Nimeweka Engine Oil 20w-50 X-trail NT30 (2003) nipo sawa?

Boeing 747 samahani sana mkuu, kama hautojali hebu sikia kilio chetu na sie wamiliki wa suzuki carry aka kirikuu.

Hivi ni oil ipi ni rafiki kwa vigari vyetu ambavyo vimetembea ma kilomita ya kutosha? natanguliza shukrani
 
Huu uzi umefanya nikubali kubadili oil leo.
Niliweka castrol 20w50 imetembea km 500 pekee.
Gari rav 4 kill time 2003 Awd
Nimeweka 5w30 ambayo ni recomended.
Kulingana na michango toka kwa wadau
Jamiiforums ni sehemu pekee kwa tunakumbushana na kufundishwa madini
Muhimu sana.
Kama uko sehemu ambayo joto linakuwa above 30 degrees utakuwa umechemka. Na pia kama uko maeneo kama Mbeya, Arusha n.k oil uliyoweka si sawa pia maana joto huwa linashuka below 20. Ili kubalance ni kuweka 5W40 ambayo viscosity yake haiko mbali sana na hiyo 5W30 na pia unaweza kuendesha mkoa wowote hapa Tanzania
 
Wakuu salama? Nimeweka Engine Oil 20W-50 kwenye X-trail niliyonujua majuzi nipo sawa? Ama nimeingia cha kike?
mileage: 41,000kms
Oil yoyote ni sawa, tofauti ni muda wa kuibadili. Oils zinazodumu muda mrefu kwenye gari ni full synthetics nathani ni 0W 50 ambayo inadumu hata 10,000 km. Hizi nyingine hasa zinazoanza na 20, ni nzito zaidi na zinachoka haraka kwa hiyo huna budi kuibadili baada ya km chache tu.
 
Boeing 747 samahani sana mkuu, kama hautojali hebu sikia kilio chetu na sie wamiliki wa suzuki carry aka kirikuu.

Hivi ni oil ipi ni rafiki kwa vigari vyetu ambavyo vimetembea ma kilomita ya kutosha? natanguliza shukrani
Mkuu uki-search recommended SAE viscosity ya Suzuki Carry aka KIRIKUU ni 5w30 au 15w30..

Ushauri...oili hii ni nyepesi hivyo siyo rafiki kwa gari ambalo lina umri mkubwa kama limeshavuka 150k KM za mile age.

Swala la pili, kwa hapa bongo Kirikuu huwa kinapewa shuruba nzito za kubeba mizigo, bado sae 5w30 haitakuwa rafiki kwake..

Kwa maelezo yako tumia 10w40 au 15w 40..

Ila kama madereva wameshakiharibu sana especially engine, basi tena hapo Malizia tu maisha kwa SAE 40 kavu..
 
Oil yoyote ni sawa, tofauti ni muda wa kuibadili. Oils zinazodumu muda mrefu kwenye gari ni full synthetics nathani ni 0W 50 ambayo inadumu hata 10,000 km. Hizi nyingine hasa zinazoanza na 20, ni nzito zaidi na zinachoka haraka kwa hiyo huna budi kuibadili baada ya km chache tu.
okay, shukrani ndugu
 
Mkuu uki-search recommended SAE viscosity ya Suzuki Carry aka KIRIKUU ni 5w30 au 15w30..

Ushauri...oili hii ni nyepesi hivyo siyo rafiki kwa gari ambalo lina umri mkubwa kama limeshavuka 150k KM za mile age.

Swala la pili, kwa hapa bongo Kirikuu huwa kinapewa shuruba nzito za kubeba mizigo, bado sae 5w30 haitakuwa rafiki kwake..

Kwa maelezo yako tumia 10w40 au 15w 40..

Ila kama madereva wameshakiharibu sana especially engine, basi tena hapo Malizia tu maisha kwa SAE 40 kavu..
15w40
 
Ukweli kuhusu engines. Engine yoyote kwanza matumizi yake yanahesabiwa kwa masaa engine ilipofanya kazi na siyo km kama wauza/ watengeneza magari magari walivyojiwekea, na kuwajaza watu huo uongo. Fikiria tu Meli,Matrekta, Ndege na mitambo mingi inatumia engines ma hakuna kati ya hizo zinahesabiwa km zilizotembea!
Na kwa mantiki hiyo, kama kila engine inafanyiwa service kama aliyeitengeneza alivyosema, engine itadumu maisha yote. Engine zinakufa kwa kukosea service tu.
Maana yake ni hii.
1. Fikiria kuwa una gari unaamua hutembezi unalipaki lakini kila ukiamka asubuhi unalipiga start na unalizima jioni baada ya saa kumi. Gari hilo kwa mwezi, miezi mwaka litakuwa halikutembea ila engine imeshafanya kazi kila siku masaa 10.

2. Fikiria pia unaamua gari lako hilo unalifunga kamba na kulivuta kwa gari lingine kila siku kwenye mizunguko yako yote, tuseme km 150 lakini hulipigi start, dash itasoma imetembea km 150/day x 24 kwa mwezi tuseme kuna weekend n.k. Engine itakuwa as new maana haitumiki.

Hii wauza magari hawataki mtu ajue lakini ndio ukweli gari la kwanza litakuwa na km chache zilizotembea lakini engine ni mbaya maana imechakazwa na gari la pili limetembea km nyingi lakini engine ni mpya.

Muhimu ni kufuata manuals za manufacture wa gari wanataka oils za specification gani na kubadili baada ya muda gani, engine yoyote ile itadumu.
 
Unambiwa ubadili oili kila badaa ya kilomita efu 3000 au miezi mitatu..

Maaana yake ka ukitembea zikifika kilomita 3000 badili..

Kama unapaki sana unaendesha mara moja moja ikifika miezi mitatu pia badili...

Ila kwa kuwa wabongo sie service wabishi na magari tunfosi kumiliki basi kufikisha kilomita 5000 bila service kawaida tu...

Na kukaa na oili mwaka kisa haijafika kilomita efu 3 hyo ndio kabisaa utatuambia nini
 
Kwa hali hiyo, gari lolote utakalokuwa nalo halitodumu.
 
Wakuu salama? Nimeweka Engine Oil 20W-50 kwenye X-trail niliyonujua majuzi nipo sawa? Ama nimeingia cha kike?
mileage: 41,000kms
Weka na mwaka ambao gari imetengenezwa ili ukishauriwa upewe full answer na sio nusu nusu...
 
Yangu ni Toyota ya 2001, recommended oil specs ni 5w30. Nikiweka oil yenye viscosity nzito kama hizo za malori (20w50, 15w40), haya hutokea:
1. Injini kuvuma sana asubuhi
2. Fuel consumption kwenda juu sababu ya uzito wa oil.
3. Gari kuwa nzito barabarani

Ushauri: mtoa mada aweke recommended oil, 5w30. Hizo nzito nzito zina changamoto zake.
Asante sana
 
Back
Top Bottom