Naombeni ushauri biashara gani ya kufungua saa 10 jioni mtaji wa kuanzia million 1

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,572
44,797
Nina kazi mwisho saa Tisa na nusu nataka niwekeze kwenye biashara ambayo kwanza nitaisimamia mwenyewe peke yangu niweze kuona Hasara na faida hata Kama nikijitia Hasara nisababishe Mimi muhusika kuliko ile hofu ya kupigwa na mtu anayekuuzia...pili, mtaji uwe unaanzia million japo katika muda wowote unaweza kuongezeka mtaji mwingine Tena wa Million kutoka chanzo kingine Cha ajira na kuendelea hivyo hivyo kuongezeka Kama itabidi.

Sasa naombeni idea zenu kwa Mimi binafsi nilifikiri labda ningeweza grocery ya pombe maana unaweza kufungua jioni mkawa mnauza labda na mdada uliyemwajiri ila changamoto za biashara hio naijua hasa kwenye madeni nimewahi kuifanya watakuja wateja marafiki watakuchangia sana Ila siku hawana hela utashindwa kuwanyima utawakopesha halafu ndio wanakuhama kabisa..nataka biashara ambayo kila siku akija mteja NI mpya anachukua anatoa cash anapita... Ila ndo Kama tunavyojua biashara nyingi hufunguliwa mida ya kazi yaani asubuhi jioni ni mahesabu.

Nipeni ushauri niuze vifaa gani au Mali gani ambazo hata jioni zinatoka kwa wingi. Kingine Cha kuNote:Kuna kipindi pia nitakuwa nasafiri week moja au mbili au zaidi so itanibidi kufunga biashara hio kwa muda najiuliza je biashara gani ambayo kusafiri Huku hakutaathiri biashara na hizo bidhaa pia zisiwe za kuharibika ziweke kukaa hata mwaka natanguliza shukrani zangu.
 
jionijioni nenda stendi kubwakubwa ya kusafirisha abiria nje ya mkoa wako hapo utakuta abiria kibao wamelala au wakivuta muda kungoja magari ya kuondoka kesho yake. angalia mahitaji yao, unaweza kuwauzia usiku kucha hadi asbh wanapoondoka na wewe unarudi hom kujiandaa na mishe zako za mchana. ukikaa vizuri kodi sijui tozo gani za biashara utakuwa unazisikia tu kwa wenzako wanaouza mchana.
 
Mkuu fungua glocery halafu nipe location, mimi nina kijiwe minada ya Mailimoja, Kibamba na Madale, ukifungua naomba kuwa mteja wa kwanza
 
Back
Top Bottom