TAHADHARI: Oil nyingi za engine za magari mtaani ni majanga

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,328
Hiki kisa kinahusu gari moja aina ya Volkswagen Polo GTI mk5 toleo la mwaka 2012. Gari ina engine ya EA211 1.4TSI twin charge.

Screenshot_2023-05-07-13-10-25-043_com.miui.gallery.jpg

Hii kazi niliunganishiwa na mtu wa humuhumu ndani japo huyo mtu alidai hanifahamu personally na hatujawahi kufanya kazi ila ameshakutana na post zangu nyingi humu JF. Nadhani huyo jamaa huu uzi atakutana nao tu.

Hiyo gari hata miezi miwili haijamaliza toka ameichukua yard. Aliiendesha kidogo siku za mwanzoni ikamletea ujumbe wa "Service Due!" kwenye Dashboard.

Akapeleka gari mahali ikafanyiwa engine service. Ikawekwa Castrol 5W-40 na Oil filter mpya. Oil aliyoweka ilikuwa ni sahihi japo sijui kama ilikuwa ni VW approved maana hiyo engine inataka 5W-30 au 5W-40 lakini iwe VW-505 approved.

Jamaa akaja kuichukua gari hakuiendesha umbali mrefu sana ikamuwakia taa nyekundu ya Oil na maandishi yanayosomeka "Oil Pressure, Engine Off! Owner's Manual " kwenye dashboard. Kama inavyoonekana Pichani.

Screenshot_20230506-141841.png

Muungurumo wa engine upo kawaida na ukifungua kifuniko cha Oil pale juu oil Inaruka kama kawaida(Wataalamu wa mambo wakiona hivi huwa wanadai Oil pressure ipo).

Akarudi kwa jamaa waliomfanyia service, wakaona kwa sababu wametoka kufanya service basi hapo shida inaweza kuwa Oil pressure switch.

Wakatoa Oil pressure switch Original iliyokuja na gari wakanunua sensor nyingine wakaweka. Shida ikawa iko palepale.

Mwenye gari akaamua kubadili fundi. Akaenda kwa mmoja wa mafundi ambao wana majina makubwa tu hapa mjini. Huyo fundi naye ili kujiridhisha akasema aifanyie service na upya.

Akanunua Oil kampuni X kiasi cha lita 5😳😳😳 kwa madai yake pamoja na oil filter(Yaani engine yakuweka 3.8L oil uweke lita 5? Maajabu). Akafanya service, kuja kuendesha gari taa ya Oil na ujumbe wa low pressure bado vipo.

Naye akasema shida itakuwa ni Oil pressure sensor, Zikanunuliwa Oil pressure switch kadhaa. Ikafungwa moja baada ya nyingine lakini bado shida ikawa palepale.

Akapimapima ule waya wa Oil pressure switch(Upo mmoja tu, signal line). Mwisho akacome up na majibu kwamba ule waya wa una short(Short circuit). Hivyo zile sensor kila ukiweka mpya zinaungua. Lakini hakuweza kufix hiyo shoti.

Mpaka hapa gari ilimeshakula zaidi ya Tsh. 2,000,000/=.

Akarudishia Oil pressure sensor iliyokuwepo ambayo ndio ile aliyonunua jamaa wa kwanza(Ikumbukwe Oil pressure sensor Original iliyokuja na gari ilishatolewa na yule jamaa wa kwanza).

Sasa week iliyopita ndio gari ikaja ofisini kwangu. Jamaa akanisimulia hayo mambo yote. Nikachukua mashine ya Diagnosis nikapima nikapata code moja tu ambayo ilikuwa active ambayo ni P164D00 (Reduced Oil pressure Switch Malfunction).

IMG_20230507_131557.jpg

Hatua ya kwanza niliyochukua. Nikadisconnect waya wa Oil pressure switch nikauunganisha na Signal generator.

View attachment IMG_20230507_131958.jpg

Hii signal generator ni kifaa ambacho kina uwezo wa kutoa signals kama zinavyotoa Sensors zilizopo kwenye gari. Hiki kifaa huwa nakitumia sana kujiridhisha kama shida ipo upande wa Sensor au Shida ipo upande wa wiring na control box (ECU).

Ni kifaa ambacho kinanirahisishia sana kwenye kubaini matatizo ya Wiring za sensors, hata kama wiring mtu kaichezea.

Basi tuendelee, Nikaunga hiyo signal generator kwenye connector ya Oil Pressure Switch.

Awamu ya kwanza nikaset signal iwe 5V, Tukaendesha gari taa Oil ikawaka.

Awamu ya pili nikaset signal 3V, Bado taa ikaendelea kuwaka.

Awamu ya tatu nikatest 8V tukatest gari bado taa ikaendelea kuwaka.

Awamu ya nne nikaseti 0.49V jamaa akatest taa haikuwaka(Hii taa ya Oil huwa inawaka ukishaanza kuvuka 30kph). Akarudi, Nikamuambia ajaribu kutest kipande kirefu kidogo. Akatika Sinza Kijiweni akaja mpaka Shekilango na Kurudi na ta haikuwaka.

Mpaka hapo nikawa nimejiridhisha kwamba gari haina shoti na shida ipo upande wa Sensor(Na mimi nilikuwa naelekea kununua Sensor nyingine). Siku ya kwanza tuliishia hapo.

Tukaja tukaonana baada ya siku 2. Nikamuomba jamaa nijiridhishe baadhi ya vitu kabla ya kununua Sensor. Kwanza nikataka nijiridhishe Je, Ni kweli ule waya wa Oil pressure switch una Short?

Basi nikaupima ukiwa switch On na ukiwa umewasha gari. Aiseeee Ule waya ulikuwa unasoma Voltage ya Battery. Hapa na mimi kichwa kikaanza kuwaka moto.

Lakini kwa sababu nilikuwa na Signal generator nikaunganisha nikapima tena ikawa inasoma ile voltage ya signal generator ambayo ni 0.49V. Hapa nikahitimisha kwamba gari haina Shoti kwa sababu sensor ikitoa voltage, ile voltage ya battery iliyokuwa inasoma kwenye wire wake inakuwa haipo tena.

Hapa sasa mawazo yaliyobakia ikawa ni kwenda kutafuta Sensor nyingine. Lakini kuna wazo likaja. Ninayo Pressure gauge ambayo huwa napimia Pressure ya Mafuta. Lakini hiyo gauge inaweza kupima Oil pressure ya Engine.

View attachment IMG_20230507_131913.jpg

Basi tukafunga hiyo gauge tukawasha gari. Aiseeee tulichokiona hatukuamini macho yetu. Oil pressure inasoma 0.2bar. Aiseee hii pressure ni ndogo mno. Yaani angalau ilitakuwa kufika 0.8 bar.

Ingawa ukikanyaga accelerator Pressure ilikuwa inapanda mpaka 1.5Bar.

Palepale nikamuambia jamaa kwamba hapa shida ni Pressure ndogo. Na kama tunaamua kwenda kubadilisha Sensor, Hicho tunachotaka kufanya ni kamali. Kuna uwezekano mkubwa kisifanye kazi.

Basi jamaa akasema tujaribu. Basi tukaenda Magomeni kwa Babu wa VW, kuna jamaa wakatuassist pale wakatupa sensor 4. Kila tukifunga sensor tukiendesha gari taa inarudi. Mpaka giza likaingia. Hii siku tukawa tumejiridhisha kwamba shida siyo Sensor.

Basi nikakubaliana na mwenye gari kwamba tujipe muda hata wa siku mbili ili tuwaze ni kitu gani kinaweza kikafanyika ili kuondokana na hilo tatizo?

The next day nikaja na solution kwamba Tununue Oil Original Castrol Edge 5W-30 kutoka kwa Dealer pamoja na Oil Filter Original, Pia ile sensor ya mwanzo iliyokuja na gari irudi tuirudishie.

Majuzi ndio vimenunuliwa hivyo vitu. Oil Lita 4 pamoja na Oil filter Original imekatika around Laki 2 kununua tu hivyo vitu. Pia Sensor Original akaenda kuifata.

IMG_20230506_170929.jpg

IMG_20230506_171036.jpg

Tumefanya service hiyo juzi tukarudishia na sensor yake Original. Tukatest gari, Guest what?

Screenshot_2023-05-07-12-40-40-656_com.miui.gallery.jpg

Taa ya Low Oil pressure haikuwaka tena. Tukatoka Sinza kijiweni mpaka Kinondoni Studio na kurudi lakini taa haikuwa tena. Na haijawaka tena mpaka leo.

Mambo niliyojifunza.

1. Kutumia test light na multimeter siyo mara zote vitakupa majibu sahihi juu ya uwepo wa shoti kwenye wiring ya gari. Nimewahi kukutana na toyota Avensis ukiweka Switch ON kila waya wa sensor unaopima una umeme na gari haina shida.

2. Ukitoa sensor fulani kwenye gari jitahidi upate kama hiyohiyo, Sensor iliyotolewa kwenye gari ilikuwa inapima pressure kwa range ya 0.3bar to 0.6bar
Screenshot_2023-05-07-15-39-26-161_com.miui.gallery.jpg

wakati iliyowekwa ilikuwa inapima 1.3bar to 2.6bar.
Screenshot_2023-05-07-15-39-38-725_com.miui.gallery.jpg

Pia muonekano wa sensor hizo upande unaofunga kwenye engine ulikuwa tofauti. Hizi sensor haziwezi kufanana kwenye output signal. Hili huenda nalo lilichangia tatizo muda fulani.

3. Unapopachika spare kwenye gari hakikisha kila kitu kimekaa sawa. Hiyo oil filter niliyoitoa kwenye gari wakati nafanya service haikuwa na Seal ya hapo juu nilipoweka arrow. Hilo ni tatizo.

View attachment IMG_20230507_123604.jpg

4. Engine za gari za mzungu zipo very Sensitive sana kwenye Oil. Jitahidi upate Oil original.

5. Kufungua mfuniko wa Oil na kuona Oil inaruka ruka na gari kutokuwa na.muungurumo mbaya siyo vipimo vya kwamba hiyo engine ina Oil Pressure ya kutosha. Mfano hiyo engine ya VW oil pressure switch yake inakaa nyuma ya engine, Oil ilikuwa inaruka ukifungua mfuniko na engine haikuwa na kelele lakini engine haikuwa na Oil pressure ya kutosha.

Gari yako ina tatizo gani? Karibu tukuhudumie.

0621 221 606.
 
Fundi msomi sana hauna baya bro. Elimu nzuri sana sana sana.

Kwenye oil hapo mi nna swali. Naona kuna mahala wamesema recommended oil 5W30 inamaana nikinunua brand yoyote (Castrol Edge, Total, Liqui Molly etc) haina shida?

Na pili, wakisema Grade ACEA C3 inamaanisha nini? Nimekuta kuna oil zote ni mfano 5W30 ila kuna ACEA C1, C2, C3.

Shukrani.
 
Hiki kisa kinahusu gari moja aina ya Volkswagen Polo GTI mk5 toleo la mwaka 2012. Gari ina engine ya EA211 1.4TSI twin charge.

View attachment 2613140

Hii kazi niliunganishiwa na mtu wa humuhumu ndani japo huyo mtu alidai hanifahamu personally na hatujawahi kufanya kazi ila ameshakutana na post zangu nyingi humu JF. Nadhani huyo jamaa huu uzi atakutana nao tu.

Hiyo gari hata miezi miwili haijamaliza toka ameichukua yard. Aliiendesha kidogo siku za mwanzoni ikamletea ujumbe wa "Service Due!" kwenye Dashboard.

Akapeleka gari mahali ikafanyiwa engine service. Ikawekwa Castrol 5W-40 na Oil filter mpya. Oil aliyoweka ilikuwa ni sahihi japo sijui kama ilikuwa ni VW approved maana hiyo engine inataka 5W-30 au 5W-40 lakini iwe VW-505 approved.

Jamaa akaja kuichukua gari hakuiendesha umbali mrefu sana ikamuwakia taa nyekundu ya Oil na maandishi yanayosomeka "Oil Pressure, Engine Off! Owner's Manual " kwenye dashboard. Kama inavyoonekana Pichani.

View attachment 2613141

Muungurumo wa engine upo kawaida na ukifungua kifuniko cha Oil pale juu oil Inaruka kama kawaida(Wataalamu wa mambo wakiona hivi huwa wanadai Oil pressure ipo).

Akarudi kwa jamaa waliomfanyia service, wakaona kwa sababu wametoka kufanya service basi hapo shida inaweza kuwa Oil pressure switch.

Wakatoa Oil pressure switch Original iliyokuja na gari wakanunua sensor nyingine wakaweka. Shida ikawa iko palepale.

Mwenye gari akaamua kubadili fundi. Akaenda kwa mmoja wa mafundi ambao wana majina makubwa tu hapa mjini. Huyo fundi naye ili kujiridhisha akasema aifanyie service na upya.

Akanunua Oil kampuni X kiasi cha lita 5😳😳😳 kwa madai yake pamoja na oil filter(Yaani engine yakuweka 3.8L oil uweke lita 5? Maajabu). Akafanya service, kuja kuendesha gari taa ya Oil na ujumbe wa low pressure bado vipo.

Naye akasema shida itakuwa ni Oil pressure sensor, Zikanunuliwa Oil pressure switch kadhaa. Ikafungwa moja baada ya nyingine lakini bado shida ikawa palepale.

Akapimapima ule waya wa Oil pressure switch(Upo mmoja tu, signal line). Mwisho akacome up na majibu kwamba ule waya wa una short(Short circuit). Hivyo zile sensor kila ukiweka mpya zinaungua. Lakini hakuweza kufix hiyo shoti.

Mpaka hapa gari ilimeshakula zaidi ya Tsh. 2,000,000/=.

Akarudishia Oil pressure sensor iliyokuwepo ambayo ndio ile aliyonunua jamaa wa kwanza(Ikumbukwe Oil pressure sensor Original iliyokuja na gari ilishatolewa na yule jamaa wa kwanza).

Sasa week iliyopita ndio gari ikaja ofisini kwangu. Jamaa akanisimulia hayo mambo yote. Nikachukua mashine ya Diagnosis nikapima nikapata code moja tu ambayo ilikuwa active ambayo ni P164D00 (Reduced Oil pressure Switch Malfunction).

View attachment 2613148

Hatua ya kwanza niliyochukua. Nikadisconnect waya wa Oil pressure switch nikauunganisha na Signal generator.

View attachment 2613475

Hii signal generator ni kifaa ambacho kina uwezo wa kutoa signals kama zinavyotoa Sensors zilizopo kwenye gari. Hiki kifaa huwa nakitumia sana kujiridhisha kama shida ipo upande wa Sensor au Shida ipo upande wa wiring na control box (ECU).

Ni kifaa ambacho kinanirahisishia sana kwenye kubaini matatizo ya Wiring za sensors, hata kama wiring mtu kaichezea.

Basi tuendelee, Nikaunga hiyo signal generator kwenye connector ya Oil Pressure Switch.

Awamu ya kwanza nikaset signal iwe 5V, Tukaendesha gari taa Oil ikawaka.

Awamu ya pili nikaset signal 3V, Bado taa ikaendelea kuwaka.

Awamu ya tatu nikatest 8V tukatest gari bado taa ikaendelea kuwaka.

Awamu ya nne nikaseti 0.49V jamaa akatest taa haikuwaka(Hii taa ya Oil huwa inawaka ukishaanza kuvuka 30kph). Akarudi, Nikamuambia ajaribu kutest kipande kirefu kidogo. Akatika Sinza Kijiweni akaja mpaka Shekilango na Kurudi na ta haikuwaka.

Mpaka hapo nikawa nimejiridhisha kwamba gari haina shoti na shida ipo upande wa Sensor(Na mimi nilikuwa naelekea kununua Sensor nyingine). Siku ya kwanza tuliishia hapo.

Tukaja tukaonana baada ya siku 2. Nikamuomba jamaa nijiridhishe baadhi ya vitu kabla ya kununua Sensor. Kwanza nikataka nijiridhishe Je, Ni kweli ule waya wa Oil pressure switch una Short?

Basi nikaupima ukiwa switch On na ukiwa umewasha gari. Aiseeee Ule waya ulikuwa unasoma Voltage ya Battery. Hapa na mimi kichwa kikaanza kuwaka moto.

Lakini kwa sababu nilikuwa na Signal generator nikaunganisha nikapima tena ikawa inasoma ile voltage ya signal generator ambayo ni 0.49V. Hapa nikahitimisha kwamba gari haina Shoti kwa sababu sensor ikitoa voltage, ile voltage ya battery iliyokuwa inasoma kwenye wire wake inakuwa haipo tena.

Hapa sasa mawazo yaliyobakia ikawa ni kwenda kutafuta Sensor nyingine. Lakini kuna wazo likaja. Ninayo Pressure gauge ambayo huwa napimia Pressure ya Mafuta. Lakini hiyo gauge inaweza kupima Oil pressure ya Engine.

View attachment 2613477

Basi tukafunga hiyo gauge tukawasha gari. Aiseeee tulichokiona hatukuamini macho yetu. Oil pressure inasoma 0.2bar. Aiseee hii pressure ni ndogo mno. Yaani angalau ilitakuwa kufika 0.8 bar.

Ingawa ukikanyaga accelerator Pressure ilikuwa inapanda mpaka 1.5Bar.

Palepale nikamuambia jamaa kwamba hapa shida ni Pressure ndogo. Na kama tunaamua kwenda kubadilisha Sensor, Hicho tunachotaka kufanya ni kamali. Kuna uwezekano mkubwa kisifanye kazi.

Basi jamaa akasema tujaribu. Basi tukaenda Magomeni kwa Babu wa VW, kuna jamaa wakatuassist pale wakatupa sensor 4. Kila tukifunga sensor tukiendesha gari taa inarudi. Mpaka giza likaingia. Hii siku tukawa tumejiridhisha kwamba shida siyo Sensor.

Basi nikakubaliana na mwenye gari kwamba tujipe muda hata wa siku mbili ili tuwaze ni kitu gani kinaweza kikafanyika ili kuondokana na hilo tatizo?

The next day nikaja na solution kwamba Tununue Oil Original Castrol Edge 5W-30 kutoka kwa Dealer pamoja na Oil Filter Original, Pia ile sensor ya mwanzo iliyokuja na gari irudi tuirudishie.

Majuzi ndio vimenunuliwa hivyo vitu. Oil Lita 4 pamoja na Oil filter Original imekatika around Laki 2 kununua tu hivyo vitu. Pia Sensor Original akaenda kuifata.

View attachment 2613159

View attachment 2613160

Tumefanya service hiyo juzi tukarudishia na sensor yake Original. Tukatest gari, Guest what?

View attachment 2613161

Taa ya Low Oil pressure haikuwaka tena. Tukatoka Sinza kijiweni mpaka Kinondoni Studio na kurudi lakini taa haikuwa tena. Na haijawaka tena mpaka leo.

Mambo niliyojifunza.

1. Kutumia test light na multimeter siyo mara zote vitakupa majibu sahihi juu ya uwepo wa shoti kwenye wiring ya gari. Nimewahi kukutana na toyota Avensis ukiweka Switch ON kila waya wa sensor unaopima una umeme na gari haina shida.

2. Ukitoa sensor fulani kwenye gari jitahidi upate kama hiyohiyo, Sensor iliyotolewa kwenye gari ilikuwa inapima pressure kwa range ya 0.3bar to 0.6bar
View attachment 2613481

wakati iliyowekwa ilikuwa inapima 1.3bar to 2.6bar.
View attachment 2613482

Pia muonekano wa sensor hizo upande unaofunga kwenye engine ulikuwa tofauti. Hizi sensor haziwezi kufanana kwenye output signal. Hili huenda nalo lilichangia tatizo muda fulani.

3. Unapopachika spare kwenye gari hakikisha kila kitu kimekaa sawa. Hiyo oil filter niliyoitoa kwenye gari wakati nafanya service haikuwa na Seal ya hapo juu nilipoweka arrow. Hilo ni tatizo.

View attachment 2613479

4. Engine za gari za mzungu zipo very Sensitive sana kwenye Oil. Jitahidi upate Oil original.

5. Kufungua mfuniko wa Oil na kuona Oil inaruka ruka na gari kutokuwa na.muungurumo mbaya siyo vipimo vya kwamba hiyo engine ina Oil Pressure ya kutosha. Mfano hiyo engine ya VW oil pressure switch yake inakaa nyuma ya engine, Oil ilikuwa inaruka ukifungua mfuniko na engine haikuwa na kelele lakini engine haikuwa na Oil pressure ya kutosha.

Gari yako ina tatizo gani? Karibu tukuhudumie.

0621 221 606.
Long live JF.
 
Hiki kisa kinahusu gari moja aina ya Volkswagen Polo GTI mk5 toleo la mwaka 2012. Gari ina engine ya EA211 1.4TSI twin charge.

View attachment 2613140

Hii kazi niliunganishiwa na mtu wa humuhumu ndani japo huyo mtu alidai hanifahamu personally na hatujawahi kufanya kazi ila ameshakutana na post zangu nyingi humu JF. Nadhani huyo jamaa huu uzi atakutana nao tu.

Hiyo gari hata miezi miwili haijamaliza toka ameichukua yard. Aliiendesha kidogo siku za mwanzoni ikamletea ujumbe wa "Service Due!" kwenye Dashboard.

Akapeleka gari mahali ikafanyiwa engine service. Ikawekwa Castrol 5W-40 na Oil filter mpya. Oil aliyoweka ilikuwa ni sahihi japo sijui kama ilikuwa ni VW approved maana hiyo engine inataka 5W-30 au 5W-40 lakini iwe VW-505 approved.

Jamaa akaja kuichukua gari hakuiendesha umbali mrefu sana ikamuwakia taa nyekundu ya Oil na maandishi yanayosomeka "Oil Pressure, Engine Off! Owner's Manual " kwenye dashboard. Kama inavyoonekana Pichani.

View attachment 2613141

Muungurumo wa engine upo kawaida na ukifungua kifuniko cha Oil pale juu oil Inaruka kama kawaida(Wataalamu wa mambo wakiona hivi huwa wanadai Oil pressure ipo).

Akarudi kwa jamaa waliomfanyia service, wakaona kwa sababu wametoka kufanya service basi hapo shida inaweza kuwa Oil pressure switch.

Wakatoa Oil pressure switch Original iliyokuja na gari wakanunua sensor nyingine wakaweka. Shida ikawa iko palepale.

Mwenye gari akaamua kubadili fundi. Akaenda kwa mmoja wa mafundi ambao wana majina makubwa tu hapa mjini. Huyo fundi naye ili kujiridhisha akasema aifanyie service na upya.

Akanunua Oil kampuni X kiasi cha lita 5 kwa madai yake pamoja na oil filter(Yaani engine yakuweka 3.8L oil uweke lita 5? Maajabu). Akafanya service, kuja kuendesha gari taa ya Oil na ujumbe wa low pressure bado vipo.

Naye akasema shida itakuwa ni Oil pressure sensor, Zikanunuliwa Oil pressure switch kadhaa. Ikafungwa moja baada ya nyingine lakini bado shida ikawa palepale.

Akapimapima ule waya wa Oil pressure switch(Upo mmoja tu, signal line). Mwisho akacome up na majibu kwamba ule waya wa una short(Short circuit). Hivyo zile sensor kila ukiweka mpya zinaungua. Lakini hakuweza kufix hiyo shoti.

Mpaka hapa gari ilimeshakula zaidi ya Tsh. 2,000,000/=.

Akarudishia Oil pressure sensor iliyokuwepo ambayo ndio ile aliyonunua jamaa wa kwanza(Ikumbukwe Oil pressure sensor Original iliyokuja na gari ilishatolewa na yule jamaa wa kwanza).

Sasa week iliyopita ndio gari ikaja ofisini kwangu. Jamaa akanisimulia hayo mambo yote. Nikachukua mashine ya Diagnosis nikapima nikapata code moja tu ambayo ilikuwa active ambayo ni P164D00 (Reduced Oil pressure Switch Malfunction).

View attachment 2613148

Hatua ya kwanza niliyochukua. Nikadisconnect waya wa Oil pressure switch nikauunganisha na Signal generator.

View attachment 2613475

Hii signal generator ni kifaa ambacho kina uwezo wa kutoa signals kama zinavyotoa Sensors zilizopo kwenye gari. Hiki kifaa huwa nakitumia sana kujiridhisha kama shida ipo upande wa Sensor au Shida ipo upande wa wiring na control box (ECU).

Ni kifaa ambacho kinanirahisishia sana kwenye kubaini matatizo ya Wiring za sensors, hata kama wiring mtu kaichezea.

Basi tuendelee, Nikaunga hiyo signal generator kwenye connector ya Oil Pressure Switch.

Awamu ya kwanza nikaset signal iwe 5V, Tukaendesha gari taa Oil ikawaka.

Awamu ya pili nikaset signal 3V, Bado taa ikaendelea kuwaka.

Awamu ya tatu nikatest 8V tukatest gari bado taa ikaendelea kuwaka.

Awamu ya nne nikaseti 0.49V jamaa akatest taa haikuwaka(Hii taa ya Oil huwa inawaka ukishaanza kuvuka 30kph). Akarudi, Nikamuambia ajaribu kutest kipande kirefu kidogo. Akatika Sinza Kijiweni akaja mpaka Shekilango na Kurudi na ta haikuwaka.

Mpaka hapo nikawa nimejiridhisha kwamba gari haina shoti na shida ipo upande wa Sensor(Na mimi nilikuwa naelekea kununua Sensor nyingine). Siku ya kwanza tuliishia hapo.

Tukaja tukaonana baada ya siku 2. Nikamuomba jamaa nijiridhishe baadhi ya vitu kabla ya kununua Sensor. Kwanza nikataka nijiridhishe Je, Ni kweli ule waya wa Oil pressure switch una Short?

Basi nikaupima ukiwa switch On na ukiwa umewasha gari. Aiseeee Ule waya ulikuwa unasoma Voltage ya Battery. Hapa na mimi kichwa kikaanza kuwaka moto.

Lakini kwa sababu nilikuwa na Signal generator nikaunganisha nikapima tena ikawa inasoma ile voltage ya signal generator ambayo ni 0.49V. Hapa nikahitimisha kwamba gari haina Shoti kwa sababu sensor ikitoa voltage, ile voltage ya battery iliyokuwa inasoma kwenye wire wake inakuwa haipo tena.

Hapa sasa mawazo yaliyobakia ikawa ni kwenda kutafuta Sensor nyingine. Lakini kuna wazo likaja. Ninayo Pressure gauge ambayo huwa napimia Pressure ya Mafuta. Lakini hiyo gauge inaweza kupima Oil pressure ya Engine.

View attachment 2613477

Basi tukafunga hiyo gauge tukawasha gari. Aiseeee tulichokiona hatukuamini macho yetu. Oil pressure inasoma 0.2bar. Aiseee hii pressure ni ndogo mno. Yaani angalau ilitakuwa kufika 0.8 bar.

Ingawa ukikanyaga accelerator Pressure ilikuwa inapanda mpaka 1.5Bar.

Palepale nikamuambia jamaa kwamba hapa shida ni Pressure ndogo. Na kama tunaamua kwenda kubadilisha Sensor, Hicho tunachotaka kufanya ni kamali. Kuna uwezekano mkubwa kisifanye kazi.

Basi jamaa akasema tujaribu. Basi tukaenda Magomeni kwa Babu wa VW, kuna jamaa wakatuassist pale wakatupa sensor 4. Kila tukifunga sensor tukiendesha gari taa inarudi. Mpaka giza likaingia. Hii siku tukawa tumejiridhisha kwamba shida siyo Sensor.

Basi nikakubaliana na mwenye gari kwamba tujipe muda hata wa siku mbili ili tuwaze ni kitu gani kinaweza kikafanyika ili kuondokana na hilo tatizo?

The next day nikaja na solution kwamba Tununue Oil Original Castrol Edge 5W-30 kutoka kwa Dealer pamoja na Oil Filter Original, Pia ile sensor ya mwanzo iliyokuja na gari irudi tuirudishie.

Majuzi ndio vimenunuliwa hivyo vitu. Oil Lita 4 pamoja na Oil filter Original imekatika around Laki 2 kununua tu hivyo vitu. Pia Sensor Original akaenda kuifata.

View attachment 2613159

View attachment 2613160

Tumefanya service hiyo juzi tukarudishia na sensor yake Original. Tukatest gari, Guest what?

View attachment 2613161

Taa ya Low Oil pressure haikuwaka tena. Tukatoka Sinza kijiweni mpaka Kinondoni Studio na kurudi lakini taa haikuwa tena. Na haijawaka tena mpaka leo.

Mambo niliyojifunza.

1. Kutumia test light na multimeter siyo mara zote vitakupa majibu sahihi juu ya uwepo wa shoti kwenye wiring ya gari. Nimewahi kukutana na toyota Avensis ukiweka Switch ON kila waya wa sensor unaopima una umeme na gari haina shida.

2. Ukitoa sensor fulani kwenye gari jitahidi upate kama hiyohiyo, Sensor iliyotolewa kwenye gari ilikuwa inapima pressure kwa range ya 0.3bar to 0.6bar
View attachment 2613481

wakati iliyowekwa ilikuwa inapima 1.3bar to 2.6bar.
View attachment 2613482

Pia muonekano wa sensor hizo upande unaofunga kwenye engine ulikuwa tofauti. Hizi sensor haziwezi kufanana kwenye output signal. Hili huenda nalo lilichangia tatizo muda fulani.

3. Unapopachika spare kwenye gari hakikisha kila kitu kimekaa sawa. Hiyo oil filter niliyoitoa kwenye gari wakati nafanya service haikuwa na Seal ya hapo juu nilipoweka arrow. Hilo ni tatizo.

View attachment 2613479

4. Engine za gari za mzungu zipo very Sensitive sana kwenye Oil. Jitahidi upate Oil original.

5. Kufungua mfuniko wa Oil na kuona Oil inaruka ruka na gari kutokuwa na.muungurumo mbaya siyo vipimo vya kwamba hiyo engine ina Oil Pressure ya kutosha. Mfano hiyo engine ya VW oil pressure switch yake inakaa nyuma ya engine, Oil ilikuwa inaruka ukifungua mfuniko na engine haikuwa na kelele lakini engine haikuwa na Oil pressure ya kutosha.

Gari yako ina tatizo gani? Karibu tukuhudumie.

0621 221 606.
Hongera sana
 
Fundi msomi sana hauna baya bro. Elimu nzuri sana sana sana.

Kwenye oil hapo mi nna swali. Naona kuna mahala wamesema recommended oil 5W30 inamaana nikinunua brand yoyote (Castrol Edge, Total, Liqui Molly etc) haina shida?

Na pili, wakisema Grade ACEA C3 inamaanisha nini? Nimekuta kuna oil zote ni mfano 5W30 ila kuna ACEA C1, C2, C3.

Shukrani.

Ukiambiwa recommended ni Ni 5W 30 unaweza kununua tu yoyote.

Lakini ukishaanza kuambiwa Labda ACEA 3, VW 505 00, MB-Approval 229.31 basi jitahidi upate 5W-30 yenye hizo approval hata ni kampuni yoyote. Kwa maana wanaweka hizo approve baada ya kuwa na wao wamefanya tests kwenye Labs zao.

ACEA ni mfumo wa European Union kugrade Viscosities za Oil. Kama tunavyosema SAE 5W-30, Hao ACEA nao wana mfumo wao ambao kwa light duty engines inaanzia C1 mpaka C6.

Mfano 5W 30 iko compatible na ACEA C3.

Tofauti kati ya hizo C1, C2, C3 naona iko iko kwenye Viscosities. Ingawa nadhani hata mimi mwenyewe bado nahitaji shule kwenye hizo grades za ACEA.
 
Back
Top Bottom