Nomben ushauri tumsaidie huyu dada.

Habari zenu wapendwa,kuna met wangu hapa oficn ana tatizo ambalo hata yeye mwenyewe haelewi ni tatizo gani,ni mtu ambaye relation zinamsumbua sana,amekuwa akitendwa mara kwa mara kwa ni mtu mwenye hasira na wivu sn,japo huwa akipenda anapenda kweli na wala huwa hatoki nje ya uhusiano anapokuwa mtu,relation yake ya mwisho ilikuwa na maumivu makali sana kwake kwan alimpata mtu aliyeza kumtuliza hasira na wivu wake na wakawa wameshatambulishana,wakiwa wanaendelea na relation met wangu akagundua jamaa ana mke wa ndoa na mtoto kupitia simu yake ila mke wake yuko mkoa mbeya ni mwalimu,alipomuuliza jamaa kutokana na ushahidi ikabidi akiri na kuomba msamaha ila ndio met wangu akakasirika na kuachana naye.

Sasa ni miezi minne tangu yuko single amekuwa ni mtu wa mawazo sn amepungua na ameshindwa hata kujipendezesha km awali,anasema upweke ndio tatizo anataman kuwa na mpnz na anahic hawezi kuwa peke yake, anataman apate mtu wa kumwonyesha mapnz yake na watu wanaomtokea wapo ila anashindwa kuwaamin na hata kuwa nao,nimejitahidi kumshauri nahata kumwonyesha sred za humu za kufanana na matatizo yake lkn tatizo haliishi na ameendelea kuwa hivyo,saa nyingine unakuta analia tu,nikimuuliza anasema anataman angekuwa na mpenz akamweleza anavyojisikia,kwakweli ni hali ambayo mie km binadamu mwenzia inanihuzunisha na nimeshindwa namna ya kumsaidia na kuamua nilete kwenu wadau tuone tumsahuri nn japo kumsaidia,nawakilisha.

Ashukuru kwanza Mungu amekuwa akimpigania kumuonyesha wapenzi ambao alikuwa nao sio waaminifu.Isije ikawa huko kulia ni kwasababu anampenda huyo mume wa mtu na alikuwa na mategemeo makubwa nae. Amsahau na awe na amani na amuombe Mungu atapata wa ukweli.
 
Maisha lazma yaendelee, tatzo lilomkuta alikua ktk mawazo ya kuolewa na longolongo za waoaji zikawa nyingi kuliko, so kwa mazngira kama hayo hana budi kuvuta subira ili kufanya uchaguzi sahihi na si ajabu kutendwa kwani ndio amejifunza so akimpata wake atajua namna ya kufanya ili kuepukana na maumivu, gem za love zinahitaji sana uvumilivu wa hal ya juu. Jambo la mcngi zaid asubiri ackimbilie kuanzisha mahusiano mapya kwan akili yake itakua bado haijatulia. Pole yake zaid.
 
Mwanangu mpendwa Cantalisia, mpe pole huyo Met wako, kwa kweli anahitaji ushauri tena wa haraka, unajua hizi thread humu JF nyingi ziko too General, hawezi kuzisoma na kuelewa moja kwa moja. mimi namshauri atafute mtaalamu wa ushauri wa mambo ya mahusiano ambaye anamuamini ili aweze kusema naye...naamini humu wapo wengi sana tu. Kwa hali aliyo nayo akikurupuka anaweza kuibuka na bomu halafu likamletea shida. anachotakiwa ni kutulia na kumuomba Mungu sana amuondolee huo msongo wa mawazo ambao naamini unatokana na kutendwa.

Mpe pole zangu.............
Asante baba,salam zimefika,anashukuru kwa ushauri ameshaanza kuufanyia kazi.
 
Samahani Cantalisia; ila naona kama huyo rafiki yako ni wewe vile!!!!!!!!!

Anyway it doesn't matter. Ushauri wangu, mwambie ajipende kwanza yeye mwenyewe, na maisha yake yamekamilika with or without mwanaume. Kuhusu wivu wa kupindukia ni dalili ya kutojiamini, hivyo akijipenda na kujithamini atajiamini na hatahitaji mtu wa pembeni kumpenda ndipo awe na thamani!

Mapenzi (mutual) yatakuja tu bila kuyavuta; wasimtishe au asijione muda umeenda kwani God's time is the right one! I hope still uko naye, home, hotel or wherever ili asome na post yangu........
Bila samahani japo umenifanya nicheke kidogo,sio mie bwana si unajua mie yakifika huwa nayaweka jamvin bila chenga na najielezea vizuri wala situmii nafsi ya mtu.
Post yako kaisoma tuko naye hapa ofisin mezan kwangu kwa vile yeye sio member humu hata ninachokijibu anakiedit atakavyo ndio nipost,anashukuru kwa ushauri na kutokana na maoni mengi ya watu amegundua hata na mapungufu mengine aliyonayo,natayari ameshaanza kuyafanyia kazi,kwa utayari alionao na nia ya kuwa na furaha km wengine soon atakuwa poa.
 
Kwanza mpe pole.
Pia kama walivyogusia baadhi, kuna umuhimu sana wa kujiunga na vitu kama gym, kwaya, swimming club au sehemu yoyote ambayo itamsaidia ku-relax mentally. Kama ilivyo addiction yoyote, njia bora kupambana nayo ni kubadili trend au tabio hiyo kwa kitu kingine. Na sehemu kama hizo (sio baa ) unaweza kukutana na watu aka wanaume na mambo yakajipa. Na kwa kuanzia sio lazima kwenda gym per see, unaweza kuwa mnakwenda wote sehemu za beach ambazo watu wanatembea as a group, au kufanya mazoezi ya viungo (anza na 3 times a week at minimum). hasira nzuri ktk kipindi hiki ni kujifua na kula vizuri- mboga, matunda fresh, samaki kwa wingi bila kusahau bamia, jitengeneza ili kama ni kung'aa basi ung'ae mara mia zaidi-

Pia siku za weekend, mara moja moja nendeni hapo Saadan mbugani au funga safari hadi mikumi angalia wanyama na mazingira, am sure you and her will feel relaxed. Again, utajifariji na over time kuna possibilities za kukutana na mtu ambaye labda ndiyo ulipangiwa....!

Nikija nitawatafuta na kuwapa company ya muda kama rafiki ( sitaki chochote) !!
Asante sana mafuluto,ameisoma post yako kwakweli imetuvutia wote na haya uliyoshauri mm ndio nitakuwa supervisor na ukija utamkuta yuko poa kbs,karibu sana!
 
Ashukuru kwanza Mungu amekuwa akimpigania kumuonyesha wapenzi ambao alikuwa nao sio waaminifu.Isije ikawa huko kulia ni kwasababu anampenda huyo mume wa mtu na alikuwa na mategemeo makubwa nae. Amsahau na awe na amani na amuombe Mungu atapata wa ukweli.
Asante DASA,kwa maelezo yake wala hana mapnz tena na huyo mume wa mtu kwan alimchukia sn baada ya kugundua alimdanganya na hakuwa na nia njema naye,kinachomliza ni upweke kwan alishazoea kuwa na mtu,ila kwa ushauri wenu wadau tangu jana hajalia tena na angalau amechangamka hope akishafanyia kazi ushauri alioupata atakuwa poa kbs.
 
Maisha lazma yaendelee, tatzo lilomkuta alikua ktk mawazo ya kuolewa na longolongo za waoaji zikawa nyingi kuliko, so kwa mazngira kama hayo hana budi kuvuta subira ili kufanya uchaguzi sahihi na si ajabu kutendwa kwani ndio amejifunza so akimpata wake atajua namna ya kufanya ili kuepukana na maumivu, gem za love zinahitaji sana uvumilivu wa hal ya juu. Jambo la mcngi zaid asubiri ackimbilie kuanzisha mahusiano mapya kwan akili yake itakua bado haijatulia. Pole yake zaid.
Asante F12,kwa sasa ameamua kutulia tu kwanza kwa muda mpaka akimwomba mungu akutanishe na mkweli.
 
Habari zenu wapendwa,kuna met wangu hapa oficn ana tatizo ambalo hata yeye mwenyewe haelewi ni tatizo gani,ni mtu ambaye relation zinamsumbua sana,amekuwa akitendwa mara kwa mara kwa ni mtu mwenye hasira na wivu sn,japo huwa akipenda anapenda kweli na wala huwa hatoki nje ya uhusiano anapokuwa mtu,relation yake ya mwisho ilikuwa na maumivu makali sana kwake kwan alimpata mtu aliyeza kumtuliza hasira na wivu wake na wakawa wameshatambulishana,wakiwa wanaendelea na relation met wangu akagundua jamaa ana mke wa ndoa na mtoto kupitia simu yake ila mke wake yuko mkoa mbeya ni mwalimu,alipomuuliza jamaa kutokana na ushahidi ikabidi akiri na kuomba msamaha ila ndio met wangu akakasirika na kuachana naye.

Sasa ni miezi minne tangu yuko single amekuwa ni mtu wa mawazo sn amepungua na ameshindwa hata kujipendezesha km awali,anasema upweke ndio tatizo anataman kuwa na mpnz na anahic hawezi kuwa peke yake, anataman apate mtu wa kumwonyesha mapnz yake na watu wanaomtokea wapo ila anashindwa kuwaamin na hata kuwa nao,nimejitahidi kumshauri nahata kumwonyesha sred za humu za kufanana na matatizo yake lkn tatizo haliishi na ameendelea kuwa hivyo,saa nyingine unakuta analia tu,nikimuuliza anasema anataman angekuwa na mpenz akamweleza anavyojisikia,kwakweli ni hali ambayo mie km binadamu mwenzia inanihuzunisha na nimeshindwa namna ya kumsaidia na kuamua nilete kwenu wadau tuone tumsahuri nn japo kumsaidia,nawakilisha.

Pole sana dada yetu,wasiliana na huyu mama ni mshahuri wa hayo mambo hasa ya vijana na ndoa au vijana na mahusiano anaitwa Mch. Salome 0713564009.Mungu akubariki
 
Asante mkuu,anakushukru sana kwa namba atawasiliana naye soon,ubarikiwe pia Manyusi.
 
Hilo la wivu ndio tatizo kubwa huwa anamwamini ila anapenda kila wakati wawe wanaongea kuchati muda wote ajue yuko wapi na mambo km hayo ambapo kwa sasa ameazimia kudeal na hali hiyo,amesoma ushauri wako na anakushukuru sana.

Kama anataka kufanya followup za hivyo ni kweli atakuwa ni kulia kila siku mwisho wa siku vidonda vya tumbo, pressure n.k. Maisha ya sasa ukamfuatilie mwanaume utadhani umezaliwa nae tumbo moja? Apunguze wivu, aache kuwaza mapenzi kila wakati, binafsi naamini mapenzi yapo tu na yana wakati wake so ajishughulishe, afanye kazi aendeleze maisha yake, wanaume wa siku hizi utadhani wametoka tumbo moja, mwisho aendelee kumuomba Mungu atapata tu kwani Mungu wetu si kiziwi hata asisikie tumuombayo
 
Mimi bana nimetokea sana kumpenda ram.........ulikuwa wapi siku zote?
 
mpe pole sana huyo met wako na nashukuru kwanza kwa wewe ambaye uko karibu naye kuelewa/ kutambua tatizo lake linalomsibu hasa kwenye kitu ambacho wengi hupenda kusema ni wivu na hasira japo wengine hujumuisha kwa kusema kisirani..
mara nyingi watu huwa tunabeba matatizo ya awali ambayo yamekutokea katika mahusiano yaliyopita kwa kukwazwa au wengi tunaamini kutendwa na wenzi wetu ..
kwanza anatakiwa ajielewe na aweze kubadilika kwenye hizo dhana asemazo ni hasira na wivu kwan yawezekana ikawa ndo kero kubwa kwa wenzi wake na ambayo yanaweza kumuumiza kwa muda mrefu kwani unajenga kiburi, dharau, hasira na kutokujiamini au kujiamini kupita kiasi pindi unapoanza mahusiano mengine lakini tatizo anashindwa kuziacha zile tabia zilizopelekea kuvunja mahusiano ya awali.
mwambie ajipe muda kabla ya kuanza mahusiano mengine, apate muda wa kufanya matembezi ya jioni (mazoezi) na kujiweka katika hali ya usafi
 
Mapenzi ni matamu sana. Hasa ukipata anayeyajulia, mkweli, mwaminifu na muelewa. Inakupasa uwe mwangalifu sana kabla hujajiingiza kwenye mapenzi. Ukikosea wakati wa kuchagua na kuamua elewa hutaweza kukwepa maumivu ya mapenzi siku za mbele. Mueleze huyo shost, afute akilini mwake kama aliwahi kupenda. Ajiandae upya kiakili kujifikiria yeye mwenyewe kwanza yukoje kimapenzi na afikirie ni mpenzi gani atamfaa kulingana na yeye alivyo. Akishajitambua alivyo itakuwa ni rahisi kupata sifa za anayemuhitaji.

Awe mwangalifu wakati wa kumchunguza mpenzi anayemtaka. Asiwe mtu wa makuu sana, aelewe hakuna binadamu aliyekamilika, ila kuna tabia ambazo zinaweza kuvumilika/kuchukulika. Endapo kuna tabia yoyote ambayo anahisi hataweza kuivumilia asikubali kujiingiza kwenye mapenzi akitegemea mtu yule ataiacha au kubadilika.

Aanze kuchagua kulingana na sifa anazozitaka. Mwambie awe mwangalifu sana wakati wa kuchagua, na asiwe na papara. Ajifunze kuutuliza moyo wake, maana wakati mwingine mioyo yetu hutuharakisha kuamua na kujikuta tunajuta.
Atulieze akili zake kwa kufanya mazoezi, kula vizuri, kulala mapema, kufurahi na marafiki na kuhakikisha anachangamka, mapenzi yasimfaye alie na kuwaza hadi akose hamu ya chakula. Hii itampelekea kutokuwa na maamuzi mazuri.
 
Kama anataka kufanya followup za hivyo ni kweli atakuwa ni kulia kila siku mwisho wa siku vidonda vya tumbo, pressure n.k. Maisha ya sasa ukamfuatilie mwanaume utadhani umezaliwa nae tumbo moja? Apunguze wivu, aache kuwaza mapenzi kila wakati, binafsi naamini mapenzi yapo tu na yana wakati wake so ajishughulishe, afanye kazi aendeleze maisha yake, wanaume wa siku hizi utadhani wametoka tumbo moja, mwisho aendelee kumuomba Mungu atapata tu kwani Mungu wetu si kiziwi hata asisikie tumuombayo
Amen ram,amesoma na amekuelewa vizuri kbs,yani post yako umempa ujasiri mpya kuhusu wanaume,ubarikiwe sn.
 
mpe pole sana huyo met wako na nashukuru kwanza kwa wewe ambaye uko karibu naye kuelewa/ kutambua tatizo lake linalomsibu hasa kwenye kitu ambacho wengi hupenda kusema ni wivu na hasira japo wengine hujumuisha kwa kusema kisirani..
mara nyingi watu huwa tunabeba matatizo ya awali ambayo yamekutokea katika mahusiano yaliyopita kwa kukwazwa au wengi tunaamini kutendwa na wenzi wetu ..
kwanza anatakiwa ajielewe na aweze kubadilika kwenye hizo dhana asemazo ni hasira na wivu kwan yawezekana ikawa ndo kero kubwa kwa wenzi wake na ambayo yanaweza kumuumiza kwa muda mrefu kwani unajenga kiburi, dharau, hasira na kutokujiamini au kujiamini kupita kiasi pindi unapoanza mahusiano mengine lakini tatizo anashindwa kuziacha zile tabia zilizopelekea kuvunja mahusiano ya awali.
mwambie ajipe muda kabla ya kuanza mahusiano mengine, apate muda wa kufanya matembezi ya jioni (mazoezi) na kujiweka katika hali ya usafi
Kwakweli hata mie nimefarijika sn kwan mpaka jana jion alishajitambua na kuainisha mapungufu yake na ameanza kuyafanyia kazi,kwa kuanza kujijali km mwanzo na ni mchangamfu ile huzun na kulia havipo tena,na tatizo la wivu na hasira ameshagundua lilikuwa na kero kwa wapnz wake baada ya kumkumbusha baadhi ya mambo yaliyowahi kutokea japo wakati huo hata nilipomwambia hakuelewa ila sasa ameelewa na anakabiliana nayo.
 
Back
Top Bottom