Nini kimempata Nassari?

Watanzania mnapenda sana kupiga makelele,sasa hapo cha ajabu kipi Joshua kutoenda leo?
hakuna kanuni yoyote amevunja.Chadema wana akili sana walijua leo wabunge wengi wa Magamba
hawatakuwepo sababu ya Jelous ili wasimuone J Nassari anavyoingia mjengoni na kuapishwa,
hivyo atakapoingia watakuwepo na ataapishwa mbele yao.
 
Kutokuwepo sio issue lakini kushindwa kutoa taarifa ya kutokuwepo huko nadhani ni issue ambayo inahitaji maelezo kutoka kwa JN.

Tutajuaje labda kila mmoja anamlilia mshikaji wake. Mmoja Lulu na mwingine marehamu Kanumba. Maana wahuni bwana
haweleweki.
 
Nasari asiwe na haraka yoyote kwani matatizo ya arumeru mashariki ni ya zaid ya miaka 50,na yeye kutokuapishwa sio tatizo,nashangaa kwa nini Nasari hakuapishwa ubunge tangi 2011,Mzee Sumary mpaka anafariki alikuwa haja apishwa kuwa mbunge sababu alikuwa mahututi,Mi nafikiri itungwe sheria kama mtu asipo apishwa ndani ya siku 60 baada ya kikao cha kwanza awe amepoteza ubunge na aliyeshika nafasi ya pili aapishwe.NASARI BIG UP
 
Hebu ajitokeze nassari mwenyewe atuambie kwa nini hakwenda bungeni leo, najua yumo humu jamvini.
 
Tusiwahukumu kwa kutokuwepo leo maana hata yeye sio malaika anaweza kupata dharura pia. Hivyo waachwe watoe taarifa kwa spika na atawaelewa lakini cdm wamefanya hivyo ili kuisubiri serikali irudi kwenye normal position maana serikali imegeuza kifo cha kanumba mtaji wa kisiasa na kusahau mambo mengine.
 
Siku ile pale Arusha NMC uongozi wa chadema ulitangaza kuwa Nassari anaapishwa Jumatano 11 April na wakatangaziwa wale wote waliotaka kumsindikiza bungeni wakutane ofisi ya chadema arumeru saa mbili asubuhi ili waanze safari. Inawezekana ndo janja za Makinda kuwauza chadema waonekane wapuuzi. Kama kuna mtu anayo audio ya Arusha NMC jumamosi aisikilize.
 
Bunge linaanza rasmi kesho tarehe 10/4/2012 mpaka 21/4/2012, hivyo kesho siku ya kwanza wataapishwa wabunge wawili wa CDM
 
CDM ni taasisi kubwa saaana kuliko unavyoijua wewe, inaendeshwa kisayansi zaidi, iko networked vizuri saaana kuliko unavyohisi, kutokuapishwa kwa Nasari na Mwenzake usihofu. bunge bado lipo na linendelea.
 
Maneno aliyoyatoa spika kwamba kutokana na wabunge hao kutokuwepo leo watasubiri mpaka kamati ya bunge iwapangie muda wakati mwingine.Je kwa kipindi hiki kuanzia kesho watakuwepo watakaa nje ya bunge bila kuhudhuria?Je spika aliwataarifu kwamba wanapaswa wawepo wakati wa kuanza kikao hiki ili wasije wakalaumiwa.Mwisho kama ushauri ofisi ya spika ifanye kazi kwa haki na si kwa jazba ili bunge liwe chombo mahsusi cha wananchi.Naomba kuwasilisha.
 
Naibu kiongozi wa upinzani Bungeni Mh Zitto amekiri CDM hakikusoma vizuri kanuni za bunge. Ameomba msamaha kwa spika, sasa wataapishwa alhmamisi. Jumatano watakuwa wanapewa maelekezo jinsi bunge linavyofanya kazi.
 
Back
Top Bottom