Nimeweka Engine Oil 20w-50 X-trail NT30 (2003) nipo sawa?

Bora choo cha kike bosi unaweza ukaona hata pichu ya mrembo...

Gari yenye mileage ya km 41k bado ni bikira kabisaa....
SAE VISCOSITY ya hiyo gari ni 5w30 au 10w30....

Hiyo 20w50 ni oil nzito sana mkuu..utachosha engine soon...hiyo ni special for high mileage engines na malori..
Gari unaweza sema ni high milage ikifika kilomita ngapi...??
 
Kwa magari yaliyomengi high mileage inaazia km 150000....Na gari likishafikisha km hizo unataona linaanxa kudai kubadilisha basdhi ya vitu ili lirejee hali ya awali
Mfano mie gari ilikuja na kilomia 52000 injini 1NZ sikuwah kujua kama inatumia 5w 30 au 10w 30 had nilipoingia humu sa hv ipo kilomita 99880 je nikirudi huko halitazingua mana lishazoea ma oil yetu haya sae 40 na 20w 50.....

NB nilikua nashangaa sana kwann asubuhi ukiwasha rpm inkua juu afu badae linarud kawaida kumbe oil dah
 
Yaah...kwa magari ambayo ni recommended kwa SAE 5W30 au 10W30, ukitumia SAE 40 kavu, huwa ukiwasha gari asubuhi injini inavuma sana na baadhi ya magari mshale wa RPM unachelewa kushuka kwenye range inayotakiwa ambayo ni kati ya 500 mpaka 1000 RPM..

Kitu kinachofanya rpm kuchelewa kushuka pia ni uzito wa oil, oil pump na oil filter kwa wakati huo vinapata kazi ya ziada kuhakikisha oil inafika sehemu za juu za injini...

Kwa kawaida SAE 40 unachelewa kufika sehemu za juu za injini kwenye cold start(pale unapowasha gari asubuhi.)

Kitendo cha hii oil kuchelewa kufika, vyuma vya juu kama valve lifters na vinginevyo vinasagika kidogo kidogo bila wewe kujua...

Madhara yake baada ya miaka si mingi utaanza kusikia knocking sound sehemu za juu za engine yako..

Magari zaidi ya 98% yaliyotengenezwa miaka ya 2000 kuja juu recommended engine oil lazima iwe MULT GRADE yaani hizi oil zenye namba mbili mfano 5W 30

Magari ya siku hizi hayatakiwi kutumia oil ambayo ni MONO GRADE mfano SAE 30,40,50......

Kwa wewe ambaye umekuwa ukitumia SAE 40 ambayo ni Mono grade kwa gari yenye 99k KM, bado hujachelewa kuhamia kwenye Mult grade kama SAE 5W30,10W30, 5W40, 10W 40 au 15w 40 endapo hiyo SAE 40 ulikuwa unaibadilisha kwa wakati yaani hupitishi muda wa service ambapo kiuhalisia SAE 40 inatakiwa kumwagwa baada ya km 3000 kwa sababu mazingira ya uendeshaji wetu wa kitanzania ni magumu...gari linapata dhoruba za milima, mabonde na mizigo.

Kama gari lako la petrol ni lamiaka ya hivi karibuni na lina mileage kubwa (over 150k KM) hapa ukitumia oil viscosity namba 40 si mbaya ila iwe MULT GRADE na isiwe 40kavu.......hapa unaweza kutumia 5w40,10w40,15w40 na kadhalika kulingana na dhoruba gari linazopitia

Faida ya kutumia Mult grade oils ni kwamba zinakupa uhakika wa kulainisha injini mapema wakati wa asubuhi hata kama umepaki gari wiki nzima ukiwasha ndani ya wastani wa dakika moja au chini ya hapo oil inakuwa imeenea maeneo yote ya engine...

Mult grade oil ina tabia ya kuwa nyepesi pale gari linapowashwa na injini ikishapata moto oil inakuwa nzito kufikia kipimo cha viscosity yake mfano 30,40 au 50

Kwa kawaida oil 5w30,5W40,10W40 ni ghali kuliko SAE 30,40,50 kama zinazalishwa na kampuni moja mfano TOTAL...
Watanzania tunapenda vya bei rahisi...mtu anakwepa Mult grade oil, anaweka mono grade lakini madhara yake yanakuja pole pole bila wewe kujua.

SAE 40 hizi tuwaachie watu wa magari ambayo ni model za kizamaninzaidi mfano watu RAV 4 MASAWE zenye 3 s wakitumia SAE 40 kavu haliharibiki jambo na magari mengine ya miaka ya 2000 kurudi nyuma..

Watu wa madaladala na Mitsubish canter hizo ndizo oil zao kwa sababu injini zao zinaruhusu oil za grade hizo na zinafanya kazi za shuruba..

Ikumbukwe oil ndiyo DAMU ya injini, ukiweka tofauti na mtengenezaji anavyotaka au kuangalia mileage ya gari lako, basi ni rahisi sana kuichosha injini yako mapema..

Usishangae kukuta gari zuri la toyota lenye injini mathalani 1NZ au 2NZ linaunguruma kama TATA za pistoni tatu....HAPO SAE 40 inakuwa imeshafanya yake
 
Njoo CAMEL patrol station BOKO NAMANGA uweze kukutana na fundi wa uwakika katika gari yako
 
Somo zuri
 
Mfano mie gari ilikuja na kilomia 52000 injini 1NZ sikuwah kujua kama inatumia 5w 30 au 10w 30 had nilipoingia humu sa hv ipo kilomita 99880 je nikirudi huko halitazingua mana lishazoea ma oil yetu haya sae 40 na 20w 50.....

NB nilikua nashangaa sana kwann asubuhi ukiwasha rpm inkua juu afu badae linarud kawaida kumbe oil dah
Mkuu rpm inakua juu, unamaanisha ni kwenye around 2000, hiyo ni kawaida kwa 1nz kufanya hivyo kama ni ya baridi.
Ila inatakiwa ndani tu ya dakika ya kwanza hiyo rpm iwe imeshaanza kushuka.
Kama inachukua muda mrefu kushuka basi kuna uwezekano ume bypass thermostat, oil nzito sana, oil ni nyingi sana au vinginevyo.
Oil capacity ya hiyo engine ni 3.7L kama utabadili na filter lakini cha kufurahisha leo nimeshuhudia fundi ikiwekea dumu lote la total 4l kwenye hiyo engine, wamiliki kuweni makini na magari yenu!
 
Back
Top Bottom