Nina mpango wa kufungua shule ya chekechea na Primary. Naombeni mawazo tafadhali

SHIGOTTO

Senior Member
Sep 4, 2018
156
280
Ndugu zangu, nimepata mawazo ya kufungua shule ya chekechea maeneo ya kiluvya, tuna eneo mimi na mkwe wangu la heka tisa. Tunataka kuanza na chekechea, baadaye tuongeze hadi primary baada ya kuisoma biashara na mwenendo wake.

Naomba mwenye uzoefu na biashara hii atuambie changa moto zake ukiondoa mambo ya vibali.

Nawakilisha kwa msaada zaidi.
 
Ndugu zangu, nimepata mawazo ya kufungua shule ya chekechea maeneo ya kiluvya, tuna eneo mimi na mkwe wangu la heka tisa. Tunataka kuanza na chekechea, baadae tuongeze hadi primary baada ya kuisoma biashara na mwenendo wake. Naomba mwenye uzoefu na biashara hii atuambie changa moto zake ukiondoa mambo ya vibali. Nawakilisha kwa msaada zaid.
Ukimaliza ujenzi nina marafiki wana degree za ualimu, naweza kukuunganisha nao.
 
Naipenda sana hii biashara au day care,nlijaribu nikashindwa ila natamani kujaribu tena
Kule Magomeni kuna walio anzisha na imewapa unafuu sana wazazi kuhusu malezi ya watoto.

Wanawapa chakula cha mchana kande za nazi au wali maharage watoto wanapenda sana.

Wazazi wanalipa 30-50,000 kwa mwezi ambayo wengi wana mudu.
 
Naipenda sana hii biashara au day care,nlijaribu nikashindwa ila natamani kujaribu tena
Labda uniambie tatizo hasa ni nini maana mwenzangu ulijaribu fanya
Kule Magomeni kuna walio anzisha na imewapa unafuu sana wazazi kuhusu malezi ya watoto.

Wanawapa chakula cha mchana kande za nazi au wali maharage watoto wanapenda sana.

Wazazi wanalipa 30-50,000 kwa mwezi ambayo wengi wana mudu.
Ni habari njema, kwa maono niliyokuwa nayo nataka kujenga darasa la shule ya chekechea kisha niongeze kidogo kidogo vyumba ili wakitoka chekechea wanaanza la kwanza hapohapo la pili hadi la saba! naomba ushauri
 
Labda uniambie tatizo hasa ni nini maana mwenzangu ulijaribu fanya

Ni habari njema, kwa maono niliyokuwa nayo nataka kujenga darasa la shule ya chekechea kisha niongeze kidogo kidogo vyumba ili wakitoka chekechea wanaanza la kwanza hapohapo la pili hadi la saba! naomba ushauri
Huduma za jamii kwanza sehemu ya vyoo. Unataka vya maji au vya mashimo. Ndiyo maana niliuliza group la watu una wahudumia. Matajiri inabidi uweke vyoo vya kukaa size ya watoto. Kuwe na vya wanawake na vya wanaume.

Jiko, kama utatoa chakula ni lazima utenge sehemu ya jiko na uweke ka sehemu ka kuhifadhia chakula ki kavu na fridge kwasababu ya perishable goods.

Madarasa ni lazima yatofautishe umri. 3-5, 2-3, kwasababu developmental play zinatofautiana kutokana na umri.
 
Thanks kwa ushauri mzuri, naufanyia kazi
 
Sina experience ya moja kwa moja Ila nimeona na ninaendelea kuona fursa na changamoto katika kuanzisha taasisi ya elimu ya awali na msingi..

Kwa kuwa eneo tayari unalo, mosi ni miundombinu, aina ya structures utakazohitaji inaendana sambamba no module of teaching, je ni chekechea tu ya kawaida kabisa au utatumia mfumo wa montensorri, Cambridge , bacalaurette.

Pili, walengwa haswa ni watu wenye watoto maeneo hayo au itakuwa una pick up points (as in school vans zinaenda kuwachukua) ..third walimu utakuwa unawalipa kwa mfumo upi ukitegemea ada za watoto hapa naomba kukutaarifu tu utarajie kufail l, itakulazimu kusource malipo kutoka vyanzo vingine.

On another note, Mimi najihusisha na ujenzi wa gharama nafuu, kwa kutumia tofali za interlocks, au za kuchoma zilizotengenezwa kwa mashine. Ukihitaji ushauri kwa upande huo karibuu unitafute.
 
Umeshajenga shule Kwa style hiyo mkuu?
Yes, nimejenga madarasa yanayotumiwa na taasisi level ya nacte.

finished.jpg
Image0077.jpg
 
Nashukuru sana kwa ushauri, kwa sasa tunapenda kutumia mfumo wa montensorri na walengwa ni watoto wa majirani na wengine wa mbali na hapo kwa kutumia pick up points, tutapofika kwenye kujenga most likely around April nitakutafuta tuone modarity ya kufanya biashara, thanks alot kwa ushauri tuko pamoja
 
Ni morogoro mjini, tulisave approx 45% ya gharama, na muda pia. Kwa Dar na viunga vyake kupata interlocks za kuchoma ni changamoto kidogo, Ila za aggr dust/moram/cement ..uwezekano wa ku save up to 30% ya cost upo inategemea scale ya project.
 
Kama una ardhi yako tayari nikupe moyo anza ila inabidi uwe mvumilivu wa miaka angalau kumi ndio uanze kupata faida ila pia ili ufanikiwe fanya vifuatavyo

1. Angalia madhaifu ya shule zinazokunguka ili uone utaboresha wapi

2 . Hakikisha unapata uzoefu na mambo ya ualimu kama vip kajitolee hata sehemu kwa miezi miwili

3.hakikisha unakuwa na misingi ya shule yako itakauokuwa tofaut kabsa na shule nyingize mfano,usiruhusu mwl kuongea kiswahili. kuchelewa kuja shule na mengineno.

4. Usifanye urafiki na mfanyakazi wako yeyote ,narudia hakikisha usifanye urafiki na mfanyakazi wako yeyote.

5. Jenga iman kwa wazazi kwa kuwatembelea watoto, kuwa na mawasiliano ya karibu na hata ikibid uwe na group la whasap la wazaz tu.

6. Kuhusu miundombinu usiwaze wewe Jenga darasa moja kila mwaka

7 . Mengine nitaendelea
 
Back
Top Bottom