bila kumjulisha kuwa nina 200k za pocket money.

Nilipokuwa shule nikamjulisha mchumba wangu kuwa nimefika nipo sawa na nimeanza masomo na nikamjulisha mahitaji ya wakati ule. Kikubwa ilikuwa tuition za masomo maana sikupata muda wa kusoma topics za comb yangu kama pre form five, so inanihitaji nikimbizane na walimu kulipia tuition zao. Akataka nimjulishe mahitaji ya wastani kwa mwezi, nikampanga akaniambia Kila mwezi atatuma 150k, wastani wa 5000 kwa siku. Kwangu sikuona shida kwa sababu wastani wangu wa matumizi kwa siku ulikua ni 2500 nikiwa pale shule.

Tukiwa pale shule jumamosi na jumapili ya Kila mwisho wa mwezi ni visiting days, na uwezi amini miezi yote huyu mchumba wangu hakukosa kuja kuniona isipokuwa mwezi wa 11 tu ambao mama alikuja. Uwezi amini Kila alipofika alinibebea makolokolo kama yote Kila nilichomwagiza kuanzia, nguo za ndani, mafuta, masaa, malotion na hata perfume nilizoletewa hakuna hata teacher mmoja amewahi kuzimudu kwa kweli nilionekana wakishua japo nyumbani kumepinda. Misosi unakuta mbuzi choma Paja na Mbavu zote zinaletwa, yaan ilikuwa ikifika tarehe hizo huwa Nina marafiki wengi mnoo wote wanajua Kuna furaha siku hizo. Kiufupi niseme huyu mtu anajitoa kwa namna kama ni upendo Basi naamini bahati au upendo wa namna hii kwangu ni mara yangu ya kwanza, japo nilikua bado sijui kulipa thamani ya upendo ninaopatiwa.

Kaka D, mkasa wangu mkubwa upo mwezi huu wa 12, ipo hivi shule tulifunga tarehe 22/12/2023 na wote tulitakiwa kurudi majumbani kwetu, kumbuka mama hakupenda nirudi kwa kuhofia nauli na apate utulivu wa kutafuta hela za baadae, lakini pia nahisi alihofu kutoa nauli maana mama ni bahiri kwelikweli. Nilipojadiliana kuhusu hilo na Yule mchumba wangu akaniambia ondoa hofu, nitakutumia nauli urudi nyumbani na nitakupatia fedha za matumizi kwa kipindi chote cha likizo. Wazo likawa limepita, tarehe ya kurudi Maza nikampa supplies huyoo nimetimba home, Maza kaduwaa wew imekuaje upo hapa na nauli umepata wapi? Kumbuka yeye kuanzia mwezi wa 8 kaniacha na buku 10 tuu. Kwa kweli hapa nilijawa na moyo wa huruma juu ya mchumba nilihisi kumficha sito mtendea haki, yani mtu aliyejivalisha ubaba, mtu ananihudumia kuliko ndugu zangu wote, sio wa ujombani wala kiumeni, nikasema kama nitamwelezea na bado atamlahumu Mimi niko tayari hata akinifukuza sitorudi tena kwake au nitaondoka muda ule ule kwa namna yule mwanaume alivyo na moyo wa upendo ajabu.

Nikafunguka kwa mama, kwamba mama Mimi usione mambo yamekuwa mepesi kwangu na kwako, nyuma ya wepesi huu Kuna mtu na nimeamua Leo nikuambie kwa sababu wewe ni mama yangu na najua unapitia magumu mengi kuhakikisha mwanao nasogea ila nimeona nikuambie kwamba pale nilipoajiriwa yule boss amenipenda anataka baadae nije kuwa mke wake, hata maandalizi yote yale alifanya yeye na sikutaka kukuambia kwa sababu nilikuwa bado sijajiridhisha kama kweli yuko na dhamira, ila Leo nakuweka wazi mama huyu mtu ndio muokozi wetu kiuchumi. Isingekuwa rahisi Mimi kuendelea na shule, sembuse tu kureport, maisha ya kule shuleni ni gharama lakini gharama zote amezichukua yeye ndio maana hata hukunisikia nalalamika. Hivyo hata hii nauli ya kurudi katoa yeye na hata ulivyosema nikiwa nyumbani nitatatiza mpangilio wako wa kutafuta na kuhifadhi fedha kasema ondoa shaka, kipindi chote nitakachobaki hapa atagharamia Kila hitaji langu la kuishi. Kwa kweli bi mkubwa nilimwona kama machozi yanamlenga machoni, nikawaza bi mkubwa kahisi nimetenda kosa kubwa la kumliza?

Baada ya muda bi mkubwa akainuka kwa maana aliinua kichwa juu baada ya kujiinamia kwa huzuni. Hapa nakuchanganyia madesa kidogo, kaka D, si umeona hata bi mkubwa amehama kutoka pale tulipokuwa tunaishi, ndio Basi nikuambie pale mama kafukuzwa na mwenye nyumba kisa ya ugumu wa maisha aupitiayo mama yangu. Na ukiangalia nyumba aliyo hamia, kwa kweli ni changamoto kapanga vyumba viwili kimoja Cha kaka G yule mabangi na kimoja ndio chetu mimi, mama na dada yangu yule mwenye mtoto. Kinachokera kingine hii nyumba vyumba vingine viwili wamekodi wamama wauza pombe za kienyeji na wanauzia hapo hapo homu na wanaume wanaingia mpaka ndani Kuna kipindi naweza kaa na mama ukasikia kelele za mapenzi mchana kweupe kutoka vyumba vya hao wamama na nyumba haina ceiling board, au usiku utasikia walevi wanagonga mlango kwetu wanataka kuingia chumbani hapo washalewa wamesahau mlango. Nyumba ipo mita chache tu kutoka mto msimbazi kasheshe juu ya kasheshe.

Mama alipoinua kichwa kutoka kufikiri kile nilichomueleza kinyume na fikra zangu labda nimemuuzi kumbe hapana, hakuwa na maneno mengi alichonijibu kama nikweli usemayo huyo mtu Mungu ambariki lakini nikuombe mwanangu tafadhali usitoke kwenye lengo la msingi, muda unakimbia sana sema binadam huwa tunaona unachelewa, angalia saa mwanangu muda wote inazunguka sawa na mapigo yako ya moyo yalivyo kasi. Nikuambiacho ni kwamba yote muyatakayo na muyaombayo yatakwenda kutimia ndani ya muda mfupi kwa kutoka sasa, ila jitahidi ujitunze usitoke nje ya reli, jitahidi umalize shule kwa mafanikio, sifa zote ulizompa Mimi sitozijali ikiwa utaishia njiani. Usije ukaniletea ujauzito kama dada yako, hebu angalia kaka zako na huyu dada yako hivi ni kweli Mungu muweza ndio kusema Mimi ameniandikia kuwa na tumbo baya?. Sasa hapa huzuni ikaama kutoka kwa mama ikarudi kwangu. Nikamjibu mama nimekusikia na nitazingatia, wakati huo kichwani nimevaa uhusika yan Mimi ndio kitinda mimba mwenye jukumu la kulitakasa na kulipa thamani tumbo la mama yangu. Basi tukamaliza maongezi maisha yakaendelea.

Sasa the mistake I did ni kwamba nikajisahau nikatumia ile simu na line ya fundi simu kumchek mchumba wangu. Nilipojitambulisha tu me J, akashtuka ghafla uko wapi? Oh niko home. Vipi mbona ulisema line ya dada wa kazi kule ulikooenda mara hii unaitumia ukiwa home? Nikajaribu kumpanga kwamba yule dada alikuja na hii line ameiacha nyumbani. Hakuonyesha kuchukizwa kumbe ghafla akaangalia upande wa usajili wa line, jina likasoma yule fundi simu anamjua na alipoangalia usajili wa namba ya yule fundi simu anayotumia jina likasoma lilelile mfanano wa Kila herufi. Kumbuka na huko nyuma alishaambiwa tetesi na kumbe yule dada mwenzangu wa dukani alinisnitch na kumueleza kweli nilikuwa natoka na fundi simu na muuza chipsi. Kesi ya muuza chipsi sikuwahi kumficha alivyonibana mara ya kwanza kabla sijaenda shule nilimfungukia na hakuwa na maswali nae tena. Shida kubwa na maswali ilibaki kwa fundi simu kwa sababu sikuwahi kukiri kwake, kwa sababu nilimpenda kiasi nilimdanganya kanitongoza ila sijawahi kutoka nae na aliamini.

Kutoka siku nilivyobugi kwa kumchek na line fundi simu kesho yake nilimuomba tuonane. Nikurudishe nyuma kidogo kaka D, nilikuambia mwezi wa 4 nilifanya mapenzi na Yule teacher wangu wa tangu tukiwa olevel, kumbe Jana yake tena na yeye kaniharibia. Siku tuliyokutana tulirecord video tukiwa watupu na mbaya zaidi yule mwalimu hakuwaga mjanja sana wa wanawake, alivyokuwa na Mimi alinitungia nyimbo karecord kabisa na bila kujua zile video za utupu na nyimbo zote kazituma kwa mchumba wangu, nyimbo za kunisifia kama anazotungiwa Manara na Zaylissa. Akijua anachart na mimi baada kujua wanafunzi wamerudi likizo tarehe ile. Kwa hiyo alikuja akiwa na kesi mbili mkononi mwake, kesi ya line na video za yule teacher. Lakini kaka D, nikuambie tangu nilipoenda shule upendo na kujali alivyonionyesha kiukweli nilishaamua kuacha utoto na sikutaka tena kujihusisha na mapenzi ya wale wengine kwani hata fundi simu nilivyorudi nilimcheck as friend na japo aliomba tukutane lakini nilishaamua kumkataa mazima, na Yule teacher nilishamkataaga mapema sana na sikuwa na hofu nae yeye alishakubaliana na ukweli na hata siku tulipokutana hiyo mwezi wa nne niseme ni bahati mbaya tu.

Tulipokutana na mchumba wangu akaja mezani na kesi mbili huku akiwa amefura hatari. Ukizingatia Kila kitu kipo wazi sikuwa na sababu ya kupinga ilibidi tu niombe msamaha kwa mara nyingine. Kilichomuumiza kuliko yote ni Mimi kuwa na mawasiliano ya Siri na fundi simu, huyu mtu ambaye ameniuliza karibia mara 10 na bado nilimficha. Tangu pale amenichukulia kama mtu msaliti na muongo muongo naona kabisa hata Jambo la kweli yeye aniamini kwa kweli.

Tulipomaliza kuzungumza akaniambia nimkabidhi ile line ya fundi simu. Sikuwa na namna ilibidi niikabidhi ile line kwake. Changamoto sasa ile line na yenyewe wakati tunarudi kutoka shule niliwapa wanafunzi wenzangu namba, tangu ameichukua anakutana na meseji nyingi sana za watu wanaonitongoza, wanaoniita baby, cjui wife and the like. Jamaa ni kama amenikatia tamaa ya kusonga na Mimi nafanyaje kaka D?

Kingine nikukumbushe kaka D, kwa siku hizi nilizorudi kutoka shuleni tunapokaa kutulia namsikia jamaa anaongea positive nyingi sana kuhusu kubadili maisha yangu na mama yangu, nikuambie majuzi aliniuliza kuhusu kazi ya ulinzi ya mama anaipenda au amfanyie mpango amfungulie mgahawa Kuna sehemu nzuri ana fremu zake. Ametuma niongee na mama kama yupo tayari kuacha kazi ya ulinzi ili amuwezeshe Kila kitu amfungulie mgahawa nzur tu na nilivyoongea na bi mkubwa kakubali mwezi wa pili ataanza. Kingine kaka D, alivyojua tumehama nyumba kabla sijaondoka nilimdanganya tunapokaa ni kwetu, amesikitika sana kuona nyumba tuliohamia na uwezi amini Jana kanipeleka site yake moja Kivule kasema ikiisha tu mwaka huu 2024 anataka Mimi na mama na familia yangu yote tukaishi pale. Ona kaka D wangapi wenye upendo huo na kwa sasa Mimi nimeacha ile tabia ya kutojitambua yaani nimeanza kujawa na upendo na huruma juu ya haya ninayotendewa ila naumizwa na matendo yangu ya nyuma, nisaidie kaka nifanyeje?

Hayo yote niliyokusimulia lakini kilichonifanya nikuombe ushauri ni hivi, wakati tunatoka Kivule Jana alinipa 300k kwa ajili ya maandalizi yangu nirudi shule tarehe 7/01. Sasa leo nimeshinda home namsubiri Maza arudi nichomoke niende barabarani kufanya manunuzi ya vifaa vya shule, Maza kachelewa kurudi, karudi saa 12 , nikamstua mchumba wangu nakimbilia road kuandaa ile safari akanikataza, time imekwenda utaenda kesho kununua na jumapili utasafiri. Nikamuomba sana naomba niende saa 1 tu nitakuwa nimerudi na nitakujulisha. Kwa kuwa huwa hapendi nitokee hilo eneo akijua fundi simu ndiko aliko na nilishamueleza udhaifu wangu wa kushindwa kujitetea kwenye maongezi magumu anajua nikikutana na Yule wa simu sitoweza kumchomolea ndio kisa hata Cha kuchukua simu na line zote. Sasa kaka D Kuna mistake imetokea nilivyoenda road sikurudi saa 1, nimerudi saa 2, niliporudi kumtext na simu ya mama sms zimeisha, maeneo ninayokaa kuanzia saa 2 huduma za maduka yamefungwa. Nimehangaika kuomba kwa watu nimekuja pata vocha saa 5:30 usiku, na saa 2 hiyo aliuliza kwa simu ya mama kwamba umerudi? Hakupata majibu. Kwa hiyo amehisi nimerudi saa 5 nyumbani na tangu nilipomtafuta kuanzia hiyo saa mpaka leo hajanijibu. Nilijua labda muda ule kalala kumbe kachukia, nimemtext ukweli wote na nimemuomba ajaribu kuongea na mama ila hajarespond hata text moja. Na nakumbuka aliniambia siku atakayoachana na Mimi hatajibu wala kupokea simu zangu, ndio dalili nimeiona sasa, nisaidie tafadhali nifanyeje huyu mtu arudishe hisia zake za uaminifu nikionacho haniamini kwa lolote kaka D, nakuomba kama mwanaume nipe mbinu za kunisaidia.

Jamani ndugu yenu nilikutana na hiki kisanga naweza kumsaidia huyu mdogo wangu anahisi kitumbua chake kinaenda kuingia mchanga aliouteka mwenyewe.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Huyo ni wa kukosa, apambane na hali yake
 
Back
Top Bottom