Nina mpango wa kufungua shule ya chekechea na Primary. Naombeni mawazo tafadhali

Kama una aridhi yako tayari nikupe moyo anza ila inabidi uwe mvumilivu wa miaka angalau kumi ndo uanze kupata faida ila pia ili utanikiee fanya vifuatavyo
1. Angalia madhaifu ya shule zinazokunguka ili uone utaboresha wapi
2 . Hakikisha unapata uzoefu na mambo ya ualimu kama vip kajitolee hata sehemu kwa miezi miwili
3.hakikisha unakuwa na misingi ya shule yako itakauokuwa tofaut kabsa na shule nyingize mfano,usiruhusu mwl kuongea kiswahili. kuchelewa kuja shule na mengineno.
4. Usifanye urafiki na mfanyakazi wako yeyote ,narudia hakikisha usifanye urafiki na mfanyakazi wako yeyote.
5. Jenga iman kwa wazazi kwa kuwatembelea watoto, kuwa na mawasiliano ya karibu na hata ikibid uwe na group la whasap la wazaz tu.
6. Kuhusu miundombinu usiwaze wewe Jenga darasa moja kila mwaka
7 . Mengine nitaendelea
Shukrani sana, tunayachukua maoni na kuyafanyia kazi!
 
Shule nyingi zinazoanzishwa zinakufa kwa sababu zifatazo:tamaa za wamiliki.mmiliki au wamiliki wengi wana tamaa sana wanataka mafanikio ya haraka mno.

Yaani pesa ikiingia tu hawazi kulipa mishahara Bali kujenga madarasa mengine na miuondo binu migine.hii hushusha molali wa walimu .epuka hilo

Hawatoi huduma inayolizisha.kwa mfano mtoto anasoma somo moja tu kwa Siku

Hawako updated.kwa mana kwamba mfumo wa elimu unatumia usajili wa mfumo wa prems.unakuta mmiliki hajali kuhusu mfumo wala hatafuti wazoefu wa mifumo ili afanye kazi kwa ufanisi.

La mwisho, wazazi wengi sana au wote wanatamani watoto wao waongee kiingereza.so jitahidi sana kwenye angle hiyo.
 
Thanks for this input
 
La mwisho, wazazi wengi sana au wote wanatamani watoto wao waongee kiingereza.so jitahidi sana kwenye angle hiyo
ukifanikiwa hili mtoto akirudi anamwaga yai walahi unateka wazazi wote, wazazi wengi wanaamini mtoto kujua English ndo kuwa na akili!
 
Nina uzoefu mkubwa sana ktk eneo Hili nikiwa kama mwalimu wa shule hizi za private.Jambo la kwanza kwa kuwa una eneo wewe Anza,mambo mengineyo waweza nicheck kwa ushauri zaidi.Nikwambie tu kuwa hutojutua kuwekeza pesa yako.
 
Huduma za jamii kwanza sehemu ya vyoo. Unataka vya maji au vya mashimo. Ndiyo maana niliuliza group la watu una wahudumia. Matajiri inabidi uweke vyoo vya kukaa size ya watoto. Kuwe na vya wanawake na vya wanaume.

Jiko, kama utatoa chakula ni lazima utenge sehemu ya jiko na uweke ka sehemu ka kuhifadhia chakula ki kavu na fridge kwasababu ya perishable goods.

Madarasa ni lazima yatofautishe umri. 3-5, 2-3, kwasababu developmental play zinatofautiana kutokana na umri.
So inatakiwa uwe na madarasa atleast matatu kwa nursery level?

Na ukitaka kusajili nursery utaratibu upoje?

Na mwalimu kwa wastani analipwaje? Mtanzania na Mganda

Ukiondoa viti na meza... facilities gani nyingine zinatakiwa darasani?

Na ada ni kiasi gani kwa wazazi middle class lets say wa bunju?
 
Nitakua Howe za kuku jibu hapa ni facilities za darasani.
Unakua na ratiba ya michezo kwa wiki. Kuna siku ya mess play, hii siku watoto wanacheza na matoy kwenye basin la maji, unaweza kuwa na boat 🚤, kuogesha madoli nk mess play nyingine ni udongo wa mfinyanzi unawaacha wafinyange vitu wanavyoweza, ukikosa udongo changanya unga wa begani, tena unga unautia rangi ya chakula unaweza kuwa mwekundu au kijani. Unawafundisha watoto rangi.

Vifaa vya kuchorea unaweka kwenye corner moja, mikado ya plastic ambayo inakata karatasi lakini ina madhara madogo kwa watoto. Hivi vyote unapata China.

TV ni muhimu kwa kuonyesha cartoons na kama walimu English is not reachable watoto wanajifunza nursery rhymes kwenye screen iwe you tube au CD.

Mvua ikivyesha unawakea Disney Movie wanaangalia.
 
Kuna mama mmoja juz kati nimekutana nae anafanya biashara hii..Aligombana na staff wake aliyemfanya mkuu wa shuke ya sekondari jamaa akaondoka na every single detail inayohusu wanafunzi..

Nafanya kaz sana na mashule na moja ya tatizo kubwa walilonalo sekta hii ya elimu (hasa private) ni utunzaji wa data.

Mwalimu akifukuzwa kazi au akiondoka bas taarifa zote especially za kitaaluma zinategemeana na ustaarab wake whether zidumu au azipoteze..

Nenda shulen anakosoma mtoto wako toka ameanza shule kisha omba databzake za 2 or 3 years back utaona wanavyohangaika na kutapa tapa.. Sky Eclat
 
Ndugu zangu, nimepata mawazo ya kufungua shule ya chekechea maeneo ya kiluvya, tuna eneo mimi na mkwe wangu la heka tisa. Tunataka kuanza na chekechea, baadaye tuongeze hadi primary baada ya kuisoma biashara na mwenendo wake.

Naomba mwenye uzoefu na biashara hii atuambie changa moto zake ukiondoa mambo ya vibali.

Nawakilisha kwa msaada zaidi.
ku share biashara na mkwe tu tayari hiyo ni changamoto moja wapo
 
Kuna mama mmoja juz kati nimekutana nae anafanya biashara hii..Aligombana na staff wake aliyemfanya mkuu wa shuke ya sekondari jamaa akaondoka na every single detail inayohusu wanafunzi..

Nafanya kaz sana na mashule na moja ya tatizo kubwa walilonalo sekta hii ya elimu (hasa private) ni utunzaji wa data.

Mwalimu akifukuzwa kazi au akiondoka bas taarifa zote especially za kitaaluma zinategemeana na ustaarab wake whether zidumu au azipoteze..

Nenda shulen anakosoma mtoto wako toka ameanza shule kisha omba databzake za 2 or 3 years back utaona wanavyohangaika na kutapa tapa.. Sky Eclat
Mwenye shule anatakiwa kumtafuta mtu wa IT ambunie muundo wake ambao utamsaidia kuhifadhi data kutokana na matumizi yake.

Mwalimu anasaini mkataba na mwanasheria kuwa hataondoka na taarifa zozote za shule.
 
Hilo eneo upo ww na mkweo , kuwa makini hapo usije pigwa na kitu kizito kisogoni alafu macho yakaona cheche
 
Nitakua Howe za kuku jibu hapa ni facilities za darasani.
Unakua na ratiba ya michezo kwa wiki. Kuna siku ya mess play, hii siku watoto wanacheza na matoy kwenye basin la maji, unaweza kuwa na boat 🚤, kuogesha madoli nk mess play nyingine ni udongo wa mfinyanzi unawaacha wafinyange vitu wanavyoweza, ukikosa udongo changanya unga wa begani, tena unga unautia rangi ya chakula unaweza kuwa mwekundu au kijani. Unawafundisha watoto rangi.

Vifaa vya kuchorea unaweka kwenye corner moja, mikado ya plastic ambayo inakata karatasi lakini ina madhara madogo kwa watoto. Hivi vyote unapata China.

TV ni muhimu kwa kuonyesha cartoons na kama walimu English is not reachable watoto wanajifunza nursery rhymes kwenye screen iwe you tube au CD.

Mvua ikivyesha unawakea Disney Movie wanaangalia.
Asante nimepata mwanga kidogo
 
Nina uzoefu mkubwa sana ktk eneo Hili nikiwa kama mwalimu wa shule hizi za private.Jambo la kwanza kwa kuwa una eneo wewe Anza,mambo mengineyo waweza nicheck kwa ushauri zaidi.Nikwambie tu kuwa hutojutua kuwekeza pesa yako.
Ninayo haja ya kukutafuta mkuu
 
Tofauti ya Gharama ya ujenzi wa interlock na block ikoje?!
Gharama utakayotumia kujenga structure with blocks utasave up to 40% ukijenga same structure kwa kutumia interlocking bricks., Na pia uwezekano wa kucut muda wa ujenzi kwa zaidi ya 50%.
 
This is Great news kabisa...

Vipi kuhusu Durability ya Majengo ya interlocking blocks vs majengo ya Block, na Je kwa nin watu wanapenda kutumia Blocks kuliko interlocking wakat ni cut cost, samahan mkuu niko curious sana🤭🤭
 
Naomba nikushauri kama kijana mwenzako ambae nina ndoto kama yako yakumiliki shule.

Ila huu ushauri wangu utakua na faida saana kama wewe utakua mwalim na una uzoefu wa kusimamia shule.

Kwa utaratibu wa sasa ushajili wa shule ya awali umekuwa na mchakato sawa na ule washule ya msingi, ila utofauti upo tu kwenye kima cha chini cha usajili. Hii ndio maana wadau wengi kwa sasa wanabarili shule zao ambazo awali waliizita nursery but kwa sasa wanaiziita daycare cause usajili wa daycare is just aimple level ya manispaa tu. Ila nursery usajili wake mpaka level ya taifa.

Ninachotaka kuonesha hapa kuna ugumu kiasi katika zoezi la kuanzisha shule kwa sasa kama una pesa za kuunga unga.

Kama una pesa za kuunga unga please fuata ushauri huu uweze kutimiza lengo lako.

Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita shule nyingi za private zilidorora katika uendeshaji na nyingine zilikufa kabisa. Ilifikia hatua wamiliki walijuta kujiingiza kwenye biashara ya mashule.

Sasa wewe kama kijana, damu inachemka, mtaalamu kutika nedani ya elimu, hii ndio fursa kwako ya kuonesha ubora wako. Mfuate mmiliki ongea nae akukabidhi shule na wewe utamlipa kodi kwa kila awamu. Kwa kawaida shule ambayo ni complete (shule ya middle class) ambayo ina idadi ya wanafunzi wapatao 50 na kuendelea kodi inaweza kuwa takriban 15mil - 20 mil kwa mwaka.

Kwahiyo hapo utakuwa na kazi kubwa na kuimarisha ufaulu, kuongeza udahuli, kuboresha huduma n.k

Mkataba utakaoingia na mmiliki wa shule utampasa mmiliki akae mbali kabisa na suala zima la uendeshaji wa shule. Na kima cha chini cha muda wa mkataba kiwe miaka 8.

Kumbuka kama haupo mahiri kwenye usimamizi wa shule usithubutu hii kitu, utaishia gerezani

Ukifanikiwa kwenye hili taratibu taratibu utakua unajenga majengo yako yakikamilika utafanya usajili na utaanza udahili taratibu.
 
Back
Top Bottom