Nini maana ya kujipanga na kujijenga?

GP

JF-Expert Member
Feb 5, 2009
2,049
160
Mabibi na mabwana!

Mie bwana nina shemeji/ wifi yenu ambaye nina kama mwaka mmoja hivi tangu tuanze mahusiano, ninaishi homu kwa dingi (servant quarter! umri wangu ni 25-27 bado nipo nipo!!), nina miaka 2 tangu nimalize chuo na mwaka mmoja na nusu tangu nianze kazi kampuni fulani.

Sasa bibie siku moja nilimwambia ninampango wa kutoka homu nianze kujitegemea, akaniambia nina haraka ya nini wakati bado natakiwa kujipanga na kujijenga kwanza?. sasa nikawa najiuliza hivi vitu maana yake nini haswa?

Nikaona isiwe tabu wacha nilipeleke hili suala JF watanisaidia kunielimisha. Naombeni mawazo yenu kujijenga na kujipanga shemeji/ wifi yenu alikua anamaanisha nini msaada plz

Nawasilisha.
 
mabibi na mabwana!,
mie bwana nina shemeji/ wifi yenu ambaye nina kama mwaka mmoja hivi tangu tuanze mahusiano, ninaishi homu kwa dingi (servant quarter! umri wangu ni 25-27 bado nipo nipo!!), nina miaka 2 tangu nimalize chuo na mwaka mmoja na nusu tangu nianze kazi kampuni fulani.
sasa bibie siku moja nilimwambia ninampango wa kutoka homu nianze kujitegemea, akaniambia nina haraka ya nini wakati bado natakiwa kujipanga na kujijenga kwanza?. sasa nikawa najiuliza hivi vitu maana yake nini haswa?
nikaona isiwe tabu wacha nilipeleke hili suala JF watanisaidia kunielimisha.
naombeni mawazo yenu kujijenga na kujipanga shemeji/ wifi yenu alikua anamaanisha nini. msaada plz

nawasilisha.

Ok kwa kweli kila mtu anajisi ya kulifafanua na kulielezea anavyokuwa anaongelea neno la kuijpanga,

Yaani rafiki yangu ambaye ni ndugu yangu alipokwambia kuwa jipange kwanza na usiwe na haraka inawezekana alisema hivyo akiwa anakuonea huruma kwa majukumu ambayo utakuwa nayo baada ya kupanga.
Kulipa kodi ya nyumba,kulipia luku,kuchangia hela ya usafi kwa wale wanaopata nyumba iliyo na wapangaji wengi,kulipia hela ya sewage system kwa wale kila kukicha wana;eta gari kwa ajili ya kudrain sewage system nk

Pili inawezeka kakwambia hivyo kwa kuwa anajua financial capability yako hivyo akaona kuwa utakuwa umejiongezea mzigo badala ya kujipanga na hayo mambo kabla ya kwenda kupanga.

Suali lisilo lasmi,Uliwahi kumgusia kuwa nimepata kiwanja na kumshirikisha kuwa badala ya kwenda kupanga ningeonelea nijenge akakutalia?

Kwa hiyo kukwambia kuwa usiwe na hara ya kukimbilia huko aliona kuwa uamusi huo siyo endelevu kwa kuwa fainancial anakujua.

ni hayo tu kwa niamba ya shost wangu.
 
Pili inawezeka kakwambia hivyo kwa kuwa anajua financial capability yako hivyo akaona kuwa utakuwa umejiongezea mzigo badala ya kujipanga na hayo mambo kabla ya kwenda kupanga.

Suali lisilo lasmi,Uliwahi kumgusia kuwa nimepata kiwanja na kumshirikisha kuwa badala ya kwenda kupanga ningeonelea nijenge akakutalia?

Actually financial niko fresh kwakweli naweza kutatua hayo mambo na yeye mwenyewe pia kumgharamia ingawa nae ni mfanyakazi, na muda wote huo nilikua nasave sana, kiasi ambacho ndio maana niliamua nifikirie kwenda kuanza maisha.

bado tuko kwenye GF-BF relationship, sasa ndio maana nafikiri nianze maisha ili tupange sasa mambo ya kujongea altareni!, siwezi kwenda altareni wakati nakaa kwa dingi, au nitoke altareni moja kwa moja nikaanze maisha ya kujitegemea nikiwa nae.
kuhusu kiwanja cha kujenga itafuata baada ya wote kua mwili mmoja.

Swali je alikua anamaanisha kujijenga na kujipanga au kitu kingine?
 
actually financial niko fresh kwakweli naweza kutatua hayo mambo na yeye mwenyewe pia kumgharamia ingawa nae ni mfanyakazi, na muda wote huo nilikua nasave sana, kiasi ambacho ndio maana niliamua nifikirie kwenda kuanza maisha
.
nenda kaanze maisha usiwe unawasikiliza sana hawa GF wao ndoto za ni maisha ya palace tu. ndiyo maana walisema mwanaume kichwa cha familia.
 
Fidel80 upoooooooooo hapooooooooooooo
Mpe jamaa mikakati yako ya 2012
 
Halafu wewe George toka lini demu akaombwa ushauri wa maisha bwana? Utamiss step mjomba, hawana maana hawa viumbe, akili ni nywele kila mtu ana zake
 
Halafu wewe George toka lini demu akaombwa ushauri wa maisha bwana? Utamiss step mjomba, hawana maana hawa viumbe, akili ni nywele kila mtu ana zake

unaniangusha mkuu, huyo binti mi ndo my wife wangu to be!, so sometimes tukiwa tumechill tunabadilishana mawazo tunajadili vitu kama hivyo. ndio maana nilimuuliza anipe ushauri.
mi nahisi hawa mademu sijui wanataka mtu uwe na gari kabisa au nyumba?, duh
icon9.gif
 
Mbali na vyote utuavyo we need to have these things before bwana.sasa lift mpaka lini?
 
halafu nimekumbuka huyo demu wako anataka ununue gari ndio maana anakwambia ujipange na kujiaandaa kwanza. Ila anashindwa kukwambia direct tu. Mademu wa kibongo na magari utawaweza kwani
 
swali la jibu lako ni rahisi sana.. ungemuuliza huyo huyo alikuwa anamaanisha nini aliposema hivyo..?? inawezekana kila mtu akawa na matazamio yake juu ya maana halisi ua kujijenga kwani kila mtu huwa ana malengo tofauti katika maisha.
 
lakini pia angalia unaweza pigwa changa la macho ukiwa unang'aang'aa macho, inawezekana binti amewaweka na msela mwingine kwenye mizani atakayeweza kujipanga fresh ndie anaingia kwenye first eleven. Changamka mjomba
 
unaniangusha mkuu, huyo binti mi ndo my wife wangu to be!, so sometimes tukiwa tumechill tunabadilishana mawazo tunajadili vitu kama hivyo. ndio maana nilimuuliza anipe ushauri.
mi nahisi hawa mademu sijui wanataka mtu uwe na gari kabisa au nyumba?, duh
icon9.gif

Mkuu sikuangushi
najaribu kusema kile nikijuacho kaka
 
lakini pia angalia unaweza pigwa changa la macho ukiwa unang'aang'aa macho, inawezekana binti amewaweka na msela mwingine kwenye mizani atakayeweza kujipanga fresh ndie anaingia kwenye first eleven. Changamka mjomba

mnhh, hapa sasa kaaaz kwelkwel
 
swali la jibu lako ni rahisi sana.. ungemuuliza huyo huyo alikuwa anamaanisha nini aliposema hivyo..?? inawezekana kila mtu akawa na matazamio yake juu ya maana halisi ua kujijenga kwani kila mtu huwa ana malengo tofauti katika maisha.

nilitaka kwanza kuja hapa jamvini, kizuri kula na nduguyo mazee!, JF ni ndugu zangu, sasa nikirudi leo lazima aniambie alikua anamaanisha nini.
 
nilitaka kwanza kuja hapa jamvini, kizuri kula na nduguyo mazee!, JF ni ndugu zangu, sasa nikirudi leo lazima aniambie alikua anamaanisha nini.

Kwa hiyo baada ya kumwambia utatuletea majibu hapa jamvini?ili tuone kama misaada ya ushauri tuitoa kama huwa inazaa matunda.si ndio shemu?
 
Kwa hiyo baada ya kumwambia utatuletea majibu hapa jamvini?ili tuone kama misaada ya ushauri tuitoa kama huwa inazaa matunda.si ndio shemu?

haina neno shem.
ila bado ngoja tusubiri michango mingine, kuna wadau bado siwaoni kabisa hapa, kina dada hasa michango yao naisubiri.
 
Back
Top Bottom