Nomben ushauri tumsaidie huyu dada.

Mapenzi ni matamu sana. Hasa ukipata anayeyajulia, mkweli, mwaminifu na muelewa. Inakupasa uwe mwangalifu sana kabla hujajiingiza kwenye mapenzi. Ukikosea wakati wa kuchagua na kuamua elewa hutaweza kukwepa maumivu ya mapenzi siku za mbele. Mueleze huyo shost, afute akilini mwake kama aliwahi kupenda. Ajiandae upya kiakili kujifikiria yeye mwenyewe kwanza yukoje kimapenzi na afikirie ni mpenzi gani atamfaa kulingana na yeye alivyo. Akishajitambua alivyo itakuwa ni rahisi kupata sifa za anayemuhitaji.

Awe mwangalifu wakati wa kumchunguza mpenzi anayemtaka. Asiwe mtu wa makuu sana, aelewe hakuna binadamu aliyekamilika, ila kuna tabia ambazo zinaweza kuvumilika/kuchukulika. Endapo kuna tabia yoyote ambayo anahisi hataweza kuivumilia asikubali kujiingiza kwenye mapenzi akitegemea mtu yule ataiacha au kubadilika.

Aanze kuchagua kulingana na sifa anazozitaka. Mwambie awe mwangalifu sana wakati wa kuchagua, na asiwe na papara. Ajifunze kuutuliza moyo wake, maana wakati mwingine mioyo yetu hutuharakisha kuamua na kujikuta tunajuta.
Atulieze akili zake kwa kufanya mazoezi, kula vizuri, kulala mapema, kufurahi na marafiki na kuhakikisha anachangamka, mapenzi yasimfaye alie na kuwaza hadi akose hamu ya chakula. Hii itampelekea kutokuwa na maamuzi mazuri.
Uko sahihi kbs happy,ameshalitambua hilo na kwa sasa anasema anapumzika kwanza ajipe mda wa kutosha kujiangalie yeye na kurekebisha mapungufu yake kabla hajajiingiza kwenye uhusiano mpya?
 
Kwakweli hata mie nimefarijika sn kwan mpaka jana jion alishajitambua na kuainisha mapungufu yake na ameanza kuyafanyia kazi,kwa kuanza kujijali km mwanzo na ni mchangamfu ile huzun na kulia havipo tena,na tatizo la wivu na hasira ameshagundua lilikuwa na kero kwa wapnz wake baada ya kumkumbusha baadhi ya mambo yaliyowahi kutokea japo wakati huo hata nilipomwambia hakuelewa ila sasa ameelewa na anakabiliana nayo.

pia hapa anaweza kuwa anaathiriwa na vitu 3 ambavyo inabidi avielewe
  1. yeye anaweza kuwa ni tatizo
  2. partners anaowapata wanaweza kuwa ni tatizo
  3. yeye na partners wanaweza wakawa ni tatizo
 
huyo rafiki yako akae chini atulize akili. aache kabisa kufikiria mpenzi kwa sasa sababu ana maumivu. mkaka yeyote atakayemwonea huruma tu kwa sasa ataona ni mpenzi wakati siyo kweli.
Mimi naamini kwenye kupata break after heartbreak, inakupa muda wa kufikiria mambo yaliyo bora zaidi..... kujifunza na kuwaza kuhusu past relationship ili ujue uanzie wapi baadae. mambo ya kuruka kutoka relationship moja hadi nyingine siyo mazuri. ndo maana walio wengi wanaofanya hivyo wanashtuka baada ya muda fulani anakuwa kabadilisha wenza kibao.
Amefanya jambo la busara kuachana na hiyo mtu, lakini a-take time yake. a-develop hobby nyingine, kuangalia sinema, JF, etc kwa muda anaojisikia lonely.
 
pia hapa anaweza kuwa anaathiriwa na vitu 3 ambavyo inabidi avielewe
  1. yeye anaweza kuwa ni tatizo
  2. partners anaowapata wanaweza kuwa ni tatizo
  3. yeye na partners wanaweza wakawa ni tatizo
Amegundua yote matatu yanatokea kwa nyakati tofauti na watu tofauti,ni km relation yake ya mwisho yeye alikuwa poa na jamaa aliweza kutuliza hasira na wivu wake na wakawa wako poa tu,ila tatizo jamaa alikuwa na mke shost alipogundua na jamaa akakiri ndio ndio akaamua kuachana naye,kwa vile ameshalijua tatizo lake anajirekebisha na kumwomba mungu ampe mtu mkweli watakaeendana na kuelewana.
 
huyo rafiki yako akae chini atulize akili. aache kabisa kufikiria mpenzi kwa sasa sababu ana maumivu. mkaka yeyote atakayemwonea huruma tu kwa sasa ataona ni mpenzi wakati siyo kweli.
Mimi naamini kwenye kupata break after heartbreak, inakupa muda wa kufikiria mambo yaliyo bora zaidi..... kujifunza na kuwaza kuhusu past relationship ili ujue uanzie wapi baadae. mambo ya kuruka kutoka relationship moja hadi nyingine siyo mazuri. ndo maana walio wengi wanaofanya hivyo wanashtuka baada ya muda fulani anakuwa kabadilisha wenza kibao.
Amefanya jambo la busara kuachana na hiyo mtu, lakini a-take time yake. a-develop hobby nyingine, kuangalia sinema, JF, etc kwa muda anaojisikia lonely.
Uko sahihi kbs,ameshaligundua hilo na kwa sasa ameamua kutulia kwanza na kujikip bize na mambo mengine kabla hajajiingiza tena kwenye relation mpya.
 
mpe pole sana na amefanya sana jambo la mbolea kuachana na mume wa mtu ...........
atulie na kumuomba sana mungu mana akisema atake faraja kwa mwanaume anaweza kuishia pabaya bure tena bora atulie na kupata faraja kwa mungu ambaye hatamuumiza wala kumletea magonjwa ya moyo huku akiomba ampate wa kufafa naye
 
Back
Top Bottom