Mama yangu mzazi kaanzisha mahusiano ya kimapenzi na kijana mdogo, inaniuma sana

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,177
1,822
Mimi ni binti wa miaka 33, baada ya kumaliza chuo nimekua nikiishi kwa Kaka yangu huu ni mwaka wa kumi sasa. Mwanzo nilikua kawaida na wifi yangu, lakini baada ya muda nilijikuta tu na mchukia sikujua sababu ni nini ila nikajikuta nilikuas namuomea wivu sana jinsi Kaka yangu alivyokua anampenda wifi yangu kwa kumhudumia kila kitu, kumjali kumtoa out wakati mimi sikua na mpenzi yoyote.

Nikajikuta nakua mtu wa hasira, nikaanza kumsingizia mambo mengi mabaya wifi yangu mpaka wakawa wanagombana. Kila wlaivyokua wanagombana mimi nilikua najisikia raha, Kaka alianza kuniamini, ukichangia na Mama alikua upande wangu akimuambia Kaka hapaswi kuamini wanawake basi kila nilichokua nikimuambia alikua akiniamini.

Miwaka miwili iliyopita Bbaa yangu alifariki dunia, hivyo Mama alikuja kuishia hapa, basi tukaanzisha kama kaumoja flani ka kumchukia wifi. Baisahra walizokua wameanzisha pamoja tulizisimamia sisi na yeye akawa Mama wa nyumbani. hali ilikua nzuri tu sisi tunafuraha, kila kitu kaka akaandika majina ya Mama yaani hakua akimuamini mtu mwingine.

Akabadilisha karibu kila kitu na kuandika majina ya Mama, mke wake akiongea basi ni kipigo, mimi pia kuna vitu aliniandikia. Mwaka jana nilipata mwanaume wangu ambaye alikua tayari kabisa kunioa. Lakini kila nikiwaza kuondoka kwa Kaka basi nilikua naona kama vile namsaliti, nikawa simpendi huyo kijana kwani kipato chake ni cha kawaida tu na anaishi mkoani.

Nilimfanyia vituko na kuachana naye, hata Mama hakumpenda, alikua ananiambia nina haja gani ya kuolewa wakati nina kila kitu. Basi nilibaki nyumbani mpaka sasa hivi nipo tu hapa kwa Kaka na sina mwanaume mwingine kwani naona kama nikiondoka na kumuacha Kaka basi wifi yangu atachukua mali zote. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, Mama yangu ni mtu mzima kidogo kama miaka 55 lakini muonekano wake ni wakijana.

Shida kaka nikuwa, Mama kuna mwanaume kampata, ni mume wa mtu sema ni kijana kabisa, yaani kijana mdogo umri kama Kaka yangu.huyo mwanaume anamchanganya sana Mama kiasi kwamba yeye ndiyo anamhudumia kila kitu, anammpa hela ya kula, analipia watoto wake ada ya shule na kila kitu. Kuna Biashara ambayo mimi nasimamia, tulikua wawili na Mama.

Ni duka kubwa tu la pikipiki la kaka lakini Kaka aliliandika jina la Mama. Mimi ndiyo najua kila kitu kuhusu pesa ila Mama anachukua pesa za mauzo zote anaondoka na huyo kijana ananiaga mimi nakuniambia nimfichie siri. Wanaweza kwenda Zanzibar wiki wanakula maisha huku kamdanganya kaka kuwa anaenda kujijini. Hajali kabisa nikimuambia anatakiwa kuwa makini kwani huyo kijana anampendea pesa hajali ananiambia kuwa ameshaongea naye atamuacha mke wake ili kumuoa yeye.

Kaka nahangaika sana, anatafuta pesa kwa bidii, yaani namuonea huruma, wakati mwingine hata kula ni shida ila Mama anatoa tu pesa kwa huyo kijana na mimi nashindwa kumuambia Kaka kwani naona kama itakua ni kumdhalilisha Mama. Nisaidie, ninachotaka uongee na Mama yangu ilia achane na mume wa mtu kwani mimi nikimuambia ananijibu hovyo kuwa nina kisirani kwakua sina mwanaume wa kufanya naye mpenzi ndiyo maana nimeng’ang’ania kwa kaka yangu.

Nisaidie, uongee na Mama kwani kuna stori za jinsi watu wanavyodhulumiwa naona kabisa Mama yangu akidhulumiwa wakati ni mali za Kaka ambazo kazichuma kwa jasho nisaidie Kaka
1703879299967.jpg
 
Mimi ni binti wa miaka 33, baada ya kumaliza chuo nimekua nikiishi kwa Kaka yangu huu ni mwaka wa kumi sasa. Mwanzo nilikua kawaida na wifi yangu, lakini baada ya muda nilijikuta tu na mchukia sikujua sababu ni nini ila nikajikuta nilikuas o nisaidie KakaView attachment 2857324
Hufai kushauriwa.Ufalme wako na mama yako umefitinika siku nyiingi.Hatuna cha kukuambia
 
Mimi ni binti wa miaka 33, baada ya kumaliza chuo nimekua nikiishi kwa Kaka yangu huu ni mwaka wa kumi sasa. Mwanzo nilikua kawaida na wifi yangu, lakini baada ya muda nilijikuta tu na mchukia sikujua sababu ni nini ila nikajikuta nilikuas namuomea wivu sana jinsi Kaka yangu alivyokua anampenda wifi yangu kwa kumhudumia kila kitu, kumjali kumtoa out asho nisaidie KakaView attachment 2857324
Hivi hilo jina Lina uhusiano na jinsia yako mkuu?
 
Karma is real.



Karma is bitch!!!!


Familia yote inaanza kupata ujira....mavuno mliyootesha kwa kuingilia unyumba wa watu.

Huyo mke wa kaka mtu anasali sana.

Amani itakuja baada ya kufilisika na huyo mama kutapeliwa.


Mungu ni wa wote
 
Mimi ni binti wa miaka 33, baada ya kumaliza chuo nimekua nikiishi kwa Kaka yangu huu ni mwaka wa kumi sasa. Mwanzo nilikua kawaida na wifi yangu, lakini baada ya muda nilijikuta tu na mchukia sikujua sababu ni nini ila nikajikuta nilikuas kwa jasho nisaidie KakaView attachment 2857324
Dhulma mnazimfanyia mwenzenu zitajibu tu



USHAURI

na wewe tafuta mwanaume kisha uwe unamuhonga kama mama yako


Si unaona wifi yako anafaidi mali na dudu la kaka yako
 
Familia ya watu wajinga hiyo

Ushauri - huyo wifi yako unabidi kuhakikisha anakuwa na Amani muondoke hapo wewe na mama yako .

Pia Una matatizo ya Akili unaweza kutafuta wataalamu Wa kiroho wakusaidie na wanasaikolojia kabla haujachanganikiwa na Ku kota makopo.

Ukitumuia nguvu kubwa kumbomoa MTU lazima ubomoke wewe mbomoaji kwanza na hii ni universe law huwezi kupata nje ya unachokiingiza.
 
Back
Top Bottom