Ndanda secondary-MGOMO WA KIDINI.....

Ni jumatatu nyingine tena kikundi kimoja cha kidini (waislam),wamesababisha kutoweka kwa amani baada ya kuanzisha mgomo kwa lengo la (a)kudai kunyimwa kupatiwa eneo la kujenga msikiti shuleni (b)kukataa uongozi wa wanafunzi kwa kudai kutokuwa na usawa katika uongozi huo(idadi sawa ya waislam na wakristo)
, kwa style hii shule itageuka eneo la kuabudia..

nashauri serikali itangaze shule hiyo kuwa ya kilimo halafu wale wadudu anaopenda bujibuji wafugwe, iwe ni zamu yaq kila mtu kuwahudimia. hii itakuwa ni njia ya kuwafundisha vijana kufikiria ujasiliamali na sio udini.

kilo moja ya mdudu ni zaidi ya kilo moja ya ng'ombe. 6,000tsh/kg kwa 4,000tsh/kg
 
FF, umezaliwa lini? Kama ni wa juzi (I hope so)jifunze. Ndanda Sec (kama ilivyokuwa Pugu sec) zilikuwa shule za Wakatoliki, hivyo sio ajabu kuwa na Kanisa shuleni. Unataka Serikali iloshindwa kujenga shule zenye kiwango kile imege maeneo ajili ya Masjid?

Hilo siyo tatizo, kwa sasa shule si ya kanisa na ina kanisa ndani kwanini na Waislaam wanapotaka kujenga mskiti wakataliwe?
 
nashauri serikali itangaze shule hiyo kuwa ya kilimo halafu wale wadudu anaopenda bujibuji wafugwe, iwe ni zamu yaq kila mtu kuwahudimia. hii itakuwa ni njia ya kuwafundisha vijana kufikiria ujasiliamali na sio udini.

kilo moja ya mdudu ni zaidi ya kilo moja ya ng'ombe. 6,000tsh/kg kwa 4,000tsh/kg

Hiyo vyema sana na utakuwa umetatuwa tatizo kabisa tena, unaakili sana wewe, unastahili sifa na pongezi.
 
Waendeshe harambee ya ujenzi wa msikiti, wakati wenzao wanaendelea kusoma! Ila msikiti waujenge uraiani nje ya shule, kwani hata kanisa halipo kwenye eneo la shule. Gadaffi yuko wapi jamani?
Dalili zinaonyesha kuwa, wengi wa wachangiaji kwenye uzi huu ni watu waliogubikwa na udini!!! Hoja za msingi hapo ni kuwa wameomba 'eneo' tu na wala sio kujengewa. Wao watajenga wenyewe.Na kingine ni usawa kwenye uongozi, sasa hapo tatizo liko wapi?
 
Kama kanisa limeruhusiwa kujengwa hapo shuleni na wao wanahaki ya kupewa nafasi ya kujenga mskiti. Kwanini kuwe na double standard? Kanisa wakubaliwe mskiti wakataliwe. Si haki, kama hapana ni wote na kama ndiyo ni wote.

Kumbuka hii shule ilikuwa ya dini(wakatoriki) hivyo hao wakatoriki hawakupewa eneo kujenga kanisa bali ni jengo walipewa kusalia na si kanisa kama unavyofikili.Isitoshe dini zote wanasalia ktk vyumba vya madarasa hata waislamu vilevile wamepewa.Waache ujinga wafanye kilichowapeleka Ndanda.Ujinga Ujinga Ujingaaaaaaaaaa...............
 
Hilo siyo tatizo, kwa sasa shule si ya kanisa na ina kanisa ndani kwanini na Waislaam wanapotaka kujenga mskiti wakataliwe?

Kwa hiyo hapo Tatizo ni Kanisa lililojengwa na "wenye shule"! Kwa kuwa Azania, Jangwani, Zanaki na Tambaza Sekondari hazina makanisa ndani yake basi Waislamu hawana haja ya kujenga misikiti ndani ya shule hizo.

HIYO NI SPECIAL MISSION NI CHOKOCHOKO ZA UDINI NA WAMEKUWA BRAIN WASHED.
 
Kama kanisa limeruhusiwa kujengwa hapo shuleni na wao wanahaki ya kupewa nafasi ya kujenga mskiti. Kwanini kuwe na double standard? Kanisa wakubaliwe mskiti wakataliwe. Si haki, kama hapana ni wote na kama ndiyo ni wote.

FF na wewe acha kuwa unakurupuka tu na kushabikia mambo hata usiyoyajua. Kuna watu hapo juu wameeleza vizuri kwamba vikundi vya wanafunzi vya kikristo Kama ukwata nk, huwa wanasali madarasani. Tycs (catholic) ndo pekee walio na kanisa, lakini kanisa Lao liko karibu na shule lakini HALIKO kwenye eneo la shule. Wao waislam ndo wamepewa jengo maalum kwa ajili ya shughuli zao za ibada. Usichoelewa hapo nini?
 
Dalili zinaonyesha kuwa, wengi wa wachangiaji kwenye uzi huu ni watu waliogubikwa na udini!!! Hoja za msingi hapo ni kuwa wameomba 'eneo' tu na wala sio kujengewa. Wao watajenga wenyewe.Na kingine ni usawa kwenye uongozi, sasa hapo tatizo liko wapi?
Kama wameomba si wasubiri majibu ya ombi lao? Mgomo na Maandamano ni maombi hayo?Serikali imelikuta Kanisa humo ilipotaifisha shule, na Serikali haina dini, sasa ikianza kugawa maeneo ya shule kujenga makanisa/misikiti si sawa
 
Maskini shule yangu sasa inataka kunajisiwa! Nimesoma pale kuanzia 1969 hadi 1972 na mambo yalikuwa murua. Wanafunzi wa dini zote tulisoma kwa kuheshimiana( suala la udini halikuwepo hata siku moja). Siku za Siku kuu za Kikristo, wanafunzi wote tulikuwa tuna hudumiwa sawa kwa kuletewa keki n.k. Vile vile, Siku kuu za Kiislam, hali ilikuwa hivyo hivyo. Waumini wa Kikriso Wakatoliki walikuwa wanasali Kanisa Kuu (Cathedral) ambalo lipo jirani. Waumini wakristo wengine walikuwa wanapewa nafasi katika mojawapo ya madarasa kusali. Wanafunzi waislam waliruhusiwa kwenda kwenye misikiti mjini, na hawakulalamika! Sasa kama imefikia hutua hiyo, nafikiri irudishwe ABBEY SECONDARY SCHOOL!
 
FF na wewe acha kuwa unakurupuka tu na kushabikia mambo hata usiyoyajua. Kuna watu hapo juu wameeleza vizuri kwamba vikundi vya wanafunzi vya kikristo Kama ukwata nk, huwa wanasali madarasani. Tycs (catholic) ndo pekee walio na kanisa, lakini kanisa Lao liko karibu na shule lakini HALIKO kwenye eneo la shule. Wao waislam ndo wamepewa jengo maalum kwa ajili ya shughuli zao za ibada. Usichoelewa hapo nini?

Nisichoelewa ni kwanini wasiruhusiwe kujenga mskiti wao?
 
hao wameshiba uji wa sembe wenye xukari na maandaz ya mama Lizi, Mwl. Mpemba na Mwl. Buku jero hawapo wakawaambia waache mgomo?!,
 
Kama kanisa limeruhusiwa kujengwa hapo shuleni na wao wanahaki ya kupewa nafasi ya kujenga mskiti. Kwanini kuwe na double standard? Kanisa wakubaliwe mskiti wakataliwe. Si haki, kama hapana ni wote na kama ndiyo ni wote.

wewe acha kiherehere,ijue kwanza historia ya shule, shule ilikuwa ya kanisa na kanisa lilikuwepo tangu enzi hizo, Ndanda seminary/hospital haikujengwa na serikali bali wakristo(wamishenari)! na waislam wamshukuru sana Nyerere kwa kutaifisha shule ambazo nyingi saaana zilikuwa zinamilikiwa na taasisi za dini ya kikristo na pia waislam wamshukuru kikwete kutokana na hotuba yake aliyotoa kwenye baraza la iddi mwaka huu kule Dodoma-kikwete alikataa serikali yake kurudisha shule zilizokuwa chini ya taasisi za dini kama ambavyo viongozi wa kiislam walitaka, jk alijua madhara ambayo yangewapata waislam kielimu kwa kuwa idadi ya shule za kiislam ni negligible ukilinganisha na idadi ya shule za kikristo na iwapo kila taasisi ingeamua kusomesha watu wa imani inayowahusu ingekuwaje? kwa hilo nampongeza sana jk kwa sababu hata mimi sipendi tusome kwa kubaguana kidini, sisi sote ni wa taifa moja, na elimu akipata mtu yeyote bila kujali dini yake na kama atakuwa muadilifu ataitumia kwa kujenga taifa letu! ila waislam wapunguze sana malalamiko na manung'uniko na kufuta kabisa dhana ya inferiority complex kitu ambacho kinawasumbua sana! kwa suala la ndanda inaonesha wazi kuwa kielimu waislam hawabaguliwi na ndo jambo la msingi linalompeleka mtu shule,sasa wanahamia kwenye mambo mengine bila kujua vizuri historia ya sehemu husika na sasa wanapoteza muda wa kusoma wakati wenzao wanaendelea kusoma halafu wakifeli wataleta mzozo mwingine kuwa wananyanyaswa kielimu!
 
Ni jumatatu nyingine tena kikundi kimoja cha kidini (waislam),wamesababisha kutoweka kwa amani baada ya kuanzisha mgomo kwa lengo la (a)kudai kunyimwa kupatiwa eneo la kujenga msikiti shuleni (b)kukataa uongozi wa wanafunzi kwa kudai kutokuwa na usawa katika uongozi huo(idadi sawa ya waislam na wakristo)
, kwa style hii shule itageuka eneo la kuabudia..

Nyie mdogo
Mmeenda kusoma au kubiri dini. Shenzi type. Mnadhani ukombozi wa kifikra unatokea msikitini au kanisani?
Hizo habari waachieni watu wa huku mtaani, fanyeni kilichowapelekeni huko.
 
Kwa hiyo hapo Tatizo ni Kanisa lililojengwa na "wenye shule"! Kwa kuwa Azania, Jangwani, Zanaki na Tambaza Sekondari hazina makanisa ndani yake basi Waislamu hawana haja ya kujenga misikiti ndani ya shule hizo.

HIYO NI SPECIAL MISSION NI CHOKOCHOKO ZA UDINI NA WAMEKUWA BRAIN WASHED.

Saa kama imeshajulikana kuwa ni chokochoko kwanini wasipewa tu eneo la kujemga mskiti wao ili kunyamazisha hiyo chokochoko? kwani mskiti ukiwepo hapo kama kanisa kuna tatizo lipi?
 
nashauri serikali itangaze shule hiyo kuwa ya kilimo halafu wale wadudu anaopenda bujibuji wafugwe, iwe ni zamu yaq kila mtu kuwahudimia. hii itakuwa ni njia ya kuwafundisha vijana kufikiria ujasiliamali na sio udini.

kilo moja ya mdudu ni zaidi ya kilo moja ya ng'ombe. 6,000tsh/kg kwa 4,000tsh/kg
Ni kivutio kizuri sana cha utalii.
[h=6][/h]
 
Wanafunzi wa kiislamu wana kila sababu ya kuomba eneo wajengo msikiti. Hawakuomba watengewe bajeti, wameomba eneo tu.
Hapo kipi kinaleta tatizo.
 
Kama kanisa limeruhusiwa kujengwa hapo shuleni na wao wanahaki ya kupewa nafasi ya kujenga mskiti. Kwanini kuwe na double standard? Kanisa wakubaliwe mskiti wakataliwe. Si haki, kama hapana ni wote na kama ndiyo ni wote.

Ndugu uwe unaelewa kwanza kabla ya kuja na zako ulizozizoea. Kwenye eneo la shule hakuna kanisa, isipokuwa jirani na shule kuna kanisa katoliki ambalo ni la watawa wabenedictine ambao ndio walikuwa wamiliki wa shule hiyo kabla haijachukuliwa na serikali. Kanisa hili sio kwa ajili ya wanafunzi bali wanajumuia wote wa ndanda.

Tena kama kungekuwa na wanaostahili kudai basi labda ni wale wa jumuia nyingine kama UKWATA, SABATO nk ambao vipindi vya kuabudu wanavifanyia madarasani, hao ndugu zako wana chumba maalum kwa ajili ya mambo yao tokea miaka mingi, wanaswali na kughani kila wanapohitaji na hawabughudhiwi na yeyote.
 
Umeandika vema, eneo la shule si kubwa kivile, kwani ukiacha lile la mlimani na pale nyuma ya uwanja wa soccer kama unaelekea Ndoro, maeneo mengine yaliyobaki ni ya Chuo cha ufundi, kanisa (masista na bruda wa kibenedikitini)

Kama vipi wapewe eneo kule shambani Liputu wakajenge huko

Hapo umenena, liputu eneo ni kubwa tu mpaka mamluki wameingia kulima mahindi na maboga. Na hivi bodaboda za kumwaga watawahi tu swala zote za siku.
 
Back
Top Bottom