Mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali kuhusu nini kibadilike katika Mfumo wa Elimu ya Tanzania kupitia Twitterspace ya Jamiiforums

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
MJADALA 1.jpg

Wadau mbalimbali wa elimu wamekuwa wakilalamikia mfumo wa sasa wa Elimu ya Tanzania.

Jamiiforums kama mdau mmoja wapo wa elimu na mabadiliko inatoa fursa kwa Wanachama wake na umma kwa ujumla kutoa maoni yao juu ya nini hasa kibadilike katika mfumo wa elimu uliopo.

Ili kupata nafasi hii tafadhali jiunge nasi katika Mjadala wa TwitterSpace ya JamiiForums utakaofanyika tarehe 16 Februari, 2023 kuanzia saa 12:00 jioni mpaka saa 02:00 Usiku.

Pia, unaweza kuandika maoni yako kwenye uzi huu ambayo yatasomwa siku ya mjadala.

Karibuni.

UPDATE
- Karibu kujiunga nasi katika Mjadala unaoendelea hivi sasa kupitia TwitterSpace ya JamiiForums kujiunga tafadhali gusa link hii Unapendekeza nini kibadilike katika Mfumo wa Elimu ya Tanzania?

BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
MDAU JFSPACES: Muda wa kukaa Darasani upungue. Shule ya awali iwe Miaka 2, ya msingi iwe Miaka 5, Elimu va upili iwe Miaka 4 vilevile hakuna haja ya A- level Mitaala ifumuliwe yote, Watoto wafundishwe kulingana na mahitaji ya sasa. Specialization (ubobezi) uanze ngazi ya msingi.

MDAU JFSPACES: Kuwe na Mtaala wa kuwajengea Watoto 'Career choice development' kuanzia Shule ya msingi yaani kuanzia primary Mtoto ajue anataka kuwa nani Masomo ya lazima yawepo mfano Hesabu na uraia ila Historia iwe option Watoto waisome tu.

MDAU JFSPACES: Mfumo wa #Elimu ufanyiwe marebisho makubwa hususani ktk kumjengea uwezo Mtoto wa kutenda Katika shule kuwepo na Miundombinu yenye kumwezesha Mtoto kujifunza vitu vingi kuboresha ufahamu. Mfano ufundi wa Ushonaji, Umeme, Ufugaji, Kilimo na Miradi ya Uzalishaji.

MDAU JFSPACES: Miradi au shughuli zingizwe kwenye vipindi kabisa ili Mwanafunzi aweze kuhudhuria na itawasaidia Wanafunzi wengi kupata Maarifa na kupanua wigo wa Soko la Ajira tofauti na sasa ambapo Wanafunzi wengi wamehitimu Shule ila katika Study za Kazi hawana ujuzi wowote.

MDAU JFSPACES: Nionavyo Mimi, Elimu yetu ijikite zaidi kujiajiri, ipunguze kukaririsha Vijana wetu. Mafunzo kwa vitendo yapewe kipaumbele. Elimu ya kujitegemea irudishwe. Elimu iwe complete. Kijana wa form four awe na ujuzi wa kumuwezesha kuishi na kutengeneza kipato.

MDAU JFSPACES: Unasoma Miaka saba unafanya Mtihani siku moja, unasoma Miaka minne unafanya mitihani siku moja halafu wanakuja kukwambia umefeli? Masomo yenyewe meeeeeengi kweli Ufundi stadi uwekwe kwenye Mitaala kuanzia shule ya msingi. Usitumike kama mbadala baada ya kufeli.

MDAU JFSPACES: Unasoma Miaka saba unafanya Mtihani siku moja, unasoma Miaka minne unafanya mitihani siku moja halafu wanakuja kukwambia umefeli? Masomo yenyewe meeeeeengi kweli Ufundi stadi uwekwe kwenye Mitaala kuanzia shule ya msingi. Usitumike kama mbadala baada ya kufeli.

MDAU JFSPACES: Masomo ya Kilimo primary na secondary yapewe kipaombele. Pia, Masomo yapunguzwe. Walimu wapewe Pikipiki mikopo kwa malipo nafuu maana wengi wanaishi mbali na vituo kwasababu Nyumba za Watumishi hazipo.

MDAU JFSPACES: Elimu ilenge kuwafundisha Wanafunzi mbinu za moja kwa moja za kukabiliana na matatizo yaliyopo. Mtu amalize form four akiwa ameandaliwa kusoma Chuo kikuu moja kwa moja. Masomo ya five na six yagawanywe mengine yaende varsity na Sekondari.

MDAU JFSPACES: Mfumo wa Elimu ubadilishwe ili Watu wasome mambo ambayo yatamsaidia ktk Maisha halisi Kwa mfano Mtoto anasomea Physics na Chemistry hadi kidato cha Sita, akifika chuo anabadili mwelekeo anasoma Political Science au BBA baada ya hapo anaingia mtaani, anakosa ajira.

MDAU JFSPACES: Mfumo wa Elimu ubadilishwe ili Watu wasome mambo ambayo yatamsaidia ktk Maisha halisi Kwa mfano Mtoto anasomea Physics na Chemistry hadi kidato cha Sita, akifika chuo anabadili mwelekeo anasoma Political Science au BBA baada ya hapo anaingia mtaani, anakosa ajira.

MDAU JFSPACES: Kwanza viboko viharamishwe mashuleni, pili mitaala inayowaandaa watoto kimtihani ibadilishwe badala yake iwe ni mitaala inayowajenga/ inayowapa wanafunzi uwezo/ maarifa (capacity building curriculum).

MDAU JFSPACES: Moja ya jambo muhimu la kubadili katika Mitaala ya Elimu ni kuachana na Elimu ya kikoloni, tufocus na Elimu ya mabadiliko ya Kisayansi na Teknolojia kwa kuwa na Elimu ambayo ni 'practical based not more theoretically' Elimu kuhusu Taifa letu iwe kipaumbele.

MDAU JFSPACES: Matumizi ya Teknolojia katika Elimu, kuwezesha Wanafunzi kupata ujuzi wa Wlimu pamoja na Teknolojia baada ya kumaliza kusoma na kupunguza idadi kubwa ya wasubiri Ajira za Serikali bali kujiajiri kupitia ujuzi wa Kompyuta.

MDAU JFSPACES: Kwanza kabisa muda wa kukaa Shuleni upunguzwe, itawezekana kwa kupunguza vitu visivyo na tija kwa wakati huu Pia, Elimu iwe kwa vitendo zaidi hasa kwa Masomo ya Sayansi. Kingine, tuangalie hii fani ya Ualimu, wengi wanaonekana kutokumudu Masomo husika.

MDAU JFSPACES: Wapunguze Masomo yasiyo na lazima na Watu wasome kwa Combination kuanzia form one. Lugha ya kufundishia iwe kiswahili Kungekuwa na Masomo 5 tu ya Kimkakati kwa ajili ya Maendeleo sio hii 'how Europe under developed Africa' Miaka yote.

MDAU JFSPACES: Kuanza kufundisha Masomo ya Biashara na Uchumi katika ngazi za Sekondari, kuondoa somo la GS ama DS kuweka Somo la Uchumi kuwa la lazima Tuachane na Ujasiriamali wa kuambiwa tupambane na Soko la Dunia Kitaalamu.

MDAU JFSPACES: Elimu inatakiwa kujikita na mambo ya msingi zaidi kuliko kuwejenga na hadithi za chopeko na mnofu Tuache kupeana Moyo kwenye kupambana na Simba kama hawafu mwenye nguvu badala yake Masomo ya Ujasiriamali yapewe nafasi kubwa huku Mtaani thamani ya X haipo.

MDAU JFSPACES: Kiukweli nafikiri ingefunguliwa Shule ya Watundu. Tuwachunguze Vijana wote ambao ni Wezi na Vibaka tuwapeleke huko, tuwachunguze vijana wote wenye uwezo wa kuiba kupitia Kompyuta tuwaweke huko, wanaoweza kuhack wote, wanaoweza kutengeneza Ndege. hao ni rasilimali

MDAU JFSPACES: Shule za Advance ziwe vyuo vya ufundi stadi (VETA). Vifundishe Ufundi wa Kilimo, na ujuzi mwingine itasaidia Watu kuishi Kuanzia chekechea hadi chuo lugha ya kufundishia iwe Kingereza, Kiswahili tunadanganyana watasoma tu Watoto wa Masikini kwenye huo Mfumo.

MDAU JFSPACES: Civics, History, Regional study liwe Somo moja lenye mwendelezo kihatua. Agriculture, Commerce na BooKeeping yawe lazima kwa asiyesoma Physics, Chemistry na Biology Masomo ya lugha za Kigeni angalau kuwe na Kujua kwa lazima lugha mbili za Kimataifa.

Kila wilaya iwepo shule ya kukuza vipaji mbalimbali, Ikianzia primary to secondary tutapata matured talents tofauti na sasa hakuna uniformity.

MDAU JFSPACES: Tuchague moja katika Lugha ya kufundishia Kiswahili au Kiingereza, hii itaepusha kupoteza muda kujifunza jambo moja Mfano kifo cha Mkwawa wasoma standard four, ukiwa kidato cha kwanza ama pili kuna Death of mkwawa tofauti ni nini? Hii tunapoteza muda kisa Lugha.

MDAU JFSPACES: Nje ya Shule, Serikali itenge Wanafunzi wawe na Kazi maalumu ya vile vitu wanavyosemea ili kukuza ujuzi wao kuwa bora zaidi Hapo Serikali ni lazima washirikiane na sekta binafsi ktk kuwapa Ajira hizo kwa ajili ya Wanafunzi. Tutapata Watu wenye uwezo mkubwa.

MDAU JFSPACES: Nje ya Shule, Serikali itenge Wanafunzi wawe na Kazi maalumu ya vile vitu wanavyosemea ili kukuza ujuzi wao kuwa bora zaidi Hapo Serikali ni lazima washirikiane na sekta binafsi ktk kuwapa Ajira hizo kwa ajili ya Wanafunzi. Tutapata Watu wenye uwezo mkubwa.

MDAU JFSPACES: Shule chakavu na Vyuo ziondolewe uchakavu kwa kukarabatiwa Mwalimu mmoja kwa Somo moja na kwa darasa moja. Mfano Mwalimu mmoja afundishe Darasa la 4 somo moja tu na asifundishe Darasa lingine. Hisabati na Kiingereza wapewe Walimu mahiri wanaoyaweza masomo hayo.

MDAU JFSPACES: Elimu ijiondoe kwenye Nadharia na kwenda kwenye Vitendo Mitaala mibovu, Tanzania tunasoma Elimu isiyoendana na Dunia ya leo. Tafiti zifanyike tujue wenzetu wanafanya nini, mazuri tukicopy sio mbaya.

MDAU JFSPACES: Elimu yetu kwa sasa ina mambo mengi mno, ukiangalia ni Mifumo ambayo tulichukua kwa Wakoloni lakini Wakoloni wameshabadilisha vingi kwenye Mifumo yao Sisi bado tumebaki palepale na hata vikibadilika ni kwa uchache na sio kwa namna ambayo Watu wanashauri.

MDAU JFSPACES: Elimu yetu itambue vipaji, ni kawaida kuona Mtoto anakuwa bize sana na Masomo lakini hana nafasi ya kuboresha au kukuza kipaji chake Mfano Mwanafunzi akiwa na kipaji cha kucheza Mpira, anapata muda mfupi sana wa kuonesha kipaji chake, tuingize kwenye Mitaala yetu.

MDAU JFSPACES: Elimu yetu itambue vipaji, ni kawaida kuona Mtoto anakuwa bize sana na Masomo lakini hana nafasi ya kuboresha au kukuza kipaji chake Mfano Mwanafunzi akiwa na kipaji cha kucheza Mpira, anapata muda mfupi sana wa kuonesha kipaji chake, tuingize kwenye Mitaala yetu

MDAU JFSPACES: Mitaala ndiyo inayotakiwa kutuongoza siyo Lugha, #Kiswahili tumezaliwa nacho Kingereza hatuwezi kukikwepa, hivyo shida yetu ni kwenye vitabu vinavyotumika, kuna mazingira tofauti ya vitabu vinavyotumika.

Mfano Shule binafsi wanafundisha Kingereza kuanzia mwanzo, wale wa Shule za Serikali wanakutana nacho Sekondari tena katika vitabu ambavyo vinatofautiana, hiyo ni ngumu.

MDAU JFSPACES: Nchi yetu tulishindwa kujua tunataka nini kwenye Elimu. Mimi nilisoma History 2 but so what, inanisaidia nini Tunatakiwa kujua kuweka mkazo katika Vitendo.

MDAU JFSPACES: Elimu yetu kwa sasa ina mambo mengi mno, ukiangalia ni Mifumo ambayo tulichukua kwa Wakoloni lakini Wakoloni wameshabadilisha vingi kwenye Mifumo yao Sisi bado tumebaki palepale na hata vikibadilika ni kwa uchache na sio kwa namna ambayo Watu wanashauri.


MDAU JFSPACES: Elimu ya msingi iwe Miaka 10. Elimu ya sekondari iwe miaka 4, tusiwe na a level, chuo iendelee ilivyo. Mtoto amalize Elimu ya Msingi akiwa angalau na Miaka 16 ili asipofaulu aende veta. Waliofaulu wasome Miaka minne yaani kwenda University angalau Mtoto awe na Miaka 20.

Maudhui yabadilishwe kuwepo na Somo la uzalishaji la lazima kwa kila Mtoto na lifanywe kwa vitendo. Ufundi, kilimo, biashara na ufugaji. Yaani watoto wanaofanya Biashara wawe wanaenda stand kuuza vitu. Kilimo wawe na mashamba. Ufugaji wawe na Mifugo. Ufundi waende workshop.

MDAU JFSPACES: Naona Mtaala wetu hakutakuwa na tatizo kama tutaenda kwenye Lugha ya Kiingereza. Wanaotumia Lugha zao huko ni kwasababu wanaweza kujitegemea Sisi hatuwezi bado kujitegemea kwenye Teknolojia.

MDAU JFSPACES: Natamani kwenye Mabadiliko ya Sera Serikali ichague Shule za Mfano wafanyike Sample na wao watakuja kuwa-train hao wengine Sioni shida ya Kiswahili na tunaweza kwenda na Lugha yetu halafu Mtu akihitaji Lugha nyingine hiyo inaweza kuwa ni Fursa kwa Wakalimani.

MDAU JFSPACES: Darasa la 7 & Kidato cha 6 hayamsaidii Mwanafunzi kwa kuwa asilimia kubwa mambo yanayofundishwa ni yaleyale. Kuna Watu ambao walipohitimu kidato cha 4 wakapita ngazi nyingine za Elimu kama cheti, wakifika Chuo wanakuwa bora kuliko yule aliyehitimu kidato cha 6.

MDAU JFSPACES: Kwa Mtaala tulionao bado kuna vitu vingi hatujafanya, tunatakiwa tuweke msingi kwenye 'Competence Based Learning' Mfumo wetu unatakiwa umpime Mtoto kwenye uelewa wake sio kwenye alichokisoma. Watoto wa darasa la 3 wanatakiwa kuingia kwenye Teknolojia.

MDAU JFSPACES: Tukiangalia takwimu za ongezeko la Watu tunatakiwa kujua pia Miaka 10 ijayo bado tutakuwa tunatumia Teknolojia ya sasa? Tujiulize kwa Mitaala yetu je, hawa Wanafunzi wa sasa wanaandaliwa kukabiliana na trend ya Mabadiliko inayokuja?

MDAU JFSPACES: Mabadiliko ya Elimu yanatakiwa kwenda na Mpango wa Kitaifa, Ningeshauri masomo yabadilike na kuachana na kuzalisha wanasiasa au maafisa tuanze kuzalisha watu wenye skills, watu wengi waliojaa kwenye soko la ajira ni wenye makaratasi zaidi.

MDAU JFSPACES: Nadhani kama Taifa tunatakiwa kuchagua aina ya Lugha ya kufundishia Shuleni Inashangaza kuona Mtoto anatoka kufundishwa kwa Kiswahili Miaka 7, akimaliza hapo anaingia kusoma kwa Kingereza, tuchague Lugha moja inayoweza kutumika kuanzia chini hadi juu
 
Elumu km ushonaji, ujenzi, fundi machuma, na kilimo vifundishwe kuanzia std 4 mpk form 4. Ili wakitoka wawe na ujuzi kamili.
 
Wondoe mitaa ya nchi za nje,pia huu mfumo na muundo wa primary mpaka chuo kikuu imekaa kisiasa sana...watumie lugha mojo kuanzia primary mpaka chuo kikuu..wafundishe elimu ya vitendo sio theory ambayo mtu anamaliza chuo kikuu hajui atajiajiri vip...

Kuanzia secondary iwe elimu ya kitalaam na vitendo
 
Sitakuwa na nafasi yakujiunga live
Maoni yangu
1. Lugha ya kufundishia iwe English kutoka shule ya msingi mpaka Vyuo vya Elimu ya Juu,hii itanoondoa kuwachangaya wanafunzi kwa kushtukizwa na lugha ngeni wakiingia Sekondari kutoka shule ya msingi.

2. Kufuta adhabu ya viboko au adhabu zisizo na uadili kwa wanafunzi.

3.Kufuta utaratibu wa kuwa na shule za vipaji, huu ushamba ambao hauko nchi yeyeto duniani.

4.Wahadhiri wa Vyuo Vikuu,kuacha utaratibu wa kufelisha na kuweka vizingiti visivyo vya msingi kwa kudhani ni sifa wanafunzi wengi wakifeli kwenye somo lake.

5. Kuweka utaratibu wa vyuo vya ufundi VETA kuwa na kozi zinazowezesha kujiunga na vyuo vikuu kwenye fani ya sayansi na uhandisi.
 
Tujifunze ujuzi, tuachane na taaluma haitusaidii ila ujuzi utatusaidia kujenga taifa, kuna wahitimu wengi wasio na ujuzi hata chembe, ila wana notisi na vyeti
Elimu ya ujuzi mbona ipo veta, mbona veta hampeleki watoto wenu wala hatuoni foleni ya watoto wakiandikishwa veta? Mnalilia elimu ya ujuzi wakati ipo veta na hamthubutu peleka watoto uko. Watanzania wanafki sana.
 
Na watoto wa viongozi wote lazima wasome shule za kata za serikali. Kiongozi akichaguliwa/kuteuliwa basi kabla ya kuapishwa watoto kwanza wakalipoti Kata sekondari/primary.
Vinginevyo uteuzi wake unatenguliwa abaki akisomesha huko anakokujua yeye.
Elimu yetu inatakiwa ianzie hapa, tutoe elimu ya kustaarabisha kizazi chote cha watanzania. Sisi shida yetu sio elimu hata kidogo sisi shida ipo kwenye utamaduni na asili yetu.

Tuna tabia za roho mbaya tuna chuki wavivu tunapenda lawama tunapenda wizi starehe bila kufanya kazi. Hao wenye ujuzi ukiwapeleaka sehemu wanaishia kurogana kuiba na ujinga ujinga mwingine wa asili yetu.
 
MAONI YANGU NI HAYA

1. Elimu ngazi ya SHULE YA MSINGI Ndo iwe elimu ya jumla (general education ) Bila specifications Ili kumuandaa mwanafunzi na maarifa na taarifa mbali mbali.
Kuanzia shule ya upili (secondary school) mwanafunzi aanze kusomea kile anachotaka kusomea na ambacho akimaliza masomo ataweza kuitumia elimu yake kutengeneza kazi (kujiajiri), Au ataweza kuifanyia kazi endapo akipata kazi (ajira), na msisitizo uwe kumwandaa mwanafunzi kujiajiri zaidi kutokana na tatizo la ajira ni changamoto ya Dunia nzima. Hapa namaanisha kwamba mtoto kama anasomea udaktari kwa mfano, aanze kujifunza mambo yanayohusu udaktari tu kuanzia form 1 na kuendelea. Huyu mwanafunzi akijakufika chuo atakuwa amebobea kwankiasi kikubwa sana

2 Mitaala ijikite kwenye stadi za kazi, kama vile KILIMO, UFUGAJI, UCHORAJI, MUZIKI, UFUNDI MBALI MBALI (ushonaji, ufundi seremala, n.k. Yaani iwe elimu ya NADHARIA NA VITENDO KATIKA MAZINGIRA NA VIFAA HALISI. Kama mtoto anajifunza ushonaji, afundishwe nadharia na vitendo kwa kutumia cherehani na vitambaa halisi.

3 Kama taifa tuchague Lugha 1 ya kufundishia na kujifunzia kuanzia shule ya msingi hadi vyuoni. Haiwezekani mtoto anasoma masomo kwa kiswahili miaka 7 halafu ghafla unambadilishia Lugha.
 
1. Chekechea, darasa la kwanza na darasa la pili kusiwe na mitihani

2. Mtihani wa darasa la saba uboreshwe, multiple choices na kutiki viboma kwenye answer sheets huvutwe. Kama mwanafunzi anatakiwa ku calculate eneo la pentagon au ujazo wa tenki atuonyeshe njia sio as tick jibu ni B.

3. kuanzia form 3 kama kunauwezekano combination zianzia hapa sio advance. Kama mtu unasoma PCB, EGM au PCM a-anzia form 3 sio kusubiri hadi advance.

4. Mtihani wa form 4 na form 6 uwe na course work, zinazotoka kwenye individual, group assignments etc kama ilivyo vyuo vikuu. Kumjaribu mtoto kwa paper moja haitoshi, lazima tujue pia kwenye kufanya kazi na wenzeke yupoje

5. Div 3 form 4 wapewe kipaimbele kujiunga na vyuo vikuu sio kwenda advance. Bora waende wakaanza diploma ili wasipoteze malengo yao

6. Waalimu wakuu wote wawe na masters degree

Etc etc etc.
 
Na watoto wa viongozi wote lazima wasome shule za kata za serikali. Kiongozi akichaguliwa/kuteuliwa basi kabla ya kuapishwa watoto kwanza wakalipoti Kata sekondari/primary.
Vinginevyo uteuzi wake unatenguliwa abaki akisomesha huko anakokujua yeye.
Ngumu kutafuna! Mwigulu atakubali?
 
Ngumu kutafuna! Mwigulu atakubali?
Tunataka viongozi wanaotaka kuchanganyika na sisi, yaani tuwaone wenzetu, sio wanaotengeneza kizazi cha kwao kikijitenga na sisi. Hao sio wenzetu na hawafai kuwa viongozi, simple! Wapiga kula wasipotambua hili tutaendelea kuliwa. Naomba katiba mpya ije kuwe na kipengele tajwa, mana kitalazimisha macho ya viongozi yasibague elimu kama ilivyo sasa
 
Binafsi naona tuangalie namna Watoto waanze kufundishwa fani zao toka utotoni. Masuala ya kusoma tu masomo yote then ukifika chuo ndiyo unaingia kufundishwa fani inachochea kuzalisha wahitimu wasio na uwezo katika maeneo yao.

Ili kufanikisha hili kwa uchache tu watoto waanze kuchunguzwa vitu wanavyovipenda tokea awali then wazazi wawasaidie watoto wao kukua katika fani husika.
 
Back
Top Bottom