Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,668
86,539
Kama huna bando ni hivi, Ndugai aliupata Uspika kwa fitna dhidi ya Mama Anne Makinda, Ndugai alitibiwa kwa mamilioni ya fedha ughaibuni na hajapona Bado, Ndugai ana tabia ya kuwachapa bakora wapinzani wake...
Na Kali kuliko zote, Ndugai anawashikilia Wabunge 19 wasio na vyama kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano....

Video Iko chini
 
JOBO ANA HOJA LAKINI NAE NI WALEWALE!

Mtu ambaye amehusika katika ongezeko kubwa la deni la matibabu nje ya nchi ni pamoja na JOBO, anaweza kuwa na hoja sasa ya msingi (kuhusu mama yenu kukopa sana, mikopo yenye masharti), hoja hiyo tutaisikiliza lakini watu timamu tutakumbuka masuala kadhaa na tutahoji. Hivi!

Kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Bunge ya mwaka 2008, katika kifungu cha 24(1), “matibabu ya mbunge yatagharamiwa na Bunge ndani na nje ya nchi.” Bunge la Jobo limekuwa linatumia kifungu hiki kuidhinisha malipo ya matibabu ya Jobo na baadhi ya wabunge, wa CCM.

Deni la matibabu nje ya nchi, liliongezeka kwa kasi isiyo ya kawaida katika kipindi ambacho watumishi wa serikali wanaotibiwa nje ya nchi wanadhibitiwa na Rais, na Jobo mwenyewe amekuwa “mgonjwa (mkuu) mashuhuri” aliyetibiwa nje katika kipindi hicho.

Na hoja zake za jana, tunaweza kuzijadili kwa mtazamo tofauti wa kizalendo zaidi kwa kupitia kwa umakini zaidi taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG), ya mwaka 2017/2018, ongezeko hili ni la kati ya tarehe 30 Juni 2017 na tarehe 31 Desemba 2017.

Na muhimu zaidi, deni hilo lilongezeka katika kipindi ambacho wagonjwa wanaokwenda nje lazima waruhusiwe na Rais, na “mgonjwa mkuu” aliyetibiwa nje ni Jobo, ongezeko la deni la matibabu linahusu pia Jobo na sikuwahi kusikia wakati wa mwendazake, Jobo akihoji lolote!

Kwa mujibu wa takwimu za CAG, jamaa alikaa India kwa takriban miezi 5, akiwa na wasaidizi wake na familia yake. Posho ya mbunge anapokuwa nje ya nchi kwa siku 1 ni US$500; mtumishi wa bunge ni US$450; mwenzi wa ndoa ni US$300. Ni vile sisi ni mazuzu, huyu mtu hafai kuwa alipo!

Kwa uchambuzi wa ripoti ya CAG, Jobo alikaa India kwa miezi 5, ambayo ni siku 150. Kama kwa siku moja alilipwa US$500, miezi 5 alilipwa US$75,000. Kwa TZS, kwa viwango vya ubadilishaji fedha vya Sh. 2,170 kwa dola moja, jamaa alitumia Shs. 162,750,000 kama posho ya kuishi India.

Akiwa India, ‘kaperanaumu’ alikuwa na wasaidizi wawili – maana alihamishia ofisi yake huko huko hotelini. Kwa gharama ya US$450 kwa siku, mara mbili, watumishi hawa walilipwa US$900 kwa siku. Kwa siku 150 walizokaa India, maana yake walilipwa US$135,000, sawa na Sh. 292,950,000.

Wakati ofisi ya Jobo inatoa gharama zote hizi kwa ajili ya matibabu ya Jobo, kuna orodha ndefu ya wabunge wa upinzani (wakati huo) ambao walinyimwa huduma kama hiyo ambayo ni haki yao kisheria. Lakini ikawa halali kabisa kwa Jobo na aliona sawa tu kuishi India miezi 5.
C$P
 
Kama huna bando ni hivi, Ndugai aliupata Uspika kwa fitna dhidi ya Mama Anne Makinda, Ndugai alitibiwa kwa mamilioni ya fedha ughaibuni na hajapona Bado, Ndugai ana tabia ya kuwachapa bakora wapinzani wake...
Na Kali kuliko zote, Ndugai anawashikilia Wabunge 19 wasio na vyama kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano....

Video Iko chini
View attachment 2064271
🙌🙌😂😂😂😂
Kuwa Mgogo ni sawa na kuwa na kovu usoni kwa sasa hapa nchini
 
Kama huna bando ni hivi, Ndugai aliupata Uspika kwa fitna dhidi ya Mama Anne Makinda, Ndugai alitibiwa kwa mamilioni ya fedha ughaibuni na hajapona Bado, Ndugai ana tabia ya kuwachapa bakora wapinzani wake...
Na Kali kuliko zote, Ndugai anawashikilia Wabunge 19 wasio na vyama kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano....

Video Iko chini
View attachment 2064271

Kwani CCM haina vikao vya chama??!!, mbona mnaanika hadharani nguo zenu za ndani??!!🤣
 
Back
Top Bottom