UmkhontoweSizwe
Platinum Member
- Dec 19, 2008
- 8,534
- 7,739
Ndugu uwe unaelewa kwanza kabla ya kuja na zako ulizozizoea. Kwenye eneo la shule hakuna kanisa, isipokuwa jirani na shule kuna kanisa katoliki ambalo ni la watawa wabenedictine ambao ndio walikuwa wamiliki wa shule hiyo kabla haijachukuliwa na serikali. Kanisa hili sio kwa ajili ya wanafunzi bali wanajumuia wote wa ndanda.
Tena kama kungekuwa na wanaostahili kudai basi labda ni wale wa jumuia nyingine kama UKWATA, SABATO nk ambao vipindi vya kuabudu wanavifanyia madarasani, hao ndugu zako wana chumba maalum kwa ajili ya mambo yao tokea miaka mingi, wanaswali na kughani kila wanapohitaji na hawabughudhiwi na yeyote.
Mkuu, kujaribu kumwelewesha FF nadhani ni sawa na kumpigia ngoma kiziwi. Nimesema hapo juu kwamba hilo kanisa (chapel) haliko kwenye eneo la shule, ingawa liko karibu na shule, na pia siyo mali ya shule, ni mali ya Ndanda Mission. Lakini yeye kanijibu jibu la ajabuajabu!
Wao wapewe upendeleo wa kujenga nyumba ya ibada kwenye eneo la shule kama nani? Dini zingine hawana nyumba za ibada kwenye eneo la shule, wao tu ndo wapewe upendeleo, kisa nini?